Ufugaji bora Tanzania

Ufugaji bora Tanzania Ufugaji bora ni pamoja na afya ya mnyama mwenyewe unayemfuga..basi jifunze jinsi ya kufanya ili uwez

15/06/2023

Nitafute kwa ushauri juu ya ufugaji

*CHANJO CHANJO CHANJO NI MUHIMU*👉Katika kipengele muhimu ambacho mfugaji hapaswi kukipuuza ni chanjo kwa kuku, Kwani cha...
28/06/2020

*CHANJO CHANJO CHANJO NI MUHIMU*

👉Katika kipengele muhimu ambacho mfugaji hapaswi kukipuuza ni chanjo kwa kuku, Kwani chanjo huongeza kinga ya kuku kupambana na vimelea vya ugonjwa husika kabla haujaanza kushambulia kuku

Zipo chanjo za aina tofauti tofauti ambazo zimegawanyika katika makundi,

👆 *Live vaccine*, hizi ni zile ambazo hutumia vimelea hai vilivyo pumbazwa ( *In active* )vya magonjwa mfn Virus husika wa magonjwa k**a

Newcastle Disease Vaccine( Chanjo ya Kideri),

Infectious Bronchitis vaccine,

Infectious Bursal Disease Vaccine(Chanjo ya Gumboro),

Fowl Pox Vaccine(Chanjo ya ndui).

Kuna baadhi ya chanjo huwa ni adimu sana kupatikana ,

K**a
👉Chanjo ya Salmonella
👉Chanjo ya Corryza
👉Chanjo ya MG

ila kwa urahisi unaweza kuwatafuta *ZOETIS* au *CEVA* , na makampuni mengine ya madawa ya mifugo huwa niwasambazaji na wauzaji wakubwa wa chanjo za mifugo.

👆 *Vitu vya kuzingatia , Kabla, wakati na baada ya chanjo.*

👉Kuku hapaswi kuwa mgonjwa.
👉Kuku hapaswi kuwa kwenye dozi ya dawa.
👉Usafi wa vyombo vya kuchanjia.
👉Kusoma Expire date na Batch namba
👉Dose ya chanjo( 500,1000,5000) usikariri kwamba chanjo zinafanana ujazo.
👉Umri wa kuku, uwiane na aina ya chanjo.
👉Chanjo zizingatie cold chain ,yaani zihifadhiwe katika hali ya ubaridi na kutolewa pale tu itakapo kua inatumika kwa chanjo

*NB: LIVE VACCINE USIBADILISHE RATIBA.*

Ratiba za chanjo zinatofautiana kutokana na aina ya kuku

👆Kwa kuku wanaotaga( Layers ,Chotara, kienyeji) mfumo wao wa chanjo kitaalamu na kwa maelekezo ya miongozo mingi ya chanjo

Siku ya kwanza Marek's Vaccine.

Siku ya 7 Newcastle Vaccine/kideri

Siku ya 14 Gumboro, Infectious Bursal Disease Vaccine

Siku ya 21 Newcastle Vaccine (kideri).

Siku ya 28 Gumboro, Infectious Bursal disease.

Siku ya 30 Fowl Pox Vaccine( chanjo ya ndui). Usiipuuze japo ni gharama kati ya (15000-18000).

Rudia Newcastle Vaccine kila baada ya miezi mitatu.

👉Kwa kuku wa nyama, *(Broilers)*

*Mfumo wa kwanza*
👆Siku ya 7 chanjo ya Newcastle/kideri.
👆Siku ya 14 Gumboro
👆Siku ya 21 Gumboro

*Mfumo wa pili*
👆Siku ya 7 newcastle /kideri
👆Siku ya 14 Gumboro/Infectious Bursal Disease
👆Siku ya 21 Newcastle/kideri

*MFUMO WA UCHANJAJI.*
👉Kwa chanjo za maji,
🐣Safisha vyombo vya maji
🐣Wape kuku chakula , na uondoe maji kwa masaa mawili kabla ya kuweka maji ya chanjo

🐣Andaa maji ya chanjo, kwa Kuchemsha, au Kuweka dawa ya kuondoa Chlorine(Cevemune-Chlorex blue) yakae dakika 15

🐣Changanya chanjo kwa kuzingatia dozi ya chanjo kwa uwiano wa idadi ya kuku.

🐣Wape kuku chanjo na maji ya chanjo yakae masaa mawili kisha yaondoe na uwape maji yasiyo na chanjo ( unaweza kuweka vitamins baada ya kutoa maji ya chanjo).

👉Chupa za chanjo, maji ya chanjo yaliyobaki yamwagwe/ kutupwa mbali na mazingira ya banda la kuku.

👆👆Kwa chanjo zinazohitaji usimamizi k**a chanjo ya *Ndui* na zote za *dead vaccine* Nivema ifanywe na Daktari wa mifugo , au Chini ya usimamizi wa Daktari wa mifugo.

*Nauza Kitabu change cha Ufugaji kuku...FUGA KUKU KITAALAMU 10000/=* mikoa yote TZ

*Nauza Formula ya kuchanganya chakula cha kuku CHOTARA na LAYERS 20000*

*CHANJO NI MUHIMU KWA KUKU USIPUUZE.*

Imeandaliwa na
*Greyson Kahise*
Mtaalamu wa Kuku
*0769799728 0715894582*

04/06/2020

Mastatis case(ugonjwa wa kiwele)fahamu njia za kufuata ilikuweza kutibu ugonjwa huu💪
Link on a bio

Jua kuhusu magonjwa hatarishi ya kuku,leo nimekuletea ugonjwa hatarishi wa kuku pamoja na dalili zake,bofya link hapo ch...
19/07/2019

Jua kuhusu magonjwa hatarishi ya kuku,leo nimekuletea ugonjwa hatarishi wa kuku pamoja na dalili zake,bofya link hapo chini uweze kuona dalili za huu ugonjwa ‘ASPERGILLOSIS’ au Brooder pneumonia...

Unaitwa Aspergillosis in poultry (Brooder pneumonia) -Ni aina ya ugonjwa ambao ni hatarishi hasa kwa kuku wadogo ambao huanza kufugwa kutoka siku ya kwanza n...

03/10/2018

UFUGAJI BORA TANZANIA we're are happy to get this far, contact with us if you need more assistant or anything to share with us.

Ufugaji bora ni pamoja na afya ya mnyama mwenyewe unayemfuga..basi jifunze jinsi ya kufanya ili uwez

My application coming soon!! Get ready and be ready to download it in playstore!!Application mpya inakujia hivi karibuni...
10/05/2018

My application coming soon!! Get ready and be ready to download it in playstore!!

Application mpya inakujia hivi karibuni!!
Kuwa tayari kuipakuwa ndani ya playstore!!

Unataka kufuga na kupata faida?Ni rahisi sana...sasa basi kupitia page hii ya ufugaji bora tutakusaidia kifikia malengo ...
11/01/2018

Unataka kufuga na kupata faida?
Ni rahisi sana...sasa basi kupitia page hii ya ufugaji bora tutakusaidia kifikia malengo yako, usisite kuwasiliana nasi na kukupa ushauri wenda ukawa unamaswali nje ya mada tajwa zilizo wasilishwa.
Ahsante....

Katika utunzaji wa afya ya mnyama leo 🆕🆕-session ya pili ya magonjwa yanayo sababishwa na kupe yaani(tick borne disease)...
27/10/2017

Katika utunzaji wa afya ya mnyama leo 🆕🆕
-session ya pili ya magonjwa yanayo sababishwa na kupe yaani(tick borne disease).

1b. Babesiosis

☆Ugonjwa huu huwaathiri wanyama k**a vile Ngo'mbe,kondoo,Ngurue na farasi.

☆dalili za ugonjwa
-mnyama huishiwa hamu ya kula na kukonda.
-joto kali kifikia 41.5°C(ndo huwa dalili ya kwanza)
-Kwa mnyama mwenye mimba hutoa kutokana na joto kuwa kali mno.
-kwa wale wanyama wanaokamuliwa hupunguza uzalishaji.
-pia mnyama hukojoa mkojo uliochanganyikana na damu.
-kupungua uzito.
-mnyama hulala chini
-kushindwa kutembea(ataxia)

☆Iwapo itatokea mnyama anakufa ukuiangalia sehemu mbalimbali za mwili utakuta vifuatavyo:
-Ini huvimba na kubadili rangi yaani dark_brown
-figo pia huvimba(dark)
-bandama pia nalo huvimba.
-Nyama hubadilika rangi baadhi ya maeneo na kuwa njano.

☆Matibabu yake
-choma mara moja(A single injection_imidocarb (imizol) 1mg/kg BW(body weight)
-au diminazene aceturate.
-kuongezea na anti_inflammatory drugs...

☆kuzuia ugonjwa
-Zuia kupe kwa kuogesha mifugo mara kwa mara
-chanjo.

Published by George C. Mkalawa(LFOII).

Address

3022 SUA
Morogoro

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00

Telephone

0657850292

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ufugaji bora Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share

Category