Halisi Naturalist Tanzania

Halisi Naturalist Tanzania Welcome Halisi Naturalist Tanzania a trusted source for herbal medicine and natural health education.

Learn how to heal and restore your body naturally with proven remedies. 🌿

Whatsapp +255788900445
πŸ“Geita, Dar es salaam Tanzania

03/08/2026

JINI MAHABA (SPIRITUAL HUSBAND OR WIFE) PART 1

Huyu ni jini mshenzi mwenye kuangamiza maisha ya watu wengi sana, leo mamilioni ya watu duniani wanaishi maisha ambayo si yao kwasababu ya huyu kiumbe, tambua kuwa Spiritual husband (mume wa kiroho) au spiritual wife (mke wa kiroho) ni kiumbe wa ulimwengu wa roho ambaye amejifungamanisha na mtu kana kwamba ni mwenzi wake wa ndoa.

Wakati mwingine kiumbe huyo humvaa mtu tangu akiwa mtoto na hukua nae mpaka anaingia utu uzima, anakuwa anakujua nje ndani, anajua kila kitu kuhusu wewe, anajua udhaifu wako na uimara wako uko wapi, huyu kumuepuka sio jambo la mchezo, unahitaji kujitoa zaidi ya unavyoweza kufikiria, ana uwezo wa kukushawishi ufanye mambo fulani kwa kukuwekea mitego kulingana na jinsi anavyokujua kitabia na akafanikiwa kukuingiza kwenye mtego.

Huyu anayekuingia ukiwa mtoto mara nyingi ni wa kutoka kwenye generation ya ukoo wako, ni spirits za kutoka kwenu eidha umamani au ubabani,
Na wengi wameona ni ngumu kumtoa na kumuepuka wakaamua kuungana nae, yaani wakaamua kumkubali na kuishi nae kwa makubaliano, naposema makubaliano namaanisha unaingia nae makubaliano kwamba akuache huru katika jambo hili na lile na wewe utamuacha huru katika jambo hili na lile, lakini si kila mtu anaweza kukubaliana nae ndio hapo linapokuja swala la kupambana ili kuhakikisha unamuepuka na kuishi huru kwenye maisha yako.

Huyu ukishindwa kumdhibiti, ukawa wa kutumia dawa kwa mzaha au unafanya maombi kwa mzaha, unatumia dawa baadae unachoka unaacha, unafanya maombi unachoka unaacha, yaani ile hali ya kujidanganya au kudanganywa utatumia dawa siku chache eti umemaliza, aloo pole sana maana cha moto utakiona, maana unakuwa umeingia nae kwenye vita, atahakikisha maisha yako yanakuwa zaidi ya jehanamu katika kila eneo.

Kiumbe huyu huweza kuonyesha wivu kwa mahusiano ya mtu, hivyo atasababisha migogoro ya kimapenzi, kuvunjika au kuwafanya watu wasioe wala kuolewa kabisa.
Amini usiamini kuna watu wengi sana wanaishi na kiumbe huyu na maisha yao ya mahusiano ni k**a hadithi fulani ya kustaajabisha.

Dalili za kuwa una kiumbe huyu nimeshazieleza kwenye video zilizopita, nitaendelea kuleta masomo mengine zaidi kumuhusu.

Hii ni sehemu ya kwanza, sehemu ya pili itakujia na nitaeleza dawa mbali mbali ambazo unaweza kuwa unatumia ili kuendelea kutafuta nusura na hatimaye uwe huru na maisha yako.

Usiache ku-share sadaka hii kwa wengine.

Asanteni sana.

Welcome Halisi Naturalist Tanzania a trusted source for herbal medicine and natural health education. Learn how to heal and restore your body naturally with proven remedies. 🌿

Whatsapp +255788900445
πŸ“Geita, Dar es salaam Tanzania

31/07/2026

Mmea unaitwa Kivumbasi, kinachojulikana pia k**a Holy Basil au Tulsi, ni mmea unaoheshimiwa kwa karne nyingi katika maeneo mbalimbali ya Asia, hasa India, Afrika na maeneo mengine duniani.

Mbali na matumizi yake ya kiafya, mmea huu umepewa nafasi ya pekee katika mila, desturi, na imani za kiroho za jamii nyingi duniani,
Sio hadithi tu bali kwa waliowahi kuutumia wanajua ufanisi wake katika tiba za kiroho na kisayansi pia.

Mmea huu huondoa nguvu hasi, huimarisha mazingira ya kiroho, hufungua vifungo vya kichawi na kijini, husafisha nyota, n.k
Mmea huu unaweza kutumia wenyewe tu au kuchanganya na dawa zingine kutokana na shida uliyonayo.
Huko India huamini kwamba harufu ya Tulsi hutuliza akili, huongeza utulivu wa nafsi, na husaidia mtu kuwa na utulivu wakati wa kutafakari au kusali.

Leo nataka niwaeleze jinsi gani mtafanya ili kujifungua na kutengeneza nyota zenu kupitia mmea huu na chumvi, k**a wanakuchukia, riziki haieleweki licha ya juhudi kubwa kwenye utafutaji, mambo yako kuishia njiani, iwe ni kazi, biashara, mahusiano, maradhi.

Basi chukua mmea huu wa kivumbasi twanga au chemsha kisha changanya na chumvi ya mawe na oga kila siku mara mbili yaani asubuhi kabla ya jua kuchomoza na jioni jua linapozama, oga kwa manuwizi, ikiwezekana usiogee chooni, baada ya wiki moja mpaka mbili utaona mabadiliko makubwa.
K**a una mapepo/majini kunywa pia muda huo huo mara mbili, kipimo na glass moja.
Kwakweli itakusaidia sana.

Mungu ameweka siri kubwa katika mimea aliyoiumba, ametuletea tiba ya kila ugonjwa ni jukumu letu kutafuta maarifa sahihi.
Hayo ni machache tu kuhusu kazi za mmea huu, ninayo mengi sana ya kuwaeleza.

Ukiweza kupata dawa hizi, (kwa lengo la kubatilisha uchawi na kupandisha nyota) itakuwa bora zaidi, utazichanganya na mmea huo..
Tafuta Italigula, Muosha fedha, Mweza na Mfumbe.
Uwe unaoga kwa mtililiko huo huo, utanishukuru baadae.

Maarifa haya ni sadaka tu, basi usisite ku-share ili na wengine wapate sadaka hii.
K**a una swali uliza kwenye comments, asante πŸ™

Welcome Halisi Naturalist Tanzania a trusted source for herbal medicine and natural health education. Learn how to heal and restore your body naturally with proven remedies. 🌿

Whatsapp +255788900445
πŸ“Geita, Dar es salaam Tanzania

Kuna mtoto wako mwanafunzi hakumbuki chochote baada ya kutoka shuleni? Au hata wewe una tatizo la kusahau sana? Basi tum...
31/07/2026

Kuna mtoto wako mwanafunzi hakumbuki chochote baada ya kutoka shuleni? Au hata wewe una tatizo la kusahau sana? Basi tumia mmea huu, ni mujarabu sana kwa kuongeza na kuimarisha kumbukumbu.

Pia kwa shida ya hedhi na uzazi kwa ujumla, mmea huu unasaidia kusafisha na kuondoa shida kwenye mirija ya fallopian, kwenye kizazi, na kuboresha mayai ya mwanamke.

Matumizi ni kunywa glass moja kutwa mara tatu.
Tumia majani yake, utaandaa kwa kutengeneza juice au chai yake.
Ponda au twanga kisha changanya na maji.

Pia mmea huu unatibu matatizo ya Nuksi, mikosi ukichanganya na dawa zingine, somo hilo nitalitoa siku zijazo.

Usiache kushare na wengine wapate sadaka hii, mimi natoa sadaka tu, tubadirishane maarifa je wewe unatumiaje mmea huu na unauitaje huko kwenu?

Sisi tunauita nyantunda na kwa kitaalamu unaitwa Lantana Camara.

NOTE: USIWEKE NAMBA YAKO YA SIMU KWENYE COMMENT, WALA USICHUKUE NAMBA YOYOTE YA SIMU ILIYOWEKWA NA MATAPELI WANAOJIFANYA WANA WAGANGA WAO, TAFADHARI ZINGATIA ILI USIJE KUTAPELIWA.

Halisi Naturalist Tanzania

31/07/2026
30/07/2026

Wazee wako wakitaka kukupa laana kwa kikwetu wanatumia mti huu.

Mti wa msazi una tiba kubwa sana ndani yake, kwa wale ambao somo hili liliwapita nimelirudia , tazama kwa umakini.

Inaitwa Umutima wi sii, kwa ajili ya matatizo ya moyo, presha πŸ‘πŸ‘
29/07/2026

Inaitwa Umutima wi sii, kwa ajili ya matatizo ya moyo, presha πŸ‘πŸ‘

29/07/2026

K**a una shida ya figo, sumu mwilini, mawe kwenye figo, kunywa maji haya utajishukuru baadae.

Mgomba wa ndizi una tiba nyingi sana, sisi tunaoishi maisha ya asili tunauheshimu sana mmea huu.

Je umewahi kutumia mgomba kujitibia?
Follow us kwa elimu ya tiba asili Halisi Naturalist Tanzania

Huu ni mchunga, figo na magonjwa ya njia ya mkojo unatibu vizuri sana
29/07/2026

Huu ni mchunga, figo na magonjwa ya njia ya mkojo unatibu vizuri sana

Ni dawa ya macho, kutoa uchawi na kinga nzuri sana. πŸ”₯πŸ”₯
29/07/2026

Ni dawa ya macho, kutoa uchawi na kinga nzuri sana. πŸ”₯πŸ”₯

29/07/2026

Nywele au ndevu za mahindi ni mujarabu kwa mtu mwenye matatizo ya kukojoa kitandani, mwenye matatizo ya miguu kuuma au kuwaka moto, na mgonjwa wa P.I.D

1. Chemsha hizo nywele muhusika awe anakunywa mara 3 kwa siku, siku 7

2. P.I.D chemsha nywele hizi kisha chukua ndimu katakata vipande vidogo vidogo tia ndani ya sifuria la ndevu hizi, chemsha kwa moto mdogo si mkali, baadae chuja, kunywa glass moja kutwa mara 2 kwa siku 7.

3.Miguu nimezungumza katika video, sikiliza kwa umakini, kisha share video na wengine wapate sadaka hii.

Halisi Naturalist Tanzania Halisi Naturalist

Address

Geita Bukombe
Geita
0000

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Halisi Naturalist Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Halisi Naturalist Tanzania:

Shortcuts

Share