24/07/2026
VIDONDA VYA TUMBO AU ACID REFLUX? USIVICHANGANYE!
Watu wengi hudhani maumivu yote ya tumbo ni vidonda vya tumbo, kumbe si kweli. Haya ni magonjwa mawili tofauti yanayohitaji uelewa sahihi.
πΉ VIDONDA VYA TUMBO (Ulcers) hutokea pale ambapo ukuta wa tumbo au sehemu ya juu ya utumbo mdogo unapata jeraha. Mara nyingi husababishwa na bakteria Helicobacter pylori au matumizi ya muda mrefu ya dawa za maumivu k**a ibuprofen na diclofenac.
Dalili zake ni: βοΈ Maumivu makali ya tumbo hasa katikati au juu ya tumbo. βοΈ Maumivu yanaweza kuongezeka au kupungua baada ya kula kutegemeana na sehemu yenye kidonda. βοΈ Kichefuchefu, kutapika, na wakati mwingine choo cheusi au kutapika damu ikiwa kidonda kimetoa damu.
πΉ ACID REFLUX (GERD) hutokea pale tindikali ya tumbo inapopanda kuelekea kwenye umio kutokana na mlango wa tumbo kushindwa kufunga vizuri.
Dalili zake ni: βοΈ Kiungulia (moto kifuani). βοΈ Tindikali kupanda mdomoni au koo kuwa na ladha chachu. βοΈ Kifua kubana, kukohoa hasa usiku, sauti kukwaruza, na dalili kuongezeka baada ya kula au unapolala.
β οΈ Usijitibu kwa kubahatisha. Dalili zinaweza kufanana, lakini chanzo na matibabu hutofautiana. Uchunguzi wa kitaalamu ni muhimu ili kupata tiba sahihi.
Afya yako inaanza na uelewa sahihi. Ukiona dalili zinajirudia au hazipungui, tafuta ushauri wa mtaalamu wa afya mapema.