Elimika NA MONIE

Elimika NA MONIE Ni jukumu langu na najisikia vizuri kuwahudumia wanawake na wanaume wenye changamoto za uzazi.

Unachokihitaji Kuna Mtu anacho Tena hayuko mbali.... Ongea na watu Wana vitu vyako
23/08/2024

Unachokihitaji Kuna Mtu anacho Tena hayuko mbali.... Ongea na watu Wana vitu vyako

16/10/2023

DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

1) KUKOSA HAMMU YA KUFANYA TENDO LA NDOA
Tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa mwanaume ni moja wapo ya dalili za upungufu wa nguvu za kiume na linaweza kusababishwa na sababu nyingi sana.Sababu hizo zinaweza kuwa za kimaumbile au kisaikolojia au za mchanganyiko zote.Baadhi ya sababu za tatizo hili ni pamoja na;

a) Msongo Wa Mawazo (Depression).

Msongo wa mawazo ni ugonjwa wa kisaikolojia unaohusisha hali ya kuwa na mawazo makali kwa muda mrefu yanapolekea kukosa raha kutokana na kujihisi si mtu wa thamani au kukosa starehe katika vitu ulivyozoea kuvifanya na kukufurahisha hapo awali.Mawazo ya namna hii huathiri mwenendo wako wa maisha yako ikiwa ni pamoja na kukosa matamanio ya kimapenzi.

b) Matumizi Ya Madawa Na Pombe.

Matumizi ya baadhi ya madawa na unywaji wa pombe wa kupindukia vinaweza kupelekea tatizo hili la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa.Madawa yanayochangia tatizo hili ni pamoja na;Madawa ya presha ya kupanda(Anti hypertensive drugs), madawa ya kuondoa msongo wa mawazo, madawa yote yanayozuia ufanyaji kazi au uzalishaji wa testosterone, kwa mfano, cimetidine,finasteride na cyproterone n.k

c) Mawazo Mengi Na Uchovu.

Matatizo ya kikazi na hadhi yako kazini vinaweza kuchangia kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa.K**a unabezwa sana kazini na kujiona hutimizi kazi yako ipasavyo au k**a unachoka sana kazini pia vinaweza kupelekea kukosa hamu ya kufanya mapenzi pindi urudipo nyumbani kwani mahusiano ya kimapenzi yanahitaji yatengewe muda wa kutosha.

d) Kuwa Na Umri Mkubwa.

Kiwango cha homoni ya testosterone inayohusika na hisia za kimapenzi kwa mwanaume hupungua kwa asilimia 1-2 kila mwaka kadri mwanaume anavyozidi kuwa na umri mkubwa.Kiwango cha testosterone kikishuka katika mwili wa mwanaume humfanya asiwe na nguvu, ashindwe kutuliza mawazo kwenye jambo alifanyalo na apoteze hamu ya kufanya mapenzi.

e) Mahusiano Mabovu Baina Ya Mwanaume Na Mwanamke.

Matatizo ya kimahusiano kati ya mwanaume na mwanamke yana mchango mkubwa sana katika kusababisha tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa, mfano uwepo wa migogoro kati ya mume na mke, ukosefu wa amani na furaha katika mahusiano huchangia sana mwanaume kukosa hamu ya kufanya mapenzi.
K**a mahusiano yako na mpenzi wako yamekuwa ya miaka mingi sana, unaweza kuwa umemzoea mno mkeo kiasi kwamba ukaanza kukosa hamu ya kufanya naye tendo la ndoa.Hili nalo hutokea mara nyingi.

f) Matatizo Ya Kiafya.

Matatizo ya kiafya ya muda mrefu(chronic diseases) husababisha kupungua kwa hamu ya kufanya tendo la ndoa, mfano tatizo la kisukari, tatizo la presha, tatizo la moyo, tatizo la kansa ya muda mrefu, bawasiri ,na hali ya kuwa na unene uliozidi kiwango(obesity) n.k

2) KUTOKUWA NA UWEZO WA KURUDIA TENDO LA NDOA ZAIDI YA MARA MBILI
Mwanaume mwenye changamoto ya upungufu wa nguvu za kiume akishakamilisha mshindo mmoja wa tendo la ndoa basi anakua hana uwezo tena wa kurudia mshindo mwingine.Hali hii husababishwa na kutokuwepo na mshukumo wa damu wa kutosha kwenye mishipa ya uume.

3) KUTOKUWA NA UWEZO WA KUSIMAMISHA UUME KABISA AU UUME KUSIMAMA LEGELEGE NA KWA MUDA MFUPI TU

Kwa kawaida uume wa mwanaume aliyekamilika(rijali) unaposimama, hutakiwa kuwa imara k**a msumari, lakini kwa mwanaume mwenye changamoto ya upungufu za nguvu za kiume uume wake hata ukisimama hubakia kuwa lege lege na unaweza kusinyaa wakati wowote.
Tatizo hili ni matokeo ya kulegea kwa mishipa ya uume ambayo ndio huufanya uume usimame barabara.

4) KUWAHI KUFIKA KILELENI CHINI YA DAKIKA 17

Kuwahi kufika kileleni ni hali ambayo inampata mwanaume mwenye changamoto ya upungufu wa nguvu za kiume ambapo hutoa shahawa kabla ya kuanza tendo la ndoa au muda mfupi tu baada ya kuanza tendo la ndoa, bila yeye mwenyewe kukusudia.Kwa kawaida mtu mwenye tatizo la kuwahi kufika kileleni hutoa mbegu zake za kiume hata baada ya maandalizi kidogo sana.

5) KUCHOKA SANA NA KUKINAI KABISA BAADA YA TENDO LA NDOA WAKATI MWINGINE KUSIKIA HADI KICHEFUCHEFU

Hii ni mojawapo ya dalili za upungufu wa nguvu za kiume.Hali hii huwapata wanaume wenye changamoto ya upungufu wa nguvu za kiume ambayo wakati mwingine huambatana na usingizi mzito(Kulala fofofo).

6) KUHISI MAUMIVU WAKATI/BAADA YA TENDO LA NDOA

Hii pia ni mojawapo pia ya dalili za upungufu wa nguvu za kiume, hali hii huweza kuchangiwa na kauthirika kwa tishu za uume ambazo hutokana na upigaji wa punyeto kupita kiasi.

7) KUCHELEWA/KUSHINDWA KABISA KUFIKA KILELENI

Ni ile hali ya mwanaume kuchukua muda mrefu kutoa manii wakati wa kushiriki tendo la ndoa.
Kwa kawaida mwanaume anatakiwa afike kileleni/kutoa manii kwa muda usiozidi dakika 30 wakati wa kushiriki tendo la ndoa.Kwa hiyo mwanaume anaposhiriki tendo la ndoa na kuchukua muda mrefu bila kufika kileleni anahitaji uchunguzi ili kubaini chanzo cha tatizo.

08/10/2023

*UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NINI??*

Upungufu wa Nguvu za Kiume *Ni hali ya kushindwa kufanya mapenzi kikamililifu au kushindwa kusimamisha vizuri na kushindwa kutungisha Mimba.* Shughuli ya tendo la ndoa huhusisha akili, homoni, neva, misuli, hisia na mirija ya damu.

*Tatizo hili huripotiwa kuwa katika wanaume watatu (3) basi mmoja kati yao anatatizo la upungufu wa nguvu za kiume.* Upungufu wa nguvu za kiume huashiria kuto kuwa sawa kiafya hivyo ni tatizo linalohitaji tiba.

*Hili tatizo huwanyima watu raha kwa kuwa na mawazo, kuwa na matatizo katika mahusiano. Watu wengi wenye tatizo hili wanahitaji kutumia dawa zisizo na madhara na kubadilisha mitindo ya maisha yao ili kuweza kurudisha hali zao na kuondoa tatizo, cha msingi ni kuzingatia yale utakayoelekezwa.*

Kuna matatizo ya kutofanya mapenzi kikamilifu, nayo ni; kuwahi kumwanga mbegu za uzazi, Kuto kumwaga, kutokuwa na hamu ya tendo la ndoa.

*Tatizo la nguvu za kiume lina vyanzo vingi ambavyo mara nyingi wengi huvipuuza, hivyo vyanzo huathiri taratibu na vingine huathiri haraka, tunashauri watu kuwa makini sana ili kujiimarisha vizuri. Kuna mitindo ya maisha inayoweza kukuweka hatarini kupata tatizo la nguvu za kiume pia.

Send a message to learn more

20/09/2023

*HABARI ZA WAKATI HUU??*

LEO KWENU WANAUME WOTE KWA PAMOJA TUNAWALETEA NAKALA NZURI NA MUHIMU ZAIDI KUHUSU UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME.

*TUTAJIKITA ZAIDI KUHUSU👇👇;*
1.MAANA UA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME KWA UJUMLA WAKE.
2. VYANZO VYA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME.
3. DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME
4. HASARA(MADHARA YA) ZA KUPUNGUA KWA NGUVU ZA KIUME
5. TIBA YA KUDUMU INAYOTOKOMEZA TATIZO SUGU LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME.

*FATANA NASI HATUA KWA HATUA.

21/08/2023

KUVURUGIKA KWA HOMONI KWA MWANAMKE [HORMONAL IMBALANCE]

HOMONI ni kemikali zenye nguvu ndani ya mwili zinazozalishwa na matezi, homoni ndizo humfanya mwanaume kuwa mwanaume na mwanamke kuwa mwanamke mf. ndevu,bass, sauti nyororoo, ngozi laini n.k

HOMONI zinapozidi au kupungua huathiri mwili kwa kiwango cha juu sana.

**DALILI ZA KUVURUGIKA KWA HOMONI**

1.Kutokushika mimba

2.Kutoka na hedhi nzito au kukosa hedhi kwa miezi kadhaa,hedhi kuruka,kutoka hedhi mfululizo

3.Kutoka chunusi usoni,kifuani na mgongoni kwa juu

4.Kupata maotea ya ngozi [skin tags]

5.Uke kuwa mkavu

6.Maumivu wakati wa tendo la ndoa

7.Maumivu ya kiuno, mgongo na tumbo chini ya kitovu

8.Maumivu ya kichwa mara kwa mara

SABABU ZINAZOPELEKEA KUVURUGIKA KWA HOMONI

1.Matumizi ya njia za uzazi wa mpango k**a sindano na vidonge .

2.Stress/msongo wa mawazo.

3.Ulaji mbovu

4.Matumizi ya tiba za kansa k**a vile mionzi

5.Kisukari

6.Goita

7. Ujauzito na kunyonyesha.

MADHARA YA KUVURUGIKA KWA HOMONI KWA MWANAMKE
1. Kutokushika mimba
2.Mimba kutoka mara kwa mara
3.Kuvurugika kwa hedhi
4.Kukaribisha magonjwa katika mfumo wa uzazi

MATIBABU
Namna ya kutatua tatizo la Kuvurugika kwa homoni kwa kutumia virutubisho lishe wasiliana nasi kwa Whatsapp namba 0789907021.

Address

Shinyanga

Opening Hours

Monday 09:00 - 22:00
Tuesday 09:00 - 22:00
Wednesday 09:00 - 22:00
Thursday 09:00 - 22:00
Friday 09:00 - 22:00
Saturday 09:00 - 22:00

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Elimika NA MONIE posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Elimika NA MONIE:

Shortcuts

Share