22/12/2025
Chukua faida hiyo.
Kizunguzungu (Vertigo / Dizziness)
ni hali ya mtu kuhisi kizunguka kichwa, kupoteza mizani, au kuona vitu vinazunguka hata akiwa amekaa au amelala.
Sababu za kizunguzungu
Kizunguzungu kinaweza kusababishwa na mambo mengi, yakiwemo:
Shinikizo la damu
Damu kushuka sana au kupanda sana
Upungufu wa damu (anemia)
Tatizo la sikio la ndani
Mf. maambukizi ya sikio, maji au ear wax nyingi
Njaa au sukari kushuka
Msongo wa mawazo (stress)
Upungufu wa maji mwilini
Homa au maambukizi
Kuchoka sana au kukosa usingizi
Mabadiliko ya ghafla ya mkao
Kusimama ghafla kutoka kukaa au kulala
Magonjwa mengine
K**a malaria, UTI, au matatizo ya moyo.
Maradhi ya kienyeji
Tiba za asili (kiasili)
1. Kunywa maji ya kutosha
Kunywa maji mengi siku nzima ili kuzuia dehydration
2. Tangawizi
Chemsha kipande kidogo cha tangawizi kwenye maji
Kunywa kikombe 1 asubuhi au jioni
👉 Tangawizi husaidia mizani ya mwili na kupunguza kichefuchefu
3. Kitunguu saumu
Kula punje 1–2 ndogo pamoja na chakula
👉 Husaidia mzunguko wa damu
4. Maji ya limao + asali
Changanya maji ya uvuguvugu, limao kidogo na asali
Kunywa asubuhi
👉 Huongeza nguvu na sukari ya asili
5. Kupumzika vizuri
Epuka kelele nyingi, simama au lala kwa utaratibu
Pata usingizi wa kutosha
6. Kuvuta pumzi taratibu
Pumua polepole ndani na nje mara 5–10
👉 Hupunguza stress na kizunguzungu cha wasiwasi
7. Majani ya kiazi kikuu, Kwa kizunguzungu cha magonjwa y kiswali.
Mambo ya kuepuka
Kusimama ghafla
Njaa ya muda mrefu
Kunywa kahawa au soda nyingi
Dawa za kienyeji zisizojulikana au zenye mchanganyiko hatari
®MUHIMU SANA
⚠️ Nenda hospitali haraka k**a:
Kizunguzungu kinaendelea siku nyingi
Kinaambatana na kutapika, kupoteza fahamu, maumivu ya kifua, kuona giza, au maumivu makali ya kichwa
Unapoteza mizani hadi kuanguka.
Kwa ushaur au msaada