Dr.habelnoah

Dr.habelnoah unaswali changamoto uliza jambo jema katika maisha ni kuuliza ili kujifunza

13/06/2026

***MALAIKA akiwa kwenye michakato 😂😂***

13/06/2026

Sasa unaingia mkoa wa dar es salaam😀

13/06/2026

Ila Dar es Salaam inafundisha mambo mengi sana..🤣 nilipokuja Dar ndio nilijua kwamba kumbe Utumbo wa kuku na vichwa vya dagaa huwa vinaliwa..🤣 huko kwetu kichwa na utumbo vilikuwa vinatolewa kwa sababu ni vichungu wanapewa kuku..lakini Dar kumbe kila kitu kinafyeka...🤣🤣hebu na wewe tuambie ni kitu gani ulipofika Dar kwa mara ya kwanza kilikushangaza..!?🤣

13/06/2026

Nyingine tena,, hii msusi wake nina namba zake karibuni😀

13/06/2026

BY DR.HABELNOAH
MESIC HOSPITAL
ARUSHA

Sababu Za Kuwashwa Baada Ya Kuoga

“Wataalamu wa afya ya ngozi pia wanabainisha kuwa kuoga muda mrefu na mara kwa mara, matumizi ya sabuni zenye harufu kali na povu jingi ni mambo mengine yanayochangia kutokea kwa mzio pamoja na ukavu wa ngozi kutokana na uwezo wake wa kuondosha kiasi kikubwa cha mafuta yanayolinda ngozi.

Ili kupunguza hali ya muwasho, “Tumia sabuni zenye mafuta, lakini zisiwe na marashi makali.”

Katika hali ya kawaida kitendo cha kuoga kinapaswa kuchukuliwa k**a jambo la kufurahisha kutokana na ukweli kwamba huufanya mwili uburudike na kuwa safi. Lakini kwa baadhi ya watu mambo ni tofauti. Kuoga huwa sawa na karaha.

Moja ya matatizo ya kiafya ambayo yanayosumbua watu wengi duniani na kuwanyima raha ya maisha, ni tatizo la mwili kuwasha mara baada ya kuoga. Muwasho baada ya kuoga unaweza kujitokeza mwili mzima au unaweza kuhusisha baadhi ya sehemu.

Hali hii inaweza kuwa inajitokeza kwa muda wa dakika chache au inaweza kuchukua muda mrefu na kwa baadhi ya watu, hili linaweza kuwa tatizo sugu. Ingawa tatizo hili la kiafya ni k**a mengine, lakini baadhi ya watu kwa kukosa taarifa sahihi, hulihusisha na imani potofu.

Ukweli wa mambo ni kwamba kuna sababu nyingi zinazochochea kutokea kwa tatizo hili na baadhi hazina madhara makubwa k**a vile kuhatarisha kwa maisha.

Pamoja na ukweli wa kisayansi kwamba asilimia 70 ya mwili wa binadamu ni maji, kwa upande mwingine yanaweza kuwa chanzo cha matatizo ya kiafya hasa pale yanapokuwa na vitu vinavyosisimua mwili au kuchochea hali ya kutokea kwa mzio. Siyo jambo la kushangaza kuona kuwa maji ambayo ni safi na salama kwa kunywa yanaweza kuwa siyo salama kwa kuoga.

SABABU ZA MUWASHO MWILINI
Miongoni mwa sababu za kutokea kwa muwasho wa mwili baada ya kuoga ni za kimazingira na sababu zingine zinahusiana na hitilafu za urithi wa vinasaba vya kijenetiki katika mfumo wa kinga ya mwili wa mhusika.

Wakati mwingine tatizo hili linaweza kuwa ni dalili muhimu inayoonyesha baadhi ya magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza k**a vile matatizo ya figo, ini, tezi shingo, matatizo ya mfumo wa damu, kisukari, saratani ya mitoki na msongo wa mawazo.

Baadhi ya tafiti zinabainisha kuwa sababu nyingine ni pamoja na uchafuzi wa mazingira ya hewa kwa kemikali zenye sumu zinazopatikana katika moshi wa tumbaku, mifuko ya plastiki, dawa za kufanyia usafi majumbani, dawa za kuua wadudu, vumbi ya ndani ya nyumba yanayobeba vimelea vya magonjwa pamoja na uchafuzi wa hewa kwa moshi wa magari na ule unaozalishwa na viwanda katika maeneo ya mijini.

Vitu hivi huufanya mwili kuathirika na kutengeneza mazingira ya ndani ambayo yanachochea kutokea kwa muwasho pindi mwili unapopata msisimuko, hali ambayo hujulikana k**a mzio.

Mzio huanza pale mfumo wa kingamwili unapobainisha kemikali hizi k**a mvamizi wa mwili na kuamuru askari wake wajulikanao k**a seli za T-lymphocites na B-lymphocytes kujibu mapigo ya wavamizi kwa kuzalisha kemikali maalumu zijulikanazo k**a immunoglobulin E na prostaglandins ambazo husababisha kuzalishwa kwa kemikali nyingine k**a vile histamine, tryptase na chymase, kwa lengo la kuvunja nguvu za kemikali vamizi.

NI KWA NAMNA GANI?
Baadhi ya watafiti wanabainisha kuwa kutokana na hitilafu za vinasaba vya kijenetiki kunakuwa na ongezeko la kemikali aina ya Cyclic Adenosine Monophosphate Phosphodiesterase ambayo inaharibu mfumo wa udhibiti wa seli za kinga mwili aina ya basophils na seli za mast na kusababisha zisisimuke kupita kiasi na kuzalisha histamine nyingi ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa mzio.

Watu wengi wana mzio wa vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na dawa za tiba, kemikali zinazotumika kutengenezea sabuni, vipodozi, aina fulani za vyakula, kemikali kadhaa zinazotumika katika usindikaji wa vyakula, kemikali zinazowekwa katika maji k**a vile chlorine (watergurd), maji ya kuoga yenye chumvi nyingi na kemikali zinazotumika katika utengenezaji wa nguo, ikiwa ni pamoja na mataulo ya kuogea.

Mapambano kati ya kinga mwili na kile ambacho mwili hukibainisha kwa makosa k**a wavamizi, yanaweza kusababisha magonjwa ya pumu, muwasho wa ngozi, muwasho wa macho, mafua ya mara kwa mara na maumivu ya tumbo.

SABABU NYINGINE
Mapambano haya pia yanaweza kusababisha hali ya mzio dhidi ya vyakula k**a vile mayai, maziwa, samaki, nyama, karanga, vyakula vitokanavyo na unga wa ngano, kahawa, pombe na baadhi ya vyakula na vinywaji vinavyotengenezwa au kusindikwa viwandani kwa kutumia kemikali. Hali hii pia inaweza kutokea kutokana na kula vyakula vyenye mchanganyiko wa vikolezo k**a pilau na viungo vingi.

Ulaji wa vyakula vyenye upungufu wa viinilishe nao unatajwa kuwa unachangia kutokea kwa tatizo la mwili kuwasha wakati wa kuoga.
Watu wengi hawatumii kiasi cha kutosha cha matunda, mboga na mafuta salama yanayotokana na mimea au samaki, jambo ambalo huathiri vibaya afya ya ngozi.

Tatizo jingine linalochangia mwili kuwasha wakati wa kuoga ni kutokutumia kiasi cha kutosha cha maji ya kunywa kila siku. Hali hiyo inafanya mwili kuwa na upungufu wa maji na kuathiri vibaya afya ya ngozi na uwezo wake wa kuondosha sumu mwilini.

Ngozi isiyokuwa na afya njema inashindwa kutunza kiasi cha kutosha cha unyevu na kusababisha ukavu. Ngozi inapokuwa kavu husisimka kupita kiasi wakati wa kuoga na kusababisha muwasho. Sababu ya mwili kuwasha baada ya kuoga ni kuishi katika hali ya msongo wa mawazo inayosababishwa na hofu, wasiwasi na sonona.

Tatizo jingine linalosisimua mwili na kusababisha muwasho wakati wa kuoga ni kujisugua kupita kiasi au kujisugua wakati wa kujifuta kwa taulo baada ya kuoga. Kwa kawaida seli za ngozi zilizokufa, jasho na vumbi ndivyo vinasababisha mwili kuchafuka.

Lakini uchafu huo huondoka mwilini tunapooga na nguvu nyingi hazihitajiki ili kuondosha uchafu na taka mwili juu ya ngozi. Matumizi ya nguvu nyingi na kusugua ngozi sana, husababisha madhara kwenye ngozi na kusababisha muwasho au ukavu wa ngozi kwa kuondosha mafuta yanayolinda usalama wa ngozi.

Watu wenye tatizo hili wanaweza kufanya mazoezi mepesi kabla ya kuoga ili kupasha mwili joto au kupaka lotion ili kuifanya ngozi kuwa na unyevu na kupunguza hali ya ukavu wa ngozi.

13/06/2026

BY DR.HABELNOAH
MESIC HOSPITAL
ARUSHA

Moshi wa sigara ukimpata mtoto uathiri mapafu yake akikua

Utafiti uliofanyika nchini Marekani umebaini kwamba watu wazima wasiovuta sigara lakini walipokuwa watoto wazazi wao walivuta sigara mbele yao,wana hatari kubwa zaidi ya kufa kutokana na maradhi ya mapafu.

Watafiti wanasema kati ya watu laki moja ,watu saba hufa kila mwaka kutokana na madhara ya sigara waliyoyapata wakiwa watoto.

Watalamu wanasema kinga bora zaidi ya kuzuia watoto kutoathirika na sigara ni wazazi kuacha kuvutaji sigara kabisa.

Aidha utafiti huo umebainisha kwamba sio watoto peke yake ndio wanaweza kuathiriwa na sigara bali hata mtu mzima ambaye havuti sigara lakini anaishi au anakuwa karibu na mtu anayevuta sigara.

Moshi wa sigara wa saa 10 au zaidi kwa kila wiki unaongeza hatari ya vifo vya ugonjwa wa moyo kwa asilimia 27,kupooza kwa asilimia 23 na madhara katika mapafu kwa asilimia 42 ukilinganisha na wale ambao wanaishi na watu wasiovuta sigara.

Utafitit huu ambao umechapishwa kwenye jarida la ' Preventive Medicine' uliwauliza watu kuhusu uvutaji sigara katika maisha yao na wanayaangaliaje maisha yao baada ya miaka 22.

Kumekuwa na kampeni ya kuwazuia watu kuvuta sigara katika maeneo ya ndani ili watoto au watu wasiovuta wasiathirike lakini maeneo maalum ya kuvuta sigara yanaonekana kuwa ni machace bado na njia pekee inayoweza kusaidia madhara yasiwepo ni watu kuacha kabisa uvutwaji sigara.

Dr Nick Hopkinson ambaye ni mshauri wa masuala ya afya kutoka taasisi ya mapafu nchini Uingereza 'the British Lung Foundation, agreed, saying' anasema kuwa kuna madhara makubwa ambayo mtoto anaweza kuyapata anapovuta moshi wa sigara.

Ni vyema kwa wazazi ambao wana watoto wadogo au wanawake wajawazito kupata msaada wa kuacha kuvuta sigara.

Sigara ina madhara yanayohatarisha Maisha
Watoto ambao wazazi wao wanavuta sigara wapo katika hatari kubwa zaidi ya kupata mangojwa k**a ya pumu na athari katika mapafu. Utafiti unaonesha kuwa madhara ya uvutaji wa sigara kwa watoto uonekana pale anapokuwa mtu mzima.

Vilevile madhara ya sigara yanaweza kusababisha ongezeko la magonjwa sugu na maisha ya utegemezi hapo badae.

Address

Arusha

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Dr.habelnoah posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share

Category