08/04/2023
USHAURI KWA WANAUME WENZANGU KUHUSU
WAKE ZAO WAJAWAZITO...
Mimi ni mwanaume, lakini leo nataka tujadili
kuhusu MIMBA.
Je! unajua kuwa mambo fulani unayomfanyia mkeo akiwa mjamzito yanachangia hali nzuri/mbaya ya afya ya mama na mtoto ambaye hajazaliwa?
Sikiliza, huwa inanisumbua sana ninapoona wanaume wanashindwa kuwajali wake zao wajawazito au kushindwa kuzoea mabadiliko fulani ya muda!!!
Ni miezi 9 tu, sio milele. Mimba hainunuliwi sokoni, wala sio App iliyodownlodiwa mtandaoni. Ni mbegu iliyopandwa na sisi wanaume na ikaota. Inabidi kuwe na mtoaji wa mbegu hiyo wakati inakua, na wanawake wamepewa jukumu la kuibeba.
Mimba ni maandalizi ya kumkaribisha Mgeni mpya kwenye familia. Mimba ni safari ya furaha..
Wanawake wametofautiana kwenye mabadiliko ya mwili. Ingawa Mimba huwafanya wanawake kufanya mambo fulani kwa pamoja.
■ Anaugua mara kwa mara
■ Anatamani kula vitu visivyofikirika k**a, udongo, mkaaa au chai iliyotiwa ndimu.
■ Anakuwa mvivu kukuandalia chakula
■Mara moja moja atataka kunyoosha miguu yake kwenye mapaja yako. Tafadhali msamehe... kubeba mtoto si rahisi.
Nusu ya kwanza ya safari inaweza kuwa ya kuudhi sana. K**a nilivyosema, wanawake hutofautiana wakati wa ujau*ito.
*😩Wengine wako busy kutapika.
*😴Wengine hulala k**a jani la maji, hulala popote hata jikoni.
*😤Wengine hushikwa na homa za mara kwa mara.
*😒Wengine wanaonekana wanyonge na wamepauka k**a poda ya Jonson.
*😱Wengine huongezeka u*ito.
*😫Wengine wanazunguka na leso Nyeupe ya kutemea mate.
HAYA YOTE BADO NI KAZI YETU.....
Tafadhali vumilia hii, ina matokeo mazuri baadaye.
Kuna wakati mambo yao yanaudhi, unapaswa kuvumilia. Lakini mimi nachoka sana ninapoona wanaume k**a mimi wakiwatelekeza wake zao wajawazito. Lazima niseme, sio safari rahisi kwa wote.
Nusu safari ya mwisho ni wakati tunatakiwa kuwa na subira zaidi, upendo, uvumilivu na kuelewa.
KUMBUKA...
1) Siku zote angalia miguu ya mkeo wakati wa ujau*ito, inavimba mara kwa mara. Tafadhali mpe beseni la maji ili aloweke mguu wake mara moja baada ya muda, ni moja ya tiba bora zaidi ambayo wanawake hufurahia wakati wa ujau*ito.
2) Muulize mara kwa mara jinsi anavyohisi na jinsi anavyomsikia mtoto. Yeye ndiye mbebaji kwa hiyo anazijua harakati zake.
3) Mwambie jinsi anavyoonekana mrembo wakati wa ujau*ito k.m
“Honey ona jinsi mimba inavyokupendeza, nitakuwa nakupa mimba kila mwezi "
au
“ni mtoto wangu anakufanya uwe mzuri namna hii kupita kawaida".
4) Usikasirike k**a atawahi kukuamsha asubuhi ili kumkanda miguu. Tunatakiwa kuhisi kidogo usumbufu na maumivu yake. Hapaswi kuhangaika peke yake, ni mtoto wetu, tunahitaji kusumbuka pamoja. (Simaanishi kubeba mimba kimwili).
5) Hakuna kitabu cha sheria kilichozuia ngono wakati wa ujau*ito, kwa kifupi ni nzuri na bora sana .... fanya hivyo, kijana endelea na kazi inayolet ujau*ito.
6) Usione aibu kumtoa out. Mtoe out mara moja moja hadi kwenye sehemu mlizokuwa mnaenda pamoja....
Natoa wito kwa wanaume wote kuwa karibu na wenzi wao wakati wa ujau*ito kwani hiyo ni moja ya nyakati anazokuhitaji sana.
Pongezi kubwa kwa wanaume wenzangu wote wanaosimama kikamilifu na wake zao wakati wa ujau*ito.
Mungu awabariki wote....