Jacob Ghump

Jacob Ghump We fight, we fix, we stay! Time the time before time to time you.

Uhalisia ni kuwa ukishakuwa na Familia yako na Watu wako kadhaa wanakutegemea kitu kinachoitwa MSHAHARA huwa hakitoshi, ...
15/11/2025

Uhalisia ni kuwa ukishakuwa na Familia yako na Watu wako kadhaa wanakutegemea kitu kinachoitwa MSHAHARA huwa hakitoshi, mbaya zaidi ukishapewa sifa kuwa wewe ni BRAND basi hakuna kitakachotosha tena baada ya hapo, uhalisia ni kuwa Watu maarufu wengi wanateseka na kupitia magumu kutokana na Mzimu unaitwa BRAND.

Kuna Mwana aliwahi kuniuliza swali kwanini huhami huku sehemu ambayo upo tangu Chuo? Unachofanya unaweza kuhama nyumba ila Mtaa ni ule ule? My very humble answer kwake ni kuwa unaweza kuwa na jina, unaweza kuwa Mtu fulani lakini mfuko wako usiakisi jina lako, sayansi ni kujikuna unapofikia na kuacha maisha yaende mpaka utakapoweza.

K**a naweza kuishi kwa elfu5 mfano kwa siku hiyo ni sehemu salama zaidi kwakuwa ndio kipato changu, k**a ninaweza kuacha gari home kisa halina mafuta halafu nikadaka Boda iniwahishe Kazini hiyo ni salama zaidi, BRAND na maisha ni vitu viwili tofauti kabisa.

Vijana wenzangu my very humble opinion kwenu msikubali mtego wa Umaarufu watu watawajengea maisha ya picha, omba Mtu msaada hataki achana nae, chukua pesa ambayo unaifanyia kazi ya halali, ukisikia Mtu anakwambia kaishi Masaki sijui Oysterbay na unajiona huna mfuko huo basi ni mtego mkali sana.

Mungu atubariki sana Ndugu zangu.

Address

Dar Es Salaam
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Jacob Ghump posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Jacob Ghump:

Share

Category