29/11/2024
UTI (Urinary tract infection) ni ugonjwa wa maambukizi katika mfumo wa mkojo na maambukizi haya yanasababishwa na bakteria, fangasi na virus. Mara nyingi bakteria wanaoingia kwenye mfumo wa mkojo hutolewa na mwili. Wakati mwingine bakteria wanaweza zidi kinga ya mwili na kusababisha maambukizi hayo.
UTIs inaweza athiri mrija wa mkojo (urethra), kibofu cha mkojo na figo.
UTI INASABABISHWA NA NINI?
Mara nyingi UTI zinasababishwa na bakteria aitwaye Escherichia coli (E. coli) ambayo husababisha 80% ya kesi zote.
Vyanzo vingine ni:
Bakteria Klebsiella pneumoniae Staphylococcus saprophyticus Chlamydia na Mycoplasma
(hususan kwa maambukizi ya mfumo wa uzazi)
Muhimu: UTI inayosababishwa na Chlamydia na Mycoplasma inahitaji wenza wote kupata tiba pamoja.
DALILI ZA UTI
Kukojoa mara kwa mara na maumivu wakati wa kukojoa
Kuhisi kuunguzwa/kuwashwa na mkojo kwenye kibofu au mrija wa mkojo
Maumivu ya misuli na tumbo
Mkojo kuwa na harufu mbaya na kubadilika rangi (nyeusi au rangi ya mawingu)
Maumivu mgongoni au kwenye mbavu (kwa maambukizi ya figo)
Kichefuchefu na kutapika
Kushikwa na hamu ya kukojoa ila mkojo unatoka kidogo
Dalili za Hatari Zaidi:
Homa ya juu
Kutetemeka
Mkojo wenye damu
Maumivu makali ya mgongo
Kutapika kwa kiwango kikubwa
NI WATU GANI WALIO KATIKA HATARI YA KUPATA UTI?
☑️Watu wenye kutumia mpira wa mkojo kwa muda mrefu na pempas
☑️Watu wenye matatizo ya mfumo wa mkojo (figo, mirija, kibofu)
☑️Watumiaji wa njia fulani za uzazi (diaphragm, s***micides, kondomu)
☑️Watu wenye mahusiano ya kimapenzi yanayoweza kuhamisha bakteria
☑️Wanawake (kutokana na maumbile yao)
☑️Wajawazito
☑️Watu wenye kisukari
☑️Watu wenye mfumo dhaifu wa kinga
KWANINI WANAWAKE NDO WAHANGA WAKUBWA?
Urethra ya wanawake ni fupi zaidi (takribani sentimita 4 tu), hivyo bakteria wana safari fupi kufika kibofu
Mrija wa mkojo uko karibu na uke na tupu ya nyuma, maeneo yenye bakteria wengi
Mabadiliko ya homoni wakati wa ujauzito na hedhi Matumizi ya baadhi ya njia za uzazi wa mpango
KWANINI UNAPATA UTI MARA KWA MARA (UTI SUGU)
Mfumo wa kinga dhaifu: Kushindwa kupambana na bakteria
Kuwa mwanamke: Hatari kubwa kutokana na maumbile
Kukaa na mkojo kwa muda mrefu
Mahusiano ya kimapenzi: Kuhamisha bakteria
Kutokunywa maji ya kutosha
Matumizi yasiyo sahihi ya antibiotiki
Mabadiliko ya homoni
Masuala ya kiafya k**a kisukari
JINSI YA KUJIKINGA NA UTI
✅Kunywa maji mengi (angalau lita 2-3 kwa siku)
✅Kukojoa mara kwa mara bila kuchelewa
✅Kujisafisha vizuri (kutoka mbele kwenda nyuma)
✅Kuvaa nguo za ndani za pamba na zisizobana
✅Kukojoa baada ya kujamiiana
✅Kula vyakula vyenye probiotics
✅Kudumisha usafi wa maeneo ya siri
ATHARI ZA KUTOKUTIBU UTI KIKAMILIFU
◾Uharibifu wa kudumu wa figo
◾Kuhitaji dialysis
◾Uzazi wa watoto wenye uzito mdogo au kuzaa kabla ya wakati
◾Prostatitis kwa wanaume
◾Sepsis (sumu katika damu)
◾Matatizo ya moyo
◾Shinikizo la damu la juu
◾Cystitis (maambukizi ya kibofu cha mkojo)
Wahi mapema tukuhudumie 🤝 kwa simu no
0654924590 au tuma ujumbe Whatsapp 👇⬇️
0684 399 389