05/09/2022
🎱 *vidonge vya kupanga uzazi*
🎱
👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿
🥏Maamuzi ya aina ya uzazi wa mpango unaotaka kutumia ni jambo binafsi. Japo muhudumu hospitalini atakupa elimu juu ya faida na hasara za kila njia, kazi yako ni kuchagua ipi itakufaa. K**a unafanya tendo la ndoa mara kwa mara, kuna umuhimu wa kutumia vidonge vya uzazi wa mpango ili usishike mimba isiyotarajiwa.
🥏 *Jinsi vidonge vya uzazi wa mpango*
👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿
🎱 vinavyofanya kazi
Vidonge vinafanya kazi kwa namna mbili. Moja vinazuia mayai kupevuka. Hii ina maana mifuko ya mayai haitatoa yai kwenye siku ya hatari, kwahivo hakutakuwa na yai la kurutubishwa na mbegu. Mbili Vidonge vinafanya uteute wa kwenye uke kuwa mzito sana. Ute mzito unazuia mbegu kuogelea na kwenda kurutubisha yai.
🥏 *Muda gani natakiwa kumeza vidonge* ????
👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿
🎱Ni muhimu kuendelea kumeza vidonge kila siku katika muda ule ule. Kupitisha hata masaa machache kunaweza kupelekea mayai yakapevuka na ukashika mimba (kikaumana)
🥏 *Ufanisi wa vidonge vya uzazi wa mpango ukoje?*
🎱K**a vikitumika ipasavyo, vidonge vinafanya kazi vizuri kuzuia mimba.
🎱ufanisi wa vidonge ni asilimia zaidi ya 91.
🧪Baadhi ya matibabu yanaweza kupunguza ufanisi wa dawa za uzazi wa mpango.
♟️Matibabu haya ni k**a👇🏿👇🏿👇🏿
🧩Baadhi ya antibiotics
🧩Dawa za Ukimwi k**a lopinavir na saquinavir
🧩Baadhi ya dawa za kifafa k**a carbamazepine na topiramate
🛝Dawa za uzazi wa mpango zinaweza kupunguza ufanisi pia kwa mgonjwa anayetapika na kuharisha.
🧪Endapo utakuwa na maumivu ya tumbo, zungumza na daktari akupime k**a uko kwenye hatari ya kushika mimba.
🧪 Unaweza pia kutumia njia nyingine k**a kondomu mpaka pale ukishapona.
🎱 *Zipi ni faida za kutumia vidonge vya uzazi wa mpango.*
Faida za vdonge ni pamoja na👇🏿👇🏿
🧩Kukukinga dhidi ya mimba isiyotarajiwa muda wowote unapofanya tendo
🧩Zinasaidia pia krekebisha mzunguko wa hedhi uliovurugika na hedhi nzito
🧩Siyo kizuizi cha moja kwa moja kushika mimba. Ukiamua kushika mimba unaacha tu kumeza vidonge.
🥳🥳🥳🥳🥳🥳🥳🥳