10/07/2026
Warsha wa Familia ya mafunzo ya lugha unaofundishwa na HearWell, unalenga kuwawezesha wazazi na walezi kwa kuwapatia ujuzi na mbinu za kuwasaidia watoto wao wanaotumia vifaa za usikivu (Hearing Aids) na vifaa vipandikizi (Cochlear Implant) katika safari ya tiba ya usemi na lugha.
Warsha huu umeandaliwa kwa ushirikiano na MED-EL, na umetafsiriwa kwa Kiswahili ili uweze kutolewa kwa urahisi na ufanisi hapa Tanzania.
Katika video hii, Rashida Hassuji, Mtaalamu wetu wa Tiba ya Usemi na Lugha, anaelezea umuhimu wa mpango huu na jinsi unavyowasaidia watoto pamoja na familia zao kufikia maendeleo bora ya lugha na mawasiliano.
HearWell inaendelea kutoa huduma za hali ya juu za tiba ya usemi na lugha nchini Tanzania.
Kwa sababu tunajali.