Yasinter health consultant

Yasinter health consultant tunahusika na uuzaji wa bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa kitaalamu zenye ubora wa kimataifa na matibabu ya magonjwa tabia k**a vile kisukari,UTI n.k

NEPBABY DISPOSABLE DIAPERS Ni aina ya DIAPERS za watoto zenye ubora wa hali ya juu sana.Matumizi Ya Diapers Yamerahisish...
08/10/2016

NEPBABY DISPOSABLE DIAPERS
Ni aina ya DIAPERS za watoto zenye ubora wa hali ya juu sana.
Matumizi Ya Diapers Yamerahisishia Wamama Wengi Hasa Walioajiriwa Kutokana Na Ufinyu Wa Muda wa kufua .Lakini Wakati Mwingine Hizi Diapers Zimeleta Matatizo Mengi Kwa Watoto Hasa Kutokana Na Aina Ya Malighafi Iliyotumika Kutengenezea.

Diapers zingine hazipitishi hewa hivyo husababisha Bacteria aina Anaerobic Bacteria kuzaliwa.Hawa ni Bacteria ambao wanazalishwa katika mazingira ambayo hewa ya Oxygen haipiti matokea yake watoto wanapata Ugonjwa Kwenye Njia Ya Mkojo Maarufu K**a U.T.I,Kuwashwa Na Fungus.

UBORA WA NEPBABY DIAPERS
Nepbaby disposable diapers zimetengenezwa kwa malighafi ya pamba laini ambayo huruhusu hewa kupita vizuri lakini pia kufanya mtoto kuwa na furaha wakati wote kwasababu haimchubui,wala kusababisha muwasho wa aina yoyote.zifuatazo ni faida zake:

1.ALOE: Nepbaby diapers zina aloe ambayo humlinda mtoto na maradhi ya aina mbalimbali ikiwemo muwasho,fungus,u.t.i na kuzuia bacteria wanaozaliwa kwenye unyevu nyevu na hasa mazingira ambayo hewa ya oxygen inakosekana.

2.INDICATOR(KIASHIRIA): Nepbaby diapers zina indicator(kiashiria) ambayo huonyesha k**a mkojo umejaa na inatakiwa kubadilishwa,hivyo kumfanya mwangalizi wa mtoto kutambua haraka kuwa anatakiwa kubadilisha.

3.POLYMERS NA PAMBA LAINI: Zimetengenezwa kwa malighafi zenye uwezo wa kufyonza mkojo au maji maji kwa wingi hivyo kumwacha mtoto kuwa mkavu na kumuepusha na muwasho wa aina yoyote na kuwa huru.

4.ZINAONDOA HARUFU MBAYA:Zinamkaa mtoto vizuri na pembeni iko na malighafi inayozuia mkojo kupita na kuondoa harufu mbaya ( foul smell).

5. UTUNZAJI WA MUDA: Zinamsaidia mama kupata muda wa kufanya shughuli zingine za kiuchumi

UKIHITAJI DIAPER HIZI AMBAZO NI MKOMBOZI WA MTOTO WASILIANA NAMI KWA NAMBA
TEXT/Whatsapp only 0753425148
Yasinter Health Consultant
Mwanza Tanzania
Mikoani unatumiwa
Pia k**a unahitaji kuwa wakala wa diaper hizi unakaribishwa sana

Neplily PedAsili ya Jina la Neplily imetokana na muunganiko wa majina mawili ambayo ni“Nep” kutoka kwa neno Neptunus“Lil...
19/08/2016

Neplily Ped
Asili ya Jina la Neplily imetokana na muunganiko wa majina mawili ambayo ni
“Nep” kutoka kwa neno Neptunus
“Lily” kutoka kwa maua yaitwayo Lily
Maua ya Lily ni kivutio kikubwa hasa kwa wanawake.
Mara nyingi maua haya hutumiwa kuonyesha ishara ya urembo, uzazi, upendo, huruma, usafi….n.k. yaani mambo yote wanawake
wanayohusika nayo na kupenda.

MATATIZO YAWAPATAO WANAWAKE WAKATI WA HEDHI
♧Kichwa kuuma
♧Maumivu ya tumbo
♧Kukosa hamu ya kula
♧kusikia kichefuchefu
♧kuingia hedhi zaidi ya siku 7

Pads za Neplily zimetengezwa na cotton material iliyo laini na ina uwezo wa hali ya juu kufyonza hedhi kwa haraka . Hii inamfanya mwanamke kuwa na faraja na uhuru.

Imewekwa anion plate: ambayo imewekwa katikati ya pamba nyepesi,na hii anion plate ikilowa damu tu inafyonza damu yote na kuruhusu upepo upenye ili kuondia joto na unyevu unyevu na kusababisha bakteria kukosa sehemu ya kuotea.Baada ya pedi hii ya Neplily kupata unyevu unyevu inaanza kusambaza anions kupanda na kuingia kwenye kizazi,mirija ya uzazi hadi kwenye damu pia.

ANIONS hizi hutokana na natural forces yaani nguvu asili k**a maporomoko ya maji makali,upepo mkali,mionzi mikali inapokuwa inapiga molekyuli za hewa husababisha kuzalishwa kwa chembechembe hasi ambazo huitwa Anion ambazo ni tiba tosha katika mwili wa binadamu.

Kazi kubwa ya anions hizi ni;
♧inazuia Urinary Tract Infections (UTIs)
♧Inarudisha mzunguko wa hedhi kwa mwanamke.
♧Inaondoa maumivu ya tumbo wakati wa hedhi.
♧Inatibu fungus na miwasho katika sehemu za siri.
Ina uwezo wa kunata chupi vizuri ili kuzuia kuteleza. Hivyo kumfanya mwanamke kuwa huru bila ya kuwa na wasi wasi.
Pembeni yake kuna vishikio vinavyosaidia kushika chupi vizuri na kuzuia kuvuja kwa pembeni (side leakage).

UBORA WA NEPLILY
Ni Super absorbent. Ina uwezo wa kufyoza hedhi kwa kiwango kikubwa. Zaidi ya ml 250

No leaks. Haipitishi hedhi.
Protection from UTIs. Kinga dhidi ya ugonjwa sugu wa UTIs.

Kwa mahitaji ya pedi hizi nitafute kwa namba 0753425148

FAHAMU KUHUSU UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUMEUkosefu ama upungufu wa nguvu za kiume ni ile hali ya mwanaume kutokuwa na uwezo ...
07/08/2016

FAHAMU KUHUSU UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME

Ukosefu ama upungufu wa nguvu za kiume ni ile hali ya mwanaume kutokuwa na uwezo wa kukamilisha tendo la ndoa kwa ufasaha.

Tatizo hili linawakabili mamilioni ya wanaume duniani na limekuwa na athari nyingi k**a vile kuvunjika kwa mahusiano na hata ndoa.

Mwanaume mwenye tatizo la ukosefu ama upungufu wa nguvu za kiume anakuwa hana uwezo wa kumtosheleza mwanamke kwenye tendo la ndoa.

DALILI ZA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME

Mwanaume anayekabiliwa na tatizo la ukosefu ama upungufu wa nguvu za kiume huonyesha dalili zifuatazo:-

1. Kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume wake barabara. Kwa kawaida uume wa mwanaume aliyekamilika (rijali ) unaposimama, hutakiwa kuwa imara k**a msumari, lakini kwa mwanaume anaye kabiliwa na tatizo hili uume wake hata ukisimama hubakia kuwa lege lege na huweza kusinyaa wakati wowote. Tatizo hili ni matokeo ya kulegea kwa mishipa ya uume. Mishipa ya uume ndio inayo ufanya uume usimame barabara.

Mishipa hii inapokuwa imelegea, uume hauwezi kusimama barabara hata iweje. Kulegea kwa mishipa ya kiume kunasababishwa na upigaji wa punyeto kwa muda mrefu. Mtu anaye piga punyeto anakuwa anaiminya mishipa inayo sababisha kusimama kwa uume, baada ya muda fulani, mishipa hiyo huishiwa nguvu na kulegea na hivyo linapo kuja suala la kusimamisha uume, mwanaume huyu anakuwa hana uwezo tena wa kusimamisha uume wake.

Vilevile matumizi ya madawa makali (hususani madawa ya kizungu) ya kuongeza nguvu za kiume, husababisha mishipa ya uume kulegea. Hii ni kwa sababu madawa haya hui-overdosemishipa hiyo na kuilazimisha kufanya kazi zaidi ya kiwango chake.

Matumizi haya yanapokuwa ya muda mrefu humfanya muhusika kuwa tegemezi na pia hufanya mishipa ya uume wa muhusika kulegea na kukosa nguvu.

2. Kukosa hamu ya tendo la ndoa: Hapa mwanaume anakuwa hana uwezo wa kutamani kufanya tendo la ndoa hata anapokuwa faragha na mke wake. Tatizo hili kwa kiasi kikubwa husababishwa na msongo wa mawazo.

3. Kutokuwa na uwezo wa kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara moja. Hapa mwanaume akishakamilisha mshindo mmoja wa tendo la ndoa basi anakuwa hana tena uwezo wa kurudia mshindo mwingine. Hali hii husababishwa na kutokuwa na msukumo wa damu wa kutosha kwenye mishipa ya kwenye uume.

4. Kufika kileleni mapema

5. Kutokuwa na uwezo wa kusimamisha kabisa. Hali hii hutokea pindi tatizo la kutokuwepo kwa msukumo wa damu wa kutosha kwenye mishipa ya uume, linapokuwa limekomaa. Na wakati mwingine, hali hii hutokea pindi vyanzo zaidi ya kimoja vya tatizo la kiume vinapo kuwa vimejitokeza kwa mtu mmoja.

6. Uume kusinyaa na kurudi ndani. Hapa uume wa mwanaume unakuwa umesinyaa na kurudi ndani. Uume huu unakuwa hauna uwezo wa kukamilisha tendo la ndoa. Hali hii kwa kiasi kikubwa husababishwa na upigaji wa punyeto kwa muda mrefu pamoja na magonjwa hasa hasa chango la kiume au ngiri.
Tajwa hapo juu ni dalili kuu za tatizo la ukosefu ama/na upungufu wa nguvu za kiume.

CHANZO CHA TATIZO LA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME

Kwa ufupi sana, mambo yafuatayo ndio vyanzo vikuu vya tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume:-

i. Upigaji punyeto wa muda mrefu.
ii. Msongo wa mawazo.
iii. Ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu (pressure).
iv. Kupooza kwa mwili.
v. Kuugua ugonjwa wa ngiri.
vi. Kuugua chango la kiume.
vii. Ulevi uliokithiri.
viii. Kuwa na wasiwasi wa kumudu kutekeleza tendo la ndoa.
ix. Woga wa kufanya tendo la ndoa.
x. Uzoefu wa kukatisha tamaa wa siku za nyuma.
xi. Ulaji mbovu wa vyakula haswa vyenye mafuta mengi/kupita kiasi.
xii. Mazingira yasiyoridhisha wakati wa tendo la ndoa.

ATHARI ZA UPUNGUFU / UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME

Kutokuwa na nguvu za kiume huleta madhara na athari nyingi sana kwa muhusika. Baadhi ya athari hizo ni pamoja na:-

Kuvunjika kwa mahusiano ya kimapenzi.
Kuvunjika kwa ndoa.
Kujiua: Baadhi ya wanaume hufikia uamuzi wa kujiua baada ya tatizo kuwa kubwa na kutumia dawa za aina mbalimbali bila mafanikio.
Upungufu wa nguvu za kiume huongeza chachu ya maambukizi ya V.V.U kwa wanandoa:

Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume linapokuwa sugu, hupelekea rafiki wa k**e/ mke wa mwanaume anaye sumbuliwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume, kutoka nje ya ndoa kwa ajili ya kutimiziwa haja zake za kimwili, mwisho wa siku mwanamke huyo huweza kumletea magonjwa mume wake mwenye tatizo la upungufu wa nguvu za kiume pindi wanapokutana kimwili katika hali hiyo hiyo ya kutoridhishana.
Ulevi kupita kiasi; Wakati mwingine wanaume wanao sumbuliwa na tatizo hili, huamua kuwa walevi kupita kiasi ili angalau kupunguza mawazo.

Kwa ufupi ukosefu/ upungufu wa nguvu za kiume ni tatizo kubwa sana ambalo endapo halitatafutiwa ufumbuzi na muhusika linaweza kuyaathiri maisha ya muhusika kwa kiasi kikubwa sana.

K**a unasumbuliwa na tatizo hlo nitafute kwa namba 0753425148 kwa ushauri na tiba. Pia usisahau kulike page hii

kwa wale watakaopenda kujifunza kuhusu afya nawakaribisha kwa kuandika namba zao za simu hapa niweze kuwaadd kwenye grou...
06/08/2016

kwa wale watakaopenda kujifunza kuhusu afya nawakaribisha kwa kuandika namba zao za simu hapa niweze kuwaadd kwenye group la wasapp kwa mafunzo zaidi..

LEO NINAKULETEA FAIDA ZA TIKITI MAJI TAFADHALI NDUGU SOMA HADI MWISHO UJIFUNZEIjapokuwa watu wengi huamini kuwa tikiti m...
05/08/2016

LEO NINAKULETEA FAIDA ZA TIKITI MAJI TAFADHALI NDUGU SOMA HADI MWISHO UJIFUNZE

Ijapokuwa watu wengi huamini kuwa tikiti maji ni tunda lililo na maji na sukari peke yake, lakini ukweli ni kuwa tunda hili lina aina nyingi ya virutubisho , mfano vitamini, madini na viondoa sumu( antioxidants ).

Vitamini Vitamini A 28µg
Vitamini E 0.0 µg
Vitamini C 8.1mg
Thiamine 0.03mg
Niacini 0.2mg
Vitamini B 6 0.045mg
Folic acid 3mg
Madini Kalshamu 7mg
Phosphorasi 11mg
Magnesiamu 10mg
Potasiamu 112mg
Munyu (Sodium) 1mg
Chuma 0.2
Zinki 0.1mg

PROTEIN MUHIMU
TRP(Tryptophan) 7.0mg
THR(Threonine) 27mg
ILE(Isoleucine) 19mg
LEU(Leucine) 18mg
LYS(Lysine) 62mg
MET(Methionine) 6mg
CYS(Cysteine) 2mg
PHE (Phenylalanine) 15mg
TYR(Tyrosine) 12mg
VAL(Valine) 16mg
ARG(Arginine) 59mg
HIS(Histidine) 6mg

Mbali na virutubisho vilivyoonyeshwa hapo juu, tunda hili la tikiti maji pia lina viondoa
sumu k**a flavonoids, carotenoids na triterpenoids pia kiasi kikubwa cha maji,na virutubisho hivi hulifanya tunda hili kuwa na sifa ya vyakula vyenye faida kubwa mwilini.

Tafiti nyingi zimeonyesha kuwa, kuongeza matumizi ya vyakula vitokanavyo na mimea k**a tikiti maji,matunda mengine na mbogamboga hupunguza hatari ya kupata magonjwa, kuboresha maisha na kuongeza umri wa kuishi. Twaweza kuepukana na magonjwa k**a uzito mkubwa( obesity ),kisukari na magonjwa ya moyo.

Ulaji wa vyakula hivi humfanya mtu kuwa na afya njema,ngozi yenye afya,nywele na uzito ulio wa wastani.

Tunda hili lina lycopene ambayo kazi yake ni kuondoa sumu( antioxidant)

Tafiti za awali zimeonyesha kuwa watu walao matunda k**a tikiti na mengineyo yenye lycopene kwa wingi waweza kuwa na nafasi ndogo ya kupata maradhi ya saratani hususani saratani ya tezi dume.

Katika utafiti mmoja uliochapishwa mwaka 2013 katika jarida la Kimarekani la shinikizo la damu,ulionyesha ulaji wa tikiti maji kwa watu wazima walio na uzito mkubwa uliweza kupunguza
shinikizo la damu la aota ( aortic BP).

L- citrulline ni aina ya protini iliyo katika tikiti maji na ambayo hubadilishwa mwilini katika figo na kuwa protini ijulikanayo k**a L-arginine . L- citrulline pia huongeza utengenezwaji wa nitric oxide, ambayo hufanya mishipa ya damu kutokukak**aa na kuboresha mzunguko wa damu mwilini na hii ndiyo sababu ya kupungua kwa shinikizo la damu.

Tunda hili limejipatia umaarufu kwa wale walio katika ndoa,kwa kuwa nitric oxide huongeza pia mzunguko wa damu
katika viungo vya uzazi, kwa hiyo wale walio na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume kwa kiwango kidogo na kati, waweza kufaidika na
tunda hili.

Kwa wana michezo ulaji wa tunda hili au juisi yake ni wa faida kubwa kwa kuwa husaidia kupunguza maumivu ya misuli na kuondokana na uchovu kwa haraka baada ya mazoezi au michezo ya kutumia nguvu. Watafiti wanaamini kuwa hii ni kwa sababu ya uwepo wa protini ya L-citrulline katika tikiti maji.

Tikiti maji ni tunda muhimu katika kurekebisha mmeng’enyo. Kwa kuwa tunda hili limetengenezwa na kiasi kikubwa cha maji na fiba husaidia kuondoa matatizo ya kukosa choo ( constipation) na kuboresha mmeng’enyo w chakula tumboni.

Pia kwa kuwa tunda hili lina
asilimia 92 ya maji na madini, huwa ni chaguo zuri kwa wagonjwa wenye upungufu wa maji mwilini.

Hatari ya kupata ugonjwa wa pumu ni ndogo kwa wale wanaokula aina fulani ya virutubisho.Katika moja ya virutubisho hivi ni vitamini C ambayo hupatikana katika aina nyingi za matunda na mbogamboga likiwemo tikiti maji.

Tikiti maji husaidia afya ya ngozi kwa kuwa lina vitamini A na C.

Vitamini A husaidia katika ukuaji wa tishu za mwili,zikiwemo ngozi na nywele.

Vitamini C husaidia katika utengenezaji wa kolageni mwilini na husaidia kupona haraka kwa tishu zilizo na majeraha ikiwemo ngozi.

K**A UMEIPENDA LIKE NA SHARE..LAKINI PIA KWA USHAURI NA TIBA KUHUSU MASUALA YA AFYA K**A VIDONDA VYA TUMBO,PRESHA,UTI SUGU,KISUKARI NA MATATIZO YA NGOZI nk USISITE KUWASILIANA NAMI KUPITIA 0753425148

04/08/2016

FAIDA KUU TANO(5) ZA KUTUMIA MAZIWA YA MTINDI (MGANDO)
Karibu tena katika Makala zangu ndugu mpendwa uliyelike page hii ya afya yako na pamoja nawewe ambaye hujalike au ni mara yako ya kwanza kusoma Makala za afya za page hii basi leo nataka nikupe faida tano au sababu za kuanza kutumia maziwa ya mtindi siku ya leo
Mtindi unaorodheshwa kuwa miongoni mwa vyakula bora kutokana na kuwa na virutubisho vingi vya aina mbalimbali ambavyo vina faida nyingi katika mwili wa binadamu.
Baadhi ya virutubisho hivyo vilivyothibitika ni kwamba mtindi ni chanzo kizuri cha Calcium, Phosphorus, Riboflavin (vitamin B2), Iodine, vitamin B12, Pantothenic acid (vitamin B5), Zinc, Potassium na Molybdenium. Mbali ya virutubisho hivyo, ndani ya mtindi kuna BAKTERIA HAI ambao ni muhimu kiafya katika mwili.
1. HUREFUSHA MAISHA
Utafiti unaonesha kuwa unywaji wa mtindi mara kwa mara, hasa katika kundi la wazee, uwezo wa mwili wa kupambana na magonjwa mbalimbali umeonesha kuongezeka na kufanya mfumo wa kinga ya mwili kuwa imara zaidi.
Katika utafiti mmoja, walichaguliwa wazee 162 ambao walipewa utaratibu wa kunywa mtindi na maziwa zaidi ya mara 3 kwa wiki na kufuatiliwa maendeleo yao kwa muda wa miaka mitano. Baadaye utafiti huo ulionesha kuwa idadi ya vifo vya wazee hao ilipungua kwa asilimia 38 ukilinganisha na kundi la wazee wasiotumia au waliotumia mtindi kiasi kidogo sana.
2. KINGA KWA KINA MAMA
Aidha, mtindi umeonesha kuwa na uwezo mkubwa wa kutoa kinga dhidi ya maradhi ya kuambukiza ukeni (va**nal infections).
Katika utafiti mmoja uliohusisha wanawake mwenye magonjwa ya kuambukiza sehemu za siri, baada ya kutumia mtindi kiasi cha paketi moja kila siku kwa muda wa miezi sita, maambukizi waliyokuwanayo wanawake hao kabla yalitoweka.
3. KINGA YA MWILI
Utafiti uliofanywa kwa wanyama, wakiwemo panya na kuchapishwa kwenye jarida moja la masuala ya virutubisho nchini Marekani (Journal Of Nutrition), umeonesha kuwa unywaji wa mtindi kila siku, huamsha na kuupa nguvu mfumo wa kinga ya mwili kupambana na magonjwa kadhaa ya maambukizi, ikiwemo saratani ya utumbo.
4. HUONDOA LEHEMU MBAYA MWILINI
Katika hatua nyingine, mtindi umeonekana kuwa na uwezo wa kupunguza kiwango cha lehemu mbaya mwilini (LDL (bad) cholesterol) na wakati huo huo kupandisha kiwango cha lehemu nzuri mwilini (HDL (good) cholesterol). Kwa maana nyingine, ikiwa mtindi unaondoa lehemu mbaya, mtumiaji anajiepusha pia na hatari ya kupatwa na tatizo la shinikizo la damu pamoja na stroke.
5. KUPUNGUZA UZITO
Mbali ya faida hizo, mtindi pia umeonekana kupunguza mafuta (fat) mwilini na kwa maana hiyo una uwezo wa kupunguza unene unaotokana na mafuta mengi mabaya mwilini.
MUHIMU KUZINGATIA
Jambo muhimu la kuzingatia ni unywaji wa mtindi halisi uliotengenezwa kutokana na maziwa halisi ya ng’ombe, siyo mtindi uliotengenezwa kutokana na maziwa ya unga. Siri kubwa iliyomo kwenye mtindi ni ule uchachu unaotokana na BAKTERIA HAI wanaopatikana baada ya maziwa kuganda na kuchachuka.
Naamini umejifunza kitu rafiki yangu ni jukumu lako sasa kufanya maamuzi ya kuanza kutumia maziwa ya mgando(mtindi)
Karibu tena uungane nami katika Makala zijazo kupitia page hii k**a hujalike like sasa ufurahie elimu ya afya yako bure kabisa .
MAWASILIANO
0753425148
WhatsApp +255753425148
share na marafiki zako wanufaike na elimu hii ya bure kabisa

29/07/2016

FAHAMU TATIZO LA MIGUU/MIKONO KUFA GANZI
Karibu tena msomaji wa makala zangu za afya siku ya leo nmependa ujifunze zaidi juu ya tatizo ambalo limekuwa likionekana ni la kawaida katika jamii nyingi.
Katika mwili wa binadamu, kuna tatizo la kiafya ambalo huambatana na dalili za mtu kuhisi maumivu, kuhisi kuwaka moto na kufa ganzi kwa viungo vya pembezoni mwa mwili yaani miguu na mikono. Tatizo hili kitaalamu hujulikana kwa jina la Peripheral Neuropathy.
Matatizo haya ya kiafya (miguu/mikono kuhisi ganzi, baridi au maumivu) husababishwa na kuumia au kudhoofika kwa neva za pembezoni mwa mwili (miguuni au mikononi) na hivyo kupotea kwa uwezo wa kufanya kazi wa neva katika sehemu husika, miguuni au mikononi.
Dalili zinazoambatana na ugonjwa huu ni hizi zifuatazo
1.Mtu kuhisi ganzi
2. kushindwa kushika au kunyanyua kitu, kuchoka kwa misuli na kadhalika.
3.maumivu au kuwaka moto maeneo ya miguuni/mikononi,
Miongoni mwa mambo ambayo hupelekea neva hizi za pembezoni kudhoofika na kushindwa kufanya kazi vizuri ni haya yafuatayo:
1.Kupungua kwa virutubisho mwilini,hasa mkusanyiko wa vitamini B, (Vitamin B Complex).
2.Matumizi ya dawa, mfano dawa za kutibu MAUMIVU
3.Uzito mkubwa wa mwili,
4.Ugonjwa wa kisukari,(diabetic polyneuropathy).
5.Shinikizo la damu(PRESHA),
MATIBABU
1.Fanya mazoezi
2.kula vyakula vyenye virutubisho na kula mboga mboga na matunda KWA WINGI.
WATU WENGI SAANA HUKAA NA TATIZO HILI WAKIJUA HALITIBIKI TATIZO HILI SASA LIMEPATA SULUHISHO NA LINAONDOKA
Usisite kuwasiliana nami kupitia namba 0753425148
Whatsapp 0753425148
Pia unaweza like page yangu facebook Yainter health consultant
na kushare elimu hii kwa wengine..

ZIJUE FAIDA KUMI NA NNE(14) ZA KUTUMIA MATANGO(CUCUMBER)Karibu sana rafiki yangu mpendwa msomaji na mfatiliaji wa Makala...
27/07/2016

ZIJUE FAIDA KUMI NA NNE(14) ZA KUTUMIA MATANGO(CUCUMBER)
Karibu sana rafiki yangu mpendwa msomaji na mfatiliaji wa Makala za afya kupitia page yetu hii ya Yasinter Health consultant ,leo tutazungumzia umuhimu wa kutumia matango kwa ajili ya afya zetu
Matango yanashika nafasi ya nne kwa kulimwa katika aina ya mbogamboga zinazolimwa duniani kote na tunda hili linafahamika kuwa miongoni mwa vyakula bora kwa afya yako maranyingi yanaitwa superfood.
JINSI YA KUCHAGUA TANGO BORA KWA AFYA YAKO
1.Angalia tango lenye rangi ya kijani mkozo(dark green)

2.Angalia tango ambalo bado ni ligumu vizuri halijalegea(firm).
Baada ya kuchagua tango osha vizuri kwa maii safi sasa unaweza kulitumia kwenye kachumbari,au kwa kulikata na kula hivyovyo,pia kutengenezea juisi
FAIDA ZA KUTUMIA MATANGO
1.Kuupatia mwili maji ya kutosha
Kwa wale ambao ni wavivu au wako busy sana hata kupata muda wa kunywa maji ya kutosha inakuwa ngumu,Tafuta matango ya baridi ambayo asilimia tisini ni maji,Yatasaidia kurudisha maji yaliyopotea mwilini

2.Husaidia kupambana na joto kali ndani na nje ya mwili
Kula tango husaidia kupunguza joto kali ndani ya mwili(heartburn) na pia kupaka kwenye ngozi kutakusaidia kpunguza kuungua na jua

3.Huondoa sumu mwilini(toxins)
Maji yaliyopo kwenye matango huwa k**a fagio ambalo linasafisha uchafu wote ndani ya mwili,Ulaji wa matango mara kwa mara huyeyusha mawe kwenye figo(dissolve kidney stones)
4.Husaidia kuongeza vitamin ndani ya mwiili A B na C
Vitamin A,b na C huongeza kinga ya mwili na kukupatia nguvu za kutosha,Unaweza kutengeneza juice ya tango ukichanganya na spinach pamoja na karoti kuifanya nzuri na yenye nguvu Zaidi,vitamin c ni nzui kwa ngozi asilimi 12 inashauriwa

5.Matango yana madini ya potassium ,magnesium na silicon kwa wingi ndio maana yanafaa katika tiba

6.Yanasaidia katika umeng’enyaji na kupuguza uzito
Matango kwa sababu ya maji mengi na low carlories ni mazuri kwa kupunguza uzito,pia kutokana na fiber zilizpo zitafanya mmeng’enyo wako uende taratibu,,Ulaji wa matango mara kwa mara husaidia kuondoa tatizo la kupata choo
7.Husaidia sana kusafiha macho

8.Juice ya matango inatibu na kuondoa harufu mbaya kweny fizi zllizodhofika na magonjwa
Chukua kipande cha tango na ubonyezee kwenye ukuta wa mdomo wako kwa ulimi wako kwa muda wa dakika moja,pythochemicals ambazo zipo kwenye tango zitaua bacteria waliopo mdomoni mwako ambao wanasababisha harufu mbaya

9.Maajabu ya madini ya silica yaliyopo kwenye tango yatafanya nywele zako na kucha kung’aa na kuwa imara Zaidi

10.Matango yanaongeza afya ya joint zako na kuondoa maumivu ya kwenye magoti na arthritis
Kwa maana yana silica nyingi yanapochanganywa na karoti kutengeneza juice yanaondoa maumivu ya magoti kwa kushusha level ya uric asidi

11.Inatibu kabisa hangover
Kuepuka kuumwa kichwa asubuhi au hangogver unaweza ukatafuna vipande kadhaa vya matango kabla ya kwenda kulala,Matango yana vitamin B ya kutosha ,sukari na electrolyte ambayo inalishe za muhimu ambazo zinasidia kuondoa hangover na maumivu ya kichwa

12.Matango yanasaidia figo kuwa katika umbo lake halisi
Matango yanasaidia kushusha level ya uric aside na kufanya figo kuwa na afya

13.Yanasaidia kupambana na kansa
Matango yana secoisolariciresinol,lariciresinol na pinoresinol,vitu hivi vitatu husaidia kupambana na kansa ya titi,kansa ya mfuko wa uzazi,tezi dume, na kansa ya yai la k**e(ovarian)

14.Husaidia kutibu kisukari,kupunguza lehemu na kudhibiti presha
Matango yana hormone inayohitajika na kongosho kwa ajili ya kuzalisha insulin, na pia yana compound(muunganiko wa k**emikali) inayoitwa sterol ambayo husaidia kudhibiti presha,Pia matango yana madini ya potassium na magnesium na fiber ,vitu hivi husaidia kudhibiti presha
Hii ndio sababu matango ni mazuri kutibu presha ya kushuka na presha ya kupanda
Asante sana kwa kusoma Makala hii mpaka mwisho naamini umetoka na kitu ambacho kitakufanya ulione tango kwa utofauti mkubwa k**a tiba
Imeandaliwa na
Yasinter Health Consultant

KARIBU SANA NDUGU YANGU KWA MAKALA ZIJAZO ZA AFYA NA K**A HUJALIKE PAGE HII LIKE LEO KWA KUJIPATIA MAKALA ZA AFYA ,
PIA KARIBU SANA KWA USHAURI NA TIBA JUU YA MAGONJWA SUGU
TUNATIBU KABISA PRESHA ,VIDONDA VYA TUMBO,KISUKARI NA MENGINE MENGI
MAWASILIANO
0753425148
WhatsApp 0753425148

FAIDA 17 ZA KUTUMIA MAJANI YA MPERA(GUAVA LEAVES).Habari yako rafiki yangu mpendwa ambae unaendelea kufuatilia Makala za...
26/07/2016

FAIDA 17 ZA KUTUMIA MAJANI YA MPERA(GUAVA LEAVES).
Habari yako rafiki yangu mpendwa ambae unaendelea kufuatilia Makala za afya kwenye page hii iitwayo Yasinter Health Consultant na k**a hujalike bofya like sasa uendelee kupata Makala zinazohusu afya yako. Siku ya leo ningependa kueleza kuhusu faida za kutumia mmea ambao umeonekana ni mmea wa kawaida ila unafaida nyingi katika afya yetu
Mapera ni matunda ya msimu yenye wingi wa vitamini A na C, madini ya potasiam, nyuzi nyuzi nzuri yani fiber na 'lycopene' vyote hivi ni muhimu kwa afya.
Watu wengi hutumia tunda tu pasipokujua si tunda pekee lenye manufaa kwa afya zao. Majani ya mpera ni mazuri sana kwa ajili ya kisukari,ngozi, nywele na afya yako kwa ujumla.

FAIDA ZA KUTUMIA MAJANI YA MPERA KWA AJILI YA AFYA YAKO.
1.Chai ya majani ya mpera inasaidia mwili kuwa stadi, inasaidia madini ya carbohydrates yasigeuzwe kuwa sukari ndani ya mwili hivyo kupunguza hamu ya kula.
2.Chai ya majani ya mpera pia inashusha kiwango cha sukari mwilini na kuzuia mwili kuondoa 'insulin'. Kwa sababu hii wagonjwa wa sukari wanashauriwa kuitumia mara kwa mara.
3.Chai ya majani ya mpera pia hupunguza lehemu mbaya(bad cholestrol) bila kudhuru lehemu nzuri.
4.Chai hii ina nguvu za kudhibiti vijidudu vya magonjwa mwilini hasa kuzuia magonjwa ya kuharisha na kipindupindu.
5.Chai hii inalinda mchafuko wa tumbo na pia inasaidia kukabili madhara yaletwayo na chakula chenye sumu.
6.Chai hii hutibu kukohoa na kupumua kwa tabu.
7.Upatapo uvimbe wa fizi na maumivu mdomoni k**a jino kuuma, tafuna majani ya mpera.
8.Kwa matatizo ya homa ya dengue, chemsha glasi mbili na nusu na majani ya mpera (kadiria majani 9) mpaka maji yabakie nusu ya ujazo wa awali.
9.Chai ya majani ya mpera imefahamika kutibu kansa na 'prostate' kwa wanaume.
10.Chai hii inasaidia kwa wanaume wenye tatizo la kuzalisha (Infertility).
11.Ponda majani ya mpera na kuweka sehemu ya kidonda au iliyokatika kuondoa maambukizi. Kwa maumivu nje ya sikio tumia chai ya majani ya mpera. Tia matone ya chai hii iliyopoa kwenye sehemu iliyoathirika.
13.Majani ya mpera hupondwa na kupakwa eneo lenye muwasho uletwao na allergy.
14.Unapoumwa na wadudu majani yaliyopondwa ni tiba sahihi.
15.Majani ya mpera yana saidia kupigana na mba na chunusi kutokana na wingi wake wa vitamini C.
16.Kuondoa madoa meusi kwenye ngozi ponda majani ya mpera changanya na maji kiasi na upake badala ya dawa za kawaida.
17.Fanya k**a namba16. kwa tatizo la ngozi kuzeeka mapema.
18.Majani ya mpera yanaondoa tatizo la kukatika kwa nywele. Chemsha majani kisha wacha yapoe na ukande kwenye paji na eneo la ngozi taratibu kwa dakika 15. Wacha kwa dakika 30 kisha osha na maji safi bila shampoo au sabuni. Fanya hivyo mara 3 kila wiki.
Wengi wananiuliza namna ya kuitengeza chai ya majani ya mpera. Kuna namna mbili. Aidha chemsha maji k**a glasi nne mpaka itokote sana, chukua majani k**a 10 ya mpera, weka ndani ya yale maji moto kisha funika kwa dakika 10 - 15 koroga, chuja, chai yako tayari. Aina ya pili ni chemsha maji hayo pamoja na majani yakiwa ndani. Ikitokota ondoa kwenye moto, wacha kwa dakika 10 -15 chuja, chai tayari. Waweza ukatumia majani yaliyo kauka pia.
Zingatia ukichanganya na asali badala ya sukari ndio bora zaidi.

Najua umepata kujifunza kitu rafiki yangu k**a umependezwa na tiba hii ya leo share na marafiki zako na magroup mbalimbali
Pia kwa ushauri juu ya afya yako mpendwa wasiliana nami kwa
NAMBA 0753425148
WhatApp 0753425148

16/07/2016

PEARL BEAUTFYING SOAP....TIBA YA KWELI KABISA.

ni sabuni iliyotengezwa kutokana na magamba ya viumbe wa baharini km simbi, konokono na viumbe wengine wa baharini.
Magamba hayo yanasagwa na kutolewa Mali ghafi ya kutengeneza sabuni bora pearl soap...!
Sabuni hii ina aina18 za amino acid..zaid ya aina 30 za trace element.na vitamins ambazo zinasafirisha material za virutubisho ndani ya ngozi na kuondoa vitu vigeni katika ngozi.

KAZI ZAKE.............!!
1.kutengeneza uzuri wa ngozi iwe na ubora wake..
2.inaimarisha uasili wa ngozi..
3.inaondoa mafuta na jasho na kuifanya ngozi kubaki kavu na safi..4.inasafisha na inaondoa sumu ndani ya ngozi..
5.inaondoa mabaka na upele..
6.kuponya muendelezo wa tishu zilizo haribika ndani ya ngozi..7.kuondoa mafuta yaliyoganda na kuziba vinyweleo na kuifanya ipumue vzr...
8.inaondoa chunusi na kuifanya sura ing'ae.
9.inang'arisha ngozi
10.inazuia uharibifu wa ngozi unaotokana na miali ya jua na miali na kemikali nyingine kupitia ngozi...!!
11,Inaondoa mba wa shingoni, mwilini na hata kichwani,
12,Inaondoa Fungus za aina zote hata kwa wanaonuka miguu wameliwa vidole wakivua viatu, .

Utaalamu huu wa kutumia viumbe wa bahari katika usafi na uimara wa ngozi ulianza karne nyingi nchini china na unaendelea hadi leo na hata wazee wakichina hawachoki ngozi na akili.

Ni nzuri kwa wanawake na wanaume watoto, vijana na wazee...!!

matumizi .
1.loweka ngozi kwa maji..
2.paka sabuni juu ya ngozi..
3.sugu kwa dakika 1-3.....
4.suuza kwa maji safi.
5.tumia mara 2 kwa siku kupata matokeo mazuri

Enjoy harufu nzuri na isiyoumiza pua zako yenye kukufanya upende kuendelea kuoga tu, harufu salama ya maua na zabibu..!

ANGALIZO,,
sabuni hii haijatengenezwa kwa kemikali za viwandani ni Tiba mbadala, hivyo unashauriwa kuitumia na kutokupaka vipodozi vya kemikali, hasa Lotion zenye hydroquinone, ina maana unatibu Kisha unajeruhi tena, Tumia Lotion zisizo na hizo kemikali.

Kwa Kuzipata sabuni hizi wasiliana nami
Kupitia namba 0753425148

TATIZO LA KUWASHWA SEHEMU ZA SIRI KWA WANAWAKE/VAGINAL ITCHING:Kwa kawaida kuwashwa sehemu za siri husababishwa na maamb...
06/07/2016

TATIZO LA KUWASHWA SEHEMU ZA SIRI KWA WANAWAKE/VAGINAL ITCHING:
Kwa kawaida kuwashwa sehemu za siri husababishwa na maambukizi ya fangasi au maambukizi mengine ya bacteria katika sehemu husika.Wakati mwingine mzio(allergy) pia inaweza kusababisha muwasho katika sehemu za siri.
-Muwasho maeneo ya ndani ya uke au kwenye mashavu ya uke husababishwa na mambo mengi. Muwasho ndani ya uke (va**na) unaweza kutokana na;
1.Matumizi ya kemikali au sabuni zilizowekewa dawa ya kuua bakteria ( detergents or medicated soaps),
2.Kwa kuosha ndani ya uke kwa sabuni zenye dawa ya kuua wadudu au kuondoa harufu (kitaalamu tunasema va**nal douching) na kitendo hiki hupelekea kuua bakteria wanaoishi kwenye uke (normal flora) kwa ajili ya kuulinda,
3.Kwa kutumia cream au manukato kwenye uke,
4.Kwa kutumia sabuni za bafuni(bath products)kwa kunawia maeneo hayo nyeti.
5. Wanawake ambao wameacha kuingia kwenye hedhi wanaweza kupata mwasho kutokana na kubadilika kwa kiwango cha homoni ya Oestrogen. Kwa kipindi hiki kuta za uke huwa nyembamba na kukauka na hivyo kupelekea kupata miwasho.

NAMNA GANI TUNAWEZA KUZUIA MWASHO SEHEMU ZA SIRI?
Wanawake wanatakiwa kuchukua hatua zifuatazo kuzuia mwasho sehemu za siri:
1.Namna ya kujitawaza baada ya haja ndogo au kubwa: Wanawake wanashauriwa kujitawaza kutokea mbele kuelekea nyuma ili kuzuia bakteria wa kwenye njia ya haja kubwa(anus) kuingia kwenye uke (va**na)
2.Kuzuia matumizi ya kemikali au sabuni zilizowekewa dawa ya kuua bakteria (detergents or soaps), kuosha ndani ya uke kwa sabuni zenye dawa ya kuua wadudu au kuondoa harufu (kitaalamu va**nal douching), kutumia cream kwenye uke, karatasi za chooni (toilet papers) na sabuni za bafuni (bath products)
3.Kuhakikisha sehemu za siri ni kavu baada ya kujisaidia au kuoga.
4.Kutokuvaa nguo za ndani ambazo hazibani sana (Wear loose natural fiber underwear and clothing)
5.Hakikisha sehemu za siri ni safi na kavu wakati wote,
6.Zuia kukaa na nguo zenye unyevunyevu kwa muda mrefu, 7.Jiepushe kufanya ngono zembe.
8.Tumia pedi bora zilizotengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu(anion chip technology) ili kujikinga na kujiepusha na miwasho na michubuko sehemu za siri pamoja na UTI.(Machukizo mbalimbali wakati wa hedhi)
KWA MAHITAJI YA PEDI HIZI WASILIANA NASI: 0753425148-calls & whatsapp.
Yasinter
Health Consultant
Karibu sana.

20/06/2016

FAHAMU UGONJWA WA UTI, DALILI NA JINSI YA KUEPUKA UTI SUGU
UTI(Urinary tract infection) ni ugonjwa wa maabukizi katika mfumo wa mkojo na maambukizi haya yanasababishwa na viumbe k**a bakteria,fangasi na virus. Maranyingi bakteria wanaoingia kwenye mfumo wa mkojo hutolewa na mwili,Wakati mwingine bakteria wanaweza zidi kinga ya mwili na kusababisha maambukizi hayo.
UTIs inaweza athiri urethra,kibofu cha mkojo na figo

MFUMO WA MKOJO
Mfumo wa mkojo ni mfumo wa mwili unaotumika kuondoa uchafu na maJi ya ziada
Mfumo huu unaundwa na ureta,kibofu cha mokojo,figo na urethra sitachambaua kwa undani hizi sehemu

KISABABISHI CHA UTI
Mara nyingi UTI zinasababishwa na bakteria aitwaye Escherichia coli (E. coli) na UTI nyingine zinaweza sababishwa na Chlamydia na Mycoplasma na UTI hizi zina athiri hadi mfumo wa uzazi na wanandoa wanapaswa kupata tiba pamoja,
Maambukizi ya UTI ni makubwa sana dunian Zaidi ya watu milioni 8 pointi 1 wanaathiriwa na ugonjwa huu

KWANINI WANAWAKE NDO WAHANGA WAKUBWA?
Wanawake ni wahanga wakubwa sana wa ugonjwa huu kulingana na maumbile yao ya nje
1.Urethra(mrija wa mkojo kutoka kwenye kibofu) kwa wanawake ni mfupi sana hivyo kuruhusu bakteria kufika kwa haraka kwenye kibofu
2.Pia mrija huo unafungukia sehemu ambazo zinaweza kuwa ni vyanzo bakteria ambayo ni sehemu ya uke na pili ni puru
Kwa wanaume ni vigumu sana ila wakipata tatizo linaweza kuwa zito kutibu tofauti na kwa wanawake

WATU WALIO KATIKA HATARI YA KUPATA UTI
wenye vidonda kwenye uti wa mgongo
yeyote mwenye tatizo katika mfumo wa mkojo
la ndoa linaweza likahamisha bakteria kutoka kwenye uke kwenda kwenye urethra
ya njia za uzazi k**a kutumia diaphragm,spermicides,kondomu nk

KURUDIARUDIA KWA UTI(UTI SUGU)
Mara nyingi wanawake wakipata UTI inaweza ikawa inajirudia mara kwa mara kulingana na sababu zifuatazo
1.Uwezo wa bakteria kujishika kwenye njia ya mkojo hivyo kutotibika na kurudia tena
2.Sababu nyingine ni wanawake kuwa non sector yani kuwa na damu grupu A,B na AB ambao hawawez kuzalisha kinga nzur kwa ajili ya hao bakteria

DALILI ZA UTI
1.Kukojoa mara kwa mara na maumivu wakati wa kukojoa
2.Kuhisi kuunguzwa na mkojo kwenye kibofu au mrija wa mkojo
3.Maumivu ya misuli na tumbo
4.Mkojo kuwa na harufu mbaya na pia kubadilika rangi kuwa nyeusi au rangi ya mawingu nk
5.Kwa mtu aliyeathiriwa figo anaweza kuwa na maumivu mgongoni au kwenye mbavu pia kichefuchefu na kutapika
6.Kushikwa na hamu ya kukojoa ila mkojo unatoka kidogo

JINSI YA KUZUIA UTI SUGU
1.Kunywa maji mengi kunsaidia kusafisha bakteria kwenye mfumo
2.Mtu anatakiwa akojoe mara kwa mara kila anapojiskia kukojoa
Mkojo ukikaa sana kwenye kibofu unaweza zalisha bakteria
Na baada ya kukojoa wanawake wanatakiwa kujisafisha kuanzia mbele kurudi nyuma ili kulinda urethra
3.Vaa nguo za ndani za pamba na ambazo hazibani sana kuruhusu hewa kupita vizuri ,epuka jinsi zinazobana sana ambazo zinaweza kukusanya na kuleta tatizo.
4.Tumia ped za neplily ped pekee zenye uwezo wa kuzuia na kutibu UTI na pia zinaruhusu hewa kupita vizuri
MATIBABU YA UTI SUGU
Tumia package yetu ya siku 90 ANTI-UTI PACKAGE package yenye dawa ya kuondoa tatizo la UTI sugu pamoja na pedi zake ambayo itakusaidia kuondokana na tatizo hilo package ambayo imesaidia wengi na inazidi kutoa ushuhuda kwa jamii
PACKAGE HII IPO YA WANAUME NA YA WANAWAKE UTI INATIBIKA
Kwa ushauri na matibabu wasiliana nasi kupitia no 0753425148 whatssap 0753425148

Address

Nyakato
Mwanza

Telephone

0753425148

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Yasinter health consultant posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share

Category