Mr Health

Website

Mr Health Mtaalamu wa afya ya uzazi kwa wanaume na wanamke, Miongozo ya lishe bora na Ushauri wa Kisaikolojia..🩺

Siri ya Limao na Kitunguu Saumu Ambayo Inarekebisha Homoni kwa ndani ya siku 14..🧄🍋— Hormone imbalance ni tatizo linalos...
13/11/2026

Siri ya Limao na Kitunguu Saumu Ambayo Inarekebisha Homoni kwa ndani ya siku 14..🧄🍋

— Hormone imbalance ni tatizo linalosababisha uchovu sugu, kukosa hamu ya tendo, mabadiliko ya hisia, na hata kuharibika kwa ngozi— Bila hata wewe kujua chanzo chake...

↳ Kitaalamu, mchanganyiko wa Limao na Kitunguu Saumu husaidia...

↳ Kusafisha ini (liver detox), Chanzo kikuu cha usawa wa homoni

↳ Kurekebisha uzalishaji wa homoni za k**e na kiume....

↳ Kuimarisha kinga na kuongeza nguvu ya mwili kwa ujumla...

Tuone Namna ya kuandaa Tiba formula hii ukiwa nyumbani kwako...👇

↳ Menya vitunguu saumu punje 15 hadi 20, vikate vipande vidogo au twanga kwenye kininu...

↳ Kamulia Limao 1 ndani ya maji glasi 2 na maji...

↳ Changanya Chemsha dakika 10–15 kisha chuja.

↳ Kunywa nusu glasi asubuhi na nusu jioni kwa siku 14 ...

Ni formula ya asili ambayo imeonyesha matokeo makubwa kwa wale wanaotaka kurejesha mwili katika usawa wa homoni bila kutumia dawa kali..

Umewahi kuhisi dalili za hormone imbalance?

Funguka kwenye comment —Tujadili njia salama za kurejesha usawa wa mwili wako kitaalamu..🩺

By Mr Health A sound of health | Jifunze na chukua hatu kuboresha afya yako...🩺🫡

Mwanamke anaweza kuvumilia kipindi ambacho huna pesa, kusimama nawewe katika wakati mgumu....Anaweza kusamehe makosa yak...
10/11/2026

Mwanamke anaweza kuvumilia kipindi ambacho huna pesa, kusimama nawewe katika wakati mgumu....

Anaweza kusamehe makosa yako, hata kukupa nafasi nyingine baada ya kumvunja moyo...

Broo, usijipe uhakika kwamba kila kitu kiko sawa kwa sababu bado yupo pembeni yako...

Kuna jambo moja ambalo wanaume wengi hulikwepa kulizungumzia....

Broo, usidanganyike kwamba tendo la ndoa ni suala la nguvu, muda au uwezo wa kusimamisha uume pekee.

Ni zaidi ya hapo..!

Msongo wa mawazo, mawasiliano, mzunguko wa damu, homoni na hali ya kihisia vinaweza kuathiri utendaji wako kitandani..

Na hapa ndipo siri ilipo…Unaweza kuwa mwanaume mwenye mafanikio makubwa nje ya chumba chako...

Lakini k**a unakataa kujifunza kuhusu afya yako ya uzazi na mahitaji ya mwenza wako, unapuuzia eneo muhimu la ukaribu wenu.....

Usisubiri mpaka mwenza wako aanze kunyamaza ndipo utambue kuwa kuna jambo halipo sawa.....

Kujifunza si udhaifu, Kutafuta msaada sio aibu, Na changamoto za uzazi si hukumu ya uanaume wako.

Broo, elimu ya afya ya uzazi sio anasa, Ni sehemu ya uwajibikaji wako k**a mwanaume....📌

Kuna watu wanatamani kusikia Kuliko cha mtoto ndani ya nyumba zao, Lakini haswajui watafute wapi Faraja ya mioyo Yao.🥹Ku...
08/11/2026

Kuna watu wanatamani kusikia Kuliko cha mtoto ndani ya nyumba zao,

Lakini haswajui watafute wapi Faraja ya mioyo Yao.🥹

Kuna mwanamke anayechoka kuona kila mwezi hedhi ikianza, Bila matumaini aliyokuwa nayo...

Wapo wanaume wanayejilaumu kimyakimya, akihisi ameshindwa kutimiza ndoto ya kuwa baba...

Na kuna ndoa ambazo zimeanza kuishi kwa presha ya swali moja: "Mtapata mtoto lini?" 😭

Lakini sikiliza hili kwa makini…👇

Changamoto ya kupata mtoto sio hukumu ya thamani yako k**a mwanamke na mwanaume au mwenzi wa ndoa...

Kitaalamu, changamoto ya kupata ujauzito inaweza kuhusisha mwanamke, mwanaume au wote wawili.

Ndiyo maana uchunguzi wa afya ya uzazi unapaswa kuwahusisha wenzi wote, badala ya kumlaumu mmoja...

Usifiche tatizo kwa aibu, Usijitibu kwa kutumia dawa au virutubisho bila ushauri wa kitaalamu.

Tafuta uchunguzi sahihi na mwongozo wa wataalamu wa afya...

Na zaidi ya yote, msiruhusu changamoto hii ivunje upendo, heshima na amani ya familia yenu....

"Kwa wote wanaosubiri kuitwa Mama na Baba"

Mungu awatie nguvu katika safari hii, Mwaka 2027 uwe mwaka wa matumaini mapya, amani katika ndoa zenu na baraka katika familia zenu..

LIKE 👍Post hii Kisha comment AMEN 🙏 Nakuja na Mwongozo Kamili nini chakufanya..📌

Unaposikia neno DETOX Usifikirie sumu ya panya, au ni kwa mtu aliye kunywa sumu, HAPANA..!Detox ni nini..?— Ni mchakato ...
02/11/2026

Unaposikia neno DETOX Usifikirie sumu ya panya, au ni kwa mtu aliye kunywa sumu, HAPANA..!

Detox ni nini..?

— Ni mchakato unaotokea ndani ya mwili kila siku, pale ini, figo na damu zinaposhirikiana kusafisha mwili kutoka kwenye taka sumu zinazojikusanya taratibu kutokana na vyakula, hewa chafu na msongo wa mawazo.

Lakini kuna siri ambayo wengi hawajui...

kuna vyakula vinavyoweza kuongeza kasi na ufanisi wa huu mchakato.

Na moja ya mashujaa wa kimya katika familia ya detox ni BEETROOT tunda au mboga nyekundu inayong’aa k**a damu.....

Kwa nini Beetroot..?

↳ Ina betalains, antioxidant yenye nguvu inayosaidia ini kuvunja sumu na kuondoa haraka.

↳ Huchochea mtiririko mzuri wa damu, hivyo kubeba sumu na taka mwilini kwa ufanisi.

↳ Hupunguza oxidative stress, moja ya chanzo kikubwa cha magonjwa sugu...

↳ Huweka mwili kwenye hali ya alkaline, kupunguza mazingira ya magonjwa...

Fikiria hivi… mtu anayeishi kwenye jiji lenye hewa chafu, anakula vyakula vya haraka (junk foods) kila siku, na hana muda wa mazoezi...

Taratibu mwili wake hujaa taka na sumu, hali ambayo hupelekea uchovu wa mara kwa mara, kupungua kwa kinga ya mwili na hata mabadiliko ya homoni (hormone imbalance).

ipo hivi...

↳ Imbalance ya homoni k**a insulin, cortisol, testosterone, estrogen hutokana pia na sumu mwilini na mfumo wa maisha usio na usawa...

Na hapa ndipo Beetroot Detox inapoleta ukombozi — Husaidia kurejesha usawa wa homoni na nguvu za mwili....

Lakini kumbuka

Beetroot pekee haitoshi, Ili kufanikisha mchakato wa detox na kurekebisha homoni zako...

↳ Fanya mazoezi mara kwa mara (angalau dakika 30 kwa siku).

↳ Punguza vyakula vilivyosindikwa na sukari nyingi.

↳ Kunywa maji ya kutosha, Pata muda mzuri wa kupumzika, walau masaa 7-8 USIKU....

NB: Beetroot ni formula ya ukombozi wa afya yako, Ongeza kwenye juisi, au saladi yako ya kila siku....

Mwili wako utakushukuru…

Beetroot Detox, Siri ya asili ya kuondoa sumu, kurudisha nguvu na kusawazisha homoni zako.🩺

Comment neno "MWANAUME PROGRAM" nikuunge na group letu BURE, kujifunza Mbinu na Tiba Leo...🔥🔥

K**a jibu ni "HAPANA" tuambie kwanini...!? 😁
01/11/2026

K**a jibu ni "HAPANA" tuambie kwanini...!? 😁

Samahani yako unayo kula Leo inaweza kuwa na mchango katika afya yako ya uzazi kesho...⚡1. VYAKULA VYA  WANGA KWA WINGI....
30/10/2026

Samahani yako unayo kula Leo inaweza kuwa na mchango katika afya yako ya uzazi kesho...⚡

1. VYAKULA VYA WANGA KWA WINGI...

Mkate, ugali, wali, chapati, Kutegemea sana vyakula hivi bila uwiano sawa wa vyakula vya nyuzinyuzi huathiri Ubora wa hormone.

2. NYAMA ZILIZOSINDIKWA..

Sausages, nyama za kopo, Huusishwa na mifumo ya lishe isiyofaa ni hatari kwa ubora wa mbegu za kiume...

3. VINYWAJI VYENYE SUKARI NYINGI ..

Soda juice za makopo, huongeza hatari ya usugu wa insulini na matatizo ya hormone Huvuruga uwiano wa homoni.....

4. CHIPS NA VYAKULA VYA KUKAANGA...

Kuongeza mafuta na kalori nyingi mwilini, na kuchangia unene unaoweza kuathiri mfumo wa homoni....

5. VYAKULA VYA SUKARI NYINGI...

Keki, biskuti na p**i, Huchangia unene na usugu wa insulini, Adui mkubwa wa afya ya uzazi.

6. POMBE NA SIGARA..

Matumizi makubwa ya pombe na sigara yanaweza kuvuruga uzalishaji wa homoni

Huathiri ubora wa mbegu za kiume pamoja na uwezo wa uzazi wa mwanamke....

Linda afya yako ya uzazi kabla hujaanza kutafuta majibu ya matatizo ambayo ungeweza kuyapunguza kwa kubadili mtindo wa maisha..

Tumia vyakula vya asili k**a, Tangawizi, vitungu saumu na Mdalasini kwa Afya Bora ya Uzazi....

Binti, si kila anayekutazama anakuthamini, na sio kila anayekusifia ana nia njema na wewe.Wengine wanavutiwa na kile wan...
28/10/2026

Binti, si kila anayekutazama anakuthamini, na sio kila anayekusifia ana nia njema na wewe.

Wengine wanavutiwa na kile wanachokiona, lakini hawana hata chembe ya nia ya kuwajibika kwa maumivu utakayo yapitia baadaye.....

Usisubiri siku ambayo utachoka kutafutwa na kuanza kujiuliza kwa nini hakuna anayekuchagua kwa dhati.

Uzuri wako unaweza kuvuta macho mengi, lakini thamani yako haipaswi kutegemea macho hayo.

Kinachotia huzuni ni pale unapogeuza mwili wako kuwa chombo cha kutafuta uthibitisho wa thamani yako kutoka kwa watu wengine,

kiasi kwamba unaanza kuamini kuwa usipoanika matrako hutavutia, hutapendwa, wala hutazungumziwa....

Binti, usije ukaishia kujulikana kwa mwili ulioanika, badala ya thamani uliyoshindwa kuilinda. 📌

Kitendo cha kushiriki tendo kipindi cha hedhi kina madhara makubwa kwa wanaume na wanawake...Matatizo ya tezi dume "PROS...
27/10/2026

Kitendo cha kushiriki tendo kipindi cha hedhi kina madhara makubwa kwa wanaume na wanawake...

Matatizo ya tezi dume "PROSTETITS" Ni tatizo linalo wakumba wanaume na hata kupelekea ugumba...

Maambukizi ya pelvic inflammatory disease (PID), Saratani ya shingo ya kizazi na Kuziba kwa mirija ya uzazi....

Damu ya hedhi unapelekea kulegea kwa mishipa ya uume nakupelekea tatizo la Uume Legelege....

Mwanamke kupatwa na maumivu makali ya tumbo hasa kwa wale wanaopatwa na maumivu wakati wa hedhi....(DYSMENORRHEA)

Kuongezeka kutoka kwa damu nzito nyeusii na yenye mabonge, Sio hali ya kwaida ya hedhi, nihatari kwa afya ya Uzazi...

Harufu mbaya mazingira machafu kusababisha adhari ya kisaikolojia...Hivyo kupelekea kutofulahia tendo na kutoka mchezoni Mapema tuache tamaa aseeeh....

NB: Tuwapende wapenzi wetu, aseeh siku 3-4 hizo sio nyingii heshimu hedhi ya mpenzi wako mjali, Misikilize anahitajinini nasio kumlazimisha akiwa katika hali ya hedhi yake...📌

Wanawake wengi hukosea kuelewa tofauti kati ya kumridhisha mwanaume kimwili na kumfanya ajisikie salama kihisia....Kisai...
26/10/2026

Wanawake wengi hukosea kuelewa tofauti kati ya kumridhisha mwanaume kimwili na kumfanya ajisikie salama kihisia....

Kisaikolojia, mwanaume anaweza kuvutiwa na mwili wako, lakini kile kinachojenga ukaribu wa kudumu ni namna anavyojisikia akiwa karibu nawe....

Sikiliza vizuri, Binti…👇

Unaweza kuwa na uzuri unaovutia macho yake, lakini k**a kila anaporudi kwako anakutana na lawama, dharau, mashindano ya mamlaka na uchovu wa kihisia

Amani ni kuwa na mtu ambaye mnaweza kutofautiana bila kuumizana, kuzungumza bila kuogopana na kusahihishana bila kudhalilishana...

Kwa sababu mwanaume hahitaji tu mwanamke anayemvutia...

Anahitaji pia uhusiano ambao ndani yake kuna heshima, uaminifu, ukaribu na usalama wa kihisia.

Mwisho wa siku, Binti..Usijiulize tu “Ninawezaje kumfanya anitamani..?”

Jiulize pia...👇

“Anapokuwa karibu nami, anapata nafasi ya kupumua kihisia, au anatafuta nafasi ya kukimbia...?”

Kitaalamu, hapa tunazungumzia "Mixed Signals" ishara zinazoweza kutafsiriwa kwa namna tofauti...Mtu anaweza kuwa na mata...
25/10/2026

Kitaalamu, hapa tunazungumzia "Mixed Signals" ishara zinazoweza kutafsiriwa kwa namna tofauti...

Mtu anaweza kuwa na matarajio fulani moyoni, lakini akashindwa kuyaeleza wazi kwa maneno...

Tatizo ni kwamba, matarajio yasiyosemwa hayawezi kuwa kipimo cha kile ambacho mtu mwingine alipaswa kufanya...✍️

Address

Masaki
Dar Es Salaam
14111

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mr Health posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share