20/08/2025
Watu wengi wanaona mafanikio ni pesa na bidii, lakini leo nataka kukumbusha kuwa akili yako mara nyingi inachukua njia rahisi za haraka katika mambo mbalimbali huku ikipotosha maamuzi yako
Hali hiii inamaanisha unaweza kufanya uamuzi unaonekana sahihi, lakini kwa kweli unakupotezea hasa katika fursa za biashara kwa baadhi ya watu
Akili hupendelea kuona tu kile unachotaka kuona. Mfano,Ukiwa na wazo la biashara,au ukichagua tu taarifa zinazokubaliana na wazo lako, au kupuuzia ishara za hatari au fursa nyingine.
Hii hupelekea biashara kushindikana bila sababu za wazi, bali kwa upotoshaji wa akili yako, na mara nyingi ni ngumu kugundua hili kuwa akili inakupotosha.
Wakati mwingine unashikilia wazo la awali au bei ya bidhaa, bila kuzingatia hali mpya ya soko. mfano,umeweka bei kulingana na bei ya mwaka jana,sasa soko limeshuka katika aina ya bidhaa uliyo nayo;
haiuzwi tena kwa thamani ya mwaka jana lakini akili yako inasema “bei ilikuwa sawa hapo awali.”
Hili linaweza kupunguza mauzo na kupoteza wateja ikiwa hutaangalia hali halisi.
Ubongo unahofia kupoteza zaidi kuliko furaha ya kupata faida. Unaona fursa nzuri ya uwekezaji au biashara, lakini unashuku na kuwa na mashaka ya kupoteza kidogo, huku ukiacha nafasi kubwa ya faida.
Kujua hili kunakupa uhakika wa kuchukua hatua ndogo ndogo, bila kushindwa au kuogopa.Wakati mwingine unajiona una uwezo mkubwa zaidi ya kweli, ukipuuzia hatari halisi.
Mfano: Kuongeza bidhaa kwenye soko bila utafiti wa wateja, kwa sababu “nina uhakika itauzwa.”Hii hupelekea hasara zisizohitajika,
suluhisho ni kuchukua muda kuthibitisha taarifa kabla ya kuamua Kujua upotoshaji wa akili ni silaha kubwa ya mafanikio.
Ukijua biases zako, unaweza kupanga maamuzi sahihi, kuondoa hatari zisizo za lazima, na kuongeza faida kwa kila hatua.
Hii ndiyo sababu wataalamu wa biashara wanaweza kuongeza mapato kwa 20–50% kwa kuelewa na kudhibiti akili yao.
Alex Kedmon
0621301181.
*Habari maelfu ya watu hujifunza kupitia status zangu na wengi