AFYA.Ni.UREMBO

AFYA.Ni.UREMBO GUNDUA KUJITUNZA NA AFYA KUTOKA NDANI | FURAHIA SAFARI YAKO YA KIPEKEE YA AFYA | KUWEZESHA KUJIPENDA

AFYA YAKO. JE WAJUWA KUUSU BROKOLI?Brokoli ni mboga ya cruciferous inayohusiana na kabichi, kolifulawa na koliflower amb...
06/01/2024

AFYA YAKO. JE WAJUWA KUUSU BROKOLI?

Brokoli ni mboga ya cruciferous inayohusiana na kabichi, kolifulawa na koliflower ambayo hupata uwakilishi wake wenye afya kutokana na ukweli kwamba ina virutubisho vingi, ikiwa ni pamoja na vitamini C, A na K. Kwa hakika, kikombe cha nusu cha brokoli mbichi iliyokatwakatwa hutoa 43% ya thamani ya kila siku ya vitamini C.

Manufaa nyingine ya broccoli ni kwamba pia ina phytochemical sulforaphane, ambayo inaweza kusaidia kuzuia dhidi ya aina mbalimbali za saratani. Zaidi ya hayo, imejazwa vioksidishaji vingine vikali k**a vile lutein, beta-carotene na zeaxanthin, ambayo inaweza kupunguza hatari ya kuharibika kwa macular kuhusiana na umri na kusaidia afya ya macho kwa ujumla. Kula mbichi, kuchomwa au kuoka au kuchemshwa ili kupata faida kubwa zaidi za lishe.

Pendelea kuila walau mara 2 kwa mwezi, k**a unaweza kununua Kilo ya nyama kila siku na kula nyumbani basi haza leo kununua Kilo moja ya brokoli na kuanza kuijaza familia yako afya na sio magonjwa yajayo.

Like na toa maoni yako kuusu mboga hii.

Tikiti Maji Sio Tu Tunda La Kuburudisha Na Ladha Bali Pia Hutoa Faida Nyingi Kiafya.  Ni Chanzo Bora Cha Unyevu Kwa Saba...
17/11/2023

Tikiti Maji Sio Tu Tunda La Kuburudisha Na Ladha Bali Pia Hutoa Faida Nyingi Kiafya. Ni Chanzo Bora Cha Unyevu Kwa Sababu Ya Kiwango Chake Cha Juu Cha Maji, Usaidia Kudumisha Utendaji Mzuri Wa Mwili. Tunda Hili Lina Vitamini Nyingi, Ikiwa Ni Pamoja Na Vitamini C, Ambayo Inasaidia Mfumo Wa Kinga,Ngozi Na Pia Vitamini A, Ni Muhimu Kwa Afya Ya Macho Na Ngozi Pia.

Kwa Kuzingatia Madini, Tikiti Maji Ina Potasiamu, Ambayo Husaidia Kudhibiti Shinikizo La Damu, Na Magnesiamu Ni Muhimu Kwa Athari Mbalimbali Za Biochemical Katika Mwili. Zaidi Ya Hayo, Hutoa Kiasi Kidogo Cha Vitamini B K**a B1, B5, Na B6, Na Kuchangia Katika Kimetaboliki Ya Nishati.

Uwepo Wa Antioxidants K**a Lycopene Kwenye Tikiti Ni Muhimu, Kwani Zinaweza Kusaidia Kulinda Dhidi ya Mafadhaiko Ya Kioksidishaji Na Uchochezi. Lycopene Imehusishwa Na Faida Zinazowezekana Kwa Afya Ya Moyo Na Inaweza Pia Kuchukua Jukumu Katika Kuzuia Aina Fulani Za Saratani.

Ili Kufurahia Faida Za Tikiti, Ni Bora Kuliwa Likiwa Asili Sio Lililofungwa Viwandani Pata Likiwa Katika Hali Yake Ya Asili. Kuikata Na Kuchanganya Na Matunda Ya Aina Hata 4 Na Kula Pamoja. Ikiwa Na Pamoja Na Kuchanganya Katika Saladi Au Kuchanganya Katika Smoothies Ni Njia Za Ubunifu Za Kulitumia Tunda Hili La Lishe Katika Mlo Wako. Hata Hivyo, Kula Kiasi Ni Muhimu Kutokana Na Sukari Yake Ya Asili Na Pia Kumbukuka Usichanganye Na Matunda Mengi Yenye Sukari Ukala Kwa Pamoja Weka Tunda Moja Lenye Sukari Na Aina Nyingi Za Matunda.

Toa Maoni Yako Kwenye Comment Wewe Unafurahia Vipi Tunda La Tikiti Maji.

Changamoto Za Magonjwa Zimekuwa Nyingi Si Kwa Wakubwa Si Kwa Watoto. Tunaweza Kujiweka Mbali Kabisa Na Hatari Na Changam...
11/11/2023

Changamoto Za Magonjwa Zimekuwa Nyingi Si Kwa Wakubwa Si Kwa Watoto.

Tunaweza Kujiweka Mbali Kabisa Na Hatari Na Changamoto Zozote Za Magonjwa Kwa Kubadilisha Mfumo Wetu Wa Chakula Na Wa Kimaisha.

Walinde Na Tuwatunze Tuwapendao, Jilinde Na Ujiepushe Na Magonjwa.

Jiepushe Na Tabia Zitakazo Kupeleka Katika Hatari Za Magonjwa.

Mlo Kamili Ndio Chanzo Kikuu Cha Kuwa Na Afya Bora Na Kujiepushe Na Magonjwa.

Unaweza Kuungana Nasi Katika Group La "Safari Ya Mlo Kamili" ili uweze kujifunza Mengi Na Namna Gani Unaweza Kujiepushe Na Magonjwa Na Kuwa Mtu Mwenye Afya.

Tuma ujumbe "Safari Ya Mlo Kamili " kwa kubonyeza link kwenye bio na kuja WhatsApp ( 0699899039)

Ngozi kavu inaweza kuwa suala la kudumu na la kusumbua kwa watu wengi.  Mara nyingi husababisha usumbufu, udhaifu, Muone...
09/11/2023

Ngozi kavu inaweza kuwa suala la kudumu na la kusumbua kwa watu wengi. Mara nyingi husababisha usumbufu, udhaifu, Muonekano mbaya, mabaka na wakati mwingine hata kuwasha.
Ingawa kuna bidhaa nyingi kwenye soko zilizoundwa kupambana na ngozi kavu,

Lakini kuna mambo ya muimu ya kufata ili kusaidia kujiepushe na tatizo kwanzia ndani. mbinu moja ya kipekee na yenye ufanisi inazingatiwa ni kuanzia kwenye lishe bora na kile unacho kitumia kwenye ngozi.

matumizi ya mafuta ya mimea ni njia muimu ya pili katika swala zima la kutunza ngozi yako na ikiwa jambo la kwanza la muimu ni LISHE BORA.

Je ni changamoto gani sana unapitia kwenye swala zima la ngozi? Toa maoni(comment) yako na namna gani unapambana nayo.

Kupata elimu zaidi bonye link kwenye bio utajifunza mengi.

"Ngozi Yangu Haina Nuru, Ni Kavu Sana Nimejitaidi Kutumia Bidhaa Za Aina Mbalimbali Na Za Garama Lakini Sijapata Matokeo...
06/11/2023

"Ngozi Yangu Haina Nuru, Ni Kavu Sana Nimejitaidi Kutumia Bidhaa Za Aina Mbalimbali Na Za Garama Lakini Sijapata Matokeo Sahii. Sijui Nini Ni Fanye?"

Usiendele Kuwaza Tena Ni Namna Gani Ngozi Yako Itakufuraisha Na Itakuwa Na Muonekano Mzuri.

Tunakupa Sababu Ya Kupata Tabasamu Jipya Kwenye Urembo Wako Kwa Sababu Tunaanza Kutatua Changamoto Ndani Na Tunakuja Nje.

K**a Ujatatua Changamoto Kwanzia Ndani Uto Pata Matokeo Sahii Na Utajikuta Unabadili Vipodozi Mara Kwa Mara Bila Kupata Matokeo.

Lishe Ni Jawabu La Urembo Wako, Afya Zuri Ni Matokeo Ya Urembo Wako.
Lishe Bora Vipodozi Sahii.

Kwa Changamoto Zozote Za Ngozi, Nywele, Uzito Kudumaa Na Unataka Kuwa Na Muoneka Mzuri Wa Ngozi Yako Njoo WhatsApp tuma neno "Afya.ni.urembo"

WhatsApp:- 0699899039. Call:- 0788915913

Matatizo Na Changamoto zote za Afya zinatoka na Lishe mbovu ya Chakula tunachukula kila Siku na Vinywaji tunavyo weka ka...
19/10/2023

Matatizo Na Changamoto zote za Afya zinatoka na Lishe mbovu ya Chakula tunachukula kila Siku na Vinywaji tunavyo weka katika matumbo yetu.

Tunaweza kutokomesha matatizo ya magonjwa kwa mpangilio wa chakula.

Niambie Unachangamoto gani ya afya tuweze kukupa suluu kwa kupitia lishe na mpangilio wa chakula.

Bonyeza kwenye link.

Karibu katika ukurasa wetu wa AFYA.Ni.UREMBO.Tunashukuru kuwa mmoja wa jumuiya yetu na ya kujali Afya zetu.Katika safari...
16/10/2023

Karibu katika ukurasa wetu wa AFYA.Ni.UREMBO.
Tunashukuru kuwa mmoja wa jumuiya yetu na ya kujali Afya zetu.
Katika safari ya afya watu wengi tumeingia katika changamoto nyingi za kiafya kwa sababu ya mfumo mbovu wa chakula. Tunapoteza ndugu zetu kwa magonjwa ya KISUKARI, PRESSURE na nk kwa sababu ya nini tunachokula na tunachokula.
Tumekuwa na afya mbana na ngozi mbaya ni kwa sababu tumesahau kujali afya zetu kwanzia ndani ya miili yetu ndio maana tunapata matatizo na changamoto mbalimbali za kiafya.
Basi na kualika ndugu yangu katika ukurasa huu ili tuweze kutatua changamoto zetu za afya kwanzia ndani ya miili yetu kwa kupitia Lishe bora.

TUJILINDE NA TUWALINDE TUWAPENDAO KWA KUWAPA MFUMO BORA WA AFYA.

Address

Dar Es Salaam Mwenge Mpakani
Dar Es Salaam
00043

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when AFYA.Ni.UREMBO posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to AFYA.Ni.UREMBO:

Share