16/09/2026
Najua zile siku zinavyoweza kuwa ngumu.
Tumbo linavuta, mgongo unauma, wakati mwingine unashindwa kufanya shughuli zako vizuri…
halafu unajua kabisa: “Ngoja nitumie painkiller, yatapoa.”
Na kweli, dawa za maumivu zinaweza kusaidia kupunguza maumivu ya hedhi.
Lakini swali langu kwako ni hili
Je, kila mwezi lazima usubiri maumivu yaanze ndipo uanze kuyafikiria?
Kwa baadhi ya wanawake, kuna hatua nyingine za kujisaidia ambazo zinaweza kusaidia kupunguza maumivu, k**a
➡️ Tangawizi — tafiti zimeonyesha inaweza kusaidia kupunguza ukubwa wa maumivu ya hedhi kwa baadhi ya wanawake.
➡️ Kutumia Joto tumboni — kutumia hot-water bottle/heating pad kunaweza kusaidia kupunguza maumivu na misuli kujikaza.
➡️ Mazoezi ya kutembea — kutembea au kufanya mazoezi mepesi kunaweza kusaidia baadhi ya wanawake wakati wa hedhi.
Lakini niseme hili kwa uwazi tu
k**a maumivu yako ni makali kiasi cha kukuzuia kuishi maisha yako kawaida, yanazidi kuwa makali, au yameanza kuwa tofauti na kawaida yako, usiyafiche kwa kutumia painkiller kila mwezi,tafuta chanzo kwa mzizi wa tatizo.
Kwa hiyo, lengo si kusema “usitumie dawa.”
Lengo ni kukusaidia kufahamu kwamba
Maumivu ya hedhi hayapaswi kuwa kitu unachovumilia tu kila mwezi bila kuelewa mwili wako unapitia vitu gani mpaka kupelekea kupata maumivu hayo makali hasa wakati wa hedhi.
Save na share post hii kwa rafiki yako unaejua anapitia maumivu ya hedhi kila mwezi 📌.