TFNC Tanzania

TFNC Tanzania Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from TFNC Tanzania, Nutritionist, Ilala.

11/08/2026

Je, ni kweli kwamba mama akiwa na matiti madogo, hawezi kuzalisha maziwa mengi ukilinganisha na mama mwenye matiti makubwa?

08/08/2026
Heri ya Sikukuu ya Nanenane
08/08/2026

Heri ya Sikukuu ya Nanenane

Tunafurahi kuona kizazi kipya kikijifunza na kuonesha shauku kubwa ya maarifa! Karibuni katika banda letu kwenye Maonesh...
07/08/2026

Tunafurahi kuona kizazi kipya kikijifunza na kuonesha shauku kubwa ya maarifa! Karibuni katika banda letu kwenye Maonesho ya Nanenane, Viwanja vya Dkt. John Samweli Malecela, Nzuguni jijini Dodoma. 📚✨

06/08/2026

TFNC YATOA WITO KWA WAJASIRIAMALI NANENANE: NJOONI MJIFUNZE UANDAAJI SAHIHI WA UNGA MCHANGANYIKO

Dodoma, na Mwandishi Wetu.

Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) imetoa wito kwa wajasiriamali na wazalishaji wa unga mchanganyiko wa vyakula vya watoto kutembelea banda lao katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Nanenane ya yanayoendelea kufanyika jijini Dodoma katika Viwanja vya Dkt. John Samweli Malecela Nzuguni, ili kujifunza dondoo muhimu za namna ya kuandaa unga huo kwa usahihi.

Wito huo umetolewa Afisa Lishe Mtafiti kutoka TFNC, Stephano Ngunzwa, wakati akizungumza kuhusu umuhimu wa lishe bora kwa makundi maalumu, hususan watoto wadogo wenye umri wa kati ya miezi 6 hadi 23.

“Tunawakaribisha wajasiriamali na wazalishaji wote wanaofanya biashara hii au wanaonuia kuanza, waje kwenye banda letu. Lengo letu ni kuwapa miongozo na dondoo sahihi za namna ya kuandaa unga mchanganyiko (composite flour) unaokidhi vigezo vya afya na ukuaji bora wa mtoto,” alisema Ngunzwa.

Aida Nguzwa amesema Wajasiriamali watakaotembelea banda la TFNC watanufaika na mafunzo ya vitendo yanayohusu:

* Uwiano Sahihi wa Nafaka: Namna ya kuchanganya nafaka, mikunde, na mbegu za mafuta bila kuharibu mfumo wa usagaji chakula wa mtoto.

* Usafi na Usalama wa Chakula: Mbinu za kuzuia sumukuvu (aflatoxins) wakati wa kukausha na kusaga mazao.

* Uongezaji wa Thamani: Jinsi ya kuzalisha bidhaa zinazokubalika sokoni kulingana na miongozo ya ubora wa chakula nchini.

Ushiriki wa TFNC kwenye maonesho ya mwaka huu unaenda sambamba na kaulimbiu ya Nanenane 2026 inayosisitiza utambuzi wa soko na kuongeza tija kuelekea Dira ya Maendeleo ya 2050. Kupitia elimu hii, taasisi inalenga kutokomeza udumavu na utapiamlo kwa watoto, huku ikisaidia wajasiriamali wa ndani kuzalisha bidhaa salama na zenye ushindani wa kibiashara.

Maonesho ya Nanenane yanatarajiwa kilele chake tarehe 8 Agosti 2026, hivyo wananchi na wadau wote wa lishe wanahimizwa kufika viwanjani hapo mapema kujipatia maarifa.

04/08/2026
04/08/2026

Je, maziwa ya mwanzo ya mama ni machafu?

TFNC YAWAKUTANISHA WADAU KUBORESHA MAPAMBANO DHIDI YA UTAPIAMLO KWA WATOTO CHINI YA MIAKA MITANO.Taasisi ya Chakula na L...
03/08/2026

TFNC YAWAKUTANISHA WADAU KUBORESHA MAPAMBANO DHIDI YA UTAPIAMLO KWA WATOTO CHINI YA MIAKA MITANO.

Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) imewakutanisha wadau mbalimbali wanaojihusisha na programu ya kupambana na ukondefu kwa watoto wenye umri wa miaka mitano ili kutambua na kujadili maeneo yenye changamoto katika utekelezaji wa  mwongozo wa kuzuia na kutibu utapiamlo mkali (ukondefu) na kisha kupendekeza mikakati na hatua za kufuata .

Kikao kazi hicho cha siku mbili kinafanyika mkoani Morogoro kikilenga kujadali masuala mbalimbali ikiwemo kuthamini hali ya sasa, changamoto, na fursa katika uzuiaji na udhibtiti wa Utapiamlo mkali.

Mwaka 2025 Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau ilifanya mapitio ya  mwongozo wa kuzuia na kutibu utapiamlo mkali (ukondefu)  kwa watoto chini ya miaka mitano kulingana na mapendekezo ya Shirika la Afya Duniani 2023. Mapitio haya yalilenga kuboresha afua za kuzuia na kutibu utapiamlo mkali (ukondefu) katika ngazi ya jamii na katika vituo vya kutolea huduma za afya.

katika kuhakikisha mwongozo huo unatekelezwa kwa ufanisi, imeonekana kuwa ni muhimu kufanya uchambuzi wa kina kubaini maeneo yenye changamoto za utekelezaji na kujadili mikakati na hatua za kuchukua ili kutatua changamoto hizo.

Katika Maadhimisho  ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama Duniani, haya ni mambo muhimu unayopaswa kufahamu kuhusu unyo...
02/08/2026

Katika Maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama Duniani, haya ni mambo muhimu unayopaswa kufahamu kuhusu unyonyeshaji wa maziwa ya mama.

Wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama Duniani 2026 "Mwanzo imara wa Maisha ya mtoto, Huanza na maziwa ya mama"
02/08/2026

Wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama Duniani 2026

"Mwanzo imara wa Maisha ya mtoto, Huanza na maziwa ya mama"

Address

Ilala

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00

Telephone

0658990996

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when TFNC Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share

Category