Najali AFYA Yangu

Najali AFYA Yangu Dr. Kimboka healthy and nutritional clinic inakupatia ushauri juu ya afya yako na njia stahiki za ku
(1)

VYAKULA VYENYE KUONGEZA MAZIWA KWA MAMA ANAYENYONYESHA.Ikiwa tatizo hili la kukutoa maziwa ya kutosha wakati wa kunyonye...
23/11/2024

VYAKULA VYENYE KUONGEZA MAZIWA KWA MAMA ANAYENYONYESHA.

Ikiwa tatizo hili la kukutoa maziwa ya kutosha wakati wa kunyonyesha halitokani na tatizo la ugonjwa k**a vile mama kuwa na uvimbe au jipu katika t**i
Mama tunamshauri kutumia mojawapo ya vyakula vifuatavyo:

1.TENDE
Kwa kula tende pekee au tende na maziwa au Juisi ya tende yenye maziwa .
Kwa wastani robo kilo ya tende kwa siku

2.PILIPILI MANGA
Kutumia pilipili manga kwa kuiweka kwenye uji au juisi au kuichemsha yenyewe na kuinywa k**a chai

3.MBEGU ZA MABOGA
Kula mbegu za maboga na boga lake au tafuna mbegu za maboga zilizokaangwa Mara kwa Mara kunasaidia uzalishaji wa maziwa kwa wingi

4.SUPU YA TAA/PWEZA
Kunywa supu ya samaki aina ya taa/pweza nako kunasaidia kuongeza uzalishaji wa maziwa kwa wingi kwa mama anayenyonyesha

SUPU YA NG'OMBE,MBUZI NA KONDOO
Mwanamama anapotoka kujifungua ni vizuri apate supu kila asubuhi na ni vizuri zaidi akapata supu ya
kongoro,nyama ya ngombe au supu ya kondoo kwani
supu za namna hii ni tiba nzuri kwa mama mwenye
matatizo ya kutopata maziwa ya kutosha kwa ajili ya mtoto wake na pia hurejesha nguvu zilizopotea wakati wa kujifungua.

NDIZI ZA KUCHEMSHA
Pia ndizi za kuchemsha ni nzuri sana kwa kuondoa hili tatizo la kukosa maziwa kwamama mjamzito,zichemshwe vya kutosha mpaka ziwe laini na hata mtori pia unafaa katika kutibu hali hiyo.

MAJI
Mzazi anapaswa awe ni mwenye kujitahidi kunywa maji ya kutosha kila siku kwani nayo humsaidia kuongeza maziwa kwa ajili ya mwanae mpya.

UJI WA PILIPILI MTAMA/MANGA
Aidha mzazi anashauriuwa anywe uji wenye pilipili mtama,kwani pilipili mtama zina faida mbili kwa mzazi.
1.huondoa haraka makovu yaliyotokana na msuguano wa mtoto tumboni.
2.husaidia ongezeko la maziwa ya mama ili yapatikane ya kutosha kuweza kumnyonyesha mwanae na akapata afya njema
MBOGA MBOGA
K**a tunavyo juwa vyakula vya mboga mboga vinaumuhimu mkubwa sana katika kuchangia jambo hili hivyo mama mzazi anapaswa kutumia kwa bidii sana.

Kwa ushauri, elimu zaidi na matibabu unaweza kuwasiliana nasi kupitia njia ya WhatsApp no. +255767202621, .kimbokatz

Kuna makundi ya damu yafuatayo A,B,AB na OUnapopimwa kundi la damu wanaweza kubainisha k**a una Rh Factor au hauna,Rh-fa...
24/08/2023

Kuna makundi ya damu yafuatayo A,B,AB na O

Unapopimwa kundi la damu wanaweza kubainisha k**a una Rh Factor au hauna,

Rh-factor ni protein ambayo inakutwa katika baadhi ya Seli hai nyekundu za damu, na sio kila mtu anayo hii protein katika cell zake.

Waliyonayo ndo wanaitwa Positive na wasiyonayo ni negative, so ukienda hospital utaambiwa ni either A+/A- or B+/B-, AB+/AB- au O+/O-

MUHIMU: Ikitokea mama ni mjamzito na ana blood group yenye NEGATIVE, baba wa Mtoto akawa na POSITIVE,

Mara nyingi inategemewa mtoto atakuwa na POSITIVE aliyoirithi kwa baba yake, so kinachotokea ni kwamba kwa ujauzito wa kwanza tatizo linaweza lisionekane kwasababu damu ya mama na mtoto havichanganyikani,

Lakini wakati wa kujifungua damu inaweza kumix hivyo mwili wa mama utatambua hiyo RH-PROTEIN ambayo ipo kwa mtoto hivyo mwili wake huanza kuzalisha kinga mwili ikijua kwamba hicho ni kitu kigeni kinachotakiwa kushambuliwa

So, kwa mimba ya pili sasa mama mwili wake unakuwa tayari umetengeneza kinga mwili kwa ajili ya kupambana na RH positive yoyote itakayoingia hivyo cells za mtoto zitashambuliwa na kingamwili za mama k**a hatua sitahiki hazitachukuliwa

HATUA STAHIKI: Mama k**a ni negative na baba ni positive, ujauzito unapofikisha week ya 28 Mama anatakiwa kuchoma chanjo ya kuzuia uzalishaji wa kingamwili za kushambulia Cells za mtoto iitwayo ANT-D na ya pili ni ndani ya masaa 72 baada ya mama kujifungua,

K**a mama una high risk pregnancy au unajua kabisa una hili group la damu lenye negative na baba ni positive jitahidi sana uanze clinic mapema mnoooooo

NB:KAMA BABA NA MAMA NI NEGATIVE WOTE HAINA SHIDA BUT MPIME KUWA NA UHAKIKA ZAIDI NDO MAANA CLINIC YA KWANZA BABA ANASISITIZWA KUWEPO.kimbokatz
+255767202621

Unatumia dawa ipi kwa sasa kurekebisha homoni na mpangilio wa hedhi.Wakati ukiendelea na tiba zako namna homework ya kuz...
24/04/2023

Unatumia dawa ipi kwa sasa kurekebisha homoni na mpangilio wa hedhi.

Wakati ukiendelea na tiba zako namna homework ya kuzingatia kila siku walau kwa mwezi mmoja kisha uje na mrejesho

Haijalishi unaishi mazingira yapi au uchumi wako ukoje, jitahidi kuweka ulazima wa Kula parachichi zima 1 kila siku k**a huwezi walau kipande kimoja cha parachichi.

Tumia vyakula vya wanga kwa kiwango kidogo, vyakula k**a Mahindi, Ugali na Dona, Viazi, Mihogo, Ndizi, Tambi n.k, ila ongeza wingi wa mboga za majani na matunda.

Epuka kahawa, chai ya rangi, soda nyeusi na vinywaji vingine vyote vyenye kiwango kingi cha kafeina ndani yake

Relax na jipe tumaini jema, punguza msongo wa mawazo (stress) na hakikisha unapata usingizi wa kutosha kila siku (masaa walau 8-10) k**a hupati usingizi jitahidi kunywa glass ya maziwa fresh yaliyotiwa mdalasini na vijiko kadhaa vya asali mbichi, inaleta usingizi kuliko kumeza pilitoni

Usitumie vidonge vya uzazi wa mpango k**a unahitaji kuweka homoni zako sawa

Kuna vyakula tunafosi kuvitumia ila havina ulazima wowote wala havina faida mwilini, vyakula k**a chipsi, chapati, vinywaji k**a soda vinavuruga sana homoni na uzito wa mwili.... Usishindane na utandawazi kula kiasi kawaida uijenge Afya yako

Kunywa chai yako yenye tangawizi, mdalasini, iliki na mchaichai

K**a utaweza kupata Unga Wa Mbegu Ya Parachichi utumie.
Weka kijiko kimoja cha unga wa mbegu ya parachichi kwenye kikombe cha chai, unasaidia kuondoa tindikali mwilini kwa ndugu zangu ambao mmetumia au mnatumia sana uzazi wa mpango, sindano, p2, vidonge n.k

Weka nia, chukua hatua ndani ya wiki 3 hadi 4 uje na mrejesho wako

Anyway,Nambie kwa sasa unapitia changamoto gani kati ya hizi, nikusaidie kuzitatua;

• Fangasi , U.T.I au P.I.D sugu...au Mirija ya Uzazi imeziba au kujaa maji...!

• Una uvimbe kwenye vifuko vya mayai au kwenye fuko la uzazi yaani FIBROIDS or OVARIAN CYSTS...!

• Hedhi yako haina mpangilio maalumu au umekuwa ukitafuta ujauzito bila mafanikio.Huna hisia wala huna ute wakati wa tendo / siku za hatari.

Niandikie changamoto yako ya uzazi kwenda WhatsApp namba 0767202621, kupata msaada zaidi. .kimbokatz

Faida za kutumia mayai kwenye kifungua kinywa.1. Huongeza Shibe,  protein iliyopo katika mayai humfanya mtu kukaa muda m...
29/03/2023

Faida za kutumia mayai kwenye kifungua kinywa.

1. Huongeza Shibe, protein iliyopo katika mayai humfanya mtu kukaa muda mrefu Bila kusikia njaa tofauti na vyakula vyengine k**a bidhaa za ngano

2. Chanzo kikubwa Cha protein.,
Mayai Yana kiasi kikubwa Cha Amino Acid, ambazo huupa mwili kiasi kikubwa Cha protein.

3. Hulinda macho., Kemikali Aina ya Leutin, na zeaxanthin zinaaminika kulinda macho dhidi ya mionzi mikali . Pia husaidia kuepuka tatizo la mtoto wa jicho kwa wazee

4. Huimarisha afya ya ubongo, kurutubisho Aina ya "Choline" ambacho hupatkan katika ubongo husaidia kuimarisha ubongo na kuweka kumbukumbu sawa.

0767202621 .kimbokatz

Address

Victoria Tanzanite Park
Dar Es Salaam
32323

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Najali AFYA Yangu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share

Category