Uzazi Wellness

Uzazi Wellness ✨Kuimarisha Afya ya Uzazi kwa Wanawake kwa Kutumia Tibalishe na asilia💫

*🌿 ALIDHANI HATAWEZA KUPONA…* Uvimbe maji SM 2 uliotokana na P.I.D ulimpa maumivu makali na uchafu mwingi kwa zaidi ya m...
07/04/2026

*🌿 ALIDHANI HATAWEZA KUPONA…*

Uvimbe maji SM 2 uliotokana na P.I.D ulimpa maumivu makali na uchafu mwingi kwa zaidi ya mwaka 1.
Maisha yalikuwa ya mateso kila siku.
Lakini baada ya kufuata tiba asilia na lishe bora,
uvimbe ulipona kabisa na sasa hana maumivu tena.

📩 Na wewe unaweza kuanza safari ya kupona leo — nitumie ujumbe nikusaidie.

Mchana wa leo nawakaribisha tujifunze dondoo kwa ufupi zinazohusu *Mchicha pori* Jina lake kisayansi:Amaranthus caudatus...
15/03/2026

Mchana wa leo nawakaribisha tujifunze dondoo kwa ufupi zinazohusu *Mchicha pori*

Jina lake kisayansi:
Amaranthus caudatus – pia huitwa Love-lies-bleeding au Foxtail amaranth. Ni wa familia ya Amaranthaceae.(familia ya mchicha).

Muonekano wake:
Ni mmea wa msimu mmoja unaokua hadi urefu wa takribani mita 1–2.4. Una maua mekundu yanayoning’inia k**a mkia.

Sehemu zinazotumika:
Majani,Mbegu,mizizi

Matumizi ya chakula:
Majani huliwa k**a mboga (k**a mchicha).
Mbegu hutumika k**a nafaka badala ya wali au kupika uji.

Faida za kiafya:
Husaidia kupunguza sukari kwenye damu (kisukari)

Husaidia kupunguza cholesterol
Ni diuretic (huongeza mkojo)
Husaidia kuua baadhi ya vimelea

Matumizi mengine ya tiba:
Majani yaliyosagwa yakichemshwa hutumika kusukutua kinywa kutibu koo linalouma na vidonda vya mdomo.

*(Namna ya kuandaa dawa ya koo:
Chemsha vijiko 2 vya unga wa majani kwenye kikombe 1 cha maji kwa dakika 10, kisha tumia kusukutua mdomo.)*

Kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi:
Amaranthus caudatus husaidia kugandisha damu na kuzuia damu kutoka nyingi wakati wa hedhi.
Chemsha kijiko 1 cha unga wa mzizi kwenye kikombe 1 cha maji kisha kunywa.
Kwa damu inayotoka nje, nyunyiza unga kwenye sehemu iliyoathirika.

Maambukizi ya uke:
Chemsha majani na mzizi wa Amaranthus kwenye maji.
Tumia kunywa ndani na pia kuosha uke (douchi) kutibu ute.

Tahadhari:
Usitumie k**a una gout, arthritis, au matatizo ya figo.
Haipaswi kwa wajawazito, mama wanaonyonyesha, au watoto wachanga.

Karibu kwa ushauri na tiba

ndimi

Uzazi_wellness

HUO NI MTI WA MTINI(FICUS CARICA) ULIOTUMIKA KUMPONYA MFALME HEZEKIA Wakati Bwana alimwambia Hezekia kwamba angeongeza m...
10/03/2026

HUO NI MTI WA MTINI(FICUS CARICA) ULIOTUMIKA KUMPONYA MFALME HEZEKIA

Wakati Bwana alimwambia Hezekia kwamba angeongeza maisha yake kwa miaka kumi na mitano, na k**a ishara ya kutimiza ahadi yake akafanya jua lirudi nyuma kwa nyuzi kumi, kwa nini hakumponya mfalme kwa nguvu yake ya moja kwa moja?
Badala yake alimwambia apake mkate wa tini kwenye kidonda chake, na tiba hiyo ya asili, iliyobarikiwa na Mungu, ikamponya.

Mungu wa asili humwongoza mwanadamu kutumia tiba za asili hata leo. — Barua 182, 1899 (PH144 16.5) 🌿📖
2wafalme.20:1-8,Ezekieli.47:1-7;Ufunuo.22:1-6

27/02/2026

🥣 NAMNA YA KUTENGENEZA (Bila Maji)
1️⃣ Osha vizuri viungo vyote.
2️⃣ Menya karoti, rozera na tangawizi.
3️⃣ Kata vipande vidogo vidogo ili iwe rahisi kusaga.
4️⃣ Weka vyote kwenye blender au saga kwenye kinu.
🚫 Usiongeze maji – juisi ya limao, ndimu, rozera na kitunguu itatosha kusaidia kusaga.
5️⃣ Unaweza kunywa k**a ilivyo (ikiwa tumbo linaweza kuvumilia) au chujia kidogo kupata juisi nzito.

🕒 JINSI YA KUTUMIA
✔️ Kunywa vijiko 2–3 vikubwa asubuhi kabla ya kula.
✔️ Rudia jioni kabla ya kula.
✔️ Fanya kwa siku 5–7 mfululizo.
💧 Kunywa maji mengi mchana kutwa kusaidia kusafisha mfumo wa mkojo.
🚫 Epuka sukari kipindi hiki,Nyama yoyote na tumia wanga kidogo.

🌿 Afya ni uwekezaji, si gharama.
Mwili wako unahitaji msaada sahihi kwa wakati sahihi.
👉 Follow kwa elimu zaidi ya afya ya mwanamke, tiba asilia, na siri za kuimarisha kinga ya mwili.

21/02/2026
18/02/2026

Eenergetic food

*🍽️ Kula taratibu,Afya bora inaanza na jinsi unavyotafuna chakula chako* Hebu tuone hii dondooSababu ya kwanza iliyo ya ...
15/01/2026

*🍽️ Kula taratibu,Afya bora inaanza na jinsi unavyotafuna chakula chako*

Hebu tuone hii dondoo

Sababu ya kwanza iliyo ya kawaida sana ya matatizo ya mfumo wa mmeng’enyo wa chakula ni ;

*kumeza chakula haraka sana bila kutafuna vizuri.*

Tabia hii huonyesha mlaji ana

✅ wasiwasi
✅kukosa subira
✅msongo wa mawazo.

Elewa

Kula kwa haraka hupunguza uzalishaji wa mate (saliva) mdomoni, jambo ambalo ni

*Chanzo kikubwa cha Meno kutoboka.*

✍️Kazi za mate

▶️kulinda mdomo na meno dhidi ya vijidudu
▶️Kulainisha chakula
▶️Huanza kumeng'enya wanga unapofika tu mdomoni

Kuna sababu nyingine nyingi zinazoonyesha kwa nini kutafuna chakula vizuri ni muhimu kwa afya yetu. Kwa mujibu wa utafiti wa kuvutia uliofanywa katika Chuo Kikuu cha Gifu nchini Japani unaonyesha

kutafuna chakula kunaweza kuboresha kumbukumbu kwa kupunguza utolewaji wa homoni za msongo wa mawazo( stress homon k**a cortisol).

Uchunguzi wa MRI (Magnetic Resonance Imaging) umeonyesha kuwa hipokampasi (hippocampus)—sehemu ya ubongo inayosaidia kudhibiti kiwango cha homoni za msongo wa mawazo kwenye damu—huchochewa wakati wa kutafuna.
Hivyo,kitendo rahisi cha kutafuna chakula vizuri hupunguza msongo wa mawazo pamoja na homoni zake.

Haya , acha kula paparapapara unatoboa meno yako na kujiongezea wasiwasi.

18/12/2025

Salfuri (S)

Asidi/Alkalini: Hutengeneza asidi mwilin

Vyanzo vya sumu:

Dawa za kudumu za nywele (hair permanents), straighteners, na baadhi ya conditioners zinauwezo wa kuathiri kiwango cha salfuri mwilini.

Kumbuka:

Salfuri inajulikana kwa kulinda seli dhidi ya athari za sumu za metali nzito. Pia, matumizi ya tumbaku hupunguza ufyonzwaji

Faida zake kiafya:

✅Salfuri husafisha damu
✅husaidia mwili kupambana na bakteria
✅hulinda protoplasimu ya seli.
✅Husaidia katika michakato muhimu ya uoksidishaji mwilini
✅huchochea utolewaji wa nyongo
✅hulinda dhidi ya vitu vyenye sumu. Kutokana na uwezo wake wa kulinda mwili dhidi ya athari hatarishi za mionzi na uchafuzi wa mazingira
✅salfuri husaidia kupunguza kasi ya mchakato wa kuzeeka.
✅Inahitajika katika utengenezaji wa kolajeni, protini kuu inayoipa ngozi uimara na muundo wake.
✅Inahitajika pia kwa afya ya nywele, kucha, insulini, gegedu (cartilage), na damu.
✅Husaidia mmeng’enyo wa chakula na utoaji wa taka mwilini. Ni wakala wa uoksidishaji katika hemoglobini.

Muhimu:

Salfuri ni kiungo muhimu kinachofanya vitunguu saumu kuitwa “mfalme wa mimea tiba.”

Upungufu:

Kudumaa kwa ukuaji, eczema, dermatitis, ukuaji duni wa kucha na nywele au kuwa dhaifu na rahisi kuvunjika.

Sumu (Toxicity):

Huongeza hatari ya magonjwa ya moyo.

Mwl wa afya,Shambani mwa Bwana

Scientific name:Momordica charantiaL.Common name;Bitter melon,Bitter gourdKiswahili:Tikit chunguFamily:Cucurbitaceae *Un...
16/12/2025

Scientific name:Momordica charantiaL.
Common name;Bitter melon,Bitter gourd
Kiswahili:Tikit chungu
Family:Cucurbitaceae

*Unapatikana*

pembeni ya uzio wa shamba
porini
Bustanini (Unalimwa k**a mboga)

*Maelezo ya mmea*

Ni mmea unaotambaa (climber) wenye mashina laini.

Majani ni mapana, yamekatika vipande (lobes).

Maua ya njano.

Tunda ni kijani chenye vinundu, huiva na kuwa rangi ya chungwa kisha kupasuka kuonyesha mbegu nyekundu.

Ladha ya tunda ni chungu sana.

*Sehemu zinazotumika*

Majani

Tunda

Mbegu

Mizizi (kwa tahadhari)

*Matumizi ya kiafya (Tiba asilia)*

Kushusha sukari ya damu (maarufu kwa wagonjwa wa kisukari)

Kuimarisha kinga ya mwili

Magonjwa ya tumbo: minyoo, kuharisha

Magonjwa ya ngozi: vipele, fangasi

Afya ya wanawake: hutumika kwenye tiba za jadi (kwa uangalifu)

*Jinsi hutumika*

Majani au tunda huchemshwa na kunywa maji yake

Tunda hupikwa k**a mboga

Hutengenezwa juisi au unga wa kukaushwa

Tahadhari ⚠️

kujua tahadhar njoo DM

12/12/2025

100%natural

vilivyomo

Ngano nzima,mbegu maboga unga,
Unga dengu,Chachu asilia,Ndizi za kuiva,Chia seed,Chumvi magadi, Chumvi asilia na mafuta

Namna ya kupika

Changanya vitu vya unga pamoja
Changanya vimiminika pamoja
Mwisho kanda mkando k**a wa chapati ya kusukuma kisha tengeneza umbo unalotaka na weka tayari kwenye chombo cha kuokea na acha uumuke kwa masaa1.2+ utakuwa unakagua kuona ikiwa umeshauumuka.

Oka kwa moto kidogo ili uive ndani na baada ya dk 15 ongeza moto na kagua kadiri utavoona umekuwa wa kahawia ivo ipua au choma na kitu chenye ncha ikiwa hautatoka na minato basi umeiva huo.

Address

Muleba

Telephone

+255762733168

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Uzazi Wellness posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Uzazi Wellness:

Shortcuts

Share