30/12/2025
MAOMBI YA UKOMBOZI WA FAMILIA.
Mungu anapotaka kufanya jambo fulani katika eneo fulani huwa anaanza na mtu mmoja.
Mara zote hutumia mtu mmoja kuleta ukombozi katika familia, au jamii au hata taifa.
Wewe kupata nafasi ya kujua haya na kujifunza haya ni kwa sababu Mungu anataka kufanya jambo juu ya familia yako.
Ndiyo maana uko hapa leo. Na leo tunashughulika na ukombozi wa familia.
Kuna vitu vingi sana ambavyo vipo katika familia nyingi na si vya Mungu, wala havikupangwa na Mungu.
Na watu wengi hawajui chanzo chake ni nini.
Luka 11:21-22 Mtu mwenye nguvu aliyejifunga silaha zake, alindapo nyumba yake, vitu vyake vi salama; lakini mtu mwenye nguvu kuliko yeye atakapomwendea na kumshinda, amnyangβanya silaha zake zote alizokuwa akizitegemea, na kuyagawanya mateka yake.
Bwana Yesu anaongelea mtu mwenye nguvu za rohoni na sio mwilini. Na hapa anaongelea mtu ambaye ni roho inayosababisha aina fulani ya mateso au matatizo katika familia fulani.
Kila familia ina hivi vitu. Familia nyingi hasa za kiafrika zilijikabidhi kwa shetani kupitia milango ya mila, mfano ya ibada mizimu, miti, milima mawe nk
Mengineyo ni ushirikina uliokuja kwa sababu ya ndoa mitala.
Sasa hivi vitu vilitoa nafasi ya uharibifu kwa shetani katika familia.
Ndio maana familia nyingi ziko chini ya vifungo vingi.
1. Magonjwa
2. Umasikini
3. Uchawi na ushirikina
4. Chuki
Utajuaje kuwa hivi vipo katika familia.
Ni kupitia udhihirisho wa Magonjwa ya kurithi, uchumi duni, viburi, hasira zisizo za kawaida n.k
Na isipokuwa vimeshughulikiwa vitaendelea kizazi baada ya kizazi.
Ndiyo maana kwenye mstari wetu ule, Bwana Yesu anasema mtu mwenye nguvu atakapomwendea na kumshinda na kumnyanganya mateka yake.
Ni lazima apatikane mtu, na Mungu amekuandaa wewe kwa ajili ya familia yako.
Karibu tuombe.
1. Mshukuru Mungu kwa rehema zake juu ya familia yako. Mtukuze maana yeye ndiye Mungu wa kweli. Tamka hukumu ya Bwana juu ya miungu yote ilikuwa inafanya kazi katika familia yako.