Mpango wa Taifa wa Damu Salama - NBTS - Tanzania

Mpango wa Taifa wa Damu Salama - NBTS - Tanzania Ukurasa rasmi wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama Tanzania, chini ya Wizara ya Afya.

The National Blood Transfusion Service (NBTS) Policy Guidelines aim at providing guidance towards the establishment of well-organized blood transfusion services, in line with the World Health Assembly Resolution WHA 28.72 (adopted in 19th May 1975) that urges all member states to develop comprehensive and well-coordinated blood transfusion service based on voluntary, non-remunerated blood donation.

Damu inahitajika kila siku wakati wa dharura, upasuaji, kujifungua na katika hali mbalimbali za kiafya. Ndiyo maana kuch...
27/08/2026

Damu inahitajika kila siku wakati wa dharura, upasuaji, kujifungua na katika hali mbalimbali za kiafya. Ndiyo maana kuchangia damu mara kwa mara ni muhimu.

Kuna group mbalimbali za damu, na kila group ina nafasi muhimu katika kuhakikisha wagonjwa wanapata damu wanayoihitaji. ...
27/08/2026

Kuna group mbalimbali za damu, na kila group ina nafasi muhimu katika kuhakikisha wagonjwa wanapata damu wanayoihitaji. 🩸❤️
Je, unajua group yako ya damu?
Jua group yako ya damu. Mchango wako unaweza kuwa msaada muhimu kwa mtu anayehitaji.

Changia damu. Okoa maisha..

Hospitali zinahitaji damu kila siku. 🩸 Ndiyo maana kampeni au zoezi moja la uchangiaji haliwezi kuwa mwisho wa safari.Uh...
24/08/2026

Hospitali zinahitaji damu kila siku. 🩸 Ndiyo maana kampeni au zoezi moja la uchangiaji haliwezi kuwa mwisho wa safari.

Uhitaji wa damu unaendelea, na mchango wako unahitajika pia.

Kwa kuchangia damu mara kwa mara, tunasaidia kuhakikisha damu inapatikana wakati wowote inapohitajika—kwa wagonjwa wa dharura, wanaofanyiwa upasuaji, kina mama wakati wa kujifungua na wengine wanaohitaji.

Chupa moja ya damu inaweza kugawanywa katika sehemu mbalimbali na kusaidia kuokoa maisha ya hadi watu watatu.Songa mbele...
24/08/2026

Chupa moja ya damu inaweza kugawanywa katika sehemu mbalimbali na kusaidia kuokoa maisha ya hadi watu watatu.
Songa mbele. Changia damu. Okoa maisha.

Chupa moja ya damu inaweza kugawanywa katika sehemu mbalimbali na kusaidia kuokoa maisha ya hadi watu watatu.Songa mbele...
24/08/2026

Chupa moja ya damu inaweza kugawanywa katika sehemu mbalimbali na kusaidia kuokoa maisha ya hadi watu watatu.

Songa mbele. Changia damu. Okoa maisha.

Ulikuwa na wasiwasi kidogo? Fahari? Furaha? Hamasa? Hisia yoyote uliyonayo, kujua kwamba umemsaidia mtu anayehitaji ni j...
21/08/2026

Ulikuwa na wasiwasi kidogo? Fahari? Furaha? Hamasa?
Hisia yoyote uliyonayo, kujua kwamba umemsaidia mtu anayehitaji ni jambo la kujivunia.
Ulijisikiaje baada ya kuchangia damu? Tuambie hapa chini!

19/08/2026

Mchango wako hauishii pale unapochangia. Hupitia hatua muhimu za kupimwa, kuchakatwa na kuandaliwa kabla ya kuwafikia wagonjwa wanaohitaji. Kila hatua inalenga kuhakikisha mchango wako unakuwa sehemu ya safari ya kuokoa maisha.

Damu ni muhimu kwa mwili kufanya kazi vizuri, na wakati mwingine mtu anapohitaji kuongezewa damu, mchango wako unaweza k...
17/08/2026

Damu ni muhimu kwa mwili kufanya kazi vizuri, na wakati mwingine mtu anapohitaji kuongezewa damu, mchango wako unaweza kuwa tumaini na msaada mkubwa kwake.

04/08/2026

Siku moja. Kampeni moja. Kumbukumbu zitakazoishi milele. ❤️🩸

Dar es Salaam, mmetuonyesha maana halisi ya mshikamano.

Kila aliyefika, kila aliyechangia damu, kila aliyeshiriki kwa namna yoyote ile, amekuwa sehemu ya hadithi ya matumaini. Nyuma ya kila chupa ya damu lililotolewa, kuna maisha yatakayookolewa, familia zitakazopata tabasamu tena, na wagonjwa watakaopewa nafasi nyingine ya kuishi.

Kwa niaba ya waandaaji, tunawashukuru kwa moyo wenu wa kujitolea, nguvu zenu, na imani yenu katika kuokoa maisha. Dar es Salaam mmeandika historia, na historia hii itaendelea kuishi kupitia kila maisha yatakayoguswa na mchango wenu.

Asanteni kwa kuwa sehemu ya SongAmbele. Asanteni kwa kuchagua kuokoa maisha. Tuendelee kusonga mbele, pamoja. ❤️🩸

03/08/2026

Mwanza, mlijitokeza kwa nguvu. ❤️🩸

Mmetuonyesha kwamba jamii inapoungana kwa lengo moja, maisha yanaweza kubadilika.

Kila aliyefika, kila aliyechangia damu, na kila aliyeshiriki kwa namna yoyote ile amekuwa sehemu ya hadithi ya matumaini. Nyuma ya kila chupa ya damu iliyokusanywa, kuna maisha yatakayookolewa, familia zitakazorejeshewa matumaini, na wagonjwa watakaopata nafasi nyingine ya kuishi.

Kwa niaba ya waandaaji, tunawashukuru kwa moyo wenu wa kujitolea, mshikamano wenu, na imani yenu katika kuokoa maisha. Mwanza mmeacha alama isiyofutika, na matokeo ya mchango wenu itaendelea kuonekana katika maisha ya wengi.

Asanteni kwa kuwa sehemu ya SongAmbele. Asanteni kwa kuchagua kuokoa maisha. Tuendelee kusonga mbele, pamoja. ❤️🩸

Address

Dar Es Salaam
P.O.BOX65019

Opening Hours

Monday 08:00 - 18:00
Tuesday 08:00 - 18:00
Wednesday 08:00 - 18:00
Thursday 08:00 - 18:00
Friday 08:00 - 18:00
Saturday 08:00 - 18:00
Sunday 08:00 - 18:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mpango wa Taifa wa Damu Salama - NBTS - Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share