23/04/2025
Bado kuna imani potofu katika jamii wanapoona mtu amepatwa na kiharusi.
Siku zote kuwa mjanja, mtu wa kujaribu kufikiria zaidi ya waliokuzunguka, Kiharusi sio swala la kulogwa.
Inashauriwa mtu ajue presha yake inaendeleaje kadiri umri unavyozidi kuongezeka ili kuweza kudhibiti Shinikizo la juu la 🩸ambayo husababisha Kiharusi isiporatibiwa vizuri.
MOJA YA VISABABISHI VYA SHINIKIZO LA JUU LA DAMU:
🩸 Umri.
🩸 Kurithi 🧬
🩸 Uzito kupindukia ⚖️
🩸 Matumizi ya Chumvi🧂kupita kiasi.
🩸 Kutofanya mazoezi.🏋️
🩸 Matumizi ya Pombe🍺
Kubadili mtindo wa maisha, k**a kula mlo kamili, kuacha au kuounguza matumizi ya pombe na sigara, kutumia chumvi kwa kiwango sahihi, kufanya mazoezi nk, huweza kusaidia kupunguza hatari ya kupata Shinikizo la juu la damu, kwa baadhi ya watu, bado itawabidi watumie dawa.
NB:
SHINIKIZO LA JUU LA DAMU HUTAMBULIKA TU PALE AMBAPO MGONJWA AMEPIMA PRESHA KWA SIKU ZAIDI YA MOJA NA KUSOMEKA 140/90 mmHg au zaidi kwa kila siku aliyopimwa.
⚠️
Presha ni kitu cha kimya kimya, k**a hujapima, usidhubutu kusema sina.