Lubonji Wa Lubonji

Lubonji Wa Lubonji L.W.L MUSIC & INTERNATIONAL NEWS

09/08/2026

MWAKA 2000, KOFFI OLOMIDE ALITAMKA WAZI KWAMBA WERRASON NDIYE NAMNAMBA MOJA ASIYEPINGIKA KINSHASA

EN L'AN 2000 KOFFI OLOMIDE DISAIT WERRASON EST L’INCONTESTÉ NUMÉRO UN DANS LA VILLE DE KINSHASA
Kwangu mimi, kazi hubaki kuwa kazi, na umri ni umri tu.
Watu wanapaswa kunielewa vizuri:
Kwa leo hii, katika pembe zote nne za jiji la Kinshasa, Werrason ndiye anayetawala jukwaa la muziki.

Wala Hakuna Mtu kabisa hakuna anayoweza kwa sasa kulingana au kupimana na Werra ndani ya Mji mkuu.

Tuseme mambo k**a yalivyo:
Kuanzia enzi za Vieux Rochereau hadi kwenye Group la Muziki linalo fanyia mazoezi kwenye barabara ya mitaa wangu, Werrason bado ndiye Namba Moja kwa sasa Jijini Kinshasa.

Kuhusiana na Bwana Mdogo JB, yeye ni mdogo wangu; sina tatizo lolote naye.
Lakini ukizungumzia umaarufu ndani ya Kinshasa, siku ya leo, jina linalotawala ni Werrason.
Na ingekuwaje k**a tungeamua tu kukubali ukweli huo k**a ulivyo bila kusita?

Pour moi, le travail demeure le travail, et l’âge n’est que l’âge.
Que l’on me comprenne bien :
Aujourd’hui, dans les quatre coins de Kinshasa, Werrason domine la scène.
Nul, absolument personne, ne peut actuellement se mesurer à Werra dans la capitale.
Disons les choses telles qu’elles sont :
Depuis le Vieux Rochereau jusqu’aux orchestres qui résonnent aujourd’hui dans les rues de ma ville, Werrason demeure le Numéro Un à Kinshasa.

Quant à Petit JB, il est mon cadet ; je n’ai aucun problème avec lui.
Mais en termes de popularité à Kinshasa, en ce jour, c’est Werrason.
Et que se passerait-il si nous l’admettions simplement ?

BABA L.W.L

09/08/2026

PALE WERRASON KAMUALIKA KOFFI OLOMIDE KWENYE SHOW
WERRASON AVAIT CONVIÉ KOFFI OLOMIDE À PARAÎTRE SUR SCÈNE
Mwaka 2005, kwenye Show yake kubwa lililofanyika Jijini Paris kwenye Ukumbi wa LSC, Werrason alimualika Koffi Olomide jukwaani, na tukio hilo likawa mojawapo ya matukio ya kukumbukwa katika historia ya Rumba ya Congo.
Waliimba kwa pamoja “Ngobila” na “Sisi Silvie”, nyimbo ambazo zimebaki kuwa alama ya Muziki wa kizazi hicho.

Show hiyo lilipamba moto zaidi kwa uwepo wa wakongwe wawili: Papa Wemba na Bozi Boziana, wageni wa heshima walioleta uzito wa kipekee na hadhi ya kifalme katika usiku huo wa muziki.
Ilikuwa ni siku ambayo mastaa wa rumba walikusanyika k**a ishara ya kuenzi urithi mkubwa wa Muziki wa Congo.

Version Française :
En 2005, lors de son mémorable concert au LSC de Paris, Werrason avait convié sur scène l’illustre Koffi Olomide, offrant au public un moment d’une rare intensité.

Ensemble, ils interprétèrent avec éclat «Ngobila» et «Sisi Silvie», deux pièces devenues emblématiques dans l’imaginaire musical congolais.

Cette soirée, déjà historique par son ampleur, fut sublimée par la présence de deux autres géants de la rumba : Papa Wemba et Bozi Boziana, invités d’honneur dont la stature artistique ajouta une dimension supplémentaire à l’événement.

Un instant suspendu, où les maîtres de la scène congolaise se sont retrouvés unis, comme pour célébrer la grandeur d’un patrimoine musical inépuisable.

BABA L.W.L

FALLY IPUPA Kwa mtazamo wake Fally Ipupa, balozi wa kisasa wa rumba ya Congo, Wasanii wafuatao ndio wanaoonekana kuwa bo...
09/08/2026

FALLY IPUPA

Kwa mtazamo wake Fally Ipupa, balozi wa kisasa wa rumba ya Congo, Wasanii wafuatao ndio wanaoonekana kuwa bora zaidi katika historia ya muziki wa Congo :
1. Koffi Olomide,
2. Papa Wemba,
3. Reddy Amisi,
4. Madilu Multi System,
5. King Kester Emeneya,
6. Benz Bozi Boziana.
Kila mmoja wao ameacha alama isiyofutika kupitia sauti, ubunifu na urithi wa kisanii unaoendelea kuishi vizazi baada ya vizazi.
Mjadala uko wazi, kwa maana ukubwa wa Wasanii hawa haupimwi kwa muziki pekee, bali kwa urithi wanaouacha.
Kadhalika kuna wengine wengi kasahau kuwataja.
Haya twende...

Version Française :
Selon la perspective de Fally Ipupa, figure majeure et ambassadeur contemporain de la rumba congolaise, les artistes ci-après incarnent ce que la musique du Congo a produit de plus noble et de plus mémorable :
1. Koffi Olomide,
2. Papa Wemba,
3. Reddy Amisi,
4. Madilu Multi System,
5. King Kester Emeneya,
6. Benz Bozi Boziana.

Chacun d’eux a laissé une empreinte indélébile : une voix singulière, une créativité foisonnante, un héritage artistique qui continue de traverser les générations et de nourrir l’imaginaire collectif.

Leur grandeur ne se mesure pas uniquement à travers leurs œuvres, mais dans la profondeur du patrimoine qu’ils ont légué.

Le débat demeure ouvert, car la constellation des Maîtres de la rumba est bien vaste, et nombre d’autres géants que l’on omet parfois de citer mériteraient également de figurer dans cette fresque d’excellence.
Le débat est ouvert

BABA L.W.L

FALLY IPUPA / HERITIER WATANABE WAKO STUDIOFALLY IPUPA / KERITIER WATANABE EN STUDIOFally Ipupa na Héritier Watanabe wam...
03/08/2026

FALLY IPUPA / HERITIER WATANABE WAKO STUDIO
FALLY IPUPA / KERITIER WATANABE EN STUDIO

Fally Ipupa na Héritier Watanabe wamekutana studio, katika mazingira yaliyojaa ubunifu na mvuto wa siri.
Mkutano huu wa wawili hao, ambao si wa kawaida na una uzito wa kipekee, unaashiria ujio kwa kazi Babkubwa, labda hatua mpya katika Muziki ambayo mashabiki wameisubiri kwa hamu kwa miaka mingi.

Wasanii hawa wawili, mabingwa wa urithi wa rumba ya kisasa, wanaonekana kutengeneza kitu chenye uzito, kilichosukwa kwa ustadi na kilichojaa msukumo wa ndani.

Kuna jambo linapikwa, na dalili zote zinaonyesha kuwa litakuwa tukio la kukumbukwa katika historia ya muziki wa Congo.

Version française :

Fally Ipupa et Héritier Watanabe se sont retrouvés en studio, dans une atmosphère chargée de créativité et de mystère.
Cette rencontre, rare et hautement symbolique, laisse présager l’émergence d’une œuvre majeure, peut‑être même un tournant artistique que les mélomanes attendaient depuis des années.

Les deux virtuoses, héritiers d’une tradition musicale exigeante, semblent façonner quelque chose de dense, de travaillé, de profondément inspiré.

Un projet se prépare, et tout indique qu’il portera la marque des grandes heures de la rumba congolaise moderne.

BABA L.W.L

FELIX WAZEKWA NA MDOGO WAKE JP LUKOMBO Mi CorazonJP Lukombo, anayefahamika kwa Jina la Aka (Mi Corazon), ni ndugu mdogo ...
03/08/2026

FELIX WAZEKWA NA MDOGO WAKE JP LUKOMBO Mi Corazon

JP Lukombo, anayefahamika kwa Jina la Aka (Mi Corazon), ni ndugu mdogo wa damu wa Félix Wazekwa.
Ni mtu wa karibu sana na kaka yake, na amekuwa mshirika muhimu katika mzunguko wa watu wanaomzunguka Msanii huyo.

Katika historia ya Group (Cultur’A Pays‑Vie), Wanamuziki waliowahi kupita Group hilo husikika wakisema kwamba JP Lukombo ndie alie na ushawishi mkubwa, kiasi kwamba mara nyingine alishiriki katika utoaji wa maamuzi ya ndani pale kaka yake alipokuwa hayupo au alipohitaji mtu wa kuamini.

Uhusiano wao wa undugu, uliojengwa juu ya uaminifu na heshima, ulipewa heshima ya kipekee mwaka 1997, wakati Félix Wazekwa alipotoa Album (Pauvre Mais...) na kutupia Wimbo “Mi Corazon” k**a zawadi na kumbukumbu kwa JP Lukombo.

Version Française :

JP Lukombo, affectueusement surnommé Mi Corazon, est le frère cadet biologique de Félix Wazekwa.
Figure discrète mais incontournable dans l’entourage de l’artiste, il occupe une place privilégiée au sein du cercle rapproché de Cultur’A Pays‑Vie.

Sa proximité avec Félix Wazekwa est telle que plusieurs anciens sociétaires de l’orchestre ont souvent témoigné de son influence : selon eux, JP Lukombo participait activement aux décisions internes, allant parfois jusqu’à orienter certains choix stratégiques lorsque son frère n’était pas disponible.

Cette relation fraternelle, faite de confiance et de loyauté, a été symboliquement immortalisée en 1997 lorsque Félix Wazekwa lui dédia la chanson “Mi Corazon”, incluse dans l’album « Pauvre, mais… ».
Un hommage musical qui souligne l’importance de JP Lukombo dans la vie personnelle et artistique du Leader.

BABA L.W.L

02/08/2026

MPIGA GITA WA ZAMANI WA FALLY IPUPA (ALVARITO SOLO) AMEFARIKI DUNIA

LE DÉCÈS DE ALVARITO SOLO, ANCIEN SOLISTE DE FALLY IPUPA.

Nkondi Alvarito, anayefahamika k**a Alvarito Solo, ni miongoni mwa wapiga gitaa wachache wa Congo ambao ustadi wao hauishii kwenye ujuzi tu, bali unafikia kiwango cha fasihi ya sauti.

Alizaliwa Jijini Kinshasa, katika mazingira ya Muziki yaliyokuwa yakichemka kila kona la jiji.

Katika miaka ya tisini, aling’aa wakati akichangia na Group (Stars Musica) Jijini Kinshasa Lingwala, akionyesha kipaji cha kipekee kilichowavutia wakongwe wa rumba.

Baadaye alijiunga na Wenge El Paris ikiongozwa na Marie‑Paul, kadhalika na Wenge Kumbela ya Aimé Bwanga, ambako alithibitisha kuwa MPIGA Solo Gita wa kiwango cha juu.

Safari yake ilipata hadhi ya juu zaidi alipoingia katika F’Victeam, Group lake Fally Ipupa.

Hapa alitunga wimbo wake maarufu (Rosendane), na akashiriki katika nyimbo kadhaa za Album (Libre Parcours) k**a Toi et Moi, Original, na nyimbo za nyingi zilizojaa ustadi wake wa kipekee.

Gitaa lake lilikuwa na mchanganyiko wa huzuni, uzuri na hisia za ndani ambazo ziligusa mioyo ya wasikilizaji.

Mbali na hapo, Alvarito alishirikiana na Héritier Watanabe, Pierrette Adams, na Wasanii wengine wa Congo na nje ya nchi.

Aliunda pia Group lake mwenyewe wakati akiwa Nchini Angola, akionyesha dhamira ya kueneza rumba ya Congo kimataifa.

Lakini nyuma ya mafanikio haya, Alvarito alikuwa akipambana na shinikizo la damu kwa muda mrefu.

Tiba za hospitali hazikumletea nafuu. Katika kipindi hiki cha majaribu, aliamua kutafuta uponyaji wa kiroho kupitia makanisa ya Walokole.

Hatua hii haikuwa ya ghafla; ilikuwa matokeo ya safari ya ndani ya kutafuta amani.

Hatimaye akawa mwimbaji wa injili, akigeuza gitaa lake kuwa chombo cha kumtukuza Mungu.

Tarehe 1 Agosti 2026, Alvarito alifariki dunia huko Kinshasa, na Muziki wa Congo ukaingia katika huzuni kubwa.

Wasanii, Marafiki na Mashabiki walimkumbuka k**a Mtu mnyenyekevu, mwenye moyo wa upendo na kipaji kisicho na kifani.

Leo, urithi wake unaendelea kuishi katika sauti za gitaa zinazopigwa mitaani ya Jiji la Kinshasa.

Kila mpigo wa nyuzi unabeba kumbukumbu yake.
Alvarito Solo anabaki kuwa mfano wa Msanii wa Congo anayefanya gitaa liimbe k**a sauti ya binadamu, na sasa sauti hiyo inaendelea kumtukuza Mungu.

Version Française :

Nkondi Alvarito, connu sous le nom d’Alvarito Solo, appartient à cette lignée rare de guitaristes congolais dont la virtuosité ne relève pas seulement de la technique, mais d’une véritable poétique sonore.

Né à Kinshasa, il grandit dans l’effervescence musicale de la capitale, où les guitares de Lingwala, Bandalungwa et Matonge façonnaient les destins artistiques.

Dans les années 1990, il se distingue au sein du groupe Stars Musica, formation emblématique de la commune de Lingwala.

Son jeu, déjà empreint d’une sensibilité singulière, attire l’attention de figures majeures de la rumba.

Il rejoint alors Wenge El Paris de Marie‑Paul, où il affine son style, puis Wenge Kumbela d’Aimé Bwanga, formation dans laquelle il confirme son statut de soliste d’exception.

Sa carrière prend une dimension supérieure lorsqu’il intègre F’Victeam, le groupe de Fally Ipupa.

Là, il compose le célèbre titre (Rosendane), devenu une pièce incontournable du répertoire moderne.

Il participe également à plusieurs morceaux de l’album Libre Parcours, notamment Toi et Moi, Original, et divers génériques où sa guitare, à la fois mélancolique et lumineuse, impose une signature immédiatement reconnaissable.

Outre ces collaborations, Alvarito travaille avec Héritier Watanabe, Pierrette Adams, et accompagne divers artistes de la scène kinoise et internationale.

Il fonde même un groupe en Angola, témoignant de son ambition de porter la rumba au-delà des frontières.

Cependant, derrière cette ascension artistique se cache une lutte silencieuse : Alvarito souffrait depuis longtemps d’une hypertension sévère, affection qui minait progressivement ses forces.

Malgré les traitements médicaux, son état ne s’améliorait pas.

Dans cette période de fragilité, il se tourne vers les églises de réveil, cherchant une guérison spirituelle.

Sa démarche n’est pas opportuniste : elle traduit une quête intérieure profonde.

Il finit par se convertir, devenant chantre de l’Éternel, transformant sa guitare en instrument de louange.

Le 1er août 2026, il s’éteint à Kinshasa, laissant la communauté musicale dans une stupeur douloureuse.

Les hommages affluent : réalisateurs, musiciens, anciens collègues évoquent un homme humble, généreux, d’une loyauté rare et d’un talent hors du commun.

Son décès marque la disparition d’un soliste dont la guitare semblait parfois parler à la place du cœur humain.

Aujourd’hui, son héritage résonne encore dans les rues de Lingwala, Bandal, Matonge.

Chaque arpège qui s’élève dans une répétition, un studio ou un concert porte quelque chose de lui.

Alvarito Solo demeure l’incarnation de cette rumba qui sait pleurer, sourire, prier et célébrer une rumba qui, grâce à lui, continue aussi de glorifier Dieu.

BABA L.W.L

FERRÉ GOLA KAKATAA CHIKITO ASIPANDE STEJINIFERRÉ GOLA REFUSE DE FAIRE MONTER CHIKITO SUR LE PODIUM.Jana Mjini Kolwezi, k...
02/08/2026

FERRÉ GOLA KAKATAA CHIKITO ASIPANDE STEJINI

FERRÉ GOLA REFUSE DE FAIRE MONTER CHIKITO SUR LE PODIUM.

Jana Mjini Kolwezi, kwenye SHOW ya kifahari ya Ferré Gola, uwepo wa Chikito miongoni mwa hadhira haukupita bila kutambuliwa.

Wapenzi wa muziki walimshinikiza Le Padre amwalike jukwaani.
Lakini Ferré, kwa utulivu wenye mamlaka na heshima, alisema: «Chikito anabaki kuwa mdogo wangu, lakini kwa sasa yeye si tena Memba wa Group letu.
Kwa maana hiyo Siwezi kumwalika apanda Stejini».
«Te azalaka na orchestre na biso te».

Maneno mafupi, lakini yenye uzito mkubwa — yakitenganisha upendo wa kindugu na nidhamu ya kisanii.

Version Française :

À Kolwezi, lors du show fastueux de Ferré Gola, la présence de Chikito au sein du public ne passa nullement inaperçue.

La ferveur des mélomanes, presque unanime, pressa Le Padre de convier son ancien Musicien à monter sur scène.

Mais Ferré, avec ce calme empreint d’autorité et de respect qui le caractérise, répondit avec une sobriété lourde de sens :
«Chikito demeure mon cadet, mais à ce jour il n’est plus membre de notre groupe.
De ce fait, je ne puis l’inviter à rejoindre la scène».

(Te azalaka na orchestre na biso te)

Quelques mots seulement mais des mots chargés d’un poids considérable.

Ils tracent une frontière nette entre l’affection fraternelle et la rigueur artistique, rappelant que l’art, même lorsqu’il naît de liens profonds, obéit à une discipline qui ne souffre ni l’improvisation ni la confusion des rôles.

Toa Maoni yako
Ta réaction

BABA L.W.L

02/08/2026

WENGE MUSICA MAISON MERE ANNÉE 2000
DRUMS : PAPY KAKOL
NGOMA : SHORA MBONDA
WEEKEND NJEMA
BON WEEKEND À TOUS Partie 8

02/08/2026

WENGE MUSICA MAISON MERE ANNÉE 2000
DRUMS : PAPY KAKOL
NGOMA : SHORA MBONDA
WEEKEND NJEMA
BON WEEKEND À TOUS Partie 7

02/08/2026

WENGE MUSICA MAISON MERE ANNÉE 2000
DRUMS : PAPY KAKOL
NGOMA : SHORA MBONDA
WEEKEND NJEMA
BON WEEKEND À TOUS Partie 6

Adresse

Avenue D'ORADOUR SUR GLANE
Bonneuil-sur-Marne
94380

Téléphone

33668312952

Site Web

Notifications

Soyez le premier à savoir et laissez-nous vous envoyer un courriel lorsque Lubonji Wa Lubonji publie des nouvelles et des promotions. Votre adresse e-mail ne sera pas utilisée à d'autres fins, et vous pouvez vous désabonner à tout moment.

Contacter La Pratique

Envoyer un message à Lubonji Wa Lubonji:

Raccourcis

Partager