Golden rehab.

Golden rehab. Page hii inausiana na kujua aina za madawa ya kulevyia na kutambua madhara yake na namna yanaadhiri mwili,akili,na roho pamoja na uhusiano wake katika jami

Da light
01/10/2024

Da light

...shukurani x3 tumesimama kuzunguka mduara huu kuzikumbusha nafisi zetu kwamba hakuna mmoja wetu kutoka hapa na kwenda ...
22/02/2020

...shukurani x3
tumesimama kuzunguka mduara huu kuzikumbusha nafisi zetu kwamba hakuna mmoja wetu kutoka hapa na kwenda kurudia/kurejea madawa...

vilevile tunakiomba kizazi kilicho zaliwa na kinachoendelea kuzaliwa Mungu akiepushe na janga hili la madawa....

tunawaombea pia mateja wanaoteseka pale nje Mungu awashike mkono na kuwaleta kwenye umoja huu maana nafuu inapatikana....

tunawakumbuka pia mateja/waraibu wezentu waliotangulia mbele za haki,Mungu awarehemu na pia awapunguzie adhabu ya kaburi.....


$chugamaicaboi


stop it budha

  ZA KIMWILI NA KIAKILI, ZINAZOHUSIANA NA POMBE (The physiological and psychological effects of alcohol.__pombe zinatumi...
17/05/2016

ZA KIMWILI NA KIAKILI, ZINAZOHUSIANA NA POMBE (The physiological and psychological effects of alcohol.
__pombe zinatumiwa sana duniani kote kwa sababu mbalimbali na zikiingia mwilini hubadilika kuwa ethanol(spirit). Matumizi yake Mara nyingi husifiwa au kulaaniwa au kulaumiwa k**a pepo baya. Kwa binadamu pombe husababisha unyongovu wa ubongo. Kiwango kidogo cha pombe husababisha athari ndogo kwa mtu; lakini ikitumiwa kwa kiwango cha juu huleta hali kuchanganyikiwa, kukosa fahamu na hata kifo.pombe zikiingia mwilini huondolewa mwilini kupitia INI,ambayo huvyonza pombe kabla ya kuondolewa. Hata hivyo, pombe inaweza kuvuka kwa urahisi kwenye utando wa seli yeyote katika mwili wa binadamu. Kwa kawaida spirit au ethanol hutumika k**a dawa ya kuulia vijimelea hatarish.....itaendeleeeea....goldenbell.....01

28/04/2016
UDHAIFU WA NAFSI NA MAUMIVU YATOKANAYO NA MALEZI YA WAZAZI.sisi sote ni matokeo ya malezi na mafunzo ya wazazi wetu.k**a...
26/03/2016

UDHAIFU WA NAFSI NA MAUMIVU YATOKANAYO NA MALEZI YA WAZAZI.
sisi sote ni matokeo ya malezi na mafunzo ya wazazi wetu.k**a mafundisho ya wazazi ni mazuri, mtoto hukua na ujenga hisia chanya ndani ya moyo wake. Iwapo malezi ya wazazi ni mabaya, tabia ya hisia hasi hujengeka katika akili ya mtu akuapo. Malezi bora hujenga hali ya kujitathimini na kujiamni katika moyo na akili ya mtoto. Watoto wakipendwa, wanajiamini wenyewe na kuwa wanasitahili kupendwa na wao huwapenda wengine na kujidhamini/kujuamini.Kujidhamini na kujiamni hujenga picha chanya ndani ya nafsi zetu, ni muhimu kila binadamu kuwa mtu mwenye afya njema kiakili. Tunavyoamini ndivyo utu wetu wa ndani ulivyo.

K**a sisi tunajiisi wadhaifu katika nafsi zetu, basi ili ionekane hatujipendi wala kuwapenda wengine, na tutaendelea kukua katika hali ya hofu na kujichukia. Wale ambayo wanajiona ndani ya nafsi zao huisi maumivu ndani ya nafsi kwa sababu wanafikiri wao hawapendwi. Kuna mahusiano kati ya malezi mabaya ya wazazi kwa watoto wao na madawa ya kulevyia kwani hali hii humletea mtoto hisia ya kutokupendwa na mwishoe mawazo haya humwimiza na hatimaye huamua njia ya kuondoa maumivu haya ni kutumia kilevi chochote.

Wale watoto wanaojithamini kwa mtazamo hasi hijingiza kwenye madawa ya kulevyia kulko wale watoto wanaoamini mambo mema kuhusu maisha yao. Wakati mtumiaji wa madawa anapoanza matibabu,moja ya malengo yake ni kuweka wazi maumivu ya msingi yaliyoko katika moyo wake. Mraibu huyu lazima atakuwa na sababu zilizomfanya aanze ulevi/MADAWA ya KULEVYIA. K**a wewe unakabiliwa na matatizo ya ulevi na madawa ya kulevyia, moja ya hatua chanya ya kuchukua ni kukumbuka hisia zako za ndani ambazo zilikuwa zinakuumiza na zilizoendelea kukuumiza kiasi kwamba zinakisukuma kwenye tabia ya ulevi na madawa.
Hivyo ni vyema kufanya uvumbuzi wa hali ya kutokujiamini na kutokujithamini kulko kuvaa vazi la ulevi na madawa ya kulevyia.

Waraibu Mara nyingi ni Watu waliokata tamaa na huwa na hisia hasi ndani ya nafisi zao kuhusu uraibu wa pombe na madawa ya kulevyia na kuwaza yafuayayo.

1/wanajiisi ni Watu wasio na thamani
2/wanajiisi hawapendwi kutokana na hali yao.
3/wanajiisi kamwe hawatapata maitaji yao kwa kuwatengemea Watu wengine MF wazazi.
4/URAIBU wao ndilo hitaji lao muhimu zaidi kulko kitu kingine_ulevi na madawa kuchukua nafasi ya upendo (addiction replace love)
Haya maneno hasi uwafanya Watu wengi kujihusisha na uraibu wa madawa tegemezi.

MZUNGUKO WA HATIA NA AIBU KATIKA URAIBU.(the guilt and shame cycle in addiction)_wakati mtu ni mtegemezi wa dutu k**a vi...
24/03/2016

MZUNGUKO WA HATIA NA AIBU KATIKA URAIBU.(the guilt and shame cycle in addiction)
_wakati mtu ni mtegemezi wa dutu k**a vile pombe na madawa ya kulevyia, kwa kawaida tabia hizi husababisha mraibu kujisikia mwenye hatia na aibu. Tabia za uraibu umfanya mtu kujihisi mnyonge/mdhaifu na kujipa matumaini kwa kutumia vitu visivyofaa ambavyo vitampa hali au hisia ya kujihamini au kuwa mwenye kujiweza. Mraibu anapojihisi mnyonge/mdhaifu,ujiongezea matatizo ya huitaji wa madawa ya kulevyia na pombe. Matokeo yake hujenga mzunguko wa kudumu wa kutaka Kuala kutumia vilevi hivi hili kupata faraja. Mzunguko huu huendelea kusababisha hatia na aibu kwa mtumiaji, na ni vigumu kuuvunja. Katika somo hili tunaona jinsi mraibu anavyojihisi wa chini sana na kuona mazingira anayoishi kuwa magumu kwa ajili ya ulevi wa madawa ya kulevyia ambayo husababisha mraibu kujiisi kuwa na hatia na aibu. Pia tunatoa jinsi ya kuvunja mzunguko huu wa kujiisi mwenye hatia na aibu kutokana na tabia ya uraibu.

UDHAIFU WA NAFSI NA MAUMIVU YATOKANAYO NA MALEZI YA WAZAZI__..ndio MADA/SOMO linalofuata...baada ya hili.


[email protected]
+255673052213.


.

  wa music Tanzania   Benz   hali haliyonayo sasa hivi kutokana na utumiaji madawa ya kulevyia.  pombe na madawa ya kule...
20/03/2016

wa music Tanzania
Benz
hali haliyonayo sasa hivi kutokana na utumiaji madawa ya kulevyia.
pombe na madawa ya kulevyia ili uweze kuishi maisha yenye furaha kwa kuwa timamu nakuwa na afya iliyo nzuri katika maisha yako ya cku zote.

UTEGEMEZI WA MADAWA YA KULEVYIA  #0673052213  .Watu waliozoea kutumia madawa ya kulevyia ambayo haziruhusiwi kisheria au...
20/03/2016

UTEGEMEZI WA MADAWA YA KULEVYIA

#0673052213

.

Watu waliozoea kutumia madawa ya kulevyia ambayo haziruhusiwi kisheria au zinaruhusiwa ila kwa mashariti huwa zinamatokeo yanayofanana.....
Utumiaji wa dawa za kulevyia huleta madhara makubwa kwa muathirika na familia yake. kwani huathirika kiakili kimwili na kiroho na kijamii.utegemezi wa madawa husababisha matokeo makubwa mabaya kadiri yanavyozidi kutumika.

Cku hizi hatuwezi kutofautisha sana kati ya haina za usugu/uraibu k**a zilivyotumika zamani

Pombe na madawa mengine ya kulevyia yote yana athiri kumbukumbu na hisia. Watu(siyo waathirika tu) wanaotumia pombe au madawa ili kupata hali Fulani, wanataka kubadili ukweli na hisia zao. Lengo ni kijisikia kujiburudisha, kupunguza mafadhaiko kwa muda na kijisikia vizuri.

Hili kufikia hisia za hali anayotaka kwa kawaida mtumiaji anaitaji kiasi Fulani cha pombe au madawa hayo. Na hanapotumia kidogo kidogo kupata ustahimilivu na baadaye huitaji zaidi na zaidi ilikupata hisia alizozizoea. Kuendelea kusitahimili kiasi kikubwa ni dalili za kwanza za utegemezi. Watu katika mazingira yake watagundua hilo, Mara nyingi watasema au kulalamika kuwa anatumia pombe nyingi au madawa., kuanzia hapo, mtu anaanza kujieleza na kujiami hata kukana madawa au pombe. Ili ni kwasababu tabia za waathirika wengi zinazoeleka na kusemekana ni kujifanya.

Kidogo kidogo mgonjwa anapoteza uwezo wa kujitawala kunywa kiasi kikubwa na Mara nyingi au kumeza madawa, atakunywa kiasi zaidi ya alichokuwa anakunywa kabla ili kupata hisia anazoziitaji, zile hisia nzuri alizopata zinaisha katika muda mfupi na kufuatiwa na kijisikia wasiwasi na woga.

  drugs and alcohol.
12/03/2016

drugs and alcohol.

ATHARI ZA POMBE KIHISIAMatumizi mabaya ya pombe inaweza kusababisha huzuni na wasiwasi.ufafanuzi was matumizi mabaya ya ...
10/03/2016

ATHARI ZA POMBE KIHISIA

Matumizi mabaya ya pombe inaweza kusababisha huzuni na wasiwasi.ufafanuzi was matumizi mabaya ya pombe ni unyaji wa kupindukia bila utegemezi wa pombe.hats hivyo,MTU anaweza kuwa tegemezi kimwili au kisaikolojia,na hawezi kufanya kazi zake bila hivyo.hata k**a mtumiaji wa pombe siyo tegemezi was dutu hii,yeye bado anaweza kuwa na matatizo ya kihisia k**a matokeo ya tatizo lake la ulevi.pombe inaweza kufanya hali ya mtumiaji kuwa mbaya kimaisha.

Athari zifuatazo ndizo zinajitokeza zaidi.
////unyongofu(depression)
Ni tatizo inayosababishwa napo MBE,ambayo mgonjwa huendelea kuwa na huzuni na anajihisi mnyonge pombe hugandamiza kazi za ubongomaana yake inazoofisha mfumo mkuu wa Neva(CNC).k**a mgonjwa ana matatizo ya awali ya Sonoma au unyongofu,,pombe inaweza kufanya hali kuwa mbaya zaidi.wazo LA kujiua ni matokeo wa uwezekano wa matumizi mabaya ya pombe,hasa pale mgonjwa anapokuwa na matatizo makubwa ya sonona.

/////ugonjwa wa wasiwasi.(anxiety)
Shida nyingine ya akili inayosababishwa na pombe ni ugonjwa wa wasiwasi ambayo mgonjwa anakuwa na wasiwasi asiyoweza kuutawala.MTU mwenye wasiwasi hunywa pombe na uwezekano wa kujiingiza kwenye madawa mengine ya kulevyia ni mkubwa ili kupunguza kwa mida dalili za wasiwasi lakini baada ya muda,kadiri MTU atavyo endelea kunywa pombe hali yake ya ugonjwa wa wasiwasi huwa mbaya zaidi.

////kujitenga(self isolation)
MTU anayetumia pombe vibaya anaweza kunywa pombe pekee yake au kwa kujificha au kujitenga na watu wengine,kwasababu hapendi watu wafahamu kuwa anak unywa pombe. Wakati mwingine huficha pombe zake katika maeneo ya kawaida k**a vile kwenye Mfuko ya nguo,kabatini na chumbani kwake ambapo watu wengine hawawezi kuona,MTU akifikia hali hii hali yake binafisi ya kimaisha na ya familia yake hurudi nyuma kimaendeleo.

////Kukasirika au. kuumia nafisi kirahisi.
Pombe husababisha MTU kuwa na hasira hasa wakati muda wake wa kunywa pombe umekaribia au ajapata pombe, pia husababisha vurugu au ugomvi wakati amelewa na atimaye kukabiliana na vyombo vya dola.

////kutotulia(restlessness)
////kuweweseka(mental confusion)
////kukosa umakini wa usikivu (poor concentration)
/// kiharusi(stroke)
/////kifafa(seizure)
/// maluelue za macho na masikio(visual and auditory hallucinations)
////kuumwa kichwa (headache)

/Instagram.
.

Address

Arusha
255

Telephone

+255693752469

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Golden rehab. posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Golden rehab.:

Share