18/08/2026
WILCAH tunaendelea kuwa wadau muhimu katika kutoa elimu ya afya ya akili kwa vijana, kuwajengea ujasiri, uthubutu na matumaini ya kufikia malengo yao.
Kupitia Mwanzilishi & Mkurugenzi Mtendaji wa WILCAH , Dr. Cecilia Dadi, tumepata fursa ya kushiriki katika kipindi cha Kidani, kinachorushwa AzamTV kupitia channel ya UTV Tanzania .
Katika kipindi hiki, tumezungumzia nafasi ya vijana katika jamii, umuhimu wa afya ya akili, pamoja na namna wanavyoweza kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Tunatoa shukrani za dhati kwa AzamTV , mtangazaji Sauda Hussein pamoja na team nzima ya waandaaji wa kipindi cha Kidani, kwa kutupatia nafasi ya kuzungumza na jamii kuhusu masuala muhimu yanayohusu vijana na afya ya akili.
📺 Usikose kufuatilia kipindi hiki Alhamisi saa 3:30 usiku kupitia UTV Channel namba 108, Azam TV.