The Vasima Jr15 Tz

The Vasima Jr15 Tz VASIMA JR15 �
Mwanza Tz
Pharmdawa �
plan,action, discipline and patience �

STOMACH ULCERS (MADONDA YA TUMBO)____________________________________________FAHAMU KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO NA TIBA YAK...
08/09/2024

STOMACH ULCERS (MADONDA YA TUMBO)
____________________________________________

FAHAMU KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO NA TIBA YAKE.
--------------------------------------------------------------------------------------------

👉🏽 Vidonda vya tumbo (Ulcers) ni ugonjwa unaowasumbua watu wengi kutokana na mfumo wa Maisha, ulaji mbaya na Mazingira tunayoishi Kwa ujumla.

👉🏽 Ugonjwa huu unasababisha kuwa na michubuko katika kuta za tumbo au utumbo mdogo na hivyo kusababisha maumivu makubwa ya tumbo.

CHANZO CHA VIDONDA VYA TUMBO

1️⃣ BAKTERIA
Chanzo kikubwa cha ugonjwa wa vidonda vya tumbo ni Bakteria waitwao Helicobacter pylori (H. pylori). Bakteria hawa huenezwa kwa kula chakula na kunywa maji. Katika mwili wa binadamu Bakteria hawa wapo katika mate na katika ute unaotanda juu ya kuta za Sehemu ya Utumbo Mwembamba (Duodenum) na mfuko wa tumbo.

2️⃣ MADAWA:
Matumizi makubwa ya dawa za kupunguza maumivu ya kichwa na maumivu mengine madogo madogo. Dawa hizo ni k**a aspirin, diclofenac, naproxen, ibuprofen n.k. Dawa hizi hupunguza uwezo wa tumbo wa kutengeneza utando wa ute wa kulikinga tumbo hivyo kulifanya liweze kuliwa kirahisi zaidi na tindikali.

3️⃣ POMBE NA TUMBAKU
Watu wanaokunywa pombe na wale ambao wanatumia tumbaku wanakuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kuupata ugonjwa huu wa vidonda vya tumbo.

4️⃣ Kutokula chakula kwa wakati au kula vyakula vyenye viungo vingi na pilipili nyingi.

5️⃣ Msongo mkubwa wa Mawazo N.K

DALILI YA VIDONDA VYA TUMBO

▶️ Tumbo kujaa gesi.
▶️ Tumbo kuwaka moto.
▶️ Kukosa choo au kupata choo kwa shida.
▶️ Kutapika nyongo
▶️ Kutapika damu au kuharisha.
▶️ Sehemu za mwili kupata ganzi.
▶️ Kukosa hamu ya kula.
▶️ Kusahau sahau na hasira bila sababu.

Hizo ni baadhi tu ya dalili za kuwa na vidonda vya tumbo lakini zipo nyingi, hivyo basi pindi uonapo moja kati ya hizo dalili ni vyema ukaenda kupima vidonda vya tumbo mapema.

MADHARA YA VIDONDA VYA TUMBO

1️⃣ KUVUJA DAMU TUMBONI
Hali hii yaweza kusababishwa na vidonda kuenea hadi kwenye mishipa ya damu na hivyo kufanya damu kuanza kuvuja. Hali hii ni hatari sana na inahitaji tiba ya dharura.

2️⃣ KUTOBOKA UKUTA WA TUMBO
Vidonda vya tumbo huweza kusababisha tundu (kutoboka kwa ukuta wa tumbo) na kufanya vitu vilivyo ndani ya utumbo kutapakaa katika tumbo (abdomen) Hali hii huitwa peritonitis na ni hatari sana na inahitaji matibabu ya dharura.

3️⃣ Vidonda vya tumbo vinaweza pia kuenea na kuathiri pia viungo vya jirani k**a vile ini au kongosho (pancrease).

4️⃣ KUZIBA KWA NJIA YA KUPITISHIA CHAKULA
Kuvimba kwa kuta za tumbo pamoja na makovu yanayosababishwa na vidonda hivi huweza kusababisha kuziba kwa njia ya kupitishia chakula kutoka kwenye tumbo (stomach) kwenda sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo (duodenum)

5️⃣ SARATANI YA TUMBO
Iwapo vidonda vya tumbo vimesababishwa na H. pylori, kuna uwezekano wa kati ya mara tatu hadi ya sita ya mgonjwa kupata Saratani ya tumbo (stomach cancer).

PTPE: VASIMA JR15

08/09/2024

I gained 7 followers, created 3 posts and received 5 reactions in the past 90 days! Thank you all for your continued support. I could not have done it without you. 🙏🤗🎉

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when The Vasima Jr15 Tz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share