ERY Herbal Clinic

ERY Herbal Clinic Huu ni ukurasa maalumu kwa ajili ya elimu ya tiba za magonjwa kupitia mimea | piga simu 0658505671

Unaukumbuka huu Msafara?😅📍Vist Loliondo
05/08/2026

Unaukumbuka huu Msafara?😅

📍Vist Loliondo

Hawa matapeli wameanza kuja hadi whatsap😅Wewe huwa unawajibuje?
05/08/2026

Hawa matapeli wameanza kuja hadi whatsap😅

Wewe huwa unawajibuje?

MAJANI YA MWAROBAINIMajani ya Mwarobaini (Azadirachta indica) yametumika kwa karne nyingi katika tiba za jadi kutokana n...
05/08/2026

MAJANI YA MWAROBAINI

Majani ya Mwarobaini (Azadirachta indica) yametumika kwa karne nyingi katika tiba za jadi kutokana na sifa zake mbalimbali za kiafya, usafi wa mwili na kinga dhidi ya magonjwa. Tafiti za kisayansi zimeunga mkono baadhi ya matumizi hayo.

■ Huchangia kuimarisha kinga ya mwili dhidi ya maambukizi.

■ Husaidia kupambana na bakteria, virusi na fangasi.

■ Huchangia katika afya ya ngozi na kusaidia kupunguza matatizo k**a chunusi, ukurutu na baadhi ya magonjwa ya ngozi.

■ Husaidia kuharakisha uponaji wa majeraha na kupunguza hatari ya maambukizi.

■ Husaidia kupunguza mba na kuwasha kwenye ngozi ya kichwa.

■ Huchangia kuimarisha mizizi ya nywele na afya ya ngozi ya kichwa.

■ Husaidia kuboresha afya ya kinywa kwa kupunguza hatari ya magonjwa ya fizi, utando wa meno (plaque) na harufu mbaya ya mdomo.

■ Baadhi ya tafiti zinaonyesha yanaweza kusaidia katika udhibiti wa kiwango cha sukari kwa watu wenye kisukari, lakini hayapaswi kuchukua nafasi ya matibabu yaliyoshauriwa na daktari.

■ Huchangia kuboresha mmeng'enyo wa chakula na kusaidia kupunguza choo kigumu.

■ Hutumika katika tiba za jadi kusaidia kupunguza minyoo ya tumbo.

■ Huchangia katika afya ya ini na kulilinda dhidi ya baadhi ya madhara ya msongo wa oksidishaji.

■ Husaidia kupunguza uvimbe na maumivu ya viungo.

■ Yametumika katika tiba za jadi kusaidia kupunguza homa, ikiwemo homa inayohusishwa na malaria.

■ Baadhi ya matumizi ya jadi yanayahusisha na afya ya uzazi, ingawa matumizi hayo yanahitaji tahadhari.

■ Maji ya majani ya mwarobaini yametumika katika tiba za jadi kutuliza muwasho wa macho, lakini hayapaswi kuwekwa machoni bila ushauri wa mtaalamu.

■ Husaidia kupambana na maambukizi ya fangasi k**a fangasi wa miguu na upele wa mviringo (ringworm).

■ Huchangia kufanya ngozi ionekane safi na yenye afya.

■ Pia hufukuza mbu na wadudu mbalimbali kwa asili.

KWANINI NI MUHIMU SANA KUWA NA MAARIFA YA MIMEA KATIKA TIBA ASILI?Kabla haujatazama picha kisha kuscroll kwenda sehemu n...
05/08/2026

KWANINI NI MUHIMU SANA KUWA NA MAARIFA YA MIMEA KATIKA TIBA ASILI?

Kabla haujatazama picha kisha kuscroll kwenda sehemu nyingine...tulia kidogo kwa sekunde chache usome ujumbe huu

Ikiwa unaishi kwa kutazama mbele (una maono) utagundua kwamba, — kuna umuhimu mkubwa sana wa kukusanya maarifa ya tiba asili, hasa inayotokana na mimea ya Porini, Magugu na Mitishimba.

Ulimwengu tunaouendea kwa sasa, Tiba lishe haitakuwa na Nguvu tena ya kuponya magonjwa, tazama sasa namna mbegu za G.M.O zinavyokuja kwa kasi sokoni. Unabaki unajiuliza ni nini hiki?

Hii ni kwa sababu Mimea mingi inayotumika k**a Tiba lishe ipo katika masoko ya kibiashara, hapo ndipo tatizo linaanzia, hawaangalii tena ubora wa asili, wanachojali ni ubora wa mwonekano, wingi wa uzalishaji—Ili wapige pesa!

Karibia mimea yote ya mboga, viungo na matunda inazidi kufanyiwa maboresho ya kijenetiki (GMO). Je, unatarajia kupata uponyaji kutoka kwenye lishe ya mboga, viungo na matunda ambayo kwa asilimia kubwa inazalishwa viwandani?

Fikiri kwa hekima na chagua kwa busara; k**a leo ungeandaliwa mezani Mayai ya kuku wa kienyeji na Mayai ya kuku wa kisasa–ungechagua kula mayai yapi?

Miaka michache ijayo kila kitu kitabadilika kabisa huu si unabii—lakini ni ufunuo wa kweli wa mwenendo wa Ulimwengu wetu wa sasa. Usipoweka hazina ya maarifa sasa, kizazi chako kitateseka kwa maradhi k**a si kuangamia kabisa.

Kimbilio la uhakika kwa uponyaji wa asili—litabaki katika Mimea ya Porini, Magugu na Mitishamba, ambayo leo unaona hakuna umuhimu wa kuijua.

Huu si wakati wa kupuuza kila mti unaoitwa mti dawa wa porini—ndiyo, unapaswa kukusanya kila aina ya maarifa, hakuna kuchoka, hakuna kukoma! Tumia gharama zako zote kupata Maarifa na urithi wa Asili.

Naam, ERY HERBAL CLINIC—Tumekamilisha kazi yetu kubwa ya kukuandalia kitabu cha "NGUVU YA MIMEA KATIKA TIBA ASILI" Ni maarifa ya kweli na "URITHI WA ASILI" wa kudumu kwa vizazi vijavyo. Ni kitabu chenye mimea zaidi ya 50, ambayo asilimia kubwa ni mimea ya porini, magugu na mitishamba; kinatoa ufafanuzi wa kitaalamu, na mwongozo rahisi wa matumizi yake katika kutibu Magonjwa mbalimbali.

Amua sasa kuwa miongoni mwa wachache wanaoona mbali na wenye kujua thamani ya Maarifa ya Tiba asili kupitia mimea ambayo—inapuuzwa na wengi lakini yenye nguvu ya kutibu.

Huu si wakati tena wa kutegemea Tiba lishe, GMO inaendelea kuharibu kila mmea wa Lishe, ni wakati wa kutegemea kila mche ambao hauguswi kibiashara—ni magugu na mitishamba.

Kusanya maarifa sasa.

Yahifadhi sasa.

Yarithishe kwa watoto wako sasa.

Maarifa ndiyo urithi pekee ambao hauchomwi na moto, hauibiwi na mwizi wala hauishi thamani.

Bei ya Kitabu hiki
🇹🇿 Tanzania — TSh 40,000
🇰🇪 Kenya — KSh 2,000
🇧🇮 Burundi — BIF 45,000
🇨🇩 DR Congo — CDF 35,000
🌍 Nje ya Afrika Mashariki — USD 16

Piga simu: 0658505671 kupata Nakala yako.

Whatsap: 0658 505 671

Hii ndiyo "Lonzwe" kwa kisukuma, ni jamii ya cactus🌵 na mara nyingi huitwa short au min cactusJinsi ya kutofautisha Lonz...
05/08/2026

Hii ndiyo "Lonzwe" kwa kisukuma, ni jamii ya cactus🌵 na mara nyingi huitwa short au min cactus

Jinsi ya kutofautisha Lonzwe na Igandaga

Lonzwe (Euphorbia spp) ina vimiiba, k**a unavyoona
Haiwashi kabisa
Inakua kwenda juu si kutambaa

Igandaga (Cissus quadrangularis) huwa haina miiba
Inawasha sana k**a upupu
Inakua kwa kutambaa

Ongeza tofauti zingine

05/08/2026

HEKIMA YA BURE

📌Usivae T-shirt iliyoandikwa "maji ni Uhai" kwenya msiba wa mtu aliyekufa kwa Mafuriko.

Mdharau asili hufa kikatili.Huko India mbegu za Isoma ng'ombe ni dili kubwa, taarifa zinaonyesha mpaka sasa zimeshaingiz...
05/08/2026

Mdharau asili hufa kikatili.

Huko India mbegu za Isoma ng'ombe ni dili kubwa, taarifa zinaonyesha mpaka sasa zimeshaingizwa kwenye masoko makubw aya kimataifa ambapo unga unaotokana na hizi mbegu (100 gram) unauziwa kwa dolla 15

Hizi mbegu kwa babari ya upungufu wa nguvu za kiume ni🔥

Ikiwa unateseka na Magonjwa ya zinaa, kisha ukakutana na mmea huu katika shamba lako, tafadhali usiuache.Chimba na utoe ...
05/08/2026

Ikiwa unateseka na Magonjwa ya zinaa, kisha ukakutana na mmea huu katika shamba lako, tafadhali usiuache.

Chimba na utoe mizizi yake
Isafishe vizuri, kisha uikate vipande vidogo vidogo
Chemsha katika maji angalau kwa dakika 15
Chuja na anza kunywa kikombe kidogo kutwa mara tatu.
Tumia kwa siku 7 hadi 21 kutegemea usugu wa maambukizi
Naam kwa uweza wa Mungu utapona

Ni mmea unaofanya vizuri katika kutibu magonjwa ya zinaa, na yanayohusiana na njia ya mkojo.

Katika simlizi za wazee wa jadi niliokutana nao wakati nafanya tafiti za mimea mbalimbali zinaeleza kwamba, huu mmea ulitumika kijadi kuficha mimba.

K**a uliwahi kusikia mtu ameficha mimba, basi tambua kuwa alitumia mimea na huwenda miongoni mwa mimea hiyo ni huu😄

Elimu Zaidi ya kitiba ya huu mmea inapatikana kwenye kitabu cha rejesha afya yako bila gharama sehemu ya II, kilicho katika mfumo wa nakala laini (Soft copy—Pdf)

Mdharau asili hufa kikatili

Hapa ndiyo mwisho wa Pumu (Asthma)
05/08/2026

Hapa ndiyo mwisho wa Pumu (Asthma)

Kimya cha muda mchache kwenye page yangu kilisababishwa maandalizi ya kukamilisha kazi kubwa ya kutoa kitabu hiki kwa mf...
05/08/2026

Kimya cha muda mchache kwenye page yangu kilisababishwa maandalizi ya kukamilisha kazi kubwa ya kutoa kitabu hiki kwa mfumo wa nakala ngumu (hadrcopy)

Ni kitabu cha kushika mkononi mwako na kusoma

Kinapatikana sasa kwa Tsh 40,000 tu

Hii ni bei ya Ofa itakayodumu hadi tarehe 31 Augost saa 5:59 usiku.

Simu 0658505671

Address

Geita

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when ERY Herbal Clinic posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share