PriBon Herbs

PriBon Herbs Karibu ujipatie Ushauri, Elimu na Tiba Lishe za Kibingwa kutokana na Teknolojia za Kisasa za Stemcell

24/12/2022
Ina tia moyo sana kuona sasa unarudisha tabasamu lako k**a ilivyo kuwa awali, hongera kwa matokeo mazuri na tunashukuru ...
22/12/2022

Ina tia moyo sana kuona sasa unarudisha tabasamu lako k**a ilivyo kuwa awali, hongera kwa matokeo mazuri na tunashukuru kwa mrejesho wako....

ELIMU KUHUSU FIGO NA KAZI ZAKE:○ Umbo la figo/structure Figo ni miongoni mwa viungo muhimu vya mwili wa binadamu. Kukosa...
08/12/2022

ELIMU KUHUSU FIGO NA KAZI ZAKE:

○ Umbo la figo/structure

Figo ni miongoni mwa viungo muhimu vya mwili wa binadamu. Kukosa kufanya kwake kazi kunaweza kusababisha magonjwa mazito na hata mauti. Figo limejengwa kwa viungo vingi na kazi zake ni nyingi.

Kazi zake mbili muhimu ni: kutoa uchafu unaoathiri mwili na wenye sumu na kuweko usawa wa maji (fluids), madini and kemikali.

Figo hutoa mkojo kwa kutoa uchafu wenye sumu na maji zaidi kutoka mwilini. Mkojo unaotengenezwa katika figo hupitia kwenye mrija uitwao” ureta, na huteremka hadi kwenye kibofu (bladder) na mwisho hutoka kupitia mrija wa urethra.

• Watu wengi (waume kwa wake) wana figo mbili.

• Figo ziko sehemu ya juu na nyuma ya tumbo, pande zote za uti wa mgongo (tazama mchoro) zinakingwa zisiathiriwe na mbavu za chini.

• Figo huwa ndani kabisa mwa tumbo kwa kawaida mtu hawezi kuzihisi.

• Figo ni viungo jozi ya umbo la aragwe lenye urefu wa sentimita 10, upande wa sentimita 6 na wembamba wa sentimita 4. Uzito wake ni kati ya gramu 150 – 170.

• Mkojo unaotengenezwa kwenye figo huteremka hadi kwenye kibofu kupitia kwenye ureta.

• Ureta ina urefu wa karibu sentimita 25 umbo la mrija uliotengenezwa kwa misuli ya kipekee.

Muundo na kazi ya figo ni sawa katika sehemu ya viungo vya kiume na k**e.

• Kibofu ni kiungo chenye mwanya kilichoundwa kutokana na misuli inayolala.Kibofu kipo chini na mbele ya tumbo na ni stoo ya mkojo kwa muda. Chini na ndani mwa tumbo. Huwa k**a mbwawa la mkojo.

• Kibofu cha mtu mzima huweza kubeba 400 – 500 mililita ya mkojo na iwapo kimejaa karibu pomoni, mtu, hujisikia kwenda kukojoa.

• Mkojo kwenye kibofu hutolewa kupitia urethra wakati wa kukojoa. Kwa wanawake, urethra yao ni fupi ilihali ni ndefu kwa wanaume.

○ Kwa nini figo ni muhimu kwa mwili?

• Sisi hula vyakula vingi na tofauti kila siku.

• Kiwango cha maji, chumvi na tindi kali (acids) katika miili yetu hutofautiana.

• Ile hali inayoendelea ya kubadilisha chakula ili kilete nguvu hutoa vitu/sumu mwilini.

• Vitu hivi husababisha utofauti wa kiwango c tindi kali (acids) mwilini. Huu mkusanyi isiyohitajika huweza kuhatarisha maisha.

• Figo hubeba kazi muhimu sana ya kusafish vyenye sumu, tindi kali(acid) ya sumu na vi materials) hufanya hivyo wakati huo huo i kuhakikisha usawa wa kiwango cha maji, el cha tindi kali (acid base).

○ Kazi za figo ni zipi?

Kazimuhimu ya figo ni kutengeneza mkojo na huondoa vitu visivyofaa, chumvi chumvi ya ziada mwilini.

Kazi muhimu za figo zimeelezwa hapa chini.

1. Kutoa uchafu Kusafisha damu kwa kutoa uchafu ni kazi muhimu sana ya figo. Vyakula tunavyokula huwa na protini. Protini ni muhimu kwa kukua na kurekebisha mwili. Lakini jinsi protini invyotumika na mwili hutoa uchafu. Mkusanyiko wa uchafu huu ni k**a sumu kwenye mwili. Figo huchuja damu na uchafu hatari (wa sumu) na hutolewa katika mkojo. zimeshindwa, kiwango cha creatine na urea kitakuwa juu katika uchunguzi wa damu.

Creatinine na urea ni aina mbili muhimu ya uchafu ambao kiwango chake katika mwili wa binadamu huweza kupimika.Kiwango chake katika damu huonyesha jinsi figo zinavyofanya kazi Iwapo figo zote mbili.

2. Kutoa maji(fluid) mengi

Kazi ya pili muhimu ya figo ni kulinganisha fluid kwa kutoa maji zaidi k**a mkojo na kubakiza kiwango muhimu cha maji katika mwili. Kwa hivyo figo huweka kiwango kamili cha maji yanayohitajika katika mwili.

Figo zinaposhindwa, hushindwa kutoa maji zaidi k**a mkojo. Maji mengi mwilini huchangia kuvimba kwa mwili.

3. Kusawazisha madini na kemikali

Figo hufanya kazi nyingine muhimu ya kusawazisha madini na kemikali k**a sodium, potassium, hydrogen, calcium, phosphorus, magnesium na bicarbonate na husawazisha kiwango kamili cha fluid kwenye mwili. Kubadilika kwa kiwango cha sodium uweza athiri fahamu ilhali kubadilika kwa kiwango cha potassium huweza kuwa na madhara makubwa kwa mapigo ya moyo na kufanya kazi kwa mishipa. Kuweka kiwango sawa cha calcium na phosphorus ni muhimu kwa afya ya mifupa na meno.

4. Kuchunga Shinikizo la damu

Figo hutoa hormoni mbalimbali (rennin, angiotensin, aldosterone , prostaglandin ….nk) na kusawazisha maji na chumvi kwenye mwili ambayo hufanya kazi muhimu kwa kulinda msukumo wa moyo. Usumbufu wa kutoa hormoni na kusawazisha chumvi na maji kwa mgonjwa mwenye ugonjwa wa figo uongeza msukumo wa damu kwenye moyo ( shinikizo la damu / high blood pressure).

5. Uzalishaji wa chembechembe za damu nyekundu

Erythropoietin inayotolewa kwenye figo hufanya kazi muhimu katika kutoa chembechembe za damu nyekundu (RBC).Figo likishindwa husababisha figo hilo kutoa erythropoietin kidogo ambayo baadaye husababisha kupungua kwa RBC na matokeo yake huwa hemoglobin kidogo (anemia).

Kwa sababu ya kutoa erythropoietin kidogo kwa wagonjwa ambao wana shida ya kushindwa kwa figo, hemoglobin haiwezi kuongezeka hata k**a itaongezewa kwa madini ya chuma na vitamin.

6. Kuendeleza mifupa yenye afya

Figo hubadilisha vitamin D katika hali yake ya kutumika, ambayo n muhimu kwa kunyonya calcium kutoka kwenye chakula, kukua kwa mifupa na meno na kuweka mifupa yenye afya. Katika hali ya figo kushindwa kufanya kazi,na kwa sababu ya upungufu wa vitamin D kunafanya kukua kwa mifupa kunapunguzwa na kuwa hafifu. Kushindwa kukua inaweza kuwa ishara ya kwanza kwa watoto walio na shida ya kushindwa kwa figo.

○ Damu inasafishwa vipi na mkojo kutengenezwa?

Katika harakati ya kusafisha damu, figo husalia na vitu muhimu na kwa huchagua kutoa maji yaliyozidi zaidi, madini na uchafu wowote Ni muhimu tuelewe mbinu muhimu na ya kushangaza ya kutengeneza mkojo.

• Je wajua? Kila dakika ml 1200 ya damu huingia katika figo zote kwa kusafishwa, ambayo ni asilimia 20% ya damu yote inayosukumwa na moyo. Kwa hiyo kwa siku lita1700 ya damu inasafishwa!

Kazi kuu ya figo ni kutoa uchafu na vitu hatari na maji yakupindukia kutengeneza mkojo.

• Njia hii ya kusafisha mwili hutokea katika vitu vidogo vya kuchuja vinavyojulikana k**a nephron.

• Kila figo huwa na karibu na nephron million moja. Kila nephron imeundwa na glomerulus and tubules.

• Glomeruli ni vichungi na mashimo madogo madogo sana yenye sifa ya kuchuja kwa kuchagua. Maji na vitu vidogo huwa rahisi kuchujwa. Lakini chembechembe kubwa za damu nyekundu, chembechembe za damu nyeupe, platelets, protini n.k haviwezi kupita katika mianya hii. Kwa hivyo katika mkojo wa watu wenye afya hakuna vitu vikubwa katika mkojo wao.

• Hatua ya kwanza ya kutengeneza mkojo hufanyika katika glomeruli, ambapo 125 ml za mkojo hutolewa kwa dakika. Ni jambo la kushangaza kuwa kwa saa 24, lita 180 ya mkojo imetengenezwa! Haina uchafu pekee, madini na sumu lakini hata glucose na vitu vingine muhimu.

• Figo hufanya kazi ya kunyonya kwa uerevu mkubwa mno. Kutokana na lita180 za maji ambayo huingia kwenye tubules asilimia 99% ya maji hunyonywa na asilimia 1% tu hutolewa k**a mkojo.

• Katika njia hii erevu vitu vyote muhimu na lita 178 ya maji yananyonywa na vijishipa na kati ya lita1-2 ya maji, vitu vichafu, madini zaidi na vitu vingine hatari hutolewa.

• Mkojo uliotengenezwa kwenye figo huteremka kupitia ureta hadi kibofu cha mkojo (urinary bladder) na baadaye kutoka nje kupitia urethra.

Je kunaweza kuwa na tofauti ya kipimo cha ujazo cha mkojo kwa mtu mwenye figo lenye afya?

• Ndio. Kiwango cha kunywa maji na hali ya hewa (atmospheric temperature) ni sababu kuu ambazo huamua kiwango cha mkojo kwa mtu mzima.

• Iwapo kiwango cha maji yaliyonywewa ni kidogo,huwa kidogo, mkojo huwa na vitu vingi vya chumvichumvi (concentrated), na kiwango cha chinihuwa karibu 500ml. Lakini maji mengi yakinywewa, mkojo mwingi unatengenezeka.

• Wakati wa jua (summer) kwa sababu ya joto na kutoa jasho nyingi kipimo cha mkojo hupungua. Wakati wa baridi (winter) hali ni tofauti – kiwango cha joto ni cha chini,hakuna kutokwa na jasho, mkojo huwa mwingi.

• Kwa mtu anayekunywa kiwango cha maji kinachofaa, na iwapo kipimo (volume) cha mkojo anaokojoa ni chini ya 500ml lakini zaidi ya 300ml ni ishara tosha kuwa figo inahitaji uchunguzi.wa haraka.

⚠️ Kiwango kidogo sana au kingi sana cha mkojo kutengenezwa, huashiria kuwa figo yataka kuangaliwa na kuchunguzwa.

Cc: Kidney Education Foundation.

Wasiliana nasi: 0739 522 352 au 0626 522 352.

HII NI KWA WANAWAKE: Tatizo unalopitia tambua wewe sio wa kwanza, na pia changamoto yoyote inayo suluhisho na wahenga wa...
05/12/2022

HII NI KWA WANAWAKE:

Tatizo unalopitia tambua wewe sio wa kwanza, na pia changamoto yoyote inayo suluhisho na wahenga walisema hakuna lenye mwanzo lisilo na mwisho.

Wengi wamepitia changamoto za kiafya na pasipo kupata utatuzi wa kitaalamu wamejikuta tatizo limekuwa kubwa na mwisho kuwasababishia majonzi na changamoto lukuki.

Sasa Leo nakuletea bidhaa ya Tiba Lishe yenye majibu kwa maradhi ya wanawake. Ndio ni WomenPlus, bidhaa iliyotengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Stemcell au seli shina ambazo zinafanya kazi ya kushughulika na chanzo cha tatizo na kuimarisha kinga, unaweza kusema ni "kinga smart" inashughulikia tatizo husika mwilini. Vilevile kuna Ayurveda ambayo ni mfumo wa matibabu kutoka barani Asia hususani nchini India.

WomenPlus inafanya kazi gani mwilini?
• Inaimarisha Kinga ya mwili kwa ujumla kwani ina vitamins, madini na virutubisho mbalimbali kutoka kwenye matunda mekundu na kijani.

• Inakinga na kutibu Matatizo ya Uzazi kwa mwanamke.

• Inakinga na kuzuia changamoto ya kuporomoka au kutoka mimba.

• Inapambana na changamoto ya ukosefu au kuvurugika kwa hedhi, maumivu kabla ya hedhi (Premenstrual Syndrome) kunakotokana na tatizo la hormone imbalance.

• Changamoto ya kutokushika mimba (ugumba) na kuweza kurejesha tabasamu tena.

• Vimbe kwenye kizazi.

• U.T.I sugu na Changamoto za P.I.D.

• Maambukizi ya bacteria wabaya ukeni.

Na maradhi mengine yanayowakabili wanawake.

BEI: 89,000 tu kwa Box moja ya WomenPlus Dietary Supplement.

WASILIANA NASI: 0626 522 352 au 0739 522 352 au 0692 522 352, Upate Ushauri na Msaada wa haraka.

TOFAUTI YA UTASA NA UGUMBA NA SABABU ZA KUTOSHIKA MIMBA. Ni muhimu leo kuzungumzia eneo hili nyeti kwenye mahusiano na A...
05/12/2022

TOFAUTI YA UTASA NA UGUMBA NA SABABU ZA KUTOSHIKA MIMBA.

Ni muhimu leo kuzungumzia eneo hili nyeti kwenye mahusiano na Afya, Tunapaswa kuelewa kipimo cha Utasa na Ugumba, maana zao hasa na suluhisho.

● Tuanze na Hali ya kuwa Tasa (Utasa).

Wanandoa husemekana kuwa tasa ikiwa watashindwa kupata mimba baada ya kushiriki ngono mara kadhaa kwa mwezi kwa muda wa mwaka mmoja, bila kutumia mbinu yoyote ya kupanga uzazi. Wanandoa hawa pia wanaweza kuwa na shida ya utasa ikiwa takribani mimba 3 au zaidi zimeharibika mfululizo.

Mwanaume au mwanamke ambaye tayari ameshapata mtoto pia anaweza kuwa tasa. Anaweza kupatwa na shida kati ya wakati ule alipata mtoto na sasa. Wakati mwingine shida hii haitokani na mwanamke au mwanaume bali ni mchanganyiko wa pande zote mbili. Wakati mwingine wanandoa hawana afya nzuri na hakuna daktari au uchunguzi wowote unaoweza kuonyesha kinachosababisha shida hii.

● Hali ya Kuwa Mgumba ni nini?.

Hii hutokana na wanandoa kushindwa kusababisha ujauzito ndani ya kipindi tarajiwa (hawa ni wale wasiotumia njia yoyote ya uzazi wa mpango) Mgumba anaweza kupata mtoto ila kuna kuchelewa, au kupata na usipate tena.

• KUNA AINA 2 ZA UGUMBA:

1. UGUMBA MSINGI. NI ugumba ambao wanandoa hawajawahi kupata mimba baada ya angalau mwaka 1 kufanya ngono bila kutumia njia za kudhibiti uzazi.

2. UGUMBA SEKONDARI.
Ni ugumba ambao huwapata wanandoa walioweza kupata mimba angalau mara moja, lakini sasa hawawezi.

Baada ya kufahamu utofauti huu, hebu tuone visababishi vinavyopelekea changamoto hizi:

Visababishi vya mwanamke kushindwa kupata ujauzito.

1. Mayai kushindwa kupevuka.

Hili ni tatizo ambalo huwakumba wanawake kwa kiwango cha asilimia arobaini kwa hiyo

mayai yakishindwa kupevuka usababisha kuwepo kwa ugumba.



2. Maambukizi sugu ya PID.

Kwa sababu ya kuwepo kwa maambukizi ya PID usababisha sehemu mbalimbali za via vya uzazi kuziba na kushindwa kuruhusu mayai kupita kwa ajili ya urutubishaji.



3. Mvurugiko wa homoni.

Na lenyewe hili ni tatizo kubwa ambapo homoni uweza kuongezeka au kupungua kwa hiyo k**a ni homoni za uzazi zikapungua ni shida na ikiwa zikaongezeka na nalo ni tatizo jingine kwa hiyo homoni zinapaswa kulinga kabisa na kuwa sawia.



4. Kuwepo kwa uvimbe au maji maji kujaa kwenye sehemu ya kupitisha mayai.

Kuna wakati mwingine mirija ya kupitisha mayai inaweza kujaa maji maji au kwa wakati mwingine kuziba kabisa kwa sababu ya kuwepo kwa kiwango kikubwa cha maambukizi , kwa hiyo mayai hayawezi kupita kutoka kwenye ovaries na kuingia kwenye mirija kwa ajili ya urutubishaji.



5. Au wakati mwingine Kuna wakati panakuwepo na uvimbe , na pia uvimbe huo hauwezi kuruhusu mayai kupita kutoka kwenye ovaries mpaka kwenye mirija ya urutubishaji mpaka uvimbe huo kuondolewa ndipo mayai yanaweza kupita kwa ajili ya urutubishaji.



6. Mayai kuharibika kabla ya umri.

Kuna wakati mwingine mayai yanaweza kuwepo kabisa na ya kutosha na kwa sababu ya kuwepo kwa maambukizi mayai hayo uharibika kabla ya umri wake hali ambayo usababisha kuwepo kwa kiwango kikubwa cha ugumba kwa akina Mama kwa hiyo matibabu ni lazima Ili kuweza kuzuia maambukizi ya nayosababisha kutokomaa kwa mayai.



7. Kuwepo kwa matatizo au asidi nyingi kwenye mlango wa kizazi na uke .

Kwa sababu asidi ya kwenye uke uwa ni ya kawaida kwa ajili ya kuruhusu mbegu kupita na kurutubisha mayai Kuna wakati asidi inakuwa nyingi na kusababisha kuuua megu za kiume kabla hazijaendea kurutubisha mayai.



8. Kuwepo kwa makovu kwenye mji wa mimba.

Kuna wakati mwingine kunakuwepo na makovu kwenye mji wa mimba hali ambayo usababisha mimba kutoweza kutungwa kwa sababu ya kutokuwepo sehemu ya kutungwa.





9. Kulegea au kuziba kwa shingo ya kizazi.

Kuna wakati kunakuwepo kwa tatizo la kulegea na kuziba kwa shingo ya kizazi hali ambayo usababisha mimba bkushindwa kutungwa.



10. Uzito wa kupita kiasi.

Kwa sababu ya kuwepo kwa kiwango kikubwa cha mafuta mwilini usababisha kitendo cha urutubishaji kuleta shida na kusababisha ugumba, kwa hiyo akina Mama wenye uzito wa kupita kiasi ni vizuri kabisa kupunguza Uzito na kupata uja uzito.



11. Unywaji wa pombe kupita kiasi na uvutaji wa sigara kupita kiasi.

Kuna akina Mama wenye tatizo la kuvuta sigara kupita kiasi na kupiga pombe ya uhakika hali ambayo usababisha baadhi ya homoni kushindwa kufanya kazi vizuri na hatimaye kuwepo kwa ugumba.



12. Magonjwa sugu katika mfumo wa upumuaji.

Kwa kawaida Kuna tatizo la magonjwa sugu katika mfumo wa upumuaji nayo uharibu ubora wa mayai na mzunguko wa damu kwa hiyo ni vizuri kabisa kutibu magonjwa haya kabla hayajaleta matatizo.

Ukweli ni kuwa changamoto hizi zinahitaji kutatuliwa kwa kubadili mtindo wa maisha na kupata usaidizi wa kitaalamu, mfano dawa nk

Pia lishe ni muhimu ndio maana kwa kutambua changamoto zinazotukabili k**a wanawake imetupasa kutafuta suluhisho kupitia bidhaa za Tiba Lishe ili kurejesha kile kilichopungua au kukosekana kabisa.

Tiba ya kupambana na hali ya Ugumba ipo, Unaweza kurejesha matumaini ya Kuitwa Mama na Baba.

Tuwasiliane kupitia 0626 522 352 au 0692522352 au 0739522352 kwa msaada zaidi.

FAHAMU DALILI ZA SARATANI YA TEZI DUME. Watu wengi wamekuwa wakidhania kuwa tezi dume ni busha ama ngiri maji kwa jina j...
04/12/2022

FAHAMU DALILI ZA SARATANI YA TEZI DUME.

Watu wengi wamekuwa wakidhania kuwa tezi dume ni busha ama ngiri maji kwa jina jingine. Hapana hii sio sahihi kabisa. Mpenzi msomaji tambua kuwa tezi dume sio busha na haifanani kabisa na busha. Tezi dume isipotibiwa kwa haraka inaweza kuwa hatari sana kwani ina maumivu makali sana. Sasa tezi dume ni nini hasa?. katika makala hii nitakwenda kukupa mwangaza kuhusu tezi dume., dalili za tezi dume na athari za tezi dume kwa afya yako.

Nini maana ya tezi dume
Tezi hii kitaalamu hufahamika k**a prostate gland. Hii ni tezi inayopatikana katika mfumo wa uzazi wa kiume. Tezi hii inapatikana jirani na kibofu cha mkojo na mirija ya mkojo. Tezi hii ina kazi ya kuzalisha majimaji ambayo hubeba mbegu za kiume. Majimaji haya ndio yale anayotoa mwanaume anapofikia kilele. Hivyo tezi hii ni muhimu sana katika mfumo wa kizazi wa mwanaume. Tezi hii si kubwa saana inapata sentimita zisizozidi 5. lakini tezi hii hukuwa kadiri umri unavyoenda.

Kwa ufupi wa maneno ni kuwa tezi dume ipo chini ya kibofu karibu na shingo ya kibofu. Na imezunguka mrija unaotoa mkojo kutoka kwenye kibofu kuja nje (urethra). hivyo mkojo unapotoka kwenye kipofu hupitia katikati kwenye tezi dume ukiwa kwenye mrija wa urethra. Urethra ndio mrija unaotoa mkojo kutoka kwenye kibofu.

Vipi ugonjwa wa tezi dume hutokea?
K**a ulivyojifunza hapo juu mkojo ukiwa kwenye mrija hupita katikati ya tezi tume. Sasa tezi hii ina kawaida ya kukua kadiri mtu anavyozeeka au umri kusonga - inakadiriwa kuanzia miaka 45 na kuendelea, ijapokuwa Afrika athari zimeanza kuonekana hata kwa watu wa umri kuanzia miaka 25 na kuendelea. Hivyo basi kadiri tezi hii inapoongezeka ukubwa ndivyo inavyoanza kuminya mirija ya kupitisha mkojo na hatimaye huanza tatizo la ugonjwa wa tezi dume. Tatizo hili kitaalamu hufahamika k**a Benign Prostatic Hyperplasia (BPH).

Nini sababu za kutokea kwa tezi dume?
K**a ilivyokwisha kutajwa hapo juu, tezi hii hukua kadiri mtu anavyokuwa. Kwa baadhi ya watu inapokua huwa kubwa kiasi cha kuanza kuminya mirija ya mkojo na kuleta shida kwenye mfumo wa mkojo. Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa miongoni mwa mambo yanayohatarisha uwezekano wa kupata ugonjwa huu ni haya yafuatayo:-

1.Umri, kwa kawaida tezi dume huwapata watu wenye umri kuanzia miaka 40. ni mara chache sana kuwapata walio chini ya umri huo. Pia tezi dume kwa kiasi kikubwa huwapata walio kati ya miaka sitini na kuendelea. Hususani robo tatu ni wale walio na miaka kuanzia 60,na nusu yao ni wale walio na miaka kuanzia 80.

2.Tatizo la tezi dume pia huweza kurithiwa. Yaani k**a baba yako ana tezi dume ama yeyote katika damu yako hapo mwanzo alikuwa na tezi dume, hivyo upo uwezekana na wewe kurithi tatizo hili.

3.Pia inaonekana kuwa baadhi ya rangi huathiriwa sana na tatizo la tezi dume. Tafiti zinaonesha kuwa watu walio katika bara la Asia si sana kupatwa na tezi dume kuliko watu weusi na wazungu. Hata hivyo kwa watu weusi upo uwezekano wa kupatwa na tatizo hili katika umri mdogo kuliko wengine.

4.Maradhi, tafiti zinaonyesha kuwa kuna baadhi ya maradhi huweza kupelekea kupatwa na tatizo la tezi dume. Kwa mfano watu wenye maradhi ya sukari, na maradhi ya moyo wapo hatarini kupatwa na tezi dume ukilinganisha na watu wengine.
5. Mtindo mbovu wa maisha. Tafiti pia zinaonyesha kuwa watu wenye kiribatumbo na wasiofanya mazoezi wapo hatarini kupatwa na tatizo la tezi dume.

Ni zipi dalili za ugonjwa wa tezi dume?
Dalili za tezi dume zinaweza kuwa kali ama hafifu kutoka mtu hadi mtu. Ukali wa dalili hizi hautegemei ukubwa wa tezi. Inaweza kuwa tezi ni kubwa lakini dalili zisiwe kali. Miongoni mwa dalili za tezi dume ni:-

1.Kukojoa mara kwa mara, ama kuhisi kukojoa mara kwa mara
2.Kukojoa mara kwa mara wakati wa usiku
3.Kupatwa na ugumu kutoa mkojo.
4.Mruko wa mkojo kuwa dhaifu.
5.Mkojo kukatakata unapofika karibu na mwisho.
6.Kujichafua wakati wa kukojoa.
7.Kushindwa kumaliza mkojo kabisa.
8.Damu kwenye mkojo.
9.Kushindwa kukojoa kabisa.
10.Kupata mkojo mchache sana.

Kuwa na dalili tajwa hapo juu pekee hakuwezi kukupa uhakika kuwa una tatizo la tezi dume. Kwani dalili tajwa hapo juu zinaweza kuambatananna shida nyingine za kiafya kwa mfano:-
1.Maambukizi ya UTI
2.Kuvimba kwa tezi
3.Kupunguwa ukubwa wa mrija wa mkojo
4.Kuwepo na vijiwe kwenye kibofu.
5.Kuwa na shida kwenye mfumo wa neva ambazo hudhibiti ufanyaji kazi wa kibofu.
6.Kuwa na saratani.
7.K**a upasuaji katika kibofu haukufanyika sawa.

Ni zipi athari za tezi dume k**a haitawahi kutibiwa?

Tezi dume ni k**a maradhi mengine, inatibika bila wasi. Hata hivyo endapo matibabu yatachelewa athari zifuatazo zinaweza kupatikana:-
1.Kushindwa kabisa kukojoa.
2.Kupatwa na maambukizi ya UTI.
3.Kupatwa na vijiwe kwenye kibofu.
4.Uharibifu wa kibofu unaweza kutokea.
5.Figo inaweza kuharibika.

Mwisho
Napenda kumaliza kwa kusema kuwa tatizo la tezi dume linatibika bila wasiwasi, mfano kwa upasuaji japo kuna athari zake na hapa ni ikiwa tatizo limekuwa kubwa, lakini kuna virutubisho lishe kwa ajili ya kujenga mwili na kuupa madini na vitamins muhimu hasa vitamin D. Usisite kuwasiliana nasi kwa msaada zaidi:
0626 522 352 au 0739 522352 na 0692 522352.

Pia endelea kutufuatilia kwa makala nyingine za Afya.

SABABU ZA MARA KWA MARA ZINAZOPELEKEA KUKOSA HEDHI NA KUVURUGIKA KWA MPANGILIO WA HEDHI:Ukiachilia mbali ujauzito na kuk...
02/12/2022

SABABU ZA MARA KWA MARA ZINAZOPELEKEA KUKOSA HEDHI NA KUVURUGIKA KWA MPANGILIO WA HEDHI:

Ukiachilia mbali ujauzito na kukoma hedhi ambavyo vyote hivi ni vipindi vya kawaida kwa mwanamke kukosa hedhi. Zifuatazo ni sababu ambazo hupelekea mwanamke kukosa hedhi

1.Msongo wa Mawazo

Kikawaida mwili unapokutana na kitu cha kuogofya ama kinacholeta msongo wa mawazo unatunza nishati kubwa ili kuzielekeza kupambana na changamoto iliyopo mbele yako. Kwa hivo kila mara unapokuwa na msongo wa mawazo utendaji wa shuguli zingine za mwili unapungua na kudhoofika ikiwemo upevushaji wa mayai.

Homoni ya estrogen inapozalishwa kwa kiwango kidogo pamoja na homoni zingine k**a homoni ya LH na FSH ukuta ambao humeguka kila mwezi kutoka pamoja na yai hautajengwa na hivo kupelekea ukose hedhi.

kwanini mwili unapunguza kasi ya upevushaji wa mayai wakati wa msongo wa mawazo?

Mwili unatambua kwamba upo kwenye kipindi cha hatari na unatakiwa upambane ili uishi kutokana na hatari inayokuwa mbele kwa hivo maisha ni kitu cha kwanza ndipo swala na hedhi lifuate. Mwili utatengeneza stress homoni kwa wingi k**a cotisoli na adrenalini ili kukuandaa kupambana, ama kukimbia hatari iliyopo mbele yako.

Fikiria pale unapotembea usiku na ukaona kitu kisicho cha kawaida mbele yako, tazama mwili unavobadilika, sasa mabadiliko ya homoni pale unapokutana na kitu cha hatari ni sawa na vile unapopata msongo wa mawazo. Kadiri mawazo yanavokuathiri ndipo unaharibu mpangilio wako wa mwili na kukupelekea ukose hedhi.

2.Lishe Mbaya

Lishe mbaya yenye upungufu wa virutubisho ikiwemo vitamini na madini na yenye sukari na viambata vya kuongeza ladha kwa wingi hupelekea tezi za Adrenal na Thayroid kufaya kazi kupita kiasi. Kitendo hichi hupelekea uzalishaji wa kichocheo cha cotisoli ambacho kinapunguza uzalishaji wa homoni za uzazi.

Cortisol inapokuwa nyingi zaidi pia taweza kuletekeza madhara mwilini k**a udhaifu wa mifupa, ngozi kuharibika, tishu za ubongo na misuli kudhoofika. Kwahivo mtiririko huu unapojirudiarudia kila mara ndipo hali ya mwili huwa mbaya zaidi.

3.Uzito Mdogo Kupita Kiasi

Ili kupima uzito wako k**a uko sawa kiafya, tunatumia kipimo cha BMI yaani body mass index ni kipimo kinachotumika kupima uwiano wa uzito na urefu wako. BMI= Uzito wako kwa kg gawanya kwa (urefu kwa mita x 2). BMI kuanzia 18.5 mpaka 25 inaonesha kwamba uzito wako ni mzuri. Ukipata zaidi ya 25 manake uzito wako ni mkubwa na ukipata chini ya 18.5 ni kwamba una uzito mdogo kupita kiasi.

Mafuta mwilini huchochea uzalishaji wa homoni ya estrogeni kwa wanawake na ndio maana wanawake wembamba sana hukosa hedhi maranyingi zaidi. Kufanya mazoezi makali hupelekea mahitaji ya virutubisho mwilini kuongezeka na hivo uzito kupunguakupta kiasi na kuvurugika kwa homoni.

4.Kufanya Mazoezi Kupita Kiasi

Mazoezi ni muhimu kwa mwili katika kurekebisha athari za msongo wa mawazo, kuweka sawa shinikizo la damu, usingizi mzuri na kuweka sawa uzito wamo. Ila kumbuka kufanya mazoezi kupita kiasi kunachosha sana mwili kupelekea uzalishaji mkubwa wa cotisoli ambayo ndio kizuizi cha kuzalishwa kwa homoni za uzazi. Kwahivo hakikisha unafanya mazoezi mara 3 kwa week na yasiwe mazoezi yanayokula nguvu yako nyingi na kukuacha mdhaifu.

5.Matatizo Kwenye Tezi ya Thairodi.

Tezi ya thairodi ni kiungo chenye umbo la kipepeo. Kiungo hichi kipo kwenye shingo chini ya koromeo la sauti. kazi kuu ya Tezi hii ni kuzalisha homoni za (T3) na (T4), ambazo kwa pamoja hufanya kazi ya kurekebisha mzunguko wa damu na kazi mbalimbali za mwili. Matatizo kwenye tezi ya Thairodi k**a kushuka kwa uzalishaji wa homoni ama tezi kufanya kazi kupita kiasi huweza kuleta mabadiliko pia kwenye kiwango cha estrogeni na cotisoli. Kiwango cha cotisoli kwenye damu kinapokuwa kingi hupunguza uwezo wa tezi ya thairoidi ambapo matokeo yake ni kushuka kwa kazi za mwili k**a upevushaji wa mayai na uzalishaji wa homoni za k**e

6. Matumizi ya dawa za kupanga uzazi

Baadhi ya wanawake hukosa hedhi kwa muda mrefu baada ya kuacha kutumia vidonge vya uzazi wa mpango. Japo madactari hushauri kwamba hali itakaa sawa baada ya kuacha kumeza vidonge lakini bado hali huwa mbaya kwa wanawake wengine kwani tayari vidonge vimevuruga vichocheo. Kikawaida mpangilio wa hedhi unakuwa na kipindi cha kupanda na kushuka kwa homoni za estrogeni na progestene kwa kupishana, lakini vidonge vya uzazi wa mpango hufanya estrogeni kuwa juu muda wote na kuudanganya mwili kwamba una ujauzito wakati huna na hivo kukosa hedhi kabisa. Inachukua miezi ama miaka mingi mpaka mwili kurudi kwenye hali yake ya kawaida.

7.Ugonjwa wa PCOS

Polycyst ni wingi wa neno cyst, Neno cyst ni kitu chenye uwazi kwa ndani na kimezungushiwa ukuta mwembamba na laini (Membrane). Na mle ndani kunaweza kukaa damu,usaha,maji nk. kwa upande wa mwanamke hizo follicles nyingi ambazo zimekomaa na zimeshindwa kutoa mayai zinafanishwa na Cysts .Sasa inapotokea Kila mwezi hupati hedhi na vimbe hizi zinakuwa nyingi tunaziita Polycyst.

Na mkusanyiko wa dalili mbalimbali k**a uzito mkubwa na kitambi na kupanda kwa sukari kwenye damu.

Tunakupendekezea Tiba Lishe ya kurekebisha hedhi iitwayo WomenPlus.

WomenPlus imetengenezwa nchini Malaysia Kwa miaka miwili ambayo tumekuwa tukihudumia wagonjwa wetu wa matatizo ya hedhi na homoni, tumepokea shuhuda lukuki.

Baada ya kutumia WomenPlus tegemea kupata matokeo haya:

• Hedhi kutoka vizuri kwa siku chache siyo zaidi ya siku 4 ama 5.

• Maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi kuisha kabisa.

• Homoni kubalansi.

• Kupata hedhi nyepesi ya kawaida.

• Mzunguko wa hedhi kurekebika na kuanza kupata kila mwezi.

• Kizazi kuimarika sana hata kuongeza chansi ya kushika mimba k**a wewe ni muhanga wa kukosa mimba kwa muda mrefu.

WomenPlus inapatikana nchini Tanzania kwa Bei ya Tzs. 89,000 na Hii ni offer ya Mwezi December kwa wateja wetu 100 wa awali, tunafunguka mwaka kwa punguzo la bei la kipekee, kwa Wateja 100 Tu. Baada ya Hapo Bei itarudi 99,000 ya awali.

Mawasiliano ni: 0692522352 au 0626 522 352 au 0739522352.
DELIVERY: DODOMA DELIVERY NI BURE, MIKOANI TUNATUMA KWA GHARAMA ZAKO

Kwa heshima na taadhima, tunapenda kukupongeza  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dr. Samia Suluhu Hassan, PH...
01/12/2022

Kwa heshima na taadhima, tunapenda kukupongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dr. Samia Suluhu Hassan, PHD kwa kutunukiwa PHD hio. Tunatambua mchango wako kwenye Masuala ya Afya na pia intervention ya makusudi katika tiba lishe na rasilimali fedha ulizoruhusu Serikali kuwekeza kwenye eneo la Tafiti.

Uongozi wa PriBon Herbs tumekusudia kuunga mkono jitihada hizo kwa kuhakikisha jamii ya Watanzania na Wana Afrika Mashariki na Afrika kwa Ujumla wanapata huduma stahiki kwa kutoa Tiba Lishe zilizothibitishwa na Mamlaka za Kiserikali na zenye Viwango vya Kimataifa, ili tuwe huru na tuepukane na maradhi.

Kazi Iendelee.

Address

Lumumba Street, Lumumba Road
Morogoro

Opening Hours

Monday 07:35 - 19:35
Tuesday 07:35 - 19:35
Wednesday 07:35 - 19:35
Thursday 07:35 - 19:35
Friday 07:35 - 19:35
Sunday 07:00 - 12:00

Telephone

+255743777797

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when PriBon Herbs posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to PriBon Herbs:

Shortcuts

Share