Imarisha Ndoa

Imarisha Ndoa Uponyaji wa kihisia, mafunzo ya mahusiano & Ndoa na ushauri nasaha kwa wenye changamoto hizi.

13/05/2026

Kuna maneno ambayo yakitoka mdomoni wakati wa ugomvi huwa yanabaki moyoni kwa muda mrefu. 💔

Mambo 3 usiyaseme kamwe:
1️⃣ "Wewe DAIMA unafanya hivi"
2️⃣ "Talaka" au "Tutengane" Usiseme hata kwa hasira
3️⃣ Kutaja wazazi au ndugu zake ndani ya ugomvi wenu

Umewahi kusema mojawapo ya haya?

Save video hii kwa ajili ya matumizi ya baadae.

08/05/2026

Ndoa yako inahitaji amani - siyo drama!
Kila usiku unakaa ukitazama tamthilia za mahusiano, akili yako inaandika "programu mpya" bila wewe kujua.
Akili yako itatengeneza tabia sawa na program iliyowekwa.

Ndio maana kuna baadhi ya tabia watu wanazifanya bila wao kupenda na wanajikuta tu wamewafanyia wenzi wao wanaowapenda kwa dhati. Baadae wanajuta.
Ndoa nyingi zinakufa watu wakiwa bado wanapendana.

Usimruhusu mwigizaji wa TV hata k**a ni maarufu vipi, akufundishe jinsi ya kupenda mwenzi wako wa ukweli.

Akili iliyopangwa vizuri inajenga ndoa yenye furaha.
Shiriki hii kwa mtu anayehitaji kusikia leo!

Je, unakubaliana? Andika YES au NO comments!

#

06/05/2026

Ndoa yenye afya haimaanishi ndoa bila matatizo - inamaanisha ndoa inayojua jinsi ya kupita matatizo pamoja. 💪🏾

Jiulize leo:
✅ Mnazungumza hata kuhusu mambo magumu?
✅ Mnagombana - lakini mnamaliza?
✅ Mnathamiana kwa maneno na matendo?

K**a una ishara 3/3 - hongera sana! 🙌🏾
K**a bado unajivuta ujue uko njiani. Usiache

👇🏾 Niambie hapo chini — umepata maksi ngapi? 1, 2, au 3?

💾 Save video hii - utaitumia siku moja.

Afya NdoaZaAfrika

Umekuwa kwenye mahusiano na watu wengi na umeshaachana nao.Unatafuta mtu sahihi lakini hupati.Sio kwamba soul mate (mtu ...
25/03/2026

Umekuwa kwenye mahusiano na watu wengi na umeshaachana nao.

Unatafuta mtu sahihi lakini hupati.

Sio kwamba soul mate (mtu sahihi) hayupo…
Lakini ni kwamba lakini sehemu zako bado zimebaki kwao na sehemu zao zimebaki kwako.

💬 Nipe maoni yako: Je, unaamini history ya mapenzi inaweza kuathiri uwezo wa kumpata mtu sahihi?

sahihi sahihi

Mume wa maana huwezi kumpata kirahisi...* Huwezi kumpata bar,* Huwezi kumpata mtandaoni (bila uchunguzi wa kina),* Huwez...
22/03/2026

Mume wa maana huwezi kumpata kirahisi...
* Huwezi kumpata bar,
* Huwezi kumpata mtandaoni (bila uchunguzi wa kina),
* Huwezi kumpata mahali panapotawaliwa na starehe kuliko maadili (kwa haraka bila kuchunguza),
* Huwezi kumpata kwa hisia pekee bila kutumia akili,
* Huwezi kumpata kwa kuangalia muonekano kuliko tabia,
* Huwezi kumpata kwa kutegemea maneno matamu kuliko matendo,
*Huwezi kumpata bila kujijua wewe mwenyewe kwanza.

Ukweli mchungu:
Mume wa maana humtafuti...anatambuliwa.
Ujikosea unapomtafuta na unavyotafuta...utapata mume ambaye si sahihi kwa ndoa.

Anza wewe kubadilika ndipo utaweza kuchagua sahihi.

Follow akaunti hii kwa maarifa zaidi.

03/03/2026

Hii huwa wanaume hawaelewi.
Lakini ndio kiini cha huzuni kwa wanawake.

Maumivu ya moyo ni matokeo ya tafsiri tunayotoa kwa kilichotokea. Tukikazia upande wa maumivu, tunaendelea kuumia. Lakin...
09/11/2025

Maumivu ya moyo ni matokeo ya tafsiri tunayotoa kwa kilichotokea. Tukikazia upande wa maumivu, tunaendelea kuumia. Lakini tukibadilisha mtazamo na kuona tukio k**a sehemu ya ukuaji wetu, ubongo huanza kuachilia kemikali za utulivu k**a serotonin na oxytocin.

Kwa hiyo, uponyaji wa moyo hauanzi nje - unaanza pale unaposema: “Sijapoteza, ila kuna manufaa kwenye hili"

Usitafute mtu mkamilifu. Kumbuka ya kuwa hata wewe mwenyewe una mapungufu.K**a umependa ujumbe huu tafadhali fanya yafua...
25/10/2025

Usitafute mtu mkamilifu. Kumbuka ya kuwa hata wewe mwenyewe una mapungufu.

K**a umependa ujumbe huu tafadhali fanya yafuatayo:
1. Save post hii kwa matumizi ya baadae
2. Comment kitu ulichojifunza
3. Follow page hii kwa masomo zaidi
4. Share ili umsaidie mwingine






Acha kupambana na kila mtu -  baadhi hawahitaji majibu, wanahitaji kuona tu mafanikio yako.Watu wengine huwa hawaelewi m...
21/10/2025

Acha kupambana na kila mtu - baadhi hawahitaji majibu, wanahitaji kuona tu mafanikio yako.
Watu wengine huwa hawaelewi maneno, wanaelewa matokeo.

Kwa hiyo wewe tulia tuliii!!! fanya kazi kwa utulivu, endelea kusonga mbele… na acha Mungu awe msemaji wako kupitia matokeo yako.

Ukijibu kila kelele, utapoteza nguvu ya kujenga kile kinachostahili kusikika.

👉 Comment: “Nipo busy na matokeo yangu🔥”

Share kwa mtu anayepoteza muda kujibishana badala ya kujijenga.

🔔 Follow kwa hekima zaidi za maisha, ndoa na amani ya ndani.













14/10/2025

Address

Dar Es Salaam
12116

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Imarisha Ndoa posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share