10/10/2026
Kambi ya Uchunguzi na Matibabu. Apollo Hospitals - Bangalore, India na Kitengule Hospital watafanya Kambi ya Uchunguzi na Matibabu tarehe 20-21, Oktoba 2026. Kambi itakuwa na Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo, Saratani na Mfumo wa Mkojo. Kambi hii itafanyika Kitengule Hospital tarehe 20-21 Oktoba 2026. Madaktari wafuatao kutoka Apolo โ Bangalore watawahudumia wagonjwa.
Prof. Venkatesh Tekur - Daktari Bingwa wa Moyo
Wagonjwa wenye matatizo ya mishipa ya damu, shinikizo la damu, mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida, maumivu ya kifua na moyo kushindwa kufanya kazi.
Prof. Ravichandran Kosu - Daktari Bingwa wa Mfumo wa Mkojo
Wagonjwa wenye matatizo ya tezi dume, mawe kwenye figo au njia ya mkojo, shida ya kukojoa, damu kwenye mkojo na matatizo ya nguvu za kiume.
Prof. Sridhar PS - Daktari Bingwa wa Saratani
Wagonjwa wenye uvimbe wa aina mbalimbali kwa tathmini, pamoja na wanaohitaji uchunguzi na ushauri kuhusu saratani za matiti, koo, utumbo mpana, shingo ya kizazi na saratani nyingine. Pia atatoa ushauri kuhusu matibabu na ufuatiliaji wa saratani.
Kwa Appointment/ kuweka miadi ili kuweza kushiriki kambi hii, tafadhali tupigie kwa namba zifuatazo 0676 209 937 / 0766 384 851