30/06/2026
Habari za siku wadau?
Leo namalizia kwa kuwaeleza dawa za asili nne ambazo unaweza zitumia na zikapunguza kabisa tatizo lako la shinikizo lako la damu (HBP)
1.Chai ya Hibiscus
Kwa tafiti zilizofanyika tayari, chai hii ina uwezo wa kupunguza shinikizo la damu bila ya kuleta athari yoyote mwilini
2.Chai ya hamdalasini
Chai hii inasaidia kupunguza msongo unaoletwa na HBP na ina viini lishe vinavyosaidia kutanua mishipa ya damu.
3.Chai ya mvumbashi (Ocimum Suave au holly basil kwa kingereza)
Chai hii ina nyuzinyuzi nyingi na protini. Chai hii pia ina kemikali kiondoa sumu asilia mwilini inayoitwa eugenol (natural calcium channel blocker).
4.Kitunguu swaumu na Tangawizi
Kitunguu swaumu na tangawizi zilizokomaa vina uwezo mkubwa wa kupunguza shinikizo la damu (systolic na diastolic) kwa kuweka sawa mzunguko wa damu na kupunguza maumivu. Kitunguu swaumu ina kemikali inayoitwa allucin ambayo ina uwezo mkubwa sana wa kutanua mishipa ya damu
Dawa za asili hizi (Herbs) ukiambatanisha na mazoezi, chakula bora na tahadhali za mgonjwa wa shinikizo la damu, Mungu atakujalia na utaendelea kuishi kwa amani, furaha na afya tele.
Pia unakaribishwa kwa maswali, maoni na ushuhuda
ASANTENI