Sobriety Forever Rehabilitation Centre

Sobriety Forever Rehabilitation Centre "Kagera Regional First De-addiction Centre"

SOBRIETY FOREVER REHABILITATION CENTRE - KAGERA is the treatment centre for
substance dependence and therefore the centre has a rich experience in handling alcoholics and drug addicts.

Kufikia wakati mlevi anakubali kuwa, "Nina shida," tayari wamepigana vita ambayo watu wengi hawajawahi kuona.Wameanguka ...
15/07/2026

Kufikia wakati mlevi anakubali kuwa, "Nina shida," tayari wamepigana vita ambayo watu wengi hawajawahi kuona.

Wameanguka na kulala kwenye mitaro ya maji machafu kandoni mwa barabara.

Wameamka na kujikuta hawana pesa papo hapo hawana kumbukumbu wapi imepotelea.

Na bado wanaendelea na unywaji.

Wamejiaibisha mbele ya familia, marafiki, na wageni.

Wameendesha magari wakiwa wamelewa— au wameponea chupuchupu na kusababisha msiba.

Wametoa ahadi za kuacha ila wanazivunja saa chache baadaye.

Wamelia kwa siri na kuapa, “Hiki ni kinywaji changu cha mwisho,” wakajikuta wakifikia chupa nyingine.

Huo ndio ukatili wa ulevi. Sio tu juu ya kunywa. Inahusu kupoteza udhibiti.

Kwa walevi wengi, inahitaji kugonga mwamba kabla ya hatimaye kujisalimisha na kuomba msaada.

Hadi wakati huo, mtu yeyote anayewaambia waache kunywa mara nyingi anakuwa adui namba moja. Sio kwa sababu mtu huyo amekosea, lakini kwa sababu uraibu / ULEVI SUGU hujilinda kwa ukali.

Kwa hivyo usishangae wakati ujumbe wa kupinga ulevi unavutia upinzani. Baadhi ya watu wanatetea jambo ambalo linawaangamiza. Wengine wanaweza tu kuwa na maoni tofauti kuhusu ULEVI SUGU.

Ikiwa pombe imechukua afya yako, amani yako, heshima yako, fedha zako, au mahusiano yako,

Kumbuka kuna matumaini ya KUTOKA KWENYE MARADHI YA ULEVI SUGU. Uamuzi mmoja unaweza kubadilisha maisha yako yote.

Ikiwa unaamini kuwa ujumbe huu unaweza kuokoa hata maisha YAKO au mtu fulani kwenye orodha ya marafiki zako anaweza kuwa anapigana kimya kimya vita ambayo hajawahi kumwambia mtu yeyote.

Kwa msaada zaidi:

Wasiliana nami:
0789 78 05 29,
0767 05 83 51

URAIBU / ADDICTION NI NINI? SEHEMU YA PILI......tunaendelea na somo lihusianalo na / au utawezaje kujua kuwa mpendwa wak...
16/06/2026

URAIBU / ADDICTION NI NINI?

SEHEMU YA PILI.
.....tunaendelea na somo lihusianalo na / au utawezaje kujua kuwa mpendwa wako au wewe mwenyewe TAYARI U-MRAIBU kwa baadhi ya vitu.

Zifuatazo ni baadhi ya dalili za uraibu (addiction):

Inaendelea na sehemu ya.........

5. Kila ukimshauri MRAIBU / Mgonjwa kuachana na matumizi ya vileo kila mara anatoa AHADI YA KUACHANA NA MATUMIZI NA WAKATI HUO HUO ANAENDELEA NA MATUMIZI YA VILEO, HAACHI, haishi katika UHARISIA.

6. MRAIBU / Mgonjwa anakuwa na matukio mengi ya kupoteza vitu k**a simu za mikononi, computer mpakato (laptops / gadgets), pochi, miwani, funguo, viatu, nk kila akilewa au akiwa kwenye maeneo ya vileo.

7. MRAIBU / Mgonjwa uanza kutumia vileo k**a dawa ya kutuliza maumivu "painkiller" hasa katika kukabiliana na maradhi mbalimbali mara apatapo maradhi / maumivu.

8. MRAIBU / Mgonjwa uanza kutumia mara kwa mara vileo ili kukabiliana na msongo wa mawazo / kukandamiza HISIA ZOZOTE ZA UCHUNGU.

KWA MSAADA WA MPENDWA WAKO AU WEWE MWENYEWE na k**a una mojawapo ya dalili hizo basi tuwasiliane kwa namba hizi kwa msaada zaidi.

SOBRIETY FOREVER REHABILITATION CENTRE - KAGERA.

Namba:
+255 789 78 05 29
+255 620 17 62 48
Email: [email protected]

URAIBU / ADDICTION NI NINI? SEHEMU YA KWANZA.Leo nitawaletea somo lihusianalo na / au utawezaje kujua kuwa mpendwa wako ...
14/06/2026

URAIBU / ADDICTION NI NINI?

SEHEMU YA KWANZA.

Leo nitawaletea somo lihusianalo na / au utawezaje kujua kuwa mpendwa wako au wewe mwenyewe TAYARI U-MRAIBU kwa baadhi ya vitu.

Zifuatazo ni baadhi ya dalili za uraibu (addiction):

1. MRAIBU / Mgonjwa HUSHINDWA KUFUATA MAELEKEZO AU UTARATIBU MARA KWA MARA KWA KILA JAMBO. Mfano mraibu akiwa mgonjwa wa maradhi mengineyo na ukampeleka hospitali / kituo cha afya na akapewa dawa kwa maelezo ya tabibu / daktari UTAMKUTA hafuati kabisa mazingatio ya muda wa kumeza au kuchoma sindano. Kwa mfano inakuwa ni vigumu kupatikana na hata akipatikana utamkuta kalewa au yuko kwenye maeneo ya kutumia vileo na masuala ya tiba kaweka pembeni.

2. MRAIBU / Mgonjwa HAWEZI KUMALIZA saa / siku / juma / bila kutumia vileo.

3. MRAIBU / Mgonjwa kupoteza fahamu na kupata wazimu kila atumiapo kileo.

4. MRAIBU / Mgonjwa kuingia kwenye vitendo vya ufunjivu wa sheria, taratibu, kanuni, mazingatio mbalimbali na kuwa na tabia za ajabu ajabu na ambazo hazivumiliki katika jamii, na kila ukimpatia ushauri anakuwa mkali / mbogo na mara nyingi uanza kuishi maisha ya kinyama na kinyume na UTU.

Itaendelea.................

KWA MSAADA WA MPENDWA WAKO AU WEWE MWENYEWE na k**a una mojawapo ya dalili hizo basi tuwasiliane kwa namba hizi kwa msaada zaidi.

SOBRIETY FOREVER REHABILITATION CENTRE - KAGERA.

Namba:
+255 789 78 05 29
+255 620 17 62 48
+255 767 05 83 51
Email: [email protected]

ALCOHOLICS ANONYMOUS FELLOWSHIP - 91 YEARS OF HOPE.
10/06/2026

ALCOHOLICS ANONYMOUS FELLOWSHIP - 91 YEARS OF HOPE.

ULEVI SUGU K**A UGONJWA.SOBRIETY FOREVER REHABILITATION CENTRE - KAGERA ni kituo cha kutoa usaidizi kwa waathirika wa po...
01/06/2026

ULEVI SUGU K**A UGONJWA.

SOBRIETY FOREVER REHABILITATION CENTRE - KAGERA ni kituo cha kutoa usaidizi kwa waathirika wa pombe na dawa nyinginezo za kulevya.

K**a una mzazi, ndugu, mtoto, kaka, dada, jirani, rafiki, au wewe mwenyewe na unafikiri una tatizo la matumizi ya pombe kupita kiasi au dawa nyinginezo za kulevya basi tuwasiliane kwa msaada zaidi.

Hayo ni MARADHI na ipo njia kwa waathirika kuweza kupata tiba na kurudi kwenye jamii na kuchukua MAJUKUMU YAO na maisha kuendelea.

Kwa maelezo zaidi waweza kuwasiliana na kwa namba zifuatazo:
0789 78 05 29
0767 05 83 51
0620 17 62 48

Email:
[email protected]

U R A I B U | A D D I C T I O N.MLEVI SUGU asitishapo matumizi ya pombe dalili hizi hutokea......
27/04/2026

U R A I B U | A D D I C T I O N.

MLEVI SUGU asitishapo matumizi ya pombe dalili hizi hutokea......

Homa ya ini inajulikana kitaalamu k**a *Hepatitis* . Ni hali ambapo ini  linavimba na kushindwa kufanya kazi zake vizuri...
25/03/2026

Homa ya ini inajulikana kitaalamu k**a *Hepatitis* . Ni hali ambapo ini linavimba na kushindwa kufanya kazi zake vizuri k**a kusafisha sumu mwilini na kusaidia mmeng’enyo wa chakula.
‎ *Chanzo cha homa ya ini*
‎Homa ya ini husababishwa zaidi na virusi vinavyoitwa:
▪️‎Hepatitis A
▪️‎Hepatitis B
▪️‎Hepatitis C
‎Lakini pia inaweza kusababishwa na:
▫️‎Matumizi makubwa ya pombe 🍺
▫️‎Dawa kali au sumu mwilini
▫️‎Magonjwa ya kinga kushambulia ini (autoimmune)
‎ *Njia za maambukizi*
‎Inategemea aina ya hepatitis
*‎1. Hepatitis A*
▫️‎Kula chakula au kunywa maji machafu
▫️‎Usafi duni wa mikono
▫️Lakini inaweza kuambukizwa kwa ngono ya mdomo (oral–anal contact)
*‎2. Hepatitis B & C*
▫️‎Ngono zembe bila kinga
▫️‎Kuchangia sindano au vifaa vyenye damu
▫️‎Kuongezewa damu isiyopimwa
▫️‎Kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa kujifungua
‎ *Dalili za homa ya ini*
▫️‎Uchovu sana
▫️‎Homa ndogo
▫️‎Kichefuchefu na kutapika
▫️‎Maumivu upande wa juu kulia wa tumbo
▫️‎Mkojo kuwa wa rangi ya giza
▫️‎Ngozi na macho kuwa ya njano (jaundice)
▫️‎Kupoteza hamu ya kula

U J U M B E
03/03/2026

U J U M B E

"HATA IWEJE, BADO NI WETU"Katika jamii au familia tunakuwa na waathirika wa pombe (walevi sugu) na dawa nyinginezo za ku...
10/02/2026

"HATA IWEJE, BADO NI WETU"

Katika jamii au familia tunakuwa na waathirika wa pombe (walevi sugu) na dawa nyinginezo za kulevya kulevya. Tunawatenga na kuwadharau waathirika na wakati huo huo tukiwaona k**a "HASARA" NA "LAANA" ndani ya jamii bila kujua kuwa hao ni WAGONJWA NA WANAHITAJI MSAADA WA TIBA K**A WAGONJWA WA MARADHI MENGINEYO.

Tukidhani kwa namna moja au nyingine "WARAIBU" hawana maana tena, tutakuwa tunakosea sana, cha msingi ni kushirikiana na taasisi, asasi, mbalimbali za kusaidia wagonjwa hawa.

Nasi k**a SOBRIETY FOREVER REHABILITATION CENTRE kazi yetu kubwa ni kutoa usaidizi kwa waathirika wa pombe na dawa nyinginezo za kulevya.

Tuwasiliane kwa namba hii:
+255 789 78 05 29. Ili tuweze kutoa usaidizi kwa wazazi, ndugu, jamaa, watoto, marafiki na hatimaye nao waweze kurudi katika utimamu na kuchukua MAJUKUMU YAO K**A ZAMANI na maisha yaleta MAANA. Asante. NB: USHAURI NI BURE.

Address

Bukoba

Opening Hours

Monday 08:00 - 16:00
Tuesday 08:00 - 16:00
Wednesday 08:00 - 16:00
Thursday 08:00 - 16:00
Friday 08:00 - 16:00
Saturday 08:00 - 12:00

Telephone

+255789780529

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Sobriety Forever Rehabilitation Centre posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Sobriety Forever Rehabilitation Centre:

Shortcuts

Share