Tabibu Fadhili Paulo

  • Home
  • Tabibu Fadhili Paulo

Tabibu Fadhili Paulo Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa tiba asili, nauza dawa za Asili. Nipo Kibugumo Mji Mwema Kigamboni Dar Es Salaam Tanzania.

Simu|WhatsApp +255714800175

Ukiona umependezwa na huduma yangu usisahau kuniunganisha na ndugu, rafiki na jamaa zako wengine.

Magonjwa hatari 18 yanayotibika kwa kutumia mbegu za mabogaMbegu za maboga zina protini na madini ya kutosha na ya mhimu...
07/06/2026

Magonjwa hatari 18 yanayotibika kwa kutumia mbegu za maboga

Mbegu za maboga zina protini na madini ya kutosha na ya mhimu zaidi mwilini k**a madini ya zinki, kopa, maginizia, manganizi na chuma, mbegu za maboga ni tamu na zinaweza kutafunwa nyakati zozote na mahali popote hasa kwa wapenda kutafuna-tafuna k**a mimi.

Tafiti mbalimbali zimethibitisha pasipo na shaka kuwa mbegu za maboga zina faida nyingi kiafya na zina uwezo wa kukuepusha na magonjwa hatari zaidi ya 10 yafuatayo:

1. UGONJWA WA MOYO

Kiasi kingi cha madini ya magnesium katika mbegu za maboga yanazifanya mbegu hizi kuwa mhimu sana kwa watu wenye magonjwa mbalimabli ya moyo. Madini ya magnesium ni mhimu kwa ajili ya kuimarisha msukumo wa damu kwenye moyo na kuimarisha afya ya mishipa ya damu hatimaye kutibu na kuzuia magonjwa ya moyo.

Mbegu hizi pia zina mafuta mengine mhimu zaidi kwa watu wenye ugonjwa wa moyo yenye OMEGA 3.

2. HUIMARISHA KINGA YA MWILI

Mbegu za maboga zimebarikiwa kuwa na kiasi cha kutosha cha madini ya zinki (zinc). Kazi kubwa ya madini ya zink ni kuimarisha kinga ya mwili.

Upungufu wa madini ya zink unaweza kupelekea matatizo kadhaa mwilini ikiwemo kuzaa watoto njiti, kuishiwa nguvu za kiume, matatizo ya homoni, chunusi nyingi mwilini, watoto kuwa na uwezo mdogo shuleni kimasomo na matatizo mengine kadhaa ya kimwili na kiakili.

3. HUONGEZA UWEZO WA MACHO KUONA

Mbegu za maboga zina Vitamini E, vitamini A, lutein, beta-carotene na zeaxanthin, vitu hivi vinavyopatikana katika mbegu za maboga ni mhimu kwa ajili ya nuru ya macho.

Vitamini A na madini ya zinki ni mhimu kwa ajili ya uzalishaji wa ‘melanin’ kimeng’enya mhimu ambacho hutengenezwa kwa asili na miili yetu kwa ajili ya ulinzi wa afya ya macho.

4. KINGA YA KISUKARI

Kisukari ni moja ya ugonjwa unaoendelea kwa kasi kuwasumbua watu wengi kila pembe ya dunia.

Mbegu za maboga zina vitu vitatu mhimu zaidi ambavyo ni ‘Nicotinic acid’, ‘Trigonelline’ na ‘D-chiro-inositol’ ambavyo husaidia kushusha damu sukari mwilini na kudhibiti kazi za insulini hivyo kuwa kinga na kuleta ahueni kubwa kwa watu wenye kisukari.

K**a unasumbuliwa na kisukari fanya mazoea ya kutafuna mbegu za maboga kila siku na unipe mrejesho hapa.

5. DAWA BORA YA USINGIZI

Mbegu hizi zimegundulika pia kuwa na kirutubisho kinachozalisha homoni za usingizi. Kwenye mbegu za maboga kuna vimeng’enya viwili mhimu zaidi ambavyo huhusika na usingizi na afya ya akili moja kwa moja navyo ni ‘L-tryptophan’ na ‘tryptophan’.

Gramu 100 tu za mbegu za maboga zina kiasi cha kutosha cha ‘tryptophan’ mpaka mg 576. Tryptophan ndiyo inahusika kuleta usingizi wenye utulivu pia huondoa msongo wa mawazo au stress mwilini.

Kwa kuongezea mbegu za maboga zina kiasi kingi cha vitamini za kundi B. Muda mchache kabla ya kwenda kulala tafuna mbegu za maboga na utapata usingizi mtulivu kabisa mpaka asubuhi.

Kwahiyo k**a una tatizo la kukosa usingizi jaribu kutumia mbegu za maboga na uniletee majibu hapa. Kumbuka kukosa usingizi mara nyingi huwa ni matokeo ya msongo wa mawazo na k**a ulivyoona mbegu hizi zinaondoa pia stress! Kazi ni kwako ndugu.

6. DAWA BORA YA UVIMBE

Mbegu za maboga zinao uwezo mkubwa wa kuondoa sumu mwilini sambamba na uvimbe (inflammation).

K**a ujuavyo sehemu kubwa ya vivimbe mwilini ni matokeo ya sumu kadhaa mwilini. Mbegu za maboga zitakuondolea uvimbe mwilini bila kukuachia madhara yoyote mabaya hapo baadaye.

K**a unasumbuliwa na uvimbe popote jaribu kutumia mbegu za maboga na utuletee majibu.

Mbegu za maboga pia ni dawa nzuri kwa aina nyingi za kansa mwilini.

7. HUONGEZA MAZIWA KWA MAMA ANAYENYONYESHA

Mbegu za maboga zina protini nyingi bora itokanayo na mimea isiyo na madhara k**a ile ya kwenye wanyama. Pia zina OMEGA 3. Mama mjamzito hata unayenyonyesha tumia mbegu za maboga na utakuwa na uhakika wa kutoa maziwa ya kutosha kwa ajili ya mtoto.

8. DAWA NZURI KWA MATATIZO YA TEZI DUME

Wataalamu wengi wa lishe wanapendekeza mbegu za maboga zitumike kwa wanaume wa rika zote yaani vijana hadi wazee kwani zimethibitika kuwa msaada mkubwa kwa afya ya tezi dume.

Tafiti nyingi zinasema mbegu za maboga zina kiasi kingi cha madini ya Zinki madini ambayo ni mhimu SANA kwa afya ya tezi dume na husaidia uponyaji wa tatizo la tezi dume moja kuwa kubwa kuliko nyingine tatizo lijukanalo kwa kitaalamu k**a ‘benign prostatic hyperplasia’.

Wanaume kazi ni kwenu.

9. ZINAONGEZA NGUVU ZA KIUME

Maajabu mengine ya mbegu za maboga ambayo ulikuwa huyajuwi bado.

Utaniuliza kivipi zinaondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume? Kwanza kabisa zinaondoa msongo wa mawazo kitu ambacho ni namba 1 katika kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.

Lakini pia zinashusha lehemu (cholesterol), zinatibu kisukari, zinatibu tezi dume (matatizo k**a ya ngiri nk), zinashusha kisukari, zina protini nyingi ya kutosha na yenye ubora na mbaya zaidi ni kuwa zina madini ya ZINKI madini mhimu kuliko kitu kingine chochote kwenye upande wa nguvu za kiume na kinga ya mwili.

Bado huelewi? Zina madini ya chuma pia

Uzuri ni kuwa mbegu hizi hazina uchungu wowote, ni tamu kuzitafuna wakati wowote na mahali popote hata ukiwa ofisini unaweza kuwa nazo pembeni unatafuna huku unaendelea na kazi zako.

Sambamba na hilo k**a tulivyoona pale juu kwamba zinaongeza maziwa kwa mama anayenyonyesha kwa upande wa wanaume zinaongeza pia uwingi wa mbegu za kiume (s***m count) ukitafuna mbegu za maboga siku mbili tu utaona ukimwaga bao linatoka la kutosha na zito kweli kweli basi ujuwe ni mbegu za maboga hizo.

10. ZINAONDOA PIA MSONGO WA MAWAZO (STRESS)

Msongo wa mawazo au stress k**a mlivyozoea wengi ni tatizo linaloendelea kuwasumbua watu wengi miaka ya sasa. Mbaya zaidi wengi huwa hawaelewi nini madhara ya msongo wa mawazo kiafya.

Yaani stress au msongo wa mawazo unaweza kukuletea magonjwa mengine mwilini zaidi ya 50, hivyo utaona ni jinsi gani ilivyo mhimu kwako kuweka chini stress zako na uendelee na maisha kwani kuendelea kuwa na stress ni hatari zaidi kwa afya yako.

Moja ya sababu kuu ya watu wengi kuwa na stress ni usawa usio sawa wa homoni zao (hormonal imbalance).

Hivyo k**a una tatizo la homoni kwenye mwili hebu weka mazoea ya kutafuna mbegu za maboga kila siku na hutakawia kuona tofauti. Mbegu za maboga zina kimeng’enya mhimu sana kwa kutuliza mawazo kiitwacho ‘tryptophan’ na asidi amino zingine mhimu zinazohusika kutengenezwa kwa homoni nyingine ijulikanayo k**a ‘serotonin’.

K**a ulikuwa hujuwi ni kuwa serotonin ni homoni inayohusika na kazi mhimu sana ya kurekebisha matendo ya kitabia na kutoa matokeo chanya kwa mambo yanayohusu usingizi, hali ya mawazo kwa ujumla na mambo yanayohusu njaa.

11. Huzuia mchanga kwenye kibofu cha mkojo

Faida nyingine ya kushangaza kuhusu mbegu za maboga kiafya ni ule uwezo wake wa kuzuia mchanga au mawe kwenye kibofu cha mkojo.

Kinachofanya hili liwezekane kupitia mbegu hizi ni kule kuwa na kiasi kingi cha ‘phosphorous’ ambayo ni msaada mkubwa katika kuzuia mawe au mchanga kujilundika katika kibofu cha mkojo.

Pia unashauriwa kuwa unakunywa maji mengi kila siku ikiwa unasumbuliwa na tatizo hili.

12. Huimarisha afya ya mifupa

Kadri umri unavyoongezeka ndivyo na uwezo na uimara wa mifupa yako unavyopungua. Imefahamika sasa kuwa madini ya kalsiamu peke yake siyo kitu kinachoimarisha afya ya mifupa.

Kuna madini na vitamini vyngine mhimu ili kuimarisha afya ya mifupa. Mbegu za maboga ni chanzo kizuri sana cha magnesiamu, Zinki, Vitamini K na viinilishe vingine vingi mhimu katika kuimarisha mifupa na hivyo kuzuia ugonjwa wa mifupa (osteoporosis).

13. Zinasaidia kuweka sawa shinikizo la juu la damu

Shinikizo la juu la damu ni moja magonjwa sababishi ya vifo kwa watu wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo. Mbegu za maboga ni kitu mhimu kuongezwa katika mlo kwa watu wote wanaosumbuliwa na shinikizo la juu la damu.

Mbegu za maboga zina kiasi kidogo cha sodiamu na zina kiasi kingi cha potasiamu na magnesiamu vitu viwili mhimu katika kuweka sawa shinikizo la damu mwilini.

14. Zinaimarisha afya ya ubongo

Kadri unavyoendelea kukua ndivyo na uwezo wa ubongo wako unavyopungua. Hata hivyo bado unayo nafasi ya kuzuia hilo k**a utaishi na kula vizuri.

Mbegu za maboga asidi mafuta ya Omega 3 zijulikanazo kwa kitaalamu k**a ‘alpha-linolenic acid’ ambazo ni mhimu sana katika kulinda na kustawisha afya ya ubongo.

Vyakula vyenye Omega-3 husaidia kupunguza kasi ya seli za ubongo kuzeeka wakati huo huo vikizuia uharibifu wa seli za ubongo kutokana na vijidudu nyemelezi katika ubongo.

15. Zinaweka sawa Ph ya mwili

Mwili unaweza kuwa katika hali mbili, ama katika asidi au katika alkaline (Ph). Mwili unapokuwa na asidi nyingi ndipo unapopatwa na magonjwa mengi kirahisi zaidi. Magonjwa hayo ni pamoja na maumivu ya mifupa, saratani, kisukari, vidonda vya tumbo, kichwa kuuma nk

Hivyo ni mhimu chakula chako kiwe kwa sehemu kubwa ni chakula chenye alkalini na si asidi (tindikali) ili kukusaidia ubaki na Ph (Potential Hydrogen) ya 7.4 mara nyingi. Kumbuka chochote chini ya 7 Ph ni asidi.

Mbegu za maboga ni moja ya vyakula vizuri zaidi vyenye alkalini ambavyo unatakiwa kuvijumuisha kwenye mlo wako.

16. Zinatibu tatizo la upungufu wa damu

Mbegu za maboga ni chanzo kizuri cha madini ya chuma hivyo kuwa msaada kwa watu wanaosumbuliwa na upungufu wa damu unaosababishwa na kupungua kwa madini ya chuma.

Tafiti zinasema kula vyakula vyenye madini ya chuma kila mara kunasaidia kuongeza madini ya chuma kwa watoto, vijana, wanawake wanaonyenyesha na kwa wamama wajawazito. Hili linazifanya mbegu hizi kuwa msaada mkubwa kwa wale wanaopata tatizo la upungufu wa damu unaotokana na kupungua kwa madini ya chuma mwilini.

17. Zinasaidia kupunguza uzito wa mwili

Weka pembeni vyakula vyenye sukari nyingi na badala yake tafuna mbegu za maboga. Kinachotokea hapa ni kuwa mbegu hizi zinao uwezo wa kukuacha ukijisikia umeshiba kwa kipindi kirefu na hivyo kukuondolea hamu ya kutaka kula vyakula vingine feki.

Nyuzi nyuzi nyingi katika mbegu hizi zinazifanya kuwa chakula kizuri kuongezwa kwenye chakula chako cha asubuhi.

Hata hivyo sababu zina protini nyingi iwapo utazidisha kula unaweza kuongezeka uzito na unene badala ya kupungua hivyo uwe makini.

18. Zinarahisisha uponyaji wa vidonda

Mbegu za maboga pia ni msaada mkubwa kwa watu wenye vidonda kwa kuwa zinafanya kazi ya kuponya vidonda kuwa rahisi zaidi sababu zina vitamini A na madini ya zinki kwa wingi.

Kiais kingi cha vitamini A kwenye mbegu za maboga kinaweza kuwa msaada kuhamasisha uponyaji wa vidonda kwa mjibu utafiti mmoja uliofanywa na jarida moja la chuo cha afya ya ngozi nchini Marekani ‘Journal of the American Academy of Dermatology’.

Kwa mjibu wa utafiti, vitamini A ndani ya mwili inaweza kuvutia mfumo wa mwili kujiripea wenyewe ndani kwa ndani bila kuhitaji dawa.

K**a unasumbuliwa na vidonda au kidonda kwa muda mrefu hebu weka mazoea ya kutumia mbegu za maboga mara kwa mara na hutachelewa kuona uponyaji ukifanyika. Hii ni kweli ukizingatia pia mbegu hizi zinaongeza sana kinga ya mwili.

Mbegu za maboga ni msaada mkubwa kwa kina mama waliofikia ukomo wa siku zao na huondoa matatizo ya kiafya yatokanayo na kukoma kwa hedhi. Ni msaada kwa watu wenye saratani mbalimbali, huimarisha ukuaji na ustawi wa mifupa na meno, huondoa harufu mbaya ya kinywa na husaidia pia wenye tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu kila mara.

Namna nzuri ya kula mbegu za maboga:

Unaweza kula zikiwa kavu na ndiyo utapata faida nyingi zaidi ingawa mimi napenda kuzikaanga kidogo k**a dakika 5 hivi na huwa nazichanganya na chumvi ya mawe ya baharini kidogo kwa mbali ili kupata radha.

Unahitaji ujazo wa kiganja kimoja cha mkono wako cha mbegu za maboga kwa siku ujazo wa k**a nusu kikombe cha chai hivi kwa siku.

Unaweza pia kuzisaga na mashine maalumu au kuzitwanga katika kinu na utapata unga wake na utumie vijiko vikubwa viwili kutwa mara 1 kwenye kikombe kimoja cha juisi ya matunda uliyotengeneza mwenyewe nyumbani au katika uji.

Unaweza pia kuchanganya kwenye unga wa lishe wa mtoto

K**a unahitaji mbegu za maboga zilizokaangwa tayari kwa matumizi Niachie tu ujumbe WhatsApp 0714800175 na naweza pia kukuletea ulipo kwa Dar, natuma pia mikoani.

JITIBU MAGONJWA 300 KWA KUTUMIA MLONGEMlonge au Moringa oleifera kwa Kiingereza umekuwa ukijulikana k**a mti wa miujiza ...
02/06/2026

JITIBU MAGONJWA 300 KWA KUTUMIA MLONGE

Mlonge au Moringa oleifera kwa Kiingereza umekuwa ukijulikana k**a mti wa miujiza kwa karne nyingi katika baadhi ya nchi za Afrika, Asia na katika nchi za Caribbean.

Mti huu umeripotiwa kutibu zaidi ya magonjwa 300 yakiwemo magonjwa mbalimbali sugu.

Karibu kila sehemu ya mti huu hutumika k**a dawa au tiba lishe.

Majani ya mlonge yanaweza kutafunwa
mabichi, yaliyochemshwa k**a mboga au kuchanganywa na mboga nyingine yoyote ya majani, Unaweza kupikia mlenda au yaliyokaushwa na kusagwa kuwa unga.

Unga wa majani ya mlonge unaweza kuhifadhiwa kwa miezi kadhaa bila kupoteza ubora na faida zake za kiafya.

Mbegu za mlonge zimekuwa dili kubwa duniani kwa sasa, zinahitajika kwa kiasi kikubwa katika nchi ya Marekani na China.

Faida za mlonge zimeandikwa na majarida ya afya na lishe kadhaa duniani.

Zaidi ya tafiti 1500 za kisayansi zimefanywa kuhusu mlonge na zote zimehitimisha mlonge ni kitu cha ajabu na zawadi ya pekee ya Mungu kwa binadamu na wanyama.

Kile ulikuwa hujuwi ni kuwa viwanda na makampuni mengi ya dawa za hospitalini yamekuwa yakitumia virutubishi vilivyomo kwenye mti huu kutengenezea madawa kwa ajili ya binadamu na wanyama.

MLONGE UNA:

*Kalsiamu nyingi mara 17 zaidi ya ile ya maziwa ya ng’ombe
*Una Potasiamu mara 15 zaidi ya ile ya kwenye ndizi
*Una vitamini A mara 10 zaidi ya ile ya kwenye karoti
*Una protini nyingi mara 9 zaidi ya ile ya kwenye mtindi (Yogurt)
*Una Klorofili (kemikali ya rangi ya kijani
ipatikanayo katika mimea) mara 4 zaidi ya ile ya kwenye nyasi au majani
*Una madini chuma (iron) mara 25 zaidi ya yale ya kwenye Spinach
*Una vitamini A mpaka Z,
*Una Omega 3, 6, na 9 kwa pamoja
*Una asidi amino zile mhimu zaidi zinazohitajika na mwili
*Una kiasi cha kutosha cha madini ya Zinc ambayo ni madini mhimu katika kuongeza homoni za kiume na nguvu za kiume kwa ujumla.

MLONGE NDIYO MTI WENYE AFYA ZAIDI KULIKO MTI MWINGINE WOWOTE JUU YA ARDHI;

Mlonge una jumla ya virutubishi 92, mmea au mti mwingine wenye virutubishi vingi baada ya mlonge una virutubishi 28.

Mlonge una viondoa sumu 46 (ukitaka nikutumie majina ya hivi viondoa sumu vilivyomo kwenye mlonge kimoja baada ya kingine mpaka vyote 46 naweza).

Mlonge una viondoa uvimbe mbalimbali mwilini 36, una asidi amino 18 na asidi amino mhimu zaidi 9 ambazo miili yetu haina uwezo wa kuzitengeneza.

Majani fresh ya mlonge yana vitamini C mara 7 zaidi ya ile ya kwenye chungwa.

Unga wa majani ya mlonge unao uwezo wa kutibu magonjwa zaidi ya 300 mwilini, baadhi ya magonjwa hayo kwa kifupi ni pamoja na;

1. Huko Afrika magharibi madaktari hutumia mlonge kutibu Kisukari
2. Huko India mlonge hutumika kutibu shinikizo la juu la damu
3. Hutibu matatizo au maumivu ya mishipa
4. Hutuliza mapigo ya juu ya moyo (stroke),
5. Hutibu Kansa
6. Hutibu Pumu
7. Hutuliza wasiwasi
8. Kikohozi
9. Maumivu ya kichwa
10. Unazuia na kushusha lehemu (cholesterol) hata ile ya juu zaidi (hypocholesteremia)
11. Unapunguza mafuta tumboni
12. Unaweka sawa homoni
13. Unatibu maumivu wakati wa hedhi
(dysmenorrhea),
14. Unasafisha ini (hepatic detoxification)
15. Unasafisha mkojo na kibofu cha mkojo
16. Unarekebisha matatizo kwenye tezi
17. Unatibu kipindupindu na kuharisha
18. Kifua kikuu
19. Kichwa kizito
20. Huondoa uchovu
21. Unatibu mzio (aleji)
22. Hutibu vidonda vya tumbo
23. Maambukizi kwenye ngozi
24. Huondoa maumivu mbalimbali mwilini
25. Huondoa madoa doa meusi kwenye ngozi (blackheads),
26. Husafisha damu,
27. Hutibu matatizo kwenye koo
28. Huondoa makohozi mazito kooni
29. Huondoa taka na msongamano kifuani
30. Hutibu kipindupindu
31. Huondoa mtoto wa jicho au uvimbe kwenye jicho
32. Hutibu maambukizi kwenye macho na kwenye masikio
33. Unatibu homa
34. Huondoa maumivu kwenye maungio
35. Huondoa chunusi
36. Hutibu matatizo karibu yote ya ngozi na kinga ya mwili
37. Matatizo kwenye mfumo wa upumuwaji
38. Inatibu Kiseyeye (scurvy)
39. Huongeza wingi wa mbegu za kiume na nguvu kwa ujumla
40. Unatibu minyoo
41. Huongeza maziwa kwa wingi kwa mama anayenyonyesha
42. Huondoa uvimbe kwenye utumbo mpana (colitis)
43. Unatibu gauti (dropsy),
44. Unatibu kuhara damu (dysentery)
45. Unatibu kisonono ( gonorrhoea)
46. Unatibu tatizo la kukosa usingizi,
47. Unatibu homa ya manjano (jaundice),
48. Unatibu malaria
49. Unatibu U.T.I na matatizo mengine kwenye mfumo wa mkojo
50. Unasidia pia kujenga na kuimarisha misuli
51. Unatibu magonjwa ya mifupa

Mlonge unasafisha mwili wako wote, unasafisha ini, figo, moyo, macho, unaimarisha meno, ngozi na nywele.

Wakati unatumia mlonge unakufanya
ujisikie vizuri, ujisikie mpya (fresh) na mwenye nguvu.

Watu wengi wanaotumia mlonge huwa ni wenye afya nzuri hata kwa muonekano tu hata wanapokuwa na umri mkubwa zaidi ya miaka 90.

Majani ya mti wa mlonge pia yanaweza kutumika kutengeneza biogas (aina ya nishati ya umeme inayotokana na kinyesi cha ng’ombe au
takataka).

Hutumika pia k**a chakula cha wanyama k**a sungura, mbuzi, kuku, samaki, ng’ombe, mbwa nk. Sungura wanaonekana kupenda zaidi mlonge kuliko wanyama wote.

MBEGU ZA MLONGE:

1. Mbegu zake hutumika k**a kiuaji sumu na pia hutibu uvimbe.

Hutibu maumivu ya kwenye mishipa, baridi yabisi, gauti, kuk**aa mishipa,
magonjwa ya ngono na majipu.

2. Mbegu za mlonge husaidia watu wanaoshindwa kuzalisha mkojo.

3. Mbegu za mlonge hutumika pia kumtuliza au kumfanya mtu mwenye kifafa atulie na kurudi kwenye hali yake ya kawaida.

4. Mbegu za mti wa Mlonge ni kinga dhidi ya vijidudu (bacteria) wasababishao magonjwa na kuathiri ngozi ikiwemo fangasi.

5. Pia mbegu hutumika katika kusafisha au kuchuja maji ambapo zikipondwa na kuwekwa kwenye maji yenye tope au machafu husababisha uchafu kujikusanya na kuzama chini kisha
kuacha maji yakiwa safi na salama kwa kupikia au kunywa bila kuhitaji kuyachemsha.

6. Mbegu za mlonge pia huongeza kwa kiasi kingi kinga ya mwili (CD4), K**a una tatizo la kinga ya mwili wako kushuka basi tumia mbegu za mlonge kwa mwezi mmoja mpaka mitatu na kinga yako itaimarika sana.

MLONGE UNATOA WAPI MAAJABU YOTE HAYA?

Matatizo mengi ya kiafya ni matokeo ya lishe yenye viinilishe duni au hafifu jambo linalopelekea kuwa na kinga ya mwili isiyo na nguvu kupigana na magonjwa mbalimbali.

Unaporekebisha usawa huo usio sawa wa kinga yako ya mwili kwa kutumia mlonge hutakawia kuona matokeo mazuri kwenye afya yako.

Uwezo wa mti wa mlonge kuyaweza yote hayo ni kutokana na kuwa na vitamini, madini mbalimbali na viondowaji sumu vingi kuliko mti mwingine wowote.

Wagonjwa wengi wenye UKIMWI katika
sehemu nyingi za afrika magharibi wameripoti kuongezeka kiasi kikubwa cha kinga yao ya mwili baada ya kutumia mlonge kiasi cha kutokuhitaji
dawa nyingine yoyote zaidi.

NGUVU, UMAKINI, NGOZI YENYE KUPENDEZA, KUTOZEEKA MAPEMA NA KUPUNGUZA UZITO NA UNENE:

Mlonge una viinilishe mhimu vinavyosaidia kuuongezea uwezo mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.

Vitamini, madini na homoni mhimu
zilizomo kwenye mti huu huufanya mwili wako kuwa na usawa unaohitajika kiafya na hivyo kukupa kinga dhidi ya magonjwa mengi bila idadi.

Mlonge una kiinilishe mhimu sana kwa wingi kuliko mmea au mti mwingine wowote duniani mara maelfu kadhaa kiitwacho kwa kitaalamu k**a ‘Zeatin’.

Zeatin ndiyo hutengeneza Seli mpya za ngozi pia huzifanya seli mpya kutengenezwa kwa haraka na kwa wingi zaidi ya zile seli zinazokufa.

Hii huleta matokeo mazuri ikiwemo kuondoa mikunjo ya ngozi au ngozi
kuzeeka sehemu za uso na sehemu nyingine za mwili na kukupa afya nzuri ya ngozi.

Kwenye mlonge kuna ‘Sulfur’, hii sulfur ni mhimu katika kuunda vitu mhimu kwenye ngozi k**a collagen na keratin huku viuaji au viondowaji sumu zaidi ya 46 vinavyopatikana kwenye mlonge ni mhimu kwa ajili ya afya ya ngozi yako.

Mlonge ambao umekuwa ukitumika kwenye vituo vingi vinavyojihusisha na kupunguza uzito huwa una nguvu ya asili ya kupunguza njaa, huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na kukung’arisha wewe huku ukikuacha na virutubishi vingi mhimu zaidi.

MLONGE HUIRUDISHA UPYA AFYA YA MWILI WAKO;

Baada ya kufikisha umri wa miaka 30 hivi NGUVU zako za mwili HUANZA kushuka.

Mwili wako utaanza kuleta mchonyoto.

Utaona unaanza kupoteza umakini nyakati za mchana sababu hukuzingatia nini ule wakati ulipokuwa kijana.

Baadhi ya kuharibika kwa afya hakuwezi
kurudishwa nyuma ikiwa ni pamoja na kuzorota kwa afya ya meno.

AFYA MBOVU YA MENO INAPELEKEA MAGONJWA KADHAA NA VIFO;

Calcium, Magnesium, Manganese, Potassium, Boron na Vitamini D yote ni madini mhimu ili uwe na meno yenye afya.

Magonjwa mengi sugu ni matokeo ya upasuaji wa kwenye kinywa.

Kila mtu anapaswa kulinda afya ya meno yake kuanzia leo kwani meno yakishaoza au kuharibika huwa ni vigumu kupona na kurudi kwenye hali yake ya mwanzo.

Afya ya meno yako itaamua ni miaka mingapi unaweza kuishi.

Kila mmoja wetu anatakiwa kutimiza wajibu wake linapokuja suala la afya ya mwili wako.

Tumia google tafuta taarifa za kile unachokula au kunywa kila siku.

Kichwa kitakuuma utakapojua ni nini unakula!.

Nenda YouTube angalia video hizi: “Food Matters” na “Dying to have know”.

Tafuta kwenye chaneli ya Discovery huko YouTube movie inaitwa “Moringa The Miracle Tree” na video nyingine inaitwa ‘Moringa Oleifera’.

BIDHAA NYINGI ZA AFYA HAZINA AFYA YOYOTE;

Bidhaa nyingi za afya hazina utafiti halisi
(genuine) unaojitegemea au zina maelezo kutoka kwa mtengenezaji tu wa hiyo bidhaa.

Mlonge una mfululizo wa tafiti za watu wengi na shuhuda za watu kote duniani zaidi ya miaka 4000 iliyopita.

Ni mtishamba kwa asilimia 100.

Matumizi ya mlonge k**a kiua vijasumu (antibiotic) kwenye tiba asili yalianza miaka maelefu iliyopita.

Mlonge ulitumika kwa mara ya kwanza k**a dawa zaidi ya miaka 2000 kabla ya Kristo.

Watabibu wa zamani wa Misri na Ugiriki waliona faida nyingi za mti huu na wakautambulisha kwa Warumi na baadaye mlonge ukaenea mashariki mwa India na sehemu ya chini ya nchi ya Uchina, kusini mashariki mwa Asia na Ufilipino na magharibi mwa Misri kuzunguka mediterania na mwishowe ukafika kwa Wahindi mashariki mwa Amerika.

Leo zaidi ya watu milioni 400 wanatumia mlonge. Shirika la afya duniani (W.H.O) limekuwa likitumia mlonge zaidi ya miaka 40 sasa.

Unga wa majani ya mlonge unapaswa uwe ni wa kijani kweli kweli na majani yake yawe yalianikwa kivulini na siyo juani.

Mti wa mlonge sasa umeanza kuwa maarufu huko Marekani hii ni kutokana na mti wenyewe kuendelea kupata umaarufu miongoni mwa watu wanaojali afya zao.

Ingia google andika ‘Moringa plants for sale’ utagundua keyword hiyo inatafutwa kila siku mara maelfu.

Mti wa mlonge ni moja ya miti mhimu katika sehemu yote ya dunia.

Kadri watu wanavyoendelea kuutafiti na kuusoma mti huu ndivyo mahitaji ya unga wa majani yake, mbegu zake, unga wa mbegu zake na mafuta ya mbegu
zake yatakavyozidi kuongezeka na kuongezeka.

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa tiba asili, nauza dawa za Asili, nipo Kibugumo Mji Mwema Kigamboni Dar Es Salaam.

Ikiwa unahitaji Unga wa Majani ya mlonge au mbegu za mlonge niachie ujumbe kwenye WhatsApp 0714800175

Angalizo, Vigezo & Masharti :

1. Siyo kila mti wa mlonge ni dawa, kuna aina tofauti tofauti za mlonge 13 na ni mlonge mmoja tu ujulikanao k**a moringa oleifera ndiyo pekee hutumika k**a dawa.
2. Mlonge lazima uanikwe ndani kivulini kwa siku 7 au zaidi siyo kwenye jua
3. Mlonge unaotarajiwa kutumiwa k**a dawa huchumwa asubuhi mapema siyo mchana au jioni na Tabibu au mtaalamu wa tiba asili hunena maneno maalum na kutoa sadaka kabla ya kuanza kukata mti. Kila kitu kina taratibu zake na watu wake.
4. Lazima mlonge huo hasa Unga wa Majani yake uwe ni wa kijani kweli kweli ndipo hufaa k**a dawa.
5. Usitumie mlonge bila ushauri au uangalizi wa karibu wa daktari wako hasa k**a umekuwa ukisumbuliwa na ugonjwa fulani na unatumia dawa za hospitali kwa kipindi kirefu. Pia usiache kutumia dawa yoyote ya hospitali ambayo umekuwa ukiitumia bila kushauriana na daktari wako.
6. Sihusiki na hali yoyote inayoweza kukutokea wakati unatumia mlonge ikiwa hukununua kwangu huo mlonge.
7. Siwajibiki kukupa maelezo juu ya namna ya kutumia mlonge ikiwa BADO hujanunua kwangu huo mlonge.

Tafadhali share post hii kwa ajili ya wengine uwapendao.

Like au follow ukurasa huu ili kuendelea kupata dondoo na elimu mbalimbali kuhusu kwa tiba asili.

Sababu kuu 4 kwanini huponi tatizo lako la upungufu wa nguvu za kiume1. Unasubiri upone ndipo uendelee kushiriki tendo l...
27/05/2026

Sababu kuu 4 kwanini huponi tatizo lako la upungufu wa nguvu za kiume

1. Unasubiri upone ndipo uendelee kushiriki tendo la ndoa

Moja ya kosa kubwa unalolifanya linalokusababishia usipone tatizo lako la upungufu wa nguvu za kiume ni kusubiri upone ndipo uendelee na tendo la ndoa.

Ni kosa kusubiri upone hali yako ya kuwahi sana kufika kileleni kila mara, hali yako ya uume kuwa mlegevu au uume uliosinyaa sababu ya punyeto ndipo uje ushiriki tendo la ndoa.

Unaweza kujiuliza kwanini ni kosa kusubiri kupona lakini jibu lake ni jepesi tu kwamba tendo la ndoa lenyewe ni sehemu ya matibabu ya tatizo lako.

K**a una tatizo la kuwahi sana kufika kileleni na unatumia dawa kisha unasubiri umalize dawa ndipo uendelee na tendo la ndoa basi unaweza usipone kabisa.

Unatakiwa uendelee kutumia dawa kwa uaminifu wote wakati huo huo unaendelea kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara.

Kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara ni dawa pia ya tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Mhimu hapa ni kuwa na kiasi kwa sababu ukizidisha sana kushiriki tendo la ndoa nayo hiyo tabia inaweza kukuletea upungufu wa nguvu za kiume!

Walau mara 2 au 3 kwa wiki ni sawa, lakini usikae wiki 3 au mwezi mmoja bila kushiriki tendo la ndoa.

Kinachowafanya wanaume wengi wasubiri wapone ndipo washiriki tendo la ndoa ni aibu ya kuonekana si lolote mbele ya mwanamke sababu tu amewahi kufika kileleni na hawezi kurudia tena.

Unalotakiwa kufahamu ni kuwa ni bora upate hiyo aibu sasa na baadaye ufurahie maisha yako ya ndoa kuliko uipe aibu nafasi kubwa na uishi na tatizo milele.

Vile vile tambua wanawake wengi hawapo vile k**a ambavyo tunadhani wapo, Ukiwa mkweli na muungwana atakuelewa tu bila shida yoyote.

Unaweza kumwambia kabisa mapema kwamba ni kweli nimetaka kushiriki tendo la ndoa na wewe lakini mwenzio nisikudanganye nina tatizo la kuwahi sana kufika kileleni, nina tatizo la kuwa na uume mlegevu na kadharika kwa hiyo usinishangae wala usishtuke!

Mwambie tu usiogope.

Mwambie lakini upo bize na matibabu na unaamini tatizo litaisha siku za hivi karibuni.

Mwanamke ukimwambia hivyo mapema atakuona una akili na unajali na pengine anaweza kukuambia ufanye nini ili na yeye afike kileleni bila kutumia uume wako.

Kwahiyo endelea kutumia dawa wakati huo huo endelea kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara hata k**a hupati matokeo mazuri kwa wakati uliopo.

Ukifanya hivi kupona tatizo la upungufu wa nguvu za kiume ni uhakika.

Ukiwa mwanaume usiwe muoga, kuwa jasiri ndiyo sifa kuu ya mwanaume.

Na k**a unaona kufanya hivyo na mke wako au na mke wako mtarajiwa ni jambo la aibu sana basi jaribu mechi za kirafiki huko nje huku ukiweka tahadhari kubwa usije kuambukizwa magonjwa ya zinaa na utakapoona umepona utarudi kuendelea na maisha yako na mkeo au na mke wako mtarajiwa (mchumba).

Usijiwekee wewe mwenyewe au hata Mungu mipaka sana, maisha ni mafupi na ni haya haya.

Fanya lolote hata k**a siyo la kawaida sana machoni pa wengi lakini kichwani kwako umejiwekea lengo kwamba unafanya hayo ili upone uume wako na ukipona utatubu kwa Mungu dhambi zako na kuendelea na maisha yako.

Mungu wetu ni Mungu wa neema na rehema, hatoi hukumu kwa jinsi ya kibinadamu na mara zote kabla ya kukuhukumu kwanza anatanguliza rehema.

Kwa sehemu kubwa tunaokolewa kwa neema na rehema na siyo kwa matendo yetu kwa asilimia 100.

Umeamka mzima leo siyo kwa sababu huna dhambi au wewe ni mtakatifu au kuna jambo lolote ulifanya jana kwa Mungu ndiyo akaona uamke na leo mzima!

Kuna watakatifu wengi tu wamefariki jana ila kwa neema zake tu amekupendelea wewe kuwa hai mpaka leo

Unaweza kulala pia na mwanamke kwa usiku mmoja au dakika kadhaa tu bila kulazimika muwe wapenzi na ukatafuta mwingine tena siku nyingine mpaka umepona.

Mapenzi hayo ya siku 1 au ya dakika kadhaa wazungu huyaita “one night stand”.

Sitapenda kuongea sana lakini na wewe mwenyewe jiongeze na k**a unahitaji msaada wa kimawazo zaidi tafuta muda tuonane mimi napatikana Kibugumo Mji Mwema Kigamboni Dar Es Salaam.

2. Unategemea nguvu za mwili peke yake

Nguvu za kiume bado ni msamiati kwa watu wengi.

Wengi hawajuwi nguvu za kiume ni nini hasa.

Wengi unapozungumzia nguvu za kiume akili yao yote inawaza uume!

Uume umeundwa kwa nyama na mishipa ya damu, hakuna mfupa wowote kwenye uume.

Nguvu za kiume hazina uhusiano wa moja kwa moja na uume wako.

Nguvu za kiume ni nguvu za mwili wako wote zikijumuisha nguvu za akili pia.

Sasa kuna wanaume mpo bize na kujenga nguvu za mwili yaani kujenga misuli na muonekano wa nje wa mwili kwa ujumla huku mkisahau kutengeneza pia nguvu za ndani ya mwili (nguvu za akili, nguvu za ubongo, utulivu wa nafsi, usingizi).

Kwahiyo kuwa bize na mazoezi peke yake, kuwa bize na vyakula peke yake bila kuwa bize na afya ya akili yako pia kutaendelea kukuzuia usipone kabisa tatizo lako la upungufu wa nguvu za kiume.

Ninaposema nguvu za akili simaanishi kuwa na akili nyingi darasani au shuleni, hapana, sizungumzii akili za namna hiyo.

Bali ninaposema afya ya akili hapa namaanisha utulivu wa nafsi yako kwa ujumla.

Una amani ya kiasi gani?

Ndiyo nguvu ya akili ninayomaanisha.

K**a huna utulivu wa nafsi basi kunyanyua kwako vyuma, kwenda mazoezini kila siku na kula vizuri hakutasaidia upone tatizo lako la upungufu wa nguvu za kiume.

Unatakiwa uwe na akili iliyotulia na amani nyingi kwenye maisha yako.

K**a una madeni sugu kila kona, watoto hawana ada ya shule, unadaiwa kodi ya nyumba, chakula chenyewe kinapatikana kwa shida, una mawazo mawazo (stress) kila siku, hupati usingizi mzuri na wa kutosha kila siku basi ni vigumu sana wewe kupona tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Kwahiyo huponi tatizo lako la upungufu wa nguvu za kiume kwa sababu upo bize na nguvu za mwili bila kufanya lolote kuhakikisha akili yako pia ina nguvu za kutosha.

Ni mhimu kuwa na maisha ya kawaida na ya kuridhika, ila k**a una tamaa ya kuishi maisha ya kitajiri sana na uwezo huo huna basi utaendelea kudhuru afya yako ya kitandani bila hata wewe mwenyewe kujua.

Kuwa mtu wa shukrani japo kwa kidogo ulichonacho tayari, kaa karibu na Mungu na ishi vizuri na watu wengine wote bila kujali ni maskini au matajiri.

3. Unadhani kuimarisha nguvu za kiume ni kazi ya siku moja

Hapa ndipo wanaume wengi sana wanapoferi.

Shida kubwa ya tatizo la upungufu wa nguvu za kiume inaanzia hapa.

Wanaume wengi hudhani upungufu wa nguvu za kiume ni jambo linaloweza kutibika kwa wiki 2, kwa kunywa dawa mwezi mmoja halafu umepona milele!

Poleni sana.

Hata malaria tu hakuna dawa ya kunywa mara 1 kisha umepona milele.

Huwa nakutana na wanaume wanaotafuta dawa ya asili kwa ajili ya kuimarisha nguvu za kiume na kutibu madhara yatokanayo na punyeto na wengi wao huuliza k**a dawa nitakayowapa itaenda kutibu tatizo lao na hawatahitaji tena dawa milele.

Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume haliishi kwa staili hiyo.

Ni jambo endelevu la kila siku maisha yako yote.

Kila siku ukiamka lazima ujue utaishi vipi siku hiyo ili kuendelea kuongeza na kuimarisha nguvu zako za kiume.

Ni sawa na kinga ya mwili.

Hata kuimarisha Kinga ya mwili siyo kazi ya siku 1 au ya dawa 1, ni maisha yako ya kila siku siku zote za uhai wako.

Unapotumia dawa ili kuondokana na tatizo lako la kuwahi sana kufika kileleni au kuwa na uume mlegevu haina maana ni jambo utakalolifanya mara 1 kisha umepona milele!

Hata baada ya kupona bado utahitaji dawa tena huko mbeleni baada ya miezi kadhaa au miaka kadhaa bado utatakiwa kutumia dawa tena ili kuendelea kujiimarisha.

Utatakiwa kuendelea kufanya mazoezi ya viungo mara kwa mara hata k**a huna tatizo lolote la upungufu wa nguvu za kiume, utatakiwa uendelee kula vizuri na kuwa na utulivu wa nafsi wakati wote ukiendelea kuishi.

Mhimu ni kuhakikisha unatumia dawa rafiki hasa za asili zisizo na madhara mengine kiafya hata k**a utatumia mara nyingi.

Kwahiyo moja ya sababu kwanini tatizo la upungufu wa nguvu za kiume haliishi kwako ni kudhani matibabu yake ni jambo la wakati mmoja kisha umepona milele!

Sababu kuu 4 kwanini huponi tatizo lako la upungufu wa nguvu za kiume

4. Umeweka imani yako yote kwenye dawa na hela unayotoa unaponunua dawa

Siyo jambo baya kuweka matumaini yako kwenye dawa, lakini siyo sawa kuweka imani yako yote kwenye dawa peke yake.

Hili ni kosa kubwa ambalo matabibu tunaliona siyo kwa upande wa nguvu za kiume tu bali karibu kwa magonjwa mengine yote.

Watanzania wengi wanaamini sana kwenye bidhaa kuliko kwenye ushauri na elimu.

Kwa nchi k**a Marekani au Ulaya ishu siyo dawa, ishu ni daktari au Tabibu uliyeamua kumtumia kukutibu tatizo lako.

Watu wengi wanatamani kupona na shida yao kubwa ni kupona tu.

Lakini kutegemea dawa peke yake na hela zako bila kuwa karibu na daktari ni kosa kubwa litakaloendelea kukugharimu miaka na miaka mpaka utakapobadilika.

Ndiyo maana mimi huwa napenda tuwasiliane kupitia WhatsApp na siyo kwa simu ya kawaida.

Kwanini?

Ni kwa sababu kwenye WhatsApp tunaweza kuendelea kuchat na kuchat, kuchat na kuchat kila siku na kila mara utakapokuwa na jambo lolote.

Kwenye WhatsApp pia naweza kukutumia hii makala yote unayosoma hapa na ukabaki nayo milele kwenye simu yako.

Siwezi kukutumia makala hii kwa njia ya simu au kwa sms ya kawaida!

Lakini wengi wanapenda kupiga simu na wapewe dawa haraka.

Katika hali tu ya kawaida huwezi kumpigia mtu simu mara 10 kwa siku, lakini unaweza kuchat na mtu WhatsApp hata mara 50 kwa siku.

Kwenye WhatsApp naweza kukutumia picha, naweza kukutumia video, lakini siwezi kufanya hivyo kwa simu ya kawaida au kwa sms ya kawaida.

Lakini sababu watu wanapenda vitu vya haraka haraka bila kuzingatia elimu na ushauri mwingine basi hawaponi na kupata suluhisho la kudumu kwa matatizo yao.

Kwahiyo k**a umekuwa ukijiuliza kwanini huponi tatizo lako la upungufu wa nguvu za kiume hata baada ya kunywa dawa kadhaa na kutumia hela nyingi ni kwa sababu umeweka imani yako yote kwenye dawa peke yake bila kuwa karibu na daktari anayekupa dawa.

Kuna mambo mengine mengi ambayo hayahusiani na dawa moja kwa moja na ni ya mhimu ili upone na mambo hayo utayapata tu kwa kuwa karibu na Tabibu aliyekupa hiyo dawa.

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba asili, nauza dawa za Asili, nipo Kibugumo Mji Mwema Kigamboni Dar Es Salaam.

Ikiwa unatafuta dawa ya asili kwa ajili ya kuimarisha nguvu za kiume na itakayokuondolea tatizo lako la kuwahi kufika kileleni pamoja na kutibu madhara yatokanayo na punyeto niachie ujumbe kwenye WhatsApp 0714 800 175

Like au follow ukurasa huu ili kuendelea kupata dondoo na elimu nyingine nyingi kuhusu nguvu za kiume na afya ya mwanaume kwa ujumla.

Tafadhali SHARE post hii kwa ajili ya wengine uwapendao.

*****

Address

Kibugumo Mji Mwema Kigamboni

Telephone

+255714800175

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tabibu Fadhili Paulo posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

  • Want your practice to be the top-listed Clinic?

Share