Harmony Memorial Polyclinic

Harmony Memorial Polyclinic Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Harmony Memorial Polyclinic, Hospital, Dar es Salaam.

Utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) umeonyesha kuwa, takriban mtu mmoja kati ya kila watu nane duniani a...
10/10/2022

Utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) umeonyesha kuwa, takriban mtu mmoja kati ya kila watu nane duniani ana changamoto ya ugonjwa wa akili. Taarifa hiyo inaendelea kuonyesha kuwa kila kifo kimoja kati ya vifo 100 duniani husababishwa na mtu kusitisha uhai wake mwenyewe. Asilimia 50 ya vifo hivyo hutokea kwa watu wenye umri chini ya miaka 50. Kujiua imeelezwa kuwa ni sababu moja wapo kati ya sababu kuu zinazo pelekea vifo vya watu katika umri wa miaka 15-29. Kwa nchi yetu ya Tanzania, inakadiriwa kuwa na watu takribani millioni saba wanapitia changamoto za afya ya akili, wanawake wakitajwa kua ni kundi linalo athiriwa zaidi na changamoto hizi.

Afya ya akili imetajwa kuwa muhimu si tu katika ubora wa maisha lakini pia katika maswala ya uchumi na uzalishaji.

Jali Afya kwa ajili ya maisha Bora

KIFAFA  CHA MIMBAHii ni hali ambayo inatokea kipindi cha ujazito hasa kuanzia wiki ya 20.Na kiukweli tunaposema kifafa c...
06/09/2022

KIFAFA CHA MIMBA

Hii ni hali ambayo inatokea kipindi cha ujazito hasa kuanzia wiki ya 20.
Na kiukweli tunaposema kifafa cha mimba hiii ni hatua ya juu na ya hatari zaidi kwa mama mjazito..

Kabla ya hapo mama anaweza kuanza na dalili mbalimbali ambazo hasa ni presha kupanda na kuvimba miguuu sana..(Preeclampsia) Na sehemu zingine za mwili...
Vingine vinaweza kuonekana zaidi vipimo vya maabara vikifanyika
K**a hali haitadhibitiwa mapema Kifafa cha mimba kinaweza kutokea ambapo mama atapata degedege ambalo ni hatari kwake na mtoto pia...

*CHANZO(RISK FACTORS)*

➡️Kuzaa mapema sana au kuchelewa sana..
➡️Mzao wa kwanza
Kuwa na magonjwa k**a.. Kisukari... Figo.. Magonjjwa ya vinasaba...
➡️Kwa kiasi k**a imetokea kwenye familia
➡️Kwa kiasi pia mapacha inaweza kuchangia
➡️Kubadilisha mume
➡️Uzito mkubwa sana
➡️Mpishano mkubwa wa mimba. (Zaid ya miaka kumi)

*DALILI*

➡️Shinikizo la damu kuanza kuwa juu
➡️Kuvimba mwili kwa ujumla kuanzia miguu
➡️Kichwa kuuma sana
➡️Kuona kizunguzungu
➡️Tumbo kuuma sehemu ya juu kulia
➡️Kupungua kwa utokaji wa mkojo

*MAMBO YAKUZINGATIA*

Ni muhimu sana k**a imegundulika una dalili za shinikizo la damu katika ujauzito(linaloweza sasa kupelekea KIFAFA CHA MIMBA)
Ufanye yafuatayo...

➡️Hudhuria kliniki mara kwa mara..
➡️Ukiona dalili zozote tulizotaja chukua hatua
➡️Tumia dawa kwa umakini
➡️Fanya vipomo vyote unavyoshauriwa
➡️Hakikisha mtoto hapunguzi kucheza... Ikitokea toa taarifa haraka kwa daktari wako na uwahi kituo cha huduma
➡️Jitahidi kuwa unapima presha kwa jinsi utakavyoshauriwa

*MADHARA YA UGONJWA*

Mara nyingi ugonjwa usipodhibitiwa vizuri....

Unaweza kupata
➡️KIFAFA CHA KIFAFA CHA MIMBA Ambacho ni hatari kwa mama na mtoto
➡️Figo zinaweza kushindwa kufanya kazi
➡️Mtoto anaweza kufia tumboni
➡️Mtoto anaweza kuzaliwa njiti
➡️Mtoto kuzaliwa akiwa amedumaa... ➡️Uzito mdogoo
Unaweza kupata stroke

NB.. Ni ugonjwa ambao ukikutokea unahitaji kuwa karibu sana na daktari wako na watoa huduma ili kufika safari hii ya miezi tisa salama kwa mama na mtoto kwa kushirikiana!

HARMONY MEMORIAL POLYCLINIC
health For everyone.

Special thanks to our medical and non medical staffs for the devoted hard working spirit.  We are who you are
01/05/2022

Special thanks to our medical and non medical staffs for the devoted hard working spirit.

We are who you are

Thank you for your hard work
01/05/2022

Thank you for your hard work

Tunakutakia wewe na familia yako Heri ya SIKUKUU YA MUUNGANO
26/04/2022

Tunakutakia wewe na familia yako Heri ya SIKUKUU YA MUUNGANO

Katika maadhimisho ya siku ya malaria duniani tarehe 25/04/2022 kituo cha Afya cha Harmony Memorial Polyclinic kitatoa H...
24/04/2022

Katika maadhimisho ya siku ya malaria duniani tarehe 25/04/2022 kituo cha Afya cha Harmony Memorial Polyclinic kitatoa Huduma zifuatazo bure:

Kupima Malaria,
Kupima Presha, Joto, Urefu na uzito,
pamoja na Kumuona Daktari bure

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Harmony Memorial Polyclinic posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share

Category