08/02/2023
MAALUM KWA WANAWAKE
Kuna changamoto ya mawasiliano linapokuja swala la kumsahihisha mwanaume. Wanawake wengi wanashangaa kwa nini wanaweza kutumia maneno makali au ya dharau na kejeli lakini mwanaume asibadilike, na mwisho wa siku ni k**a anaendelea na tabia yake.
Sikia hii, MWANAUME hasahihishwi au kukosolewa kwa kutumia lugha mbaya ya ukali au kejeli. Mfano mwanajme ni mchafu ukamwambia " mwanaume gani unakuwa mchafu namna hii, hivi umelelewaje kwenu wewe" au mwanaume gani hujitambui hujali mkeo!
Kauli k**a hizo zinamfanya mwanaume azidishe tabia yake inayokukera kwa sababu ndio njia pekee ya kukuonesha kwamba hapendi kauli zako. Kwa hiyo k**a una mpango mwanaume wako abadilike chunga mdomo wako TUMIA LUGHA NZURI laini ya k**e na MHAMASISHE kwa shukrani anapofanya kitu ambacho ungependa awe anafanya kila siku.
Bro M***a Kisoma
0753 469525
Masomo zaidi yako kwa website www.muyo.co.tz na pia unaweza kupakua Muyo App kwenye Playstore.