Afya Online na DR. Kilatenga

Afya Online na DR. Kilatenga Kwa ushauri na Tiba kuhusu Afya ya uzazi wa mwanaume na Mwanamke..karibu sana tukuhudumie.

31/07/2026

*ACHA KUTUMIA SABUNI ZA KUOGEA (SHOWER GEL) KUFULIA NGUO ZAKO ZA NDANI....!*

Watu wengi hutumia shower gel kufulia nguo za ndani wakiamini ni salama kwa sababu hutumika kuoshea mwili. Hata hivyo, si chaguo bora kwa kufulia nguo za ndani.

1. Huacha Mabaki ya Kemikali

Shower gel imeundwa kwa ajili ya ngozi, si vitambaa. Inaweza kuacha mabaki kwenye nguo ambayo yanaweza kugusa sehemu za siri na kusababisha muwasho au mzio kwa baadhi ya watu.

2. Huongeza Hatari ya Muwasho

Manukato na kemikali zilizopo kwenye baadhi ya shower gel zinaweza kuchangia kuwasha, kuungua au kuleta usumbufu kwenye ngozi nyeti ya sehemu za siri.

3. Haiui Vimelea Vizuri Kwenye Nguo

Shower gel haijatengenezwa kuondoa bakteria na uchafu kwenye vitambaa k**a sabuni za kufulia, hivyo nguo zinaweza kubaki na vijidudu.

4. Huathiri Ngozi Nyeti

Kwa watu wenye ngozi nyeti, mabaki ya shower gel kwenye nguo za ndani yanaweza kuongeza uwezekano wa kupata vipele au mzio.

Jinsi Sahihi ya Kufua Nguo za Ndani

- Tumia sabuni maalumu ya kufulia au sabuni isiyo na manukato makali.
- Suuza nguo vizuri ili kuondoa mabaki ya sabuni.
- Zikaushe juani inapowezekana, kwani mwanga wa jua husaidia kupunguza baadhi ya vijidudu.
- Hakikisha nguo zimekauka kabisa kabla ya kuvaa.

*➑️ NA HII NI MOJA KATI YA SABABU ZA KWANINI MIWASHO HAIISHI KWAKO..! 🫡*

Dr. Kilatenga
0746 846 891

29/07/2026

*Kwako mwanamke, K**a wakati wa hedhi unaona damu yenye mabonge (blood clots)...πŸ‘‡*

↳ Kutoka mabonge makubwa kuliko kawaida (zaidi ya ukubwa wa sarafu)

↳ Kubadilisha pedi mara kwa mara kila baada ya muda mfupi...

↳ Kujisikia udhaifu, kizunguzungu, au uchovu mwingi...

*NB:* Binti hiyo ni dalili ya muhimu kiafya ambayo hupaswi kuipuuzia..🫡

Mabadiliko yasiyo ya kawaida ya hedhi ni ishara inayoweza kuhusishwa na changamoto za afya ya uzazi...

↳ Mvurugiko wa homoni (Hormonal imbalance)

↳ Uvimbe kwenye mfuko wa uzazi (Uterine fibroids)

↳ Maambukizi ya mfumo wa uzazi

↳ Unene wa ukuta wa mfuko wa uzazi (Endometrial thickening)

*Usithubutu kutumia Madawa bila kujua chanzo cha tatizo lako... Hakikisha unaenda hospitali kufuatilia changamoto hiyo kwa vipimo..🫡*

Dr. kilatenga
0746846891

28/07/2026

*MAPENZI WAKATI WA HEDHI (PERIOD): FAHAMU UKWELI NA TAHADHARI ZA AFYA*

Kufanya mapenzi wakati wa hedhi ni uamuzi wa wanandoa. Kiafya, si jambo lililokatazwa moja kwa moja, lakini kuna baadhi ya hatari zinazoweza kuongezeka endapo tahadhari hazitachukuliwa.

*A. Athari Kwa Mwanamke*

1. Hatari ya Maambukizi

Wakati wa hedhi, mlango wa kizazi (cervix) huwa wazi zaidi kuliko kawaida. Hali hii inaweza kuongeza uwezekano wa bakteria au maambukizi ya zinaa kuingia kwenye njia ya uzazi ikiwa mmoja wa wenzi ana maambukizi.

2. Maumivu na Kutokwa na Damu Zaidi

Baadhi ya wanawake wanaweza kupata maumivu makali zaidi ya tumbo au kuona damu ikiongezeka wakati wa kufanya mapenzi kipindi cha hedhi.

3. Hatari ya Pelvic Inflammatory Disease (PID)

Ikiwa kuna maambukizi ya bakteria au magonjwa ya zinaa, hatari ya maambukizi kupanda hadi kwenye mji wa mimba na mirija ya uzazi inaweza kuongezeka.

4. Uwezekano wa Kupata Mimba

Ingawa nafasi ni ndogo, mimba inaweza kutungwa wakati wa hedhi, hasa kwa wanawake wenye mzunguko mfupi wa hedhi kwani mbegu za mwanaume zinaweza kuishi ndani ya njia ya uzazi kwa hadi siku 5.

B. Athari Kwa Mwanaume

1. Hatari ya Kuambukizwa Magonjwa ya Zinaa

Iwapo mwenzi ana maambukizi k**a vile HIV, Hepatitis B au magonjwa mengine ya zinaa, uwezekano wa maambukizi unaweza kuwa mkubwa zaidi bila matumizi ya kondomu.

2. Msongo wa Kisaikolojia

Baadhi ya wanaume wanaweza kuhisi kutokuwa huru kutokana na damu, harufu au hali ya hedhi. Hili hutofautiana kulingana na mtazamo wa kila mtu.

_*Jinsi ya Kupunguza Hatari*_

βœ… Tumia kondomu ili kupunguza hatari ya maambukizi ya zinaa.

βœ… Hakikisha wote wawili mnaridhia kufanya tendo hilo.

βœ… Dumisha usafi kabla na baada ya tendo la ndoa.

βœ… Epuka kufanya mapenzi ikiwa mmoja ana dalili za maambukizi k**a usaha, vidonda, harufu kali au maumivu makali.

➑️Kufanya mapenzi wakati wa hedhi kunawezekana, lakini kunaweza kuongeza hatari ya maambukizi ikiwa tahadhari hazitachukuliwa.

Matumizi ya kondomu, usafi na kufahamu hali ya afya ya kila mwenzi ni njia bora za kupunguza hatari.

Ikiwa kuna maumivu makali, kutokwa damu isiyo ya kawaida au dalili za maambukizi, ni vyema kumwona daktari kwa uchunguzi na u

26/07/2026

*UCHAFU UNAOTOKA UKENI UNAWEZA KUELEZA HALI YA AFYA YAKO πŸ‘‡*

🀎 Kahawia β€” Mara nyingi huonekana kabla au baada ya hedhi, lakini ukiwa na harufu au maumivu ni vizuri kufanya uchunguzi.

🀍 Mweupe β€” Unaweza kuwa wa kawaida, lakini ukiwa mzito k**a mtindi na muwasho inaweza kuwa fangasi.

🀍 Clear β€” Ute mwepesi usio na harufu mara nyingi huwa kawaida hasa kipindi cha ovulation.

πŸ’› Njano β€” Inaweza kuashiria maambukizi hasa ukiwa na harufu mbaya au muwasho.

πŸ’š Kijani β€” Mara nyingi sio kawaida, inaweza kuwa dalili ya maambukizi na ni muhimu kuwahi hospitali.

⚠️ Ukiona harufu mbaya, maumivu, kuwaka au muwasho usipuuzie afya yako.

Wahi kupata ushauri wa daktari mapema ❀️

*karibu kwa tiba na ushauri*

Dr. Kilatenga
0746 846 891

25/07/2026

Binti mzuri...
Utamu wa ice cream wa leo unaweza kuwa chanzo cha changamoto ya kesho k**a matumizi ya sukari yatakuwa ya kupita kiasi.

Huu ni ukweli ambao wanawake wengi hawaujui...

Ipo hivi...πŸ‘‡

Kwa mujibu wa tafiti za kisayansi, matumizi ya sukari nyingi yanaweza kuongeza kiwango cha insulin mwilini.

Insulin inapobaki juu kwa muda mrefu, baadhi ya watu hupata hali inayoitwa insulin resistance (mwili kushindwa kuitumia vizuri insulin).

Hali hii inaweza kuongeza hatari ya kupata Polycystic O***y Syndrome (PCOS) kwa baadhi ya wanawake.

PCOS ni tatizo la homoni linaloweza kusababisha:

- Kushindwa kwa mayai kupevuka vizuri.
- Kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi.
- Changamoto ya kushika mimba.

Matumizi ya sukari kupita kiasi yanaweza pia:

↳ Kuvuruga ovulation (utoaji wa yai).
↳ Kuchangia kuongezeka kwa uzito, jambo linaloweza kuongeza hatari ya PCOS.
↳ Kuongeza uvimbe wa ndani wa mwili (chronic inflammation).
↳ Kuathiri ubora wa mayai kwa njia isiyo ya moja kwa moja, hasa pale yanapoambatana na matatizo ya kimetaboliki.

πŸ“Œ Kumbuka:

K**a unapanga kupata ujauzito, ni muhimu kuzingatia lishe bora, kupunguza matumizi ya sukari nyingi na vyakula vya kusindikwa (junk foods), kufanya mazoezi, na kudumisha uzito unaofaa.

Afya ya uzazi huanza na mtindo mzuri wa maisha.

Mwili wako ni maabara. Unapolinda mizani ya homoni zako, unaongeza nafasi ya kuwa na afya njema ya uzazi. ❀️

24/07/2026

UKAVU UKENI: Usiupuuzie!

Je, unahisi uke wako ni mkavu, unawasha au unauma wakati wa tendo la ndoa? Hii inaweza kuwa dalili ya ukavu ukeni.

Ukavu ukeni unaweza kusababishwa na mabadiliko ya homoni, kunyonyesha, msongo wa mawazo, baadhi ya dawa au maambukizi. Hali hii inaweza kupunguza hamu ya tendo la ndoa na kufanya tendo liwe na maumivu.

Habari njema ni kwamba ukavu ukeni unaweza kutibiwa kulingana na chanzo chake.

Nikiwa k**a Mtaalamu wa Afya ya uzazi, napenda kutoa suruhisho la changamoto hii kwa offer kubwa sana...

Nitakupatia TRE-EN-EN ambayo itakusaidia kuondoa, ukavu ukeni, kurejesha hamu ya tendo la ndoa, kubalance homoni, na kuondoa maumivu Wakati wa hedhi...

Arafu utapata REPROCARE buree kabisa k**a offer kwa atakae chukua Full Tre en en..

*Hii utapata kwa Tsh. 120000 badala ya Tsh. 150000/=*

_*πŸ‘‰Wahi Offer hii itakwisha Jumapil jioni...*_

🌸 Afya yako ya uzazi ni muhimu. Usione aibu kutafuta msaada mapema.

**TAARIFA ZA MALIPO:-*

VODA, 0746846891(ERICK KILATENGA).

YASS, LIPA 19848280(Dr.kilatenga).

22/07/2026

Je, umewahi kufikiria kutumia dawa za kuchelewesha au kukata hedhi kwa sababu ya safari, sherehe au tukio maalum? πŸ€”

Kabla hujafanya uamuzi, fahamu kuwa dawa hizi si za kutumia kiholela.

Zinapaswa kutumiwa kwa ushauri wa daktari kwa sababu zinaweza kuwa na faida katika hali maalum za kitabibu, lakini pia zinaweza kuwa na madhara endapo zitatumika vibaya.

Afya yako ni muhimu kuliko tukio lolote la muda mfupi. Usihatarishe mwili wako kwa ushauri wa marafiki au taarifa zisizo sahihi kutoka mitandaoni.

Soma maelezo yote kwenye chapisho hili, kisha tuambie maoni yako au uliza swali kwenye sehemu ya maoni. Elimu sahihi ndiyo kinga bora ya afya. πŸ’™

*Dr. Kilatenga*
*0746 846 891*

21/07/2026

*🚨UTE WA KAWAIDA UKENI (Normal vaginal discharge)πŸ’§πŸ’§πŸš¨*

*Rangi:* Mweupe k**a maji masafi au uwazi (clear)

*Harufu:* Haina harufu mbaya, bali harufu ya asili ya kuvutia ya uke

*Muonekano:* Laini, wa kunata kidogo (k**a ute wa yai)

*Dalili:* Hakuna muwasho, maumivu wala kuwaka moto

*Chanzo:* Mabadiliko ya kawaida ya homoni (ovulation, hedhi)

*πŸ›‘UCHAFU USIO WA KAWAIDA UKENI (Abnormal discharge)πŸ©ΈπŸ©ΈπŸ›‘*

*Rangi:* Maziwa, Njano, kijani, kijivu au kahawia

*Harufu:* Huwa na harufu mbaya (mfano ya samaki)

*Muonekano:* Mwepesi, Nzito, wa povu au k**a maziwa yaliyoganda

*Dalili:* Muwasho, kuwaka moto, maumivu wakati wa kukojoa au tendo

*Chanzo:* Maambukizi k**a Bacterial Vaginosis au Candidiasis

*UTE ni sehemu ya ulinzi wa uke, wakati UCHAFU ni dalili ya ugonjwa.*

πŸ‘‰Usichukulie poa dalili zote zisizo za kawaida ukeni... Chukua hatua ya kutambua tatizo na upate Tiba ya uhakika..

*Dr. Kilatenga*
*0746 846 891*

17/07/2026

Njia rahisi ni kuuliza mtu unayemuamini akuambie kwa uaminifu au kufanyiwa uchunguzi hospitalini.

Pia ukiona harufu kali isiyo ya kawaida, uchafu wenye rangi tofauti, au miwasho, nenda ukapimwe.

Epuka kujitathmini kwa kunusa peke yako, kwani unaweza usitambue mabadiliko ya harufu.

K**a unatokwa na uchafu unao ambatana na harufu mbaya na Miwasho uken pamoja na UTI....

Usijar...
Kipo kirutubisho maalum kwaajili ya changamoto hiyo kinacho itwa REPROCARE..

Hiki kipo katika mfumo wa kimiminika ambayo utaitumia kwa kunywa na kujisafisha sehem za siri..

Hii itakusaidia kuondoa Fungus, UTI pamoja na uchafu unao ambatana na harufu mbaya ukeni pamoja na Miwasho..

Wasiliana nasi Sasa...

0746846891

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Afya Online na DR. Kilatenga posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share