Afya Track

Afya Track Mtandao #1 Kwa Afya ya Ujauzito na Mtoto kwa Lugha ya Kiswahili Afrika Mashariki. Taarifa, Ushauri na Huduma za Afya Mtandaoni

Mtandao  #1 kwa afya ya mama na mtoto ulioboreshwa sasa umerudi rasmi. Tunashukuru kwa uvumilivu wenu kipindi cha miaka ...
28/01/2025

Mtandao #1 kwa afya ya mama na mtoto ulioboreshwa sasa umerudi rasmi.

Tunashukuru kwa uvumilivu wenu kipindi cha miaka kadhaa tuliyokiwa hatupo hewani.

Yajayo yanafurahisha. Pia mtuwie radhi wote mliotuma jumbe pepe kuulizia app ya AfyaTrack kwani tupo mbioni kuirudisha tena ikiwa bora zaidi.

Karibu kwa taarifa, ushauri na huduma bora kwa

Link kwenye bio 👆🏾

05/11/2021

Makala Mpya!
Ujauzito huongeza nafasi ya mama kupata kiungulia kwasababu homoni ya projesteroni hulegeza kiwambo hicho na kusababisha tindikali (acid) inayozalishwa tumboni hasa baada ya kula kurejea katika koromeo la chakula na kusababisha kiungulia.
Kawaida dalili za kiungulia zinatokea baada ya kula au kunywa, vilevile unaweza kupata dalili hizi wakati wowote kipindi cha ujauzito lakini mara nyingi zinatokea sana wiki ya 27 ya ujauzito na kuendelea. Miongoni mwa dalili hizo ni pamoja na:
➡Kujisikia kuungua, kuchoma au maumivu kifuani kutokana na tindikali za tumboni kurudi kwenye umio (esophagus)
➡Tumbo kujaa gesi
➡Uchachu mdomoni
➡Kujisikia kuumwa
➡Kubeua mara kwa mara
➡Kukohoa mara kwa mara
➡Kupata malengelenge kwenye mdomoni
➡Kujisikia kutapika.
Karibu kusoma makala yetu inayopatikana katika tovuti yetu (buff.ly/31MeSaG), upate kujua kiungulia kinasababishwa na nini na mbinu mbalimbali za kuzuia kiungulia wakati wa ujauzito.

https://buff.ly/31MeSaGmagonjwa-na-hali/kiungulia-wakati-wa-ujauzito/

   ⠀⠀Tunapoanza mwezi huu mpya tunawatakia amani,afya njema na mafanikio tele. Tunashukuru kwa kuendelea kutufuatilia tu...
01/11/2021

⠀⠀
Tunapoanza mwezi huu mpya tunawatakia amani,afya njema na mafanikio tele. Tunashukuru kwa kuendelea kutufuatilia tunapoendelea kuelimisha, kutoa taarifa na ushauri katika kupata ujauzito, ujauzito, malezi na mtoto.⠀⠀
Je, umeshapakua ?â €au umeshatembelea tovuti yetu (buff.ly/31MeSaG)?â €
Tuambie kwenye “comment". Karibu AfyaTrack

   ⠀⠀⠀⠀⠀⠀Nani k**a mama?⠀⠀⠀Ni siku nyingine ya kutambua na kuthamini uwepo wa mama katika familia na jamii zetu.⠀⠀⠀⠀⠀⠀Mt...
29/10/2021

⠀⠀⠀⠀⠀⠀
Nani k**a mama?⠀⠀⠀
Ni siku nyingine ya kutambua na kuthamini uwepo wa mama katika familia na jamii zetu.⠀⠀⠀⠀⠀⠀
Mtag mama yeyote unayemjua na kumpa neno moja la shukrani kwa malezi na kazi nzuri anayoifanya. Twende kazi💪⠀⠀⠀⠀⠀⠀
Je,umeshasoma makala zetu mpya ziliyoongezwa kwenye tovuti yetu?⠀⠀
Tunapenda kuwakumbusha kutembelea tovuti yetu ya afyatrack (buff.ly/31MeSaG) na kupakua inayopatikana googleplay store kwa watumiaji wa android tu.

   ⠀⠀Maneno ya kutia moyo na ujumbe wa shukurani kutoka kwa watumiaji wetu wa   na tovuti yetu ni moja ya mambo yanayole...
28/10/2021

⠀⠀
Maneno ya kutia moyo na ujumbe wa shukurani kutoka kwa watumiaji wetu wa na tovuti yetu ni moja ya mambo yanayoleta furaha,bidii na kujitoa zaidi.⠀⠀⠀⠀
Timu nzima ya afyatrack inapenda kukushukuru ndugu yetu Cain Chuhira kwa maneno ya kututia moyo na kuichagua AfyaTrack na huduma zetu. Mungu akubariki.⠀⠀
Asante sana na kila la kheri.⠀⠀

Makala Mpya!⠀⠀⠀Je, umesoma makala ipi kati ya hizi zilizoongezwa kwenye tovuti yetu hivi karibuni?⠀A. Kwikwi kwa mtoto m...
26/10/2021

Makala Mpya!⠀⠀⠀
Je, umesoma makala ipi kati ya hizi zilizoongezwa kwenye tovuti yetu hivi karibuni?â €
A. Kwikwi kwa mtoto mchanga baada ya kumnyonyesha.
B. Tatizo la kondo la nyuma kuachia kabla ya mtoto kuzaliwa (Placenta Abruption)â €
Tembelea tovuti yetu (www.afyatrack) ili usipitwe na makala zinaoongezwa kila wiki zenye ushauri na taarifa muhimu kuhusu kupata ujauzito, ujauzito, mtoto na malezi kwa lugha rahisi ya kueleweka. â €
Karibu AfyaTrack.â €

 Muonekano na jinsi ya kuitumia App yetu katika huduma ya ujauzitoHatua ya kwanza:Baada ya kupakua app yetu kutoka googl...
21/10/2021


Muonekano na jinsi ya kuitumia App yetu katika huduma ya ujauzito
Hatua ya kwanza:
Baada ya kupakua app yetu kutoka google playstore kwa watumiaji wa simu za Android (link ya kupakua app yetu inapatikana kwenye bio yetu), jisajili (register) kwa kujaza taarifa utakazoulizwa. Baada ya kujisajili ni muda wa kuingia (login) kwa kutumia namba ya simu uliyosajili au barua pepe yako pamoja na neno la siri (password).
Hatua ya pili:
Chagua huduma unayotaka kufuatilia
Hatua ya tatu:
Kwa huduma ya ujauzito, utahitajika kujaza tarehe yako ya kwanza ya mzunguko wako wa hedhi ya kawaida na idadi ya siku za mzunguko wako (cycle length) ili kukusaidia kukokotoa umri wa ujauzito wako.
Hatua ya mwisho:
Angalia k**a taarifa zilizotokea ni sawa na umri ujauzito wako, hakikisha kufuatilia taarifa utakazopewa kila wiki kulingana na umri wa ujauzito wako. Sambamba na taarifa hizo za ufuatiliaji kuna makala mbalimbali.
Karibu Afyatrack. K**a tayari umeshapakua na unaitumia tuambie kweye “comment".

   ⠀⠀⠀⠀Karibuni katika wasaa wa chemsha bongo kutoka AfyaTrack. Kipindi hichi chemsha bongo zetu zitatoka katika makala ...
20/10/2021

⠀⠀⠀⠀
Karibuni katika wasaa wa chemsha bongo kutoka AfyaTrack. Kipindi hichi chemsha bongo zetu zitatoka katika makala zinazopatikana katika tovuti yetu (buff.ly/31MeSaG) na . Kupitia chemsha bongo hizi wanafamilia wetu wa afyatrack mtapata wasaa wa kujua makala na taarifa za ufuatiliaji zinazopatikana katika tovuti na app yetu. Karibu kushiriki sasa⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀
Chemsha bongo ya wiki hii inapatikana katika makala yetu ya “Zifahamu aina mbalimbali za uzazi wa mpango" iliyoongezwa katika tovuti yetu siku kadhaa zilizopita.⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀
Shirikisha ndugu,jamaa na marafiki kadiri uwezavyo katika chemsha bongo hii. Twende kazi💪⠀⠀⠀⠀⠀

Makala za AfyaTrack!⠀⠀⠀Wiki hii katika tovuti yetu ya Afyatrack makala tatu zinatarajiwa kuongezwa katika tovuti yetu kw...
18/10/2021

Makala za AfyaTrack!⠀⠀⠀
Wiki hii katika tovuti yetu ya Afyatrack makala tatu zinatarajiwa kuongezwa katika tovuti yetu kwaajili ya kuongeza ufahamu na taarifa muhimu kwa familia yetu ya Afyatrack.⠀⠀
Tuambie kwenye “comment" makala ipi kati ya hizi tatu ungependa iongezwe ya kwanza katika tovuti yetu? ⠀

   ⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀Jumapili yako na familia inaendaje? Mtag ndugu na jamaa na kuwatakia jumapili njema na familia zao.⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀...
17/10/2021



⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀
Jumapili yako na familia inaendaje? Mtag ndugu na jamaa na kuwatakia jumapili njema na familia zao.⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀
Je, umeshasoma makala zetu mpya zilizoongezwa hivi karibuni katika tovuti yetu? Tembelea tovuti yetu (buff.ly/31MeSaG) sasa.
Makala zilizoongezwa hivi karibuni katika tovuti yetu ni pamoja na:
➡Tatizo la kondo la nyuma (yaani plasenta)kuachia kabla mtoto kuzaliwa.
➡Kwikwi kwa mtoto baada ya kunyonyeshwa.
➡Zifahamu aina mbalimbali za njia za uzazi wa mpango.

16/10/2021

Makala Mpya!
Karibu kusoma makala yetu mpya inayopatikana katika tovuti yetu sasa.
Tatizo la kondo la nyuma (yaani placenta) kuachia kabla mtoto kuzaliwa linasababishwa na mambo/hali kadhaa ambazo ni pamoja na:
Ulipata tatizo hili katika mimba zilizopita. K**a tatizo hili lilishawahi kukupata hapo awali una nafasi ya takribani asilimia kumi tatizo hili kutokea tena katika ujauzito wa sasa.

Uvutaji sigara. Utafiti mmoja ulionyesha wanawake waliokuwa wanavuta sigara kabla ya kushika ujauzito waliongeza nafasi ya kupata tatizo la kondo la nyuma kuachia kwa asilimia 40 kila mwaka waliovuta sigara.

Matumizi ya kokeni au madawa mengine ya kulevya. Tatizo hili linatokea kwa asilimia 10 ya wanawake wanaotumia madawa haya katika miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito (third trimester).

Shinikizo kubwa la damu kabla na baada ya kupata ujauzito, hakikisha mnalitafutia ufumbuzi tatizo hili wewe na mkunga wako ili liweze kudhibitiwa. Takribani ya nusu ya vifo vya watoto wachanga vinavyotokana na tatizo hili vinasababishwa na shinikizo kubwa la damu wakati wa ujauzito.

Matatizo ya kifuko cha maji yanayopatikana katika mfuko wa uzazi. Kifuko hichi cha maji kinatumika kumlinda mtoto ndani ya mfuko wa uzazi. Ikiwa kitu chochote kitapasua au kusababisha kuvuja kabla hujawa tayari kujifungua, nafasi ya kupata tatizo la kondo la nyuma kuachia inaongezeka.

Kushika ujauzito ukiwa na umri mkubwa. Nafasi ya kupata tatizo hili huongezeka k**a una umri wa miaka 35 au zaidi. Mara nyingi k**a mama ana umri zaidi ya mika 40.

Ukishika ujauzito wa mtoto zaidi ya mmoja. Wakati mwingine kujifungua mtoto wa kwanza kunafanya plasenta ijiachie kabla mtoto mwingine hajawa tayari kuzaliwa.

Kuumia eneo la tumbo. Inaweza kutokea k**a ulidondoka au kupata kipigo kikali tumboni. Inaweza kutokea k**a ulihusika katika ajali ya gari, kumbuka kufunga mkanda wa gari kila mara.
Unataka kufahamu dalili na ishara za mjamzito atakayepata tatizo hili? Tembelea tovuti yetu upate kusoma makala hii kamili. Link 👇

https://buff.ly/3j7IyJq

   ⠀⠀⠀Nani k**a mama?⠀⠀Ni siku nyingine ya kutambua na kuthamini uwepo wa mama katika familia na jamii zetu.⠀⠀⠀⠀Mtag mam...
15/10/2021

⠀⠀⠀
Nani k**a mama?⠀⠀
Ni siku nyingine ya kutambua na kuthamini uwepo wa mama katika familia na jamii zetu.⠀⠀⠀⠀
Mtag mama yeyote unayemjua na kumpa neno moja la shukrani kwa malezi na kazi nzuri anayoifanya. Twende kazi💪⠀⠀⠀⠀
Je,umeshasoma makala zetu mpya ziliyoongezwa katika tovuti yetu?
➡Kwikwi kwa mtoto baada ya kumnyonyesha
➡Tatizo la kondo la nyuma kuachia kabla mtoto kuzaliwa (Placenta Abruption) ⠀⠀
Tunapenda kuwakumbusha kutembelea tovuti yetu ya afyatrack (buff.ly/31MeSaG) na kupakua inayopatikana googleplay store kwa watumiaji wa android.⠀⠀
Karibu⠀⠀

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Afya Track posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Afya Track:

Share