14/08/2026
Muda sahihi wa mjamzito kujifungua ni upi?
1.Wiki 39 hadi 40 ndiyo kipindi cha “full term”
Kwa mujibu wa American College of Obstetricians and Gynecologists (ACOG), ujau*ito wa wiki 39 hadi 40 huitwa full term. Hiki ndicho kipindi kinachochukuliwa kuwa ukomavu kamili wa ujau*ito, na kwa mimba isiyo na matatizo, kujifungua katika kipindi hiki kwa kawaida huwa salama zaidi.
2. Kujifungua wiki 37–38 kunawezekana, lakini huitwa “early term”
Mtoto anayezaliwa kuanzia wiki 37 hadi wiki 38 na siku 6 si mtoto njiti (preterm), lakini kitaalamu huitwa early term. Hii ina maana kwamba mtoto amefikisha muda wa kuzaliwa, lakini bado hajafikia kipindi cha full term.
Kwa hiyo, k**a mama na mtoto wako salama na hakuna sababu ya kitabibu, madaktari kwa kawaida hawaharakishi kujifungua kabla ya wiki 39. Hata hivyo, kuna mazingira maalumu ambapo daktari anaweza kupendekeza mtoto azaliwe mapema kwa sababu kuendelea na ujau*ito kunaweza kuwa na hatari zaidi kwa mama au mtoto
3. Wiki 40 si lazima iwe siku ya kujifungua
Watu wengi hufikiri kwamba mwanamke lazima ajifungue siku ambayo ametimiza wiki 40, lakini si hivyo. Wiki 40 ni makadirio ya tarehe ya kujifungua, si tarehe ambayo mtoto lazima azaliwe.
Mimba inaweza kuendelea baada ya wiki 40, na baadhi ya wanawake huanza uchungu wenyewe katika wiki ya 40 au 41. Ndiyo maana mama hapaswi kuingiwa na hofu kwa sababu tu amefikisha tarehe yake ya makadirio bila kujifungua.
4. Wiki 41 inahitaji ufuatiliaji wa karibu zaidi
Ujau*ito unapofikisha wiki 41, huitwa late term. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), kwa mwanamke mwenye ujau*ito usio na matatizo ambaye amefikisha wiki 41 kamili, kuanzishwa kwa uchungu wa kujifungua (induction of labour) kunapendekezwa ikiwa umri wa ujau*ito umejulikana kwa uhakika.
5. Wiki 42 au zaidi huitwa “post-term”
Ujau*ito unapofikisha wiki 42 au zaidi, huitwa post-term. Katika hatua hii, hatari zinazohusiana na kuendelea kwa ujau*ito huongezeka, ndiyo maana si vizuri mama kusubiri bila ufuatiliaji wa kitabibu. Ukifika huku unahitaji hatua za Haraka Zaidi.