Tumaini letu hospital

Tumaini letu hospital Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Tumaini letu hospital, Hospital, Tumaini letu hospital, Mbeya.

UGONJWA WA MKANDA WA JESHI (SHINGLES)Huu ni ugonjwa wa ngozi na mishipa ya fahamu unaosababishwa na virusi aina ya ”vari...
31/07/2026

UGONJWA WA MKANDA WA JESHI (SHINGLES)

Huu ni ugonjwa wa ngozi na mishipa ya fahamu unaosababishwa na virusi aina ya ”varicella-zoster”, virusi hao ndio walewale wanaosababisha ugonjwa wa “tetekuwanga.”

Mara nyingi mtoto akiugua tetekuwanga akiwa kisha akatibiwa, virusi hivyo huwa havifi badala yake vinabaki kwenye mishipa ya fahamu kwa miaka mingi sana.

Sasa endapo itatokea kinga ya mwili ikashuka kwa sababu eidha umri mkubwa, kula vyakula visivyo na kinga kwa mwili, matumizi ya dawa za saratani, au dawa za kushusha kinga ya mwili — steroids, magonjwa ya saratani, virusi vya ukimwi na kisukari. Basi virusi hivi huamka upya na kuhambulia na kuleta mkanda wa jeshi.

�Dalili za mkanda wa jeshi.

Ugonjwa huu hushambulia upande mmoja wa mwili tu ndio maana uliitwa mkanda wa jeshi kwa kiswahili...inaweza kuwa Usoni-shingo au mgongo hadi tumboni. Kumbuka mkanda wa jeshi haupitilizi upande wa pili wa mwili. Bali uvimbe k**a wa mtu aliyeungua na majimaji hutokea sehemu zilizo athirika huku ukiambatana maumivu makali sana k**a ya moto na kuwasha.[moto wa mungu]

Dalili zingine ni k**a;
-Homa kali,
-Kichwa kuuma,
-Misuli kuuma,
-Uchovu mkubwa.
-Maumivu ya viungo
-Kuvimba kwa mitoki/matezi

�Mkanda wa jeshi kwa wajawazito.

Japokua sio kawaida kwa mama mjamzito kupata mkanda wa jeshi lakini anaweza kupata pia hasa akigusana na mgonjwa husika, hali hii ni hatari kwani husababisha kuathirika kwa mtoto aliyoko tumboni kwa kuzaliwa akiwa na matatizo ya kimaumbile.

�Jinsi ya kutambua ugonjwa huu

Daktari mzoefu anaweza kuutambua ugonjwa huu bila vipimo kabisa na kwa hospitali ambazo zina vipimo, huchukua majimaji ya upele ule na kupimwa ili kuhakikisha ni kweli ugonjwa ni wenyewe.

�Madhara ya mkanda wa jeshi

1. Maumivu makali baada ya kupona: Mgonjwa akitibiwa ugonjwa huu kwa baadhi ya dawa za hospitalini hata baada ya kupona maumivu makali ya sehemu zilizoathirika huendelea na mgonjwa huweza kurudi hospitali kwa kudhani bado ugonjwa haujaisha. Matibabu ya hali hii ni dawa

31/07/2026

Kwa wakazi waishio karibu na ziwa na mito wapo kwenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa wa kichocho, hivyo ni vyema kuchukua tahadhari za mapema ikiwepo kutumia dawa za kichocho kila baada ya miezi mitatu na kupima hali zao mara kwa mara katika hospitali na vituo vya afya, sisi tumaini letu hospital tunaifikia jamii hiyo na kuipa elimu ya kujikinga dhidi ya ugonjwa huu hatari. follow na ku share na malafiki

31/07/2026

Dalili Za Hatari Kwa Mimba Changa.

Mimba changa, au mimba ya mapema, inaweza kuwa na dalili tofauti kwa kila mwanamke na inaweza kutofautiana kulingana na wiki za ujauzito. Hata hivyo, kuna dalili kadhaa za hatari ambazo zinaweza kutokea wakati wa mimba changa na zinapaswa kuchukuliwa kwa umakini.

Ikiwa una dalili hizi, ni muhimu kuwasiliana na daktari wako au kutafuta huduma ya matibabu haraka iwezekanavyo;

1) Kutokwa Na Damu.

Kutokwa na damu sehemu za siri ni dalili inayoweza kuashiria tatizo kwenye mimba. Hata hivyo utoaji damu wowote wakati wa ujauzito unapaswa kuchunguzwa na daktari.

2) Maumivu Ya Chini Ya Tumbo.

Maumivu makali au maumivu ya chini ya tumbo yanaweza kuwa dalili ya tatizo la mimba. Maumivu haya yanaweza kuambatana na kutokwa na damu au bila kutokwa na damu.

3) Maumivu Makali Ya Kifua.

Maumivu makali ya kifua yanapaswa kuchukuliwa kwa umakini, kwani yanaweza kuwa ishara ya tatizo la moyo au matatizo mengine ya kiafya yanayohitaji matibabu haraka.

4) Kichefuchefu Na Kutapika.

Ikiwa unapata kichefuchefu na kutapika sana, ambayo inaweza kusababisha upotezaji mkubwa wa maji (severe dehydration), unapaswa kutafuta matibabu haraka ili kuzuia utapiamlo (malnutrition) na kuwa na mzunguko mzuri wa maji mwilini.

5) Maumivu Ya Mgongo Au Kichwa.

Maumivu ya mara kwa mara ya mgongo au kichwa, haswa ikiambatana na kutokwa na damu au shinikizo la juu la damu, yanaweza kuwa ishara ya matatizo ya afya wakati wa ujauzito.

6) Kupoteza Fahamu Au Kuzirai.

Kupoteza fahamu au kuzirai kunaweza kuashiria matatizo makubwa ya afya wakati wa mimba.

7) Mabadiliko Ya Kasi Ya Mapigo Ya Moyo.

Ikiwa unaona kuwa mapigo ya moyo yameongezeka sana au kudhoofika sana, hii inaweza kuwa ishara ya tatizo la moyo au shinikizo la damu.

Ni muhimu kutambua kuwa dalili hizi za hatari zinaweza kuwa ishara ya matatizo yanayohitaji matibabu haraka ili kulinda afya yako na afya ya mtoto wako. Ikiwa una hofu au wasiwasi wowote kuhusu hali yako wakati wa mimba, usisite kumwambia daktari wako au kutafuta huduma ya matibabu mara moja. Daktari ataweza kuchunguza hali yako na kutoa ushauri na matibabu sahihi.

Dalili Za Sikoseli Kwa Mtoto.Sikoseli ni ugonjwa wa kurithi unaoathiri seli nyekundu za damu, unaojulikana pia k**a ugon...
31/07/2026

Dalili Za Sikoseli Kwa Mtoto.

Sikoseli ni ugonjwa wa kurithi unaoathiri seli nyekundu za damu, unaojulikana pia k**a ugonjwa wa seli mundu (sickle cell disease).

Katika hali ya kawaida, seli nyekundu za damu ni mviringo na rahisi kusafiri kwenye mishipa ya damu ili kusafirisha oksijeni mwilini. Hata hivyo, kwa watu wenye sikoseli, seli hizi hubadilika na kuwa na umbo la mundu (k**a mwezi mwandamo).

Matokeo yake ni kwamba seli hizi haziwezi kusafiri vizuri kwenye mishipa ya damu, na zinaweza kukwama kwenye mishipa midogo, jambo ambalo linaweza kuzuia mtiririko wa damu. Hii husababisha maumivu makali na matatizo ya kiafya k**a vile uharibifu wa viungo, upungufu wa damu, na maambukizi mara kwa mara.

Lakini pia Seli hizi huwa na maisha mafupi zaidi kuliko seli nyekundu za kawaida, jambo linalopelekea upungufu wa damu (anemia), hali ambayo pia ni ya kawaida kwa wagonjwa wa sikoseli.

Dalili za sikoseli kwa mtoto huanza kuonekana mara nyingi baada ya umri wa miezi mitano au sita. Baadhi ya dalili hizo ni pamoja na;3

1) Upungufu Wa Damu (Anemia).

Seli za sikoseli huvunjika haraka na kuacha mwili ukiwa na idadi chache ya seli nyekundu, hali inayoweza kusababisha uchovu na udhaifu kwa mtoto.

2) Maumivu Makali.

Watoto wanaweza kupata maumivu ya ghafla yanayojulikana k**a “pain crisis,” ambayo yanaweza kutokea kwenye mifupa, kifua, au tumbo. Maumivu haya hutokana na seli za sikoseli zinazoziba mishipa ya damu.

3) Kuvimba Vidole.

Kuvimba vidole kunaweza kutokea kutokana na kutokana na mzunguko mbovu wa damu (ukosefu wa oksijeni) kwenye vidole, hali inayoweza kusababisha maumivu.

4) Kuchelewa Kukua.

Watoto wenye sikoseli wanaweza kuchelewa kukua na kubalehe kutokana na upungufu wa oksijeni na virutubisho muhimu mwilini.

5) Maambukizi Mara Kwa Mara.

Watoto wenye sikoseli wako katika hatari kubwa ya kupata maambukizi mara kwa mara k**a vile nimonia kutokana na uharibifu wa mfumo wa kinga.

6) Uchovu Mara Kwa Mara.

Watoto wanaweza kujisikia uchovu mara kwa mara

31/07/2026

K**a unasumbuliwa na Acid Reflux, epuka mambo haya k**a unataka kuona mabadiliko.
Watu wengi hutumia dawa au virutubisho lakini wanaendelea kufanya tabia zinazochochea kurudi kwa tindikali tumboni.
❌ Usile chakula kingi kwa mkupuo.
❌ Usilale ndani ya saa 2–3 baada ya kula.
❌ Epuka vyakula vinavyokuchochea dalili, k**a vyenye mafuta mengi, pilipili nyingi, au vinywaji vyenye kafeini ikiwa vinaongeza dalili zako.
❌ Epuka pombe na uvutaji wa sigara.
❌ Usivae nguo zinazobana sana tumboni.
❌ Punguza msongo wa mawazo na hakikisha unapata usingizi wa kutosha.
❌ Usiruke milo mara kwa mara.
Kumbuka: Acid reflux haihitaji matibabu pekee, bali pia mabadiliko ya mtindo wa maisha. Mara nyingi tabia unazofanya kila siku zinaweza kuchangia dalili kuendelea.
💬 Ni kitu gani ukikila au ukikifanya ndicho huongeza kiungulia chako? Andika kwenye maoni, tujadili pamoja.

31/07/2026

KIUNGULIA ( Heartburn/Acid reflux)

Kiungulia mara nyingi hutokea kutokana na tindikali-tumbo inapotoroka kutoka tumboni na kuchoma umio la chakula (oesophagus).

Mara nyingi dalili za kiungulia huweza tibika kwa dawa za kupunguza tindikali pamoja na mitindo ya maisha.

Iwapo hali ya kiungulia inajirudia inawezekana una tatizo la ugonjwa wa tindikali kupanda kwenye umio gastrointestinal reflux disease (GERD).

Iwapo tatizo hili la GERD lisipotibiwa huweza kuharibu umio la chakula.

MUHIMU:

Iwapo unapata maumivu ya chembe ya moyo yanayoambatana na hali ya mgandamizo kifuani au kushindwa kupumua inaweza kuwa shambulio la moyo.

Tafuta msaada wa kitiba haraka. Ni dharura.

Nitafute WhatsApp +255612335079 nikusaidie.

31/07/2026

JE, UNASUMBULIWA NA BAWASILI NA UMECHOKA KUVUMILIA MAUMIVU? USIKUBALI KUPOTEZA FURAHA YAKO YA MAISHA KWA SABABU YA KERO HII! 🛑

Bawasili sio ugonjwa wa kuficha wala wa kuishi nao kwa mazoea. Wengi wetu tunapitia maumivu makali, choo kigumu, na hata kutoka damu bila kujua kuwa kuna suluhisho la kudumu na salama bila kuhitaji upasuaji wa aina yoyote.

NI DALILI GANI ZINAKUSUMBUA?
Unapata shida wakati wa kujisaidia (Choo kigumu).

Unaona damu wakati wa haja kubwa.

Unasikia gesi tumboni mara kwa mara.

Kuna vinyama vinavyotokea katika njia ya haja kubwa vikisababisha maumivu makali.

KWA NINI UCHAGUE TIBA YETU?
Tumeandaa matibabu ya kisasa na salama yanayokusaidia kupona haraka na kurejea katika hali yako ya kawaida ndani ya SIKU 7 TU.

✅ TIBA ASILIA NA SALAMA: Tunatumia dawa za mimea na tiba lishe zilizothibitishwa.

✅ HAKUNA UPASUAJI, HAKUNA MAUMIVU: Matibabu yetu hayahitaji vyombo vya upasuaji wala maumivu makali ya kupona.

✅ MATOKEO YA HARAKA: Unaona mabadiliko ya kweli ndani ya wiki moja tu.

✅ HUDUMA YA SIRI KABISA: Tunatambua faragha ni haki yako, hivyo huduma zetu zote zinafanyika kwa usiri wa hali ya juu.

Usisubiri tatizo liwe sugu! Chukua hatua sasa ili uishi bila maumivu na uweze kufurahia maisha yako kikamilifu.

📞 PATA MATIBABU SALAMA NA UHAKIKA SASA!
Tupigie au tuma ujumbe kupitia

WhatsApp kwa namba: 0612335079.

31/07/2026

JE, UNASUMBULIWA NA BAWASILI NA UMECHOKA KUVUMILIA MAUMIVU? USIKUBALI KUPOTEZA FURAHA YAKO YA MAISHA KWA SABABU YA KERO HII! �

Bawasili sio ugonjwa wa kuficha wala wa kuishi nao kwa mazoea. Wengi wetu tunapitia maumivu makali, choo kigumu, na hata kutoka damu bila kujua kuwa kuna suluhisho la kudumu na salama bila kuhitaji upasuaji wa aina yoyote.

NI DALILI GANI ZINAKUSUMBUA?
Unapata shida wakati wa kujisaidia (Choo kigumu).

Unaona damu wakati wa haja kubwa.

Unasikia gesi tumboni mara kwa mara.

Kuna vinyama vinavyotokea katika njia ya haja kubwa vikisababisha maumivu makali.

KWA NINI UCHAGUE TIBA YETU?
Tumeandaa matibabu ya kisasa na salama yanayokusaidia kupona haraka na kurejea katika hali yako ya kawaida ndani ya SIKU 7 TU.

� TIBA ASILIA NA SALAMA: Tunatumia dawa za mimea na tiba lishe zilizothibitishwa.

� HAKUNA UPASUAJI, HAKUNA MAUMIVU: Matibabu yetu hayahitaji vyombo vya upasuaji wala maumivu makali ya kupona.

� MATOKEO YA HARAKA: Unaona mabadiliko ya kweli ndani ya wiki moja tu.

� HUDUMA YA SIRI KABISA: Tunatambua faragha ni haki yako, hivyo huduma zetu zote zinafanyika kwa usiri wa hali ya juu.

Usisubiri tatizo liwe sugu! Chukua hatua sasa ili uishi bila maumivu na uweze kufurahia maisha yako kikamilifu.

� PATA MATIBABU SALAMA NA UHAKIKA SASA!
Tupigie au tuma ujumbe kupitia

WhatsApp kwa namba: +255612335079

Address

Tumaini Letu Hospital
Mbeya

Opening Hours

09:00 - 17:00

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tumaini letu hospital posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share

Category