National Institute For Medical Research

National Institute For Medical Research The National Institute for Medical Research (NIMR) is a government research institution under the Ministry for Health established in 1979.

NIMR has the dual mandate to conduct and regulate health research on Tanzania Mainland. The National Institute for Medical Research (NIMR) is the largest public health research institution in Tanzania. It was established by the Parliament Act No. 23 of 1979 as a parastatal organization under the Ministry of Health. The establishment of NIMR was in recognition by the government of the need to gener

ate scientific information required in the development of better methods and techniques of enhancing disease management, prevention and control in the country.

This conference provides an opportunity to engage with leading minds, exchange knowledge, and contribute to meaningful c...
28/05/2026

This conference provides an opportunity to engage with leading minds, exchange knowledge, and contribute to meaningful change in our communities. Join us as we shape the future through science, innovation, and collaboration.

27/05/2026
๐—ก๐—œ๐— ๐—ฅ ๐—ฌ๐—ฎ๐—ฎ๐—ป๐—ฑ๐—ฎ๐—ฎ ๐— ๐—ฝ๐—ฎ๐—ป๐—ด๐—ผ ๐˜„๐—ฎ ๐— ๐—ฎ๐—ป๐˜‚๐—ป๐˜‚๐˜‡๐—ถ ๐Ÿฎ๐Ÿฌ๐Ÿฎ๐Ÿฒ/๐Ÿฎ๐Ÿณ ๐—ธ๐˜„๐—ฎ ๐—Ÿ๐—ฒ๐—ป๐—ด๐—ผ ๐—น๐—ฎ ๐—ž๐˜‚๐—ถ๐—บ๐—ฎ๐—ฟ๐—ถ๐˜€๐—ต๐—ฎ ๐—จ๐—ณ๐—ฎ๐—ป๐—ถ๐˜€๐—ถ ๐—ป๐—ฎ ๐—ง๐—ถ๐—ท๐—ฎTaasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa y...
23/05/2026

๐—ก๐—œ๐— ๐—ฅ ๐—ฌ๐—ฎ๐—ฎ๐—ป๐—ฑ๐—ฎ๐—ฎ ๐— ๐—ฝ๐—ฎ๐—ป๐—ด๐—ผ ๐˜„๐—ฎ ๐— ๐—ฎ๐—ป๐˜‚๐—ป๐˜‚๐˜‡๐—ถ ๐Ÿฎ๐Ÿฌ๐Ÿฎ๐Ÿฒ/๐Ÿฎ๐Ÿณ ๐—ธ๐˜„๐—ฎ ๐—Ÿ๐—ฒ๐—ป๐—ด๐—ผ ๐—น๐—ฎ ๐—ž๐˜‚๐—ถ๐—บ๐—ฎ๐—ฟ๐—ถ๐˜€๐—ต๐—ฎ ๐—จ๐—ณ๐—ฎ๐—ป๐—ถ๐˜€๐—ถ ๐—ป๐—ฎ ๐—ง๐—ถ๐—ท๐—ฎ

Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) imeandaa Mpango wa Manunuzi kwa mwaka wa fedha 2026/27, hatua inayolenga kuongeza ufanisi katika manunuzi ya umma na kuhakikisha utekelezaji wa shughuli za utafiti unafanyika kwa tija.
Kikao kazi cha maandalizi ya mpango huo kilianza tarehe 18 Mei 2026 kikihusisha wataalamu wa manunuzi, wateknolojia wa maabara, wahasibu, watafiti na wataalamu wa mipango, ufuatiliaji na tathmini wakiwakilisha vituo, vitengo na kurugenzi tatu za taasisii kwa lengo la kuandaa mpango wenye uhalisia unaoendana na bajeti na mahitaji katika utekelezaji wa kazi za utafiti.
Akizungumza baada ya kupokea taarifa ya maendeleo ya kikao hicho, Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Prof. Said Aboud, amesisitiza umuhimu wa kuandaa mpango wa manunuzi kwa umakini mkubwa na kuzingatia uwezo halisi wa kifedha ili kuepusha changamoto za mpango kutotekelezeka kwa kiwango kilichokusudiwa.
Ameelekeza maafisa manunuzi na ugavi kujiridhisha na mpango na bajeti za kila kitengo kabla ya kuingiza taarifa kwenye mfumo wa NeST, hatua ambayo amesema itasaidia kuongeza uwiano kati ya mpango na rasilimali fedha zilizopo.
Mpango huo unatarajiwa kuwezesha upatikanaji wa bidhaa na huduma muhimu kwa wakati, huku ukizingatia sheria, taratibu, kanuni na mahitaji halisi ya utekelezaji wa shughuli za taasisi hiyo katika mwaka wa fedha 2026/27.
Wizara ya Afya Tanzania imeendelea kusimamia na kuhimiza matumizi bora ya rasilimali za umma katika taasisi zake kwa lengo la kuboresha huduma za afya nchini.
/27

๐๐ˆ๐Œ๐‘ ๐˜๐š๐ž๐ง๐๐ž๐ฅ๐ž๐š ๐Š๐ฎ๐ฐ๐ž๐ค๐ž๐ณ๐š ๐Š๐š๐ญ๐ข๐ค๐š ๐Œ๐š๐ž๐ง๐๐ž๐ฅ๐ž๐จ ๐ฒ๐š ๐–๐š๐ญ๐ฎ๐ฆ๐ข๐ฌ๐ก๐ข ๐–๐š๐ค๐žTaasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) ime...
21/05/2026

๐๐ˆ๐Œ๐‘ ๐˜๐š๐ž๐ง๐๐ž๐ฅ๐ž๐š ๐Š๐ฎ๐ฐ๐ž๐ค๐ž๐ณ๐š ๐Š๐š๐ญ๐ข๐ค๐š ๐Œ๐š๐ž๐ง๐๐ž๐ฅ๐ž๐จ ๐ฒ๐š ๐–๐š๐ญ๐ฎ๐ฆ๐ข๐ฌ๐ก๐ข ๐–๐š๐ค๐ž

Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) imeendelea kuonesha dhamira yake ya kuwekeza katika maendeleo ya rasilimali watu kwa kushiriki Mkutano wa 13 wa Kitaaluma wa Chama cha Makatibu Muhtasi na Waandishi Waendesha Ofisi Tanzania (TAPSEA), uliofanyika katika Ukumbi wa Ngurdoto, mkoani Arusha, kuanzia tarehe 18 hadi 23 Mei, 2026.
Mkutano huo uliwakutanisha makatibu muhtasi na waandishi waendesha ofisi kutoka taasisi mbalimbali nchini kwa lengo la kujadili mabadiliko ya kiteknolojia, maendeleo ya kitaaluma pamoja na kuimarisha maadili, uwajibikaji na ufanisi katika utendaji kazi.
Katika mkutano huo, NIMR iliwakilishwa na makatibu muhtasi wanane kutoka Makao Makuu na katika vituo vyake nchini ambao ni Rukia Mbwana (Makao Makuu Dodoma), Dalin Chimbonaga (Mabibo), Charity Msangi (Tanga), Sikuzani Masaka (Tabora), Jacquline Mtambi (Makao Makuu Dodoma), Asia Mwanaupanga (Mbeya), Tabitha Temhanga (Dodoma) na Laika Tibishubwamu (Mwanza).
Ushiriki wa watumishi hao unaakisi dhamira ya dhati ya ya taasisi katika kuwajengea uwezo watumishi wake ili kuongeza tija, weledi na ubora wa huduma zinazotolewa kwa wananchi.
Mgeni rasmi kwenye mkutano huo alikuwa Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye alisisitiza umuhimu wa ubunifu, uwajibikaji, uadilifu na ufanisi k**a msingi wa maendeleo endelevu katika maeneo ya kazi.
Kaulimbiu ya mkutano huo ni: โ€œUbunifu, Uwajibikaji, Uadilifu na Ufanisi ni Mojawapo ya Misingi Imara ya Maendeleo Endelevu Kwenye Utendaji Kazi.โ€
Kupitia ushiriki huo, watumishi wa NIMR wanapata fursa ya kujifunza mbinu mpya za utendaji kazi, kubadilishana uzoefu wa kitaaluma pamoja na kujengewa uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya kiteknolojia katika mazingira ya kisasa ya kazi.
Ushiriki wa NIMR katika mkutano huo unaendelea kudhihirisha maono ya taasisi ya kuimarisha utendaji kazi kwa kuwekeza katika maendeleo ya rasilimali watu, weledi na utoaji wa huduma bora kwa jamii.

๐Ÿฎ๐Ÿฌ ๐——๐—ฎ๐˜†๐˜€ ๐˜๐—ผ ๐—š๐—ผ โณ ๐—ง๐—ต๐—ฒ ๐—ฆ๐—ฐ๐—ถ๐—ฒ๐—ป๐˜๐—ถ๐—ณ๐—ถ๐—ฐ ๐—–๐—ผ๐—ป๐—ณ๐—ฒ๐—ฟ๐—ฒ๐—ป๐—ฐ๐—ฒ ๐—œ๐˜€ ๐—”๐—น๐—บ๐—ผ๐˜€๐˜ ๐—›๐—ฒ๐—ฟ๐—ฒ!Soon, Arusha will bring together experts in health, research, a...
19/05/2026

๐Ÿฎ๐Ÿฌ ๐——๐—ฎ๐˜†๐˜€ ๐˜๐—ผ ๐—š๐—ผ โณ ๐—ง๐—ต๐—ฒ ๐—ฆ๐—ฐ๐—ถ๐—ฒ๐—ป๐˜๐—ถ๐—ณ๐—ถ๐—ฐ ๐—–๐—ผ๐—ป๐—ณ๐—ฒ๐—ฟ๐—ฒ๐—ป๐—ฐ๐—ฒ ๐—œ๐˜€ ๐—”๐—น๐—บ๐—ผ๐˜€๐˜ ๐—›๐—ฒ๐—ฟ๐—ฒ!

Soon, Arusha will bring together experts in health, research, and innovation on a dynamic platform to exchange ideas and shape solutions for the future.
This is more than a conference; it is an opportunity to engage with leading minds and contribute to meaningful change in our communities.
Be part of this journey.

๐—ง๐—ฎ๐—ณ๐—ถ๐˜๐—ถ ๐˜‡๐—ฎ ๐—”๐—ณ๐˜†๐—ฎ ๐—ป๐—ฎ ๐—ง๐—ถ๐—ฏ๐—ฎ ๐—”๐˜€๐—ถ๐—น๐—ถ ๐˜‡๐—ฎ๐—ฝ๐—ฒ๐˜„๐—ฎ ๐—ž๐—ถ๐—ฝ๐—ฎ๐˜‚๐—บ๐—ฏ๐—ฒ๐—น๐—ฒ ๐—•๐—ฎ๐—ท๐—ฒ๐˜๐—ถ ๐˜†๐—ฎ ๐—”๐—ณ๐˜†๐—ฎ ๐Ÿฎ๐Ÿฌ๐Ÿฎ๐Ÿฒ/๐Ÿฎ๐Ÿฌ๐Ÿฎ๐ŸณSerikali imeendelea kusisitiza umuhimu wa tafiti ...
15/05/2026

๐—ง๐—ฎ๐—ณ๐—ถ๐˜๐—ถ ๐˜‡๐—ฎ ๐—”๐—ณ๐˜†๐—ฎ ๐—ป๐—ฎ ๐—ง๐—ถ๐—ฏ๐—ฎ ๐—”๐˜€๐—ถ๐—น๐—ถ ๐˜‡๐—ฎ๐—ฝ๐—ฒ๐˜„๐—ฎ ๐—ž๐—ถ๐—ฝ๐—ฎ๐˜‚๐—บ๐—ฏ๐—ฒ๐—น๐—ฒ ๐—•๐—ฎ๐—ท๐—ฒ๐˜๐—ถ ๐˜†๐—ฎ ๐—”๐—ณ๐˜†๐—ฎ ๐Ÿฎ๐Ÿฌ๐Ÿฎ๐Ÿฒ/๐Ÿฎ๐Ÿฌ๐Ÿฎ๐Ÿณ

Serikali imeendelea kusisitiza umuhimu wa tafiti za afya na maendeleo ya tiba asili nchini baada ya maeneo hayo kupewa kipaumbele katika Bajeti ya Wizara ya Afya ya mwaka wa fedha 2026/2027 iliyowasilishwa bungeni leo jijini Dodoma na Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa.
Akiwasilisha bajeti hiyo, Mhe. Mchengerwa amesema Serikali itaendelea kuimarisha tafiti za afya na kuhamasisha matumizi ya matokeo yake katika maeneo ya kimkakati, sambamba na kusimamia afua za tiba asili na tiba mbadala nchini.
Pia amesema Serikali inaendelea kuimarisha huduma za tiba asili na tiba mbadala kwa kuhakikisha dawa mbalimbali zinafanyiwa tafiti za usalama na ufanisi ili zijumuishwe katika mfumo rasmi wa huduma za afya. Aidha, kiwanda cha NIMRโ€“Mabibo kimetajwa kuwa miongoni mwa maeneo yanayochangia kuendeleza huduma jumuishi za tiba asili nchini.
Katika hotuba hiyo, Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu imetajwa kuwa na jukumu la kuratibu, kudhibiti na kusimamia tafiti za afya nchini. Taasisi hiyo inaendelea kutekeleza tafiti za magonjwa ya kuambukiza, yasiyoambukiza, mifumo ya afya na tiba asili.
Katika mwaka wa fedha 2026/2027. NIMR imetengewa shilingi bilioni 4 kwa ajili ya shughuli za utafiti nchini.
Katika kipindi cha Julai 2025 hadi Machi 2026, Taasisi hiyo ilitoa vibali 513 vya tafiti za afya kati ya maombi 600 yaliyowasilishwa, sawa na asilimia 86.
Sambamba na uwasilishaji wa bajeti hiyo, maonesho ya taasisi za sekta ya afya yanayoendelea bungeni yameendelea kuvutia wabunge, viongozi wa Serikali na wananchi, huku banda la NIMR likiwa miongoni mwa yaliyopata mwitikio mkubwa.
Katika banda hilo, wageni wamepata fursa ya kujifunza kuhusu tafiti za afya zinazotekelezwa na NIMR, hususan tiba asili, pamoja na matumizi sahihi ya dawa za tiba asili.
Wataalamu wa NIMR wameendelea kutoa ufafanuzi kwa wabunge na viongozi waliotembelea banda hilo, hatua iliyoonesha kuongezeka kwa hamasa ya kujifunza kuhusu mchango wa tafiti za kisayansi katika kuboresha afya za Watanzania.
Bidhaa za tiba asili zinazozalishwa na NIMR Mabibo zimevutia wageni wengi waliopata bidhaa mbalimbali ikiwemo kinywaji lishe cha NIMREVIT, dawa za tiba asili zilizofanyiwa utafiti wa kisayansi na sabuni za ngozi.
Mwitikio wa wabunge, viongozi na wananchi katika banda la NIMR umeonesha kuongezeka kwa uelewa kuhusu mchango wa Taasisi katika tafiti za afya na maendeleo ya tiba asili zinazothibitishwa kisayansi kwa ajili ya kuboresha huduma za afya nchini.

๐—ก๐—œ๐— ๐—ฅ ๐—ฌ๐—ฎ๐—ป๐—ดโ€™๐—ฎ๐—ฟ๐—ฎ: ๐— ๐˜๐˜‚๐—บ๐—ถ๐˜€๐—ต๐—ถ ๐—ช๐—ฎ๐—ธ๐—ฒ ๐—”๐˜๐˜‚๐—ป๐˜‚๐—ธ๐—ถ๐˜„๐—ฎ ๐—ง๐˜‚๐˜‡๐—ผ ๐˜†๐—ฎ ๐—จ๐˜๐—ฒ๐—ป๐—ฑ๐—ฎ๐—ท๐—ถ ๐—•๐—ผ๐—ฟ๐—ฎ ๐—ธ๐—ฎ๐˜๐—ถ๐—ธ๐—ฎ ๐— ๐—ธ๐˜‚๐˜๐—ฎ๐—ป๐—ผ ๐˜„๐—ฎ ๐—ช๐—ฎ๐˜๐—ฎ๐—ฎ๐—น๐—ฎ๐—บ๐˜‚ ๐˜„๐—ฎ ๐—ฅ๐—ฎ๐˜€๐—ถ๐—น๐—ถ๐—บ๐—ฎ๐—น๐—ถ ๐—ช๐—ฎ๐˜๐˜‚Taasisi ya Ta...
10/05/2026

๐—ก๐—œ๐— ๐—ฅ ๐—ฌ๐—ฎ๐—ป๐—ดโ€™๐—ฎ๐—ฟ๐—ฎ: ๐— ๐˜๐˜‚๐—บ๐—ถ๐˜€๐—ต๐—ถ ๐—ช๐—ฎ๐—ธ๐—ฒ ๐—”๐˜๐˜‚๐—ป๐˜‚๐—ธ๐—ถ๐˜„๐—ฎ ๐—ง๐˜‚๐˜‡๐—ผ ๐˜†๐—ฎ ๐—จ๐˜๐—ฒ๐—ป๐—ฑ๐—ฎ๐—ท๐—ถ ๐—•๐—ผ๐—ฟ๐—ฎ ๐—ธ๐—ฎ๐˜๐—ถ๐—ธ๐—ฎ ๐— ๐—ธ๐˜‚๐˜๐—ฎ๐—ป๐—ผ ๐˜„๐—ฎ ๐—ช๐—ฎ๐˜๐—ฎ๐—ฎ๐—น๐—ฎ๐—บ๐˜‚ ๐˜„๐—ฎ ๐—ฅ๐—ฎ๐˜€๐—ถ๐—น๐—ถ๐—บ๐—ฎ๐—น๐—ถ ๐—ช๐—ฎ๐˜๐˜‚

Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) imeendelea kungโ€™ara katika kuenzi utendaji bora baada ya mtumishi wake kutoka kituo cha utafiti cha NIMR Amani, Bw. Fabio Avith Massawe, kutunukiwa cheti cha kutambuliwa k**a Mtumishi Bora wakati wa Mkutano Mkuu wa Pili wa Mwaka wa Jumuiya za Wataalamu wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu katika Utumishi wa Umma Tanzania.
Mkutano huo ulifanyika jijini Arusha katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) kuanzia tarehe 5 hadi 8 Mei, 2026 na kuwakutanisha wataalamu wa utawala na usimamizi wa rasilimali watu kutoka taasisi mbalimbali za umma nchini kwa lengo la kujadili mbinu bora za kuimarisha usimamizi wa watumishi, kuboresha utendaji kazi na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa umma.
Kutunukiwa kwa Bw. Fabio Avith Massawe kunatokana na juhudi, uwajibikaji na uzalendo wake katika utekelezaji wa majukumu ya kazi, hatua inayoendelea kuonesha ubora wa watumishi wa NIMR katika kuhudumia jamii kupitia sekta ya utafiti wa afya.
Katika mkutano huo, NIMR iliwakilishwa na watumishi sita wakiongozwa na Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi, Bi. Flora Mazelengโ€™we akiambatana na Meneja wa Rasilimali Watu na Utawala, Bi. Bupe Ndelwa na Maafisa Rasilimali watu wengine wanne kutoka katika vituo vya NIMR.
Mgeni rasmi alikuwa Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais โ€“ Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, ambaye alisisitiza umuhimu wa matumizi ya teknolojia, uwajibikaji na utoaji wa huduma bora katika utumishi wa umma.
Ushiriki wa NIMR katika mkutano huo unaakisi dhamira ya taasisi ya kuendelea kuwekeza katika maendeleo ya watumishi wake kupitia kujifunza, kubadilishana uzoefu wa kitaaluma na kuimarisha utendaji wa taasisi.
Kauli mbiu ya mkutano huo ilikuwa: โ€œKufikiria upya utoaji wa huduma za umma: Jinsi Serikali inavyoweza kutumia teknolojia kuanzisha huduma bora zinazolenga wananchi, kukabiliana na ukosefu wa ajira kwa vijana pamoja na changamoto za mazingira.โ€

05/05/2026

๐——๐—ผ ๐—ป๐—ผ๐˜ ๐˜„๐—ฎ๐—ถ๐˜ ๐˜๐—ผ ๐—ต๐—ฒ๐—ฎ๐—ฟ ๐˜๐—ต๐—ฒ ๐˜€๐˜๐—ผ๐—ฟ๐˜†โ€”๐—ฏ๐—ฒ ๐—ฝ๐—ฎ๐—ฟ๐˜ ๐—ผ๐—ณ ๐˜€๐—ต๐—ฎ๐—ฝ๐—ถ๐—ป๐—ด ๐—ถ๐˜.

Join us in Arusha for AJSC 2026 as we convene leading voices in health to shape the future of healthcare in Tanzania, advancing Universal Health Coverage toward Vision 2050.
With only a few days remaining, the time to decide is now.
Engage with experts, contribute your perspective, and take part in advancing meaningful change in the health sector.
#

Address

3 Barack Obama Drive
Dar Es Salaam
P.O.BOX9653

Opening Hours

Monday 08:00 - 16:00
Tuesday 08:00 - 16:00
Wednesday 08:00 - 16:00
Thursday 08:00 - 16:00
Friday 08:00 - 16:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when National Institute For Medical Research posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to National Institute For Medical Research:

Share