Midwife Aggie

Midwife Aggie Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Midwife Aggie, Pregnancy Care Center, Dar es Salaam.

Part 2Baada ya kujifungua…..Hapa wengi mnakua mnafikiri hawa wakina mama wanakua na furaha k**a ambavyo mnawafurahia na ...
24/02/2023

Part 2
Baada ya kujifungua…..
Hapa wengi mnakua mnafikiri hawa wakina mama wanakua na furaha k**a ambavyo mnawafurahia na kuwapa hongera nyingi,
Kwanza mpunguze kwenda kuwaona,wanahitaji sana muda wa kuwa na mtoto na familia yake pamoja na kupumzika,
Mambo huwa tofauti.Wengine wanapata postpartum depression,wanaendelea kutuhitaji sana wataalam wa afya na pia katika kipindi hiki wanahitaji wasaidizi au ndugu ambaye anahitaji pia kufundishwa namna ya kuishi naye,asimchanganye kabisa na mambo yake,asimchanganye na kumfundisha kila aina ya malezi…
1. Bado wanajiuliza hivi ni mimi kweli nimepata mtoto?
2. hawawezi kulala hata k**a kuna mtu wa kumsaidia kukaa na mtoto
3. Wanashindwa kula vizuri
4. Wanahisi kila anachokifanya inawezekana atakosea mtoto atapata tatizo
Unaweza usigundue haya kwa ndugu yako unayeishi naye ambaye alihangaika kutafuta mtoto kwa muda mrefu,
Ila japo Hakikisha anatembelewa na mtoa huduma kumfanyia uchunguzi wa namna anavyoishi,

Sio kwamba anamlea mtoto k**a yai,sio kwamba anakua mkali,ana panic ndo hali halisi mnatakiwa mumuelewe,vaa kiatu chake,
Wanatakiwa kuhudumiwa kwa uangalifu sana sana na kuelekezwa kwa kitaalam sana na wakati mwingine mzindue akili arudi kwenye dunia ya kawaida😀,Wana mambo yao special na si ya kupuuza…

Part 1,Kuna tofauti kubwa kuhudumia mwanamke ambaye hajahangaika na uzazi/kupata mimba/kupata mtoto,Na kumuhudumia yule ...
24/02/2023

Part 1,
Kuna tofauti kubwa kuhudumia mwanamke ambaye hajahangaika na uzazi/kupata mimba/kupata mtoto,
Na kumuhudumia yule anbaye amepata changamoto ya kupata mtoto,
K**a vile mimba kuharibika mara kwa mara,kutoshika mimba au kujifungua mtoto mfu,
Wakina mama k**a hawa waliopitia changamoto wanahigaji huduma na ruhusu kuwapatia muda wako wa kutosha,Sio tu kuishia kusema Bad obstetric history,wengine precious baby😎au kumpa mama reassurance asubiri tu kufanyiwa operation kwa sababu amehangaika sana…Hapana kuna zaidi ya hapo,
Wana mengi,wana mizigo kwenye vichwa vyao,wana hisia mchanganyiko,
🤰🏽Wakati wa ujauzito
📌Stress za kazini (anajifanyisha,kwani yeye ndo wa kwanza kubeba mimba,analea mimba k**a yai)Mtu amekaa kwenye ndo miaka 6,10,14 hajapata mimba au mtoto kweli akiipata unafikiri atailea sawa na wengine?
Pia kuna ambao wapo bed rest acha waseme unalea k**a yai,kwa sababu hawajui changamoto ulizozipitia.
Hapa kwenye kulea k**a yai jamani wale msio na matatizo tafadhali tuendelee tu na kazi😀
📌Baadhi Wanakua na imani ndogo kuhusu kufanikiwa kumpata mtoto ambaye tayari yupo ndani yake.
(sio vibaya ni kwa sababu ya changamoto alizopotia)…
Hakikisha unamsadia kufikiri chanya kuhusu safari yake hii.
📌Wasiwasi/hofu,akuhisi kushindwa,
Kwa ridhaa Muunganishe na mwanamke unayemfahamu ambaye alipitia changamoto k**a za kwake na amefanikiwa kupata mtoto.Wawasiliane wapeane moyo,Kuna jambo ambalo watoa huduma tunafikiri kila unachomuambia mgonjwa/mteja anakubali mpaka moyoni HAPANA,Wakati mwinginr anakuitikia tu kwa sababu anaona k**a sisi ndo kazi yetu tu ya kuwatia watu moyo hata k**a tatizo ni kubwa,
Mpe mtu mwingine mwenye ushuhuda.
📌Wanahisi hawaeleweki,
Mpe muda wa kutosha kumsikiliza,Siku zinavyozidi kwenda usisikitike kuhusu changamoto zilizopita bali mpe hongera kwani atafanikiwa.
📌Siku ya kujifungua.
K**a mimba yako imeshakua na hakuna changamoto za kumfanya ajifungue kwa operation basi kuna uwezekano huo wa kujifungua kawaida basi aelezwe, kuwa nao kwa ukaribu,Monitoring is everything,
Anahitaji ukaribu sana,aambiwe kila hatua,Asiulizwe ulizwe maswali kuhusu historia mbaya iliyopita.
📌Muhakikishie atahuduniwa na watu sahihi

Hello Monday👏🏽 Dear mama mtarajiwa,kuwa katika hatua za kujifungua haikuzuii kula wala kunywa,Hili liweke kichwani mwako...
13/02/2023

Hello Monday👏🏽
Dear mama mtarajiwa,kuwa katika hatua za kujifungua haikuzuii kula wala kunywa,Hili liweke kichwani mwako na uende nalo siku ya kujifungua,japo unaweza usipata hamu ya kula ila jitahidi kula na kunywa,
Hapo tulibakiza masaa mawili tu ajifungue na alijitahidi kula japo kwa kubembeleza,na sio kulazimisha…
🤩Water birth,Tulijikuta tumekuwa na natural labor , kila hatua ilienda vizuri naturally….
🤩New mama in town🥳
🤩3.9 kgs
midwifery is a closed book🙏🏾
🤩Apgarscore zooooote🥳

Hongera sana kwa wote mliojifungua,
Nawatakia kila jema mnaotarajia kujifungua wiki hii.Uwe unajisemesha maneno haya,
I am strong,I can,I will,
Mimi ni jasiri,Ninaweza,sitaogopa,siogopi,nitakula na kunywa nikiwa leba😂,

Kwa maelezo zaidi piga simu 0679755996
02/02/2023

Kwa maelezo zaidi piga simu 0679755996

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Midwife Aggie posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share