30/04/2026
Uzazi wa Mpango!
Ni njia gani unayopendelea kutumia kupanga uzazi?
Wanawake wengi wanatoa malalamiko yanayotokana na matumizi ya dawa za uzazi wa mpango. Malalamiko ni mengi. Ingawa wataalamu tunasema kuna maudhi madogo madogo yatokanayo na matumizi ya dawa za uzazi wa mpango, lakini kwa idadi fulani ya wanawake inaonekana maudhi hayo si madogo.
Je! Umewahi kutumia njia yoyote ya uzazi wa mpango?
Una uzoefu gani juu ya maudhi yanayotokana na matumizi ya dawa za uzazi wa mpango?
Umeongezekwpa uzito kupita kiasi (umenenepeana)?
Uke unakuwa mkavu sana?
Unapata mzunguko wa hedhi bila mpangilio? Maumivu huwa makali na damu huwa nyingi au kidogo kuliko kawaida?
Kichwa kuuma mara kwa mara?
Unajisikia kuchokachoka?
Umeacha kutumia uzazi wa mpango (sindano vidonge) na sasa unataka ujauzito lakini hupati?
Unadhani changamoto hizi kubwa zinatokana na ubora mdogo wa dawa zinazotumika? Au hata katika nchi zilizoendelea changamoto hizi zipo?
Ni uzoefu wako binafsi, au umesikia, umeshuhudia?
Unadhani ni zipi njia sahihi za uzazi wa mpango ambazo mtu anaweza kutumia bila maudhi au kwa maudhi yanayovumilika?
Niambie!
Dr. Chris Cyrilo.
Nawasilisha!