15/06/2026
KUTOKA NADHARIA HADI VITENDO: HOSPITALI YA MBALIZI-IFISI YAFUNGUA MILANGO YA KITAALUMA KWA WANAFUNZI WA MUST! 🎓💼
Hospitali ya Mbalizi-Ifisi inatambua mchango mkubwa wa sekta ya afya katika kukuza elimu na weledi wa vitendo kwa wataalamu wetu wajao nchini.
Mapema leo tarehe 15/06/2026 tulipata heshima ya kuwakaribisha wanafunzi wa Mwaka wa pili kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST), wanaosomea fani ya Business Administration in Marketing and Entrepreneurship.
Wanafunzi hawa walipata fursa ya kujifunza kwa kina na kwa vitendo mifumo ya usimamizi na menejimenti ya masoko katika sekta ya afya (Hospital Marketing Management) kutoka kwa Katibu wa Afya wa Hospitali Bi. Faustina Mahenge. Kupitia darasa hili la vitendo, vijana hawa wamejionea jinsi misingi ya kibiashara, ujasiriamali, na huduma bora kwa wateja zinavyounganishwa ili kutoa huduma bora na za uhakika kwa jamii yetu.
Pia walifanikiwa kutembelea Idara Mbalimbali ikiwemo Idara ya Huduma kwa Wateja, Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Idara ya Mapokezi na Idara ya Magonjwa ya Nje (OPD) na kujionea namna vitengo hivyo vinavyowahudumia wateja.
Mafunzo hayo yalihudhuriwa na Afisa Mdhibiti Ubora wa Hospitali Ndg. Nestory Bujiku, Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Ndg. Albert Macha na Afisa Habari wa Hospitali Ndg. Sadick Issa.
Sisi k**a Hospitali ya Mbalizi-Ifisi, tunaamini katika malezi ya kitaaluma na kuwajengea uwezo vijana ili kuandaa nguvu kazi thabiti na yenye ubunifu kwa taifa letu la kesho.
Tunawashukuru viongozi na wanafunzi wa kwa kuchagua kujifunza nasi!