Isaya Febu

Isaya Febu Tunawasaidia wanaume na wanawake kutatua changamoto za afya ya uzazi kwa kutumia virutubisho.

Dalili Za Mwanamke Mwenye Hamu Ya Kufanya Mapenzi.Hamu ya kufanya mapenzi (sexual arousal) kwa mwanamke hujionyesha kwa ...
09/07/2026

Dalili Za Mwanamke Mwenye Hamu Ya Kufanya Mapenzi.

Hamu ya kufanya mapenzi (sexual arousal) kwa mwanamke hujionyesha kwa mabadiliko ya kihisia, kitabia, na kimwili. Hata hivyo, ni muhimu kukumbuka kuwa dalili za mwanamke mwenye hamu ya kufanya mapenzi hutofautiana sana kati ya wanawake, na haziwezi kutumika kuthibitisha kwamba anataka kufanya mapenzi. Ridhaa ya wazi ndiyo njia pekee ya kujua.

1) Dalili Za Kihisia Na Kitabia.

Mwanamke mwenye hamu ya kufanya mapenzi anaweza:

Kutafuta kuwa karibu na mwenza wake.
Kuanzisha mazungumzo ya kimapenzi au ya kimahaba.
Kukumbatia, kushikana mikono, au kubusu mara kwa mara.
Kuonyesha tabasamu, kucheka, na kuwasiliana kwa macho kwa muda mrefu.

Kuonyesha kuvutiwa na mguso wa mwenza na kuurudisha.
Kuonekana mwenye utulivu na kufurahia ukaribu wa kimapenzi.
Hata hivyo, baadhi ya wanawake wanaweza kuwa na hamu lakini wasionyeshe dalili hizi waziwazi kutokana na aibu, utamaduni, au hulka yao.

2) Dalili Za Kimwili.

Wakati wa msisimko wa kingono, mwili unaweza kufanya mabadiliko yafuatayo:

Uke kuwa na unyevunyevu kutokana na ute wa asili unaorahisisha tendo la ndoa.
Kinembe (cl****is) kujaa damu na kuwa nyeti zaidi.
Midomo ya uke (l***a) kuvimba kidogo na kubadilika rangi kwa sababu ya kuongezeka kwa mtiririko wa damu.
Chuchu kusimama na matiti kuwa nyeti zaidi kwa mguso.
Mapigo ya moyo na kasi ya kupumua kuongezeka.
Uso au kifua kuwa na wekundu kwa baadhi ya wanawake.
Misuli ya nyonga kukaza kidogo.
Hamu Ya Kufanya Mapenzi

3) Mambo Yanayoathiri Hamu Ya Kufanya Mapenzi.

Hamu inaweza kuongezeka au kupungua kulingana na:

Uhusiano mzuri na mwenza.
Hisia za usalama na kuaminiana.
Mzunguko wa hedhi (kwa baadhi ya wanawake hamu huongezeka karibu na kipindi cha ovulation).
Msongo wa mawazo, uchovu, au magonjwa.
Homoni na baadhi ya dawa.

HITIMISHO.

Mwanamke anaweza kuwa na unyevunyevu ukeni bila kuwa na hamu ya kufanya mapenzi, na pia anaweza kuwa na hamu lakini asiwe na unyevunyevu wa kutosha. Hivyo, dalili za mwili pekee hazitoshi kujua anachotaka.

Kuonyesha ukaribu, kutabasamu, au kuvaa kwa namna fulani hakumaanishi ametoa ridhaa ya kufanya mapenzi.

Ridhaa inapaswa kuwa ya wazi, ya hiari, na endelevu, na mtu anaweza kubadili uamuzi wake wakati wowote.

Ujue Utando Mweupe Anaozaliwa Nao Mtoto Kwenye Ngozi Na Kazi Zake.Je umewahi kuona mtoto aliyetoka kuzaliwa ana k**a vit...
06/05/2026

Ujue Utando Mweupe Anaozaliwa Nao Mtoto Kwenye Ngozi Na Kazi Zake.

Je umewahi kuona mtoto aliyetoka kuzaliwa ana k**a vitu vyeupe juu ya ngozi?

Halafu watu wanaanza kusema “labda mama wakati wa ujazito alikula chakula fulani…” au labda mama aliendelea kufanya mapenzi kipindi chote cha ujauzito mpaka anajifungua…”

K**a jibu ni NDIYO, ukweli ni kwamba, hayo maneno hapo juu na mengine mengi yanayosemwa na watu huko mtaani baada ya mtoto kuzaliwa na vitu vyeupe juu ya ngozi yake, hayana uhalisia wowote kwani ni IMANI POTOFU tu.

Hivyo vitu vyeupe unavyoviona juu ya ngozi ya mtoto aliyetoka kuzaliwa sio uchafu, bali kitaalam tunaita vernix caseosa.

Neno hili vernix caseosa linatokana na Kilatini: vernix = “mafuta/varnish” na caseosa = “k**a jibini”. Hivyo, vernix caseosa ni utando mweupe, laini k**a krimu au jibini au unaweza ita lotion ya asili kwa mtoto ambao unafunika ngozi yake akiwa tumboni na hata wakati wa kuzaliwa.

Vernix Caseosa Imetengenezwa Na Nini?

Vernix caseosa ni mchanganyiko wa vitu vitatu vikuu:

1) Mafuta (lipids).

Hutoka kwenye tezi za mafuta za mtoto (sebaceous glands). Mafuta haya hufanya vernix caseosa iwe laini na isiruhusu maji kupenya.

2) Seli Za Ngozi Zilizokufa (Corneocytes).

Hizi ni seli kutoka tabaka la juu la ngozi ambazo husaidia kuunda ule muundo mzito wa vernix caseosa.

3) Maji.

Vernix caseosa ina kiasi kikubwa cha maji (zaidi ya nusu). Hii husaidia kulainisha ngozi ya mtoto.

Pia ina vitu vingine vidogo k**a vile:

Protini za kinga (antimicrobial proteins)
Enzymes zinazosaidia kulinda ngozi

Vernix Caseosa Huzalishwa Kipindi Gani?

Vernix caseosa huanza kutengenezwa wakati wa ujauzito:

Huanzia takriban wiki ya 20–24 ya ujauzito
Huongezeka zaidi kadri mimba inavyoendelea
Hufikia kiwango kikubwa karibu wiki ya 34–38 (karibu na kujifungua)

Kwa watoto:

Waliotangulia kuzaliwa (preterm): huwa na vernix caseosa nyingi zaidi
Waliochelewa (post-term): huwa na vernix caseosa kidogo au imepungua.

Kazi Za Vernix Caseosa:

Vernix caseosa kwa mtoto hufanya kazi zifuatazo;

1) Kinga Ya Ngozi Dhidi Ya Maji Ya Uzazi.

Mtoto hukaa ndani ya maji ya uzazi kwa muda mrefu. Bila vernix caseosa, ngozi ya mtoto ingeweza kulainika kupita kiasi (maceration) lakini pia vernix caseosa hufanya k**a kinga ya asili (barrier) kulinda ngozi ya mtoto.

2) Kinga Dhidi Ya Maambukizi.

Vernix caseosa ina kemikali za asili zinazopambana na bakteria na fangasi hivyo husaidia kupunguza hatari ya mtoto kupata maambukizi kabla na baada ya kuzaliwa.

3) Husaidia Wakati Wa Kujifungua.

Vernix caseosa hufanya ngozi ya mtoto kuwa laini na yenye utelezi, hii hupunguza msuguano wakati wa kupita kwenye njia ya uzazi. Hivyo kumrahishishia mama mjamzito wakati kujifungua.

4) Kudhibiti Joto La Mwili.

Baada ya mtoto kuzaliwa, vernix caseosa husaidia mtoto kudumisha joto la mwili (temperature regulation). Lakini pia inasaidia sana kwa watoto wachanga ambao bado hawajakomaa kikamilifu (wamezaliwa kabla ya week 37, yaani preterm babies) kwa kupunguza upotevu wa joto haraka.

5) Kuimarisha Ukuaji Wa Ngozi Ya Mtoto.

Vernix caseosa husaidia kuimarisha ngozi ya mtoto kwa kuifanya iwe na afya na imara baada ya kuzaliwa.

6) Kutoa Unyevu (Moisturizing Effect).

Vernix caseosa ni k**a “lotion ya asili” kwa mtoto ambayo hulainisha ngozi ya mtoto na huzuia kukauka.

7) Ina Mchango Katika Mfumo Wa Kinga Wa Mtoto.

Vernix caseosa Ina protini na vitu vinavyosaidia kuandaa mfumo wa kinga wa mtoto.

HITIMISHO:

Vernix caseosa haina uhusiano na chakula alichokula mama wakati wa ujazito, haina uhusiano na tendo la ndoa wakati wa ujauzito, hivyo ukiona mtoto amezaliwa nayo USIHOFU kwani inaweza kuondoka kirahisi baada ya mtoto kuogeshwa au hata ikaisha yenyewe bila shida.

Kwa ushauri na tiba ya magonjwa ya afya ya uzazi wasiliana nasi kwa simu namba 0625 305 487. Ni mimi mwenye kujali afya yako Dr. Isaya Febu.

Jinsi Ya Kufanya Uume Uwe Imara.Uume Imara (Afya Ya Uume):Ili kufanya uume uwe imara (kuwa na nguvu wakati wa tendo la n...
09/04/2026

Jinsi Ya Kufanya Uume Uwe Imara.

Uume Imara (Afya Ya Uume):

Ili kufanya uume uwe imara (kuwa na nguvu wakati wa tendo la ndoa), unahitaji kuzingatia afya ya mwili, akili, na mtindo wa maisha.

Zifuatazo ni baadhi ya njia muhimu na salama kabisa zinazosaidia uume uwe imara (kuwa na nguvu wakati wa tendo la ndoa);

1) Lishe Bora (Chakula Kina Nafasi Kubwa Sana).

Lishe bora ni msingi mkubwa wa afya ya uume kwa sababu kusimama kwa uume (pe**le er****on) hutegemea mtiririko mzuri wa damu.

Mwili unapopata virutubisho sahihi, huongeza mzunguko wa damu na uzalishaji wa homoni ya kiume, testosterone ambayo ni muhimu kwa nguvu za kiume.

Vyakula muhimu vya kuzingatia ni pamoja na;
a) Matunda k**a tikiti maji, ndizi na parachichi - huongeza mzunguko wa damu
b) Mboga za majani (spinach, sukuma wiki) - zina nitrates zinazoongeza mtiririko wa damu
c) Samaki wenye mafuta (k**a salmon, sardine) - wana omega-3 ambayo huimarisha afya ya moyo, kuongeza mtiririko wa damu kwenye mishipa ya damu
d) Karanga, ufuta, mbegu za maboga– zina madini ya zinki ambayo huongeza uzalishaji wa homoni ya kiume, testosterone
e) Kunywa angalau glasi 8–10 za maji kwa siku

Vyakula vya kuepuka ni pamoja na;
a) Vyakula vya mafuta mengi (fast food)
b) Vyakula vyenye sukari nyingi

Ulaji wa vyakula hivyo mara kwa mara huchangia unene kupita kiasi (obesity) hali ambayo hufanya mishipa ya damu kuziba polepole na kupunguza mtiririko wa damu kwenye mishipa.

2) Fanya Mazoezi Ya Mwili Mara Kwa Mara.

Mazoezi ya mwili ni muhimu kwa kuboresha afya ya moyo na mzunguko wa damu, ambayo ni msingi wa afya uume wenye nguvu. Mazoezi ya mwili huongeza mtiririko wa damu kwenda kwenye uume, husaidia kupunguza mafuta mwilini ambayo yanaweza kuzuia mishipa ya damu. Lakini pia huongeza stamina na nguvu za mwili kwa ujumla.

Aina za mazoezi ya mwili unayoweza kufanya ni pamoja na;
Kukimbia au kutembea haraka
Kuruka kamba
Mazoezi ya viungo vya chini ya mwili (squat, lunges)
Mazoezi ya misuli ya nyonga (Kegel exercise)

Mazoezi ya misuli ya nyonga (kegel exercise) huimarisha misuli inayosaidia kudhibiti mkojo na pia uume kusimama (pe**le er****on). Faida za mazoezi haya ni pamoja na: Huongeza uwezo wa kudumu (kusimamisha uume kwa muda mrefu) wakati wa tendo la ndoa, husaidia kudhibiti kumaliza mapema tendo la ndoa (premature ej*******on).

3) Epuka Matumizi Ya Pombe Na Sigara Kupita Kiasi.

Pombe na sigara zina athari kubwa kwenye uwezo wa uume kusimama (er****on) kwa sababu zinaathiri mzunguko wa damu, mfumo wa neva, na homoni iinayohusika na nguvu za kiume (testosterone).

Kunywa pombe kupita kiasi kunaweza kuathiri afya ya uume k**a ifuatavyo;

a) Hupunguza uwezo wa mfumo wa neva.

Uume husimama kutokana na ishara kutoka kwenye ubongo kwenda kwenye mishipa ya damu. Hivyo pombe hupunguza ufanisi wa mawasiliano haya ya neva, hufanya mwili ushindwe kuitikia msisimko wa kimapenzi kwa haraka.

b) Kupunguza mzunguko wa damu.

Uume unahitaji mzunguko mzuri wa damu ili kusimama. Pombe inasababisha mishipa ya damu kupanuka (vasodilation) kwa muda mfupi, lakini matumizi ya muda mrefu hupunguza ufanisi wa mishipa ya damu kwenye uume. Hii inaweza kusababisha tatizo la erectile dysfunction (ED), yaani kushindwa kusimama kwa uume.

c) Hushusha homoni ya kiume (testosterone).

Pombe inaweza kupunguza uzalishaji wa homoni ya kiume, testosterone, homoni muhimu kwa ajili ya hamu ya tendo la ndo kwa mwanaume na nguvu ya uume. Hivyo kupungua kwa homoni hiyo kunasababisha kupungua hamu ya ngono na shida ya uume kusimama.

Sigara ina kemikali nyingi hatari, hasa nikotini, ambazo zinaathiri mishipa ya damu, hivyo matumizi ya sigara kupita kiasi huathiri afya ya uume k**a ifuatavyo;

a) Husababisha mishipa ya damu kubana.

Nikotini husababisha mishipa ya damu kuwa myembamba (vasoconstriction). Hii inapunguza kiasi cha damu kinachofika kwenye uume.

b) Huharibu kuta za mishipa ya damu.

Hufanya mishipa kuwa migumu na isiyonyumbulika. Hii hupunguza uwezo wa mishipa kupanuka wakati wa msisimko.

c) Hupunguza oksijeni kwenye damu.

Moshi wa sigara una hewa ya kaboni monoksidi ambayo hupunguza hewa ya oksijeni kwenye damu hali ambayo huathiri afya ya uume kwani tishu za uume zinahitaji hewa ya oksijeni ya kutosha kufanya kazi vizuri.

d) Huongeza hatari ya magonjwa.

Sigara inahusishwa na magonjwa k**a vile shinikizo la juu la damu (hypertension), magonjwa ya moyo ambapo magonjwa hayo yote yanaweza kuathiri moja kwa moja nguvu za uume.

4) Punguza Msongo Wa Mawazo (Stress).

Uume kusimama hutegemea ushirikiano kati ya ubongo, homoni, neva, na mzunguko wa damu.
Msongo wa mawazo huingilia mfumo huu kwa njia zifuatazo;

a) Huchochea homoni za stress (cortisol).

Wakati mwanaume ana msongo wa mawazo:
Mwili huzalisha cortisol kwa wingi. Cortisol ikitolewa kwa wingi hupunguza testosterone (homoni muhimu kwa hamu na nguvu za kiume)

Matokeo yake: Hamu ya tendo la ndoa hupungua na kusimama kwa uume kunakuwa dhaifu

b) Huathiri mfumo wa neva.

Msongo wa mawazo huweka mwili katika hali ya " kupigana (fight) or kukimbia (flight)". Hali hii huzuia mwili kuwa na utulivu (relaxation),ambayo ni muhimu kwa uume kusimama. Hivyo ubongo hushindwa kutuma ishara sahihi za msisimko wa kimapenzi.

c) Huongeza mawazo ya hofu na wasiwasi.

Hofu ya kushindwa (performance anxiety) inaweza kufanya uume ushindwe kusimama.
Hii huunda mzunguko: hofu → kushindwa → hofu zaidi.

d) Hupunguza mtiririko wa damu.

Msongo wa mawazo unaweza kusababisha mishipa ya damu kubana, hali inayopelekea damu kutokutiririkai vizuri kwenda kwenye uume.

Kwa hiyo kupunguza msongo wa mawazo unashauriwa kulala vizuri, kufanya mazoezi ya kupumzika (meditation, kupumua kwa utulivu).

5) Dhibiti Uzito Wa Mwili.

Unene kupita kiasi unaweza kuathiri uzalishaji wa homoni ya kiume na mzunguko wa damu, hivyo kupunguza nguvu ya uume. Dhibiti uzito wa mwili kwa kufanya mazoezi ya mwili (physical exercises) mara kwa mara k**a vile kukimbia, kutembea haraka, kuruka kamba nk.

6) Pata Usingizi Wa Kutosha.

Usingizi mzuri (saa 6–8) husaidia homoni za mwili kufanya kazi vizuri, ikiwemo homoni ya kiume, testosterone. Uchovu unaweza kupunguza hamu na nguvu za tendo la ndoa.

7) Epuka Matumizi Ya Dawa Bila Ushauri Wa Dakari.

Dawa au virutubisho visivyo sahihi vinaweza kuathiri afya ya nguvu za kiume. Ni bora kupata ushauri wa daktari kabla ya kutumia dawa yoyote.

8) Dhibiti Magonjwa Sugu.

Magonjwa sugu k**a vile kisukari, shinikizo la juu la damu, na unene kupita kiasi yanaweza kuathiri nguvu za kiume. Ni muhimu kuyadhibiti vizuri kwa kupata ushauri wa daktari.

HITIMISHO:

Kwa ujumla, uimara wa uume hutegemea zaidi afya ya mwili na mtindo wa maisha wa kila siku. Pale ambapo mwanaume anajitunza kupitia mazoezi, lishe bora, kupunguza msongo wa mawazo, kupata usingizi wa kutosha, na kuepuka tabia zinazodhuru mwili, uwezo wa mwili kufanya kazi vizuri huimarika, ikiwemo utendaji wa mfumo wa uzazi. Aidha, kudhibiti hali za kiafya na kutafuta msaada wa kitaalamu inapobidi husaidia kuhakikisha tatizo halizidi. Hivyo, kujenga na kudumisha afya bora kwa ujumla ndiyo msingi mkuu wa kuwa na uimara mzuri wa uume.

Dawa Ya Kuimarisha Misuli Ya Uume:

By the way, hivi unajua kwamba dawa ya asili iitwayo, PANACEA itakusaidia kuimarisha misuli ya uume iliyolegea kutokana upigaji wa punyeto kiasi, matumizi ya pombe na sigara kupita kiasi? Ndiyo, kupata dawa hiyo wasiliana nasi kwa simu namba 0625 305 487, tunapatikana DODOMA mjini, Makulu center.

Kwanini Uke Unatoa Harufu Mbaya?Kutokwa Na Harufu Mbaya Ukeni:Kutoa harufu mbaya ukeni ni tatizo linalowasumbua wanawake...
02/01/2026

Kwanini Uke Unatoa Harufu Mbaya?

Kutokwa Na Harufu Mbaya Ukeni:

Kutoa harufu mbaya ukeni ni tatizo linalowasumbua wanawake wengi duniani, hususani wakati wa tendo la ndoa. Uke kutoa harufu mbaya kwa kiasi kikubwa husababishwa na fangasi wa candida albicans, japo sio kila mara ndio maana kuna umuhimu wa kutafuta chanzo cha tatizo la kunuka uke.

Uke kutoa harufu mbaya kunaweza kusababishwa na mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na:

1) Maambukizi Ya Bakteria.

Maambukizi ya bakteria (Bacterial Vaginosis) ni mojawapo ya sababu inayochangia harufu mbaya ukeni. Maambukizi haya hutokea wakati kuna mabadiliko katika uwiano wa bakteria ndani ya uke, ambapo bakteria wabaya (pathogens) wanakuwa wengi kuliko bakteria wazuri (normal flora). Hali hii inaweza kusababisha harufu mbaya ukeni inayofanana na shombo la samaki, hasa baada ya kufanya tendo la ndoa.

2) Maambukizi Ya Fangasi Ukeni.

Maambukizi ya fangasi ukeni (Yeast Infection) yanaweza kusababisha harufu mbaya ukeni pamoja na dalili nyingine k**a vile kuwasha na kutokwa na uchafu mweupe ukeni unaofanana na jibini (maziwa mgando).

3) Magonjwa Ya Zinaa.

Baadhi ya magonjwa ya zinaa (Sexually Transmitted Infections) k**a trichomoniasis, gonorrhea, na chlamydia yanaweza kusababisha harufu mbaya kutoka kwenye uke.

4) Kukosekana Kwa Usafi Binafsi Wa Kutosha.

Ukosefu wa usafi binafsi kwa mwanamke unaweza kuchangia harufu mbaya ukeni. Mwanamke unashauriwa kuepuka kutumia sabuni zenye kemikali au bidhaa zenye harufu kali katika kuosha sehemu za siri kwa sababu zinaweza kuvuruga usawa wa pH ya uke.

5) Mabadiliko Ya Homoni.

Wakati wa mzunguko wa hedhi, ujauzito, au kipindi cha ukomo wa hedhi (menopause), mabadiliko ya homoni yanaweza kuathiri harufu ya uke. Mfano: Baadhi ya wanawake wanapata harufu mbaya ukeni wakati wa hedhi au baada ya hedhi kutokana na mabadiliko ya homoni na uwepo wa damu kwenye uke.

6) Matumizi Holela Ya Antibiotics Na Bidhaa Za Kemikali.

Hutumiaji kiholela wa dawa, antibiotics bila ushauri au maelekezo ya wataaalamu wa afya (daktari) ni mojawapo ya sababu ya mwanamke kutoa harufu mbaya ukeni lakini pia matumizi ya sabuni zenye harufu kali, douches, au bidhaa nyingine za kemikali kwa ajili ya kuosha uke inaweza kuvuruga usawa wa pH ya uke na kusababisha harufu mbaya ukeni.

7) Maambukizi Katika Viungo Vya Uzazi Vya Ndani Vya Mwanamke.

Maambukizi ya viungo vya uzazi vya ndani vya mwanamke (Pelvic Inflammatory Disease) k**a vile mirija ya fallopian, kizazi, na ovari. PID mara nyingi husababishwa na maambukizi ya bakteria, kawaida kupitia ngono zisizo salama. Harufu mbaya kutoka ukeni inaweza kuwa moja ya dalili za PID, ingawa si dalili pekee. Dalili zingine za PID zinaweza kujumuisha maumivu ya tumbo chini ya kitovu, kutokwa na ute wenye rangi na harufu mbaya ukeni, maumivu wakati wa kujamiiana, na homa.

Jinsi Ya Kuondoa Harufu Mbaya Ukeni:

Ili kudhibiti harufu mbaya ya uke, ni muhimu kwa mwanamke kuzingatia mambo yafuatayo:

1) Fanya usafi wa uke mara kwa mara kwa kutumia maji na sabuni isiyo na kemikali kali.

2) Vaa nguo za ndani za pamba ambazo huruhusu hewa kupita.

3) Epuka kutumia bidhaa zenye harufu kali katika maeneo ya siri.

4) Mtembelee daktari mara tu unapogundua harufu isiyo ya kawaida ili kufanyiwa uchunguzi na kupata matibabu sahihi.

HITIMISHO:

Dawa Ya Asili Ya Kutoa Harufu Mbaya Ukeni:

By the way hivi unajua kwamba dawa ya asili iitwayo PANACEA iliyotengenezwa kutokana na mimea na matunda itakusaidia mwanamke kutokomeza changamoto ya kutoa harufu mbaya ukeni?

Ndiyo ni kweli, kupata dawa hiyo wasiliana nasi kwa simu namba 0625 305 487.

Address

Majumba Sita
Dar Es Salaam
00255

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 20:00
Wednesday 09:00 - 20:00
Thursday 09:00 - 20:00
Friday 09:00 - 20:00
Saturday 09:00 - 20:00
Sunday 09:00 - 20:00

Telephone

+255625305487

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Isaya Febu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share