17/03/2026
SIRI YA WASHINDI
Huko Porini:
1) Tembo ndiye mkubwa kuliko wote
2) Twiga ndiye mrefu kuliko wote
3) Mbwa Mwitu ndiye mwerevu kuliko wote
4) Duma ndiye mwenye kasi kuzidi wote
Lakini, Simba ndiye MFALME wa pori bila hata ya kuwa na mojawapo ya sifa hizo.
Kwanini?
Kwasababu:
1. Simba ni jasiri, ana msimamo, hutembea kwa kujiamini, huthubutu kufanya chochote na kamwe haogopi.
2. Simba huamini kuwa hazuiliki
3. Simba huthubutu mambo yenye hatari
4. Simba huamini kuwa kila mnyama anamfaa kwa chakula
5. Simba huamini kuwa kila fursa inafaa kujaribiwa na haachi imponyoke mkononi mwake
Hivyo.......
1) Huhitaji kuwa mwenye kasi kuliko wote
2) Huhitaji kuwa mwerevu kuliko wote
3) Huhitaji kuwa mwenye akili kuliko wote
4) Huhitaji kuwa na kipaji kuliko wote
Unahitaji kuwa na nini?
1) Unahitaji kuwa jasiri
2) Unahitaji kuwa na utayari wa kujaribu
3) Unahitaji imani ya kuamini kuwa yote yanawezekana
4) Unachohitaji ni kujiamini kuwa unaweza kufanya!!!
Simba hulala saa 20 na hufanya kazi saa 4 na bado hula nyama.
Lakini tembo hufanya kazi saa 24 na hula nyasi tu
Mtazamo wako wa maisha ndio hujalisha zaidi katika kukabiliana na hali za maisha na matukio ili uweze kuibuka kidedea na kuwa mshindi wakati wote.
🙏🙏🙏🙏