23/03/2026
DOKTA, HIVI KUNA KINGA YA PRESHA?😂😂
Ni swali nililowahi kuulizwa na mama mmoja aliyekuwa na hofu kubwa ya kuugua presha maana alikuwa ameondokewa na mpendwa wake kwa shida hii ya Presha.
Nilimjibu kwa urahisi, ndiyo, kuna namna tunaweza kujikinga na presha k**a hatutaki kuhakangika na kuja kutibu presha. HAKUNA CHANJO YA PRESHA, HILO ULIJUE!
Wengi waliokutwa na presha haikuanza tu ghafla, sometimes unaweza usione dalili ila ikawa ipo ingawa matokeo yanaweza yakaonekana ghalfa.
Yaani ni ghafla tu mtu anasikia mapigo ya moyo k**a hayaelewi. Ni ghafla anaona mwendelezo wa maumivu ya kichwa, ni ghafla mtu anaweza pata kiharuse (stroke). Hiyo hgafla unaweza ukawa ndo umeiona wewe ili msababishaji (presha) alikuwepo kitambo.
SASA KUEPUKANA NA HAYO YOTE, TUJITAHIDI KUFANYA HAYA, KWA SEHEMU KUBWA YATATUSAIDIA. Yapo mengi ya kufany, ila anza na haya ambayo hayana gharama. Najua umewahi kuyasikia, usiyadharau😂😂 leo utayaelewa vizuri yanavyosababisha presha.
✔ Punguza chumvi kwenye chakula chako.
Kuna wale tuliwahi kusema wekeni chumvi nyingi ili tunywe maji mengi hasa k**a chakula ni kidogo kutosha familia nzima 🤔. HIYO HAIKO KITAALAMU KABISA.
Kwanini uipunguze chumvi. Kwenye chumvi kuna madini ya Sodium, haya yana kazi nyingi mwilini ikiwa ni pamoja na kusafirisha taarifa mwilini katika mfumo wa umeme (nerve impulse transmission).
Sasa mbali na kazi hiyo nzuri, Sodium pia inayopatikana kwenye chumvi huwa inasababisha mwili ushikilie maji (water retention). Huwa Sodium ions zinasambaa kwenye damu. Zikiwa kwenye damu, damu inakuwa highly concentrated ( blood become more hypertonic than extracellular fluid). Kitendo ambacho kitasababisha maji yatoke kwenye seli zingine za mwili ili kwenda kupoza hicho kiwango kilichozidi kwenye damu na kuziacha cell za mwili zimenyauka(shrikns)
Sasa kuongezeka kwa maji kwenye damu maana yake ni volume(ujazo wa damu) inaongezeka, kwa hiyo damu inasukuma kuta za mishipa ya damu kwa nguvu hali ambayo hupelekea kuongezeka kwa presha.
KWAHIYO UNAWEZA KUONA, CHUMVI INAMCHANGO MKUUBWA KWENYE KUPANDISHA PRESHA. Kwa mwenye presha apunguze chumvi, kwa ambaye hana azuie chumvi nyingi.
✔ Fanya mazoezi
Aise, ni kakitu kadogo ila katatusaidia. Mazoezi yana namna nyingi yanavyoweza kupunguza au kuzuia shinikizo la damu.
**Mazoezi yanasaidia kuunguzwa kwa mafuta mwilini, hii hupelekea kulinda mishipa ya damu kwani mkusanyiko wa mafuta kwenye mishipa ya damu hautakuwepo. Kwa hiyo njia ya mishipa ya damu haitapungu (no atherosclerosis-arterial wall thickness). Matokeo yake Damu itasafiri bila kupata uzuizi/ upinzani na hivyo presha haitakuwepo. Hapo utakuwa umeulinda na moyo wako (Moyo hautatumia nguvu kubwa kusukuma damu)
**Pili Mazoezi yatasaidia kuifanya mishipa ya damu kupanuka vizuri. Mazoezi huifanya mishipa iwe yenye elasticity, kitendo kinachoifanya ipanuke vizuri. Mishipa inayovutika/kupanuka vzr hupunguza upinzani wa damu na hivyo nguvu kidogo kutumika kusukuma damu ikiwa na maana presha haipandi.
anakushauri ufanye mazoezi, mazoezi ni afya. Tumia angalau nusu saa kila siku asubuhi au jinoni, ukiweza asubuhi na jioni kutembea, kukimbia taratibu, kuruka kamba nk. Hapo presha yako utaidhibiti.
✔ Penda kula kiasili.
Kwa bahati mbaya sana utandawazi na umjini umetuathiri. ✍✍Mifumo mbalimbali ya mwili inakufa kwa kujazwa vyakula vyenye kemikali nyingi na madawa. Ni kweli ni vitamu😂 ila vyaku vyenye mafuta mengi k**a chips, vyakula vya kusindikwa, vinywaji vyenye sukari artificial ni adui wa mifumo mbalimbali ya mwili.
Tengeneza juisi yako mwenyewe kwa kutumia matunda asili na viungo asili k**a maparachichi, malimao, tangawizi, hoho, nk. Hivyo vitasaidia sana kuimalisha afya ya mfumo wa mzunguko wa damu na kukuepusha na presha. Si hivyo tu, vitakupa pia hata kinga dhidi ya magonjwa.
Tembea na silogani hii...MBOGA ZA MAJANI NI NYAMA INAYOOTESHWA, CHIPS INAYOOTESHWA, JUISI INAYOOTESHWA😁😁 ...hiyo itakusukuma kutumia mbogamboga asili badala ya vyakula hatarishi kwa afya yako.
✔ Jitahidi kudhibiti msongo wa mawazo.
Msongo wa mawazo ni msaidizi mkubwa sanaa wa presha kuinuka.
Mwili wa binadamu una hormone ya adrenaline na Cortisol. Hizi zikiongezeka zinapandisha presha. Sasa mazingira yanayoweza kuzipandisha hizo homoni ni pamoja na msongo wa mawazo. Msongo wa mazo ukiwepo huwa na zenyewe zinazalishwa sana, zikizalishwa sana mapigo ya moyo yanaongezeka (ndo pale mtu anakwambia nasikia moyo unakimbia😔). Nisiende mbali sana kueleza inavyokuwa nisikupoteze, ila mwisho wa yote mwendelezo wa hali hii ni presha kutokea.
EASY TO REMEMBER: Avoid stress, avoid hyper-secretion of stress hormones, avoid rapid heart rate, Avoid arterial flow resistance, avoid pressure
✔ Tumia dawa ipasavyo
Hii ni kwa wale ambao tayari walisha pima presha yao mara kadha na wahudumu wa afya na kufikia hitimisho la kuambiwa wana shida ya presha. Nimekutana na case nyingi, wengi wanakuja kujieleza kwa kutoa maelezo yanayotaka dakitari ajifunge kwa kuwaambia waache kutumia dawa. JIBU LANGU HUWA NI MOJA TU, TUMIA DAWA, UKIACHA UTAKUFA GHAFLA.
Nakushauri leo, usiache dawa mpaka daktari wako akupe maelekezo mengine. Dawa sahihi, matumizi sahihi, wakati sahihi zina nafasi kubwa sana ya kukufanya ubaki salama dhidi ya madhara yatokanayo na preshaa k**a Figo kuathirika, ubongo, moyo na kukuepusha na kiharusi (Stroke)
✔ Jenga mazoea ya kupima Presha yako.
Huu nao ni ustaarabu mzuri sana. Usipime presha baada ya kush*tuliwa na presha. Jiwekee utaratibu wa kupima presha mara kwa mara, angalu mara moja kwa mwezi (Kupima mara nyingi zaidi kuna salama)
NB. Hakikisha unapima kwenye kituo cha kutolea huduma za afya chenye wataalamu wanaoelewa kuhusu presha.
..Kwa sehemu anza hivyo, presha itakuwa mabali na wewe...
Dr. Buhanda na afya yako