Dr.Amili

Dr.Amili NIULIZE KUHUSU AFYA KARIBU
WHATTASUP NO.+255719829890

FAHAMU UGONJWA WA PIDPelvic Inflammatory Disease ni maambukizi yanayotokea kwenye viungo vya uzazi vya mwanamke, k**a mf...
30/04/2026

FAHAMU UGONJWA WA PID

Pelvic Inflammatory Disease ni maambukizi yanayotokea kwenye viungo vya uzazi vya mwanamke, k**a mfuko wa uzazi, mirija ya uzazi, na ovari. Mara nyingi husababishwa na bakteria wanaotokana na magonjwa ya zinaa k**a Gonorrhea na Chlamydia.

DALILI ZA PID
Dalili zinaweza kuwa ndogo au kali, na ni pamoja na:
1. Maumivu chini ya tumbo
2. Maumivu ya nyonga au chini ya kitovu
3. Huwa makali zaidi wakati wa tendo la ndoa
Kutokwa na uchafu usio wa kawaida ukeni
4. Uchafu mwingi wenye harufu mbaya
Unaweza kuwa wa njano au kijani
5. Maumivu wakati wa kukojoa
Kuwaka au maumivu wakati wa kukojoa
6. Homa
Mwili kuwa na joto, kutetemeka, au baridi
7. Kutokwa damu isiyo ya kawaida
Damu kati ya hedhi au baada ya tendo la ndoa
8. Maumivu wakati wa tendo la ndoa
10. Maumivu ndani ya tumbo au nyonga
11. Kichefuchefu na kutapika
Hasa maambukizi yanapokuwa makali

MADHARA YA PID
Ikiwa PID haitatibiwa mapema, inaweza kusababisha madhara makubwa:
1. Ugumba
Maambukizi yanaweza kuharibu mirija ya uzazi na kufanya mwanamke ashindwe kupata mimba
2. Mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi
Mimba inaweza kujishikiza kwenye mirija ya uzazi, hali ambayo ni hatari sana
3. Maumivu ya muda mrefu ya nyonga
Maumivu yanaweza kuendelea hata baada ya maambukizi kuisha
4. Majipu kwenye mirija ya uzazi au ovari
Majipu yanaweza kusababisha maumivu makali na kuhitaji upasuaji
5. Maambukizi kuenea mwilini
Hii inaweza kuwa hatari kwa maisha ikiwa bakteria wataenea kwenye damu

MUHIMU KUFANYA
Ukiona dalili hizi:
Para ushauri WA kitaalamu mapema
Pima magonjwa ya zinaa
Tumia Tiba utakazo shauriwa
Epuka tendo la ndoa hadi utakapopona

WASILIANA NASI
KWA USHAURI NA TIBA
WHATSAPP AU PIGA
+255719829890





Address

Kimara Stopover
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Dr.Amili posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share

Category