11/08/2025
Wengi wetu tukisikia juu ya kujihurumia, kujipenda kujithamini tunadhani na sisi tupo ndani ya kundi hilo.
Unataka kipimo halisi? Tazama jinsi unavyowatendea wale wenye damu yako.
Nguzo ya Msingi: Chuki ya Kujichukia Inaakisi kwa wale wenye uhusiano nao wa damu.
Hii ndio njia rahisi ya kisayansi kujua jinsi unavyojichukia, usivyojithamini na kutojionea huruma.
Imedhibitishwa:
Mojawapo ya vioo vya ndani zaidi vya kujithamini ambavyo havijachafuliwa ni jinsi tunavyowatendea wale wanaoshiriki damu yetu, hasa wale waliounganishwa na mzazi ambapo hitilafu ilitokea (k.m., upande wa mama ikiwa hitilafu ilikuja kupitia kwake).
Katika nadharia ya mifumo ya familia, chuki binafsi si ile unayowachukia watu wengine bali chuki binafsi ni wewe unajichukia mwenyewe na itatoka nje k**a:
➡️ Kuepuka
➡️ Dhana mbaya
➡️ Kinyongo
➡️ Kujitenga
➡️ Kujitoa kwa watu wa nje kuliko wale watu wa ndani
Kwa nini?
Kwa sababu nishati ya damu inaamsha kiwewe, na wasiwasi uliojengwa utotoni.
Unapokutana na wale wenye damu yako, Inatonesha majeraha ya utotoni ambayo huwenda hata huyajui.
Ni rahisi kukataa au kuharibu mahusiano hayo kuliko kukabiliana na maumivu na aibu ndani bila kutambua kuwa unachokikataa kipo ndani yako. Ni wewe ndio hujipendi.
Je unataka chanzo cha hali hii na madhara yake kwako binafsi?