15/07/2025
MADHARA YA KUTUMIA ENERGY DRINKS KWA MGONJWA WA SUKARI
Watu wengi hupendelea kutumia energy drinks pale wanapohisi uchovu ili kurudisha nguvu ka haraka kwenye ufanyaji kazi pasipo kujua zina athari kubwa sana na hasa ukishakua muhanga wa sukari sikushauri kabisa kutumia energy drinks kwasababu zifuatazo
🤌🏿 Energy drinks zina kiwango kikubwa cha wanga (sukari) ambayo ina athari kubwa sana kwenye kuongeza sukari na presha ya mgonjwa
🤌🏿 Energy drinks zina kiwango kikubwa cha caffein hivyo huongeza mapigo ya moyo na hii hupelekea kuongeza shida kwa mgonjwa wa sukari
🤌🏿Huongeza usambazaji mkubwa wa damu kwenye mwili na kupelekea kuongeza presha ya mgonjwa na kumzidishia shida mgonjwa wa sukari
🤌🏿 Energy drinks huongeza ufanyaji kazi wa seli mwilini hivyo inaweza ikapeleka kuongezeka kwa kiwango cha presha yako na hivyo kuongeza shida kwa mgonjwa wa sukari
🚦🚦🚦 MUHIMU
USITUMIE KABISA ENERGY DRINKS
Wanaozitengeneza wao hawatumii kwanini wewe unatumia 😧