Tiba Asili ya Mimea na Chakula

Tiba Asili ya Mimea na Chakula Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Tiba Asili ya Mimea na Chakula, Therapist, Tanga.

Tibu na Boresha Afya ya Mwili Wako kwa Kutumia Mimea Tiba na Chakula. 🌿🍏

Heal and Improve Your Body’s Health Using Medicinal Plants and Nutritious Food. 🌿🍏

WhatsApp +255 687 077 717

https://youtu.be/1-8s_08vj0kTIBA YA ASILI YA PID NA CHANGAMOTO NYENGINE MBALIMBALI KATIKA MFUMO WA UZAZI WA MWANAMKE!JIF...
21/04/2026

https://youtu.be/1-8s_08vj0k

TIBA YA ASILI YA PID NA CHANGAMOTO NYENGINE MBALIMBALI KATIKA MFUMO WA UZAZI WA MWANAMKE!

JIFUNZE NAMNA YA KUANDAA TIBA YA MIMEA ASILI NYUMBANI YENYE UWEZO MKUBWA KATIKA KUTIBU CHANGAMOTO MBALIMBALI ZA KIAFYA KATIKA MFUMO WA UZAZI WA MWANAMKE

Katika Somo letu la leo utajifunza kuhusu Tiba ya Asili (Natural remedies) ya Mimea yenye viambata kemikali asili vyenye uwezo mkubwa sana wa kutibu (Natural healing) Changamoto mbalimbali za kiafya katika mfumo wa uzazi wa mwanamke (Reproductive health). Changamoto k**a vile Pelvic Inflammatory Disease (PID), Ugonjwa wa maambukizi ya bakteria katika Viungo au Mfumo wa Uzazi wa Mwanamke na Jinsi ya kuandaa tiba ya Mimea yenye viambata kemilikali asili vyenye uwezo wa kuondoa maambukizi na athari mblimbali za kiafya katika mfumo wa uzazi wa mwanamke zilizosababishwa na vimelea hivyo.

DALILI NA ATHARI ZA MAAMBUKIZI YA BAKTERIA KATIKA MFUMO WA UZAZI WA MWANAMKE (PID):

i. Kutoka Majimaji, Uchafu na Usaha Mweupe au rangi ya kahawia ukeni
ii. Uke kutoa harufu kali na ya kukela mfanano wa shombo ya samaki.
iii. Maumivu makali ya tumbo la chini ya kitovu kabla na wakati wa hedhi
iv. Maumivu sugu kwenye Nyonga, kiuno na Mgongo
v. Mvurugiko wa homoni za Uzazi
vi. Kuziba kwa mirija ya Uzazi
vii. Mimba kuharibika
viii. Mimba nje ya mfuko wa uzazi (Ectopic pregnancy)
ix. Majipu kwenye mirija ya uzazi (Tubo-ovarian abscess)
x. Ugumba (Kupoteza uwezo kabisa wa kushika ujauzito)
xi. Kupoteza hamu ya kujamiana (Kushiriki tendo la ndoa)
xii. Uke kuwa mkavu na kupata maumivu wakati wa kujamiana
xiii. Changamoto katika mfumo wa hedhi wa Mwanamke
xiv. Uvimbe kwenye kizazi au Mirija ya Uzazi (Fallopian Tubes)
xv. Kutokwa na damu ukeni wakati wa kujamiana
xvi. Saratani ya shingo ya kizazi (Cervical cancer)

Kwa Ujumla Mimea hii hufanya kazi kwa hatua nne kuu:
i. Kuua bakteria (Antibacterial action)
ii. Kupunguza uvimbe (Anti-inflammatory action)
iii. Kulinda na kurejesha tishu (Antioxidant & healing action)
iv. Kuimarisha kinga ya mwili (Immune support)

MIMEA INAYOTUMIKA:
Mimea k**a vile Mzugwa (Plectranthus barbatus), Kivumbasi (Ocimum sanctum), Mfagio (Sida acuta), Mrejesha Uhai (Boerhavia diffusa), Mziwaziwa (Euphorbia hirta)

TAHADHARI ZA MATUMIZI YA DAWA YA MIMEA (PRECAUTIONS)
NANI HAPASWI KUTUMIA (NA SABABU ZAKE):

1. Wanawake wajawazito
Sababu:
• Baadhi ya mimea (hasa Sida acuta na Euphorbia hirta) inaweza kuchochea misuli ya mfuko wa uzazi.
• Inaweza kuongeza hatari ya kuharibika kwa mimba.

2. Mama anayenyonyesha mtoto chini ya miezi 6
Sababu:
• Baadhi ya viambata vinaweza kupita kwenye maziwa ya mama na kuathiri mtoto.

3. Watu wenye magonjwa sugu makubwa
Mfano:
• Magonjwa ya figo
• Magonjwa ya ini
• Magonjwa ya moyo
Sababu:
Viambata vya mimea huchakatwa kwenye ini na figo, hivyo vinaweza kuongeza mzigo kwenye viungo hivyo.

4. Watu wanaotumia dawa za hospitali (antibiotics au dawa za homoni) bila ushauri wa daktari
Sababu:
• Mimea inaweza kuingiliana na dawa (drug interaction).
• Inaweza kupunguza au kuongeza nguvu ya dawa za hospitali.

5. Watoto walio chini ya miaka 18
Sababu:
• Mfumo wa homoni bado haujakomaa kikamilifu.
• Dozi salama kwa watoto haijathibitishwa vizuri.

6. Mtu mwenye PID kali sana au dalili hatarishi
Dalili k**a:
• Homa kali,
• Maumivu makali ya tumbo,
• Kutapika,
• Kutokwa damu nyingi ukeni.
Sababu:
Hii ni hali ya dharura inayohitaji matibabu ya hospitali haraka (antibiotics za kitaalamu).

TAHADHARI ZA JUMLA ZA MATUMIZI
• Tumia kwa muda uliopendekezwa tu.
• Usiongeze kiwango cha matumizi bila ushauri.
• Acha kutumia ukipata:
o kichefuchefu kikali,
o maumivu yasiyo ya kawaida,
o mzio au vipele.

Video hii pia inaonyesha jinsi tiba asilia (herbal remedies) zinavyoweza kusaidia katika kuimarisha Afya ya Mfumo wa uzazi wa mwanamke, ikiwemo matumizi ya mimea k**a Kivumbasi (Ocimum sanctum), Mziwaziwa (Euphorbia hirta), kirejesha uhai (Punarnava – Boerhavia diffusa), mfagio (Sida acuta), na Mzugwa (Plectranthus barbatus).

TIBA YA ASILI YA PID: TIBU CHANGAMOTO MBALIMBALI ZA KIAFYA KATIKA MFUMO WA UZAZI WA MWANAMKE

Mimea ni Uhai, ifuatayo ni mimea yenye uwezo tiba Asilia kutokana na viambata kemikali hai vilivyoundwa ndani yake:Hii m...
05/01/2026

Mimea ni Uhai, ifuatayo ni mimea yenye uwezo tiba Asilia kutokana na viambata kemikali hai vilivyoundwa ndani yake:

Hii mimea inasifa za k**emikali yenye uwezo wa kufanya yafuatayo:

-> Diuretic (Kuchochea kutoa maji yasiyohitajika mwilini kwa njia ya mkojo)

-> Anti-oxidants (Kuondoa seli zilizo haribiwa kutoka na mfumo wetu wa maisha ambazo ni chanzo cha saratani na magonjwa na kufanya seli kuwa imara zaidi)

-> Anti-bakterials (Kupambana na vimelea hatari mwilini ikiwemo bakteria)

-> Anti-inflammatory (Kupambana na uvimbe na maumivu mwilini)

-> Anti-ulcers (Kutibu vidonda na majeraha ndani ya mwilini)

Hivyo kuifanya kuweza kutatua changamoto mbalimbali za kiafya k**a vile;

1. Vidonda vya Tumbo (Stomach ulcers)

2. Kiwango kikubwa cha Tindikali Tumboni (High Acidity)
Kiungulia (Heartburn)

3. Tumbo kujaa gesi na Mingurumo

4. Maumivu ya tumbo na Maambukizi ya tumbo (Amoebiasis)
Mwili (tishu) kujaa maji (Edema)

5. Maambukizi sugu ya Njia ya Mkojo na figo (U.T.I & Pyelonephritis)
Mawe kwenye Figo na Kibofu cha Mkojo (Kidney and bladder stones)
Maambukizi katika Ini (Hepatitis)

Tumia ujazo wa kiganja kimoja kwa kila Mmea ponda au Saga kisha loweka kwenye maji Bilauri (Glasi) Moja (1) kwa masaa 3 kisha kunywa kutwa mara 2 kwa siku kwa jumla ya siku 7 hadi 21 kulingana na changamoto yako.

Hayo majani ni salama kwa Afya ila tunashauri mama mjamzito, anaenyonyesha, mtu mwenye shinikizo la damu la kushuka au mtu ambae anaendelea na matibabu makubwa ya figo au moyo ni vyema atumie kwa ushauri wa daktari.

Mfano mimea hii ususni mmea wa Mrejesha uhai au mkwayakwaya uchochea sana figo kufanya kazi ya kutoa taka mwili na maji yasiyohitajika mwilini bila kuathiri virutubisho kwenye mwili wako hivyo k**a figo zako zipo katika hatua mbaya sana zinaweza elemewa na kushindwa kufanya kazi kubwa hiyo kubwa inayolazimishwa na mimea hapo chini.

TIBA YA CHANGAMOTO ZA HEDHI KWA WASICHANA NA KINA MAMA: YouTube: https://youtu.be/h3hx_mWAMUMTiktok: https://www.tiktok....
19/10/2025

TIBA YA CHANGAMOTO ZA HEDHI KWA WASICHANA NA KINA MAMA:
YouTube: https://youtu.be/h3hx_mWAMUM
Tiktok: https://www.tiktok.com/.jterapy/video/7563013367711943992

Hbari,
Leo tutazungumzia tiba na mbinu za kukabiliana na changamoto mbalimbali za hedhi ambazo huwakumba wanawake wengi.

Changamoto hizo ni pamoja na:
• Kupata damu ya hedhi yenye mabonge - mabonge;
• Kuwai Kumaliza damu ya hedhi Mapema sana,
• Kupoteza majira (kuvurugika mpangilio wa siku zako za hedhi),
• Kupata damu ya hedhi kwa kiasi kidogo sana,
• Kupata damu ya hedhi nyepesi sana au nzito isivyo kawaida,
• Kupata damu ya hedhi zaidi ya mara moja kwa mwezi,
• Kupata damu ya hedhi mfululizo zaidi ya mwezi moja,
• Kupata maumivu makali ya tumbo wakati wa siku zako za hedhi,
• Tumbo kujaa gesi, na Minguruumo wakati wa siku za hedhi.

SABABU ZINAZOSABABISHA CHANGAMOTO ZA HEDHI:

Zipo sababu mbalimbali zinazosababisha wanawake wengi kupata changamoto mbalimbali za hedhi, sababu hizo ni k**a ifuatavyo;

A. ATHARI ZA LISHE KWA MZUNGUKO WA HEDHI:

1. Mlo usio na afya:
Kula vyakula visivyo na virutubishi muhimu au kula vyakula vingi vya kusindika (processed foods) kunaweza kusababisha usumbufu wa usawa wa homoni (Hormon imbalances) ambayo pia ni sababu kubwa ya matatizo kwenye mfumo wa hedhi kwa mwanamke,

2. Upungufu wa virutubishi:
Mwili unapokosa madini na vitamini muhimu, uwezo wake wa kudhibiti homoni hupungua, hivyo kuathiri mpangilio wa hedhi,

Madhara ya Moja kwa Moja kwenye Hedhi:
1. Kuongezeka kwa maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi.
2. Kupata hedhi nzito na ya muda mrefu kuliko kawaida.
3. Hedhi kurudi zaidi ya mara moja kwa mwezi au kutokuwa na mpangilio.
4. Kuchelewa kwa hedhi au hata kukosa kabisa kwa muda fulani (amenorrhea).

Ushauri/Angalizo:
Ni makosa kwa mwanamke kutumia vinywaji vya baridi (cold drinks) k**a vile Maji ya baridi, soda, juisi, Ice cream na vitu vingine vya baridi kwa ujumla. Pia si vyema kutumia vitafunwa (bites), ni K**a hamburger, sausage, mikate, pilipili, vitu vya kukanga k**a vile chips, mayai ya kukaanga, miogo ya kukaanga na vingine vingi, epuka vyakula vya Viwandani kwa ujumla.

Hakikisha mlo wako unajumuisha;
• Mafuta yenye afya (parachichi, karanga, mbegu),
• Kula vyakula vyenye nyuzinyuzi nyingi (majani ya majani, shayiri, matunda),
• Punguza sukari na wanga iliyosafishwa.

B. ATHARI ZA MAAMBUKIZI YA FANGASI NA BAKTERIA (PID) KATIKA HEDHI YA MWANAMKE:

Maambukizi ya fangasi na bakteria yanaweza kushambulia uke na via vya uzazi vya ndani na kusababisha hali inayojulikana k**a PID (Pelvic Inflammatory Disease). Hii ni maambukizi kwenye mfumo wa uzazi wa mwanamke ambayo huathiri shingo ya kizazi, mji wa mimba, mirija ya uzazi (fallopian tubes) na hata ovari.

1. Kuvuruga mzunguko wa hedhi: Maambukizi yanapofikia mji wa mimba na mirija ya uzazi, huchochea uvimbe na kuwasha ambao unaweza kuathiri usawa wa homoni, hivyo kusababisha kuchelewa au kukosa hedhi.

2. Hedhi nzito na ndefu: PID mara nyingi huambatana na kuvimba kwa ukuta wa mji wa mimba, jambo linalosababisha damu nyingi kutoka wakati wa hedhi, na hedhi kudumu zaidi ya siku za kawaida.

3. Maumivu makali wakati wa hedhi (Dysmenorrhea): Kuvimba na makovu (scarring) yanayotokana na maambukizi husababisha maumivu ya tumbo la chini na kiuno wakati na hata kabla ya hedhi.

4. Kutokea kwa hedhi zisizo za kawaida (Irregular bleeding): PID inaweza kusababisha damu kutoka katikati ya mzunguko (intermenstrual bleeding) au kutokwa na damu baada ya tendo la ndoa.

5. Kuvuruga uwezo wa uzazi: Endapo PID itasababisha mirija ya uzazi kuziba au kupata makovu, hali hii si tu inaleta matatizo ya uzazi bali pia inaweza kuathiri mpangilio wa hedhi kwa ujumla.

6. Maambukizi ya mara kwa mara: Fangasi na bakteria wakirudia mara kwa mara, husababisha mabadiliko ya mazingira ya uke, hivyo kuongeza uwezekano wa hedhi zenye maumivu na zisizo za kawaida.

C. ATHARI ZA MATUMIZI YA DAWA ZA KUZUIA MIMBA (P2) KATIKA HEDHI:

P2 haileti hedhi isiyo ya kawaida kwa kila mwanamke, lakini matumizi yake huathiri kwa kiwango kikubwa mzunguko wa hedhi, kiasi cha damu, na muda wa kuanza kwa hedhi kutokana na mabadiliko ya homoni.

1. Kuvuruga mzunguko wa hedhi: P2 ina kiwango kikubwa cha homoni (levonorgestrel) kinachotumika kuzuia mimba baada ya tendo la dharura. Homoni hii hubadilisha mfumo wa kawaida wa homoni mwilini, na kusababisha kuchelewa au kusogea mbele kwa tarehe ya hedhi.

2. Kubadilika kwa kiasi cha damu ya hedhi: Baadhi ya wanawake hupata hedhi nzito kuliko kawaida, huku wengine wakipata damu kidogo sana au hata doa doa tu (spotting).

3. Kuchelewa au kukosa hedhi kwa muda mfupi: Baada ya kutumia P2, inaweza kuchukua muda kwa mwili kurudi katika mzunguko wa kawaida. Hali hii mara nyingi huleta wasiwasi kwa mtumiaji.

4. Kutokwa damu katikati ya mzunguko: Baadhi ya wanawake hupata kutokwa na damu bila mpangilio, hata kabla au baada ya hedhi halisi, kutokana na mabadiliko ya ghafla ya homoni.

5. Maumivu na dalili zinazofanana na PMS: Matumizi ya P2 yanaweza kuambatana na maumivu ya tumbo la chini, kichefuchefu, kuvimba matiti, na mabadiliko ya hisia – dalili ambazo huathiri kwa muda mzunguko wa hedhi.

6. Matumizi ya mara kwa mara: Endapo P2 itatumika mara kwa mara, inaweza kusababisha kuvurugika kwa hedhi kwa muda mrefu, na wakati mwingine kuathiri afya ya mfumo wa uzazi.

D. MABADILIKO YA HALI YA HEWA NA ATHARI KWA HEDHI:

1. Mabadiliko ya homoni kutokana na mazingira: Hali ya hewa inapobadilika ghafla (baridi kali, joto kali, unyevunyevu au ukame), mwili hujaribu kujibadilisha. Hii inaweza kuathiri usawa wa homoni, na kusababisha mzunguko wa hedhi kuvurugika.

2. Kuchelewa au kukosa hedhi: Safari za mbali, kuhama mikoa au nchi zenye hali ya hewa tofauti, au mabadiliko ya ghafla ya joto la mwili, vinaweza kusababisha mwili kuchelewa kutoa mayai (ovulation). Hali hii husababisha hedhi kuchelewa au kukosa kabisa.

3. Kuongezeka kwa maumivu ya hedhi: Baridi kali mara nyingi huufanya misuli ya tumbo kukaza zaidi, na kusababisha maumivu makali wakati wa hedhi (dysmenorrhea).

4. Mabadiliko ya kiasi cha damu ya hedhi: Baadhi ya wanawake hupata damu kidogo zaidi wakiwa kwenye maeneo ya baridi kali, huku wengine hupata damu nyingi zaidi wanapokuwa kwenye mazingira ya joto au yenye shughuli nyingi za kimwili.

E. MSONGO WA MAWAZO (STRESS), WOGA AU HOFU NA ATHARI KWA HEDHI

1. Kuvuruga usawa wa homoni: Stress inapoongezeka, mwili huzalisha kwa wingi homoni ya cortisol. Hii husababisha kuvurugika kwa homoni za uzazi k**a estrogeni na projesteroni, ambazo ndizo zinazosimamia mzunguko wa hedhi.

2. Kuchelewa au kukosa hedhi: Hofu na wasiwasi wa mara kwa mara huweza kuzuia ovulation (kutolewa kwa yai), jambo linalopelekea hedhi kuchelewa au kukosekana kabisa kwa muda fulani.

3. Hedhi nzito au yenye maumivu makali:Baadhi ya wanawake wakipatwa na msongo wa mawazo hupata damu nyingi zaidi au maumivu makali ya tumbo (cramps) kuliko kawaida.

4. Hedhi isiyo na mpangilio: Woga wa mara kwa mara au msongo wa mawazo unaweza kufanya siku za hedhi kubadilika kila mwezi, mara zikatokeza mapema, mara zikachelewa, au zikawa fupi sana.

5. Dalili za awali za hedhi kuongezeka: Stress mara nyingi huongeza dalili za kabla ya hedhi (PMS), k**a vile maumivu ya kichwa, hasira, uchovu, na kichefuchefu.

F. UVIMBE KWENYE KIZAZI NA ATHARI KWA HEDHI:

1. Kuchangia hedhi isiyo ya kawaida: Uvimbe kwenye kizazi (k**a fibroids au polyps) unaweza kusababisha damu nyingi au hedhi isiyo ya kawaida, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa siku za hedhi.

2. Maumivu makali: Wakati wa hedhi, uvimbe unaweza kuongeza maumivu ya tumbo (cramps) na kutuma hisia za shinikizo au usumbufu wa ndani ya kizazi.

3. Kuchelewa au kukosa hedhi: Baadhi ya uvimbe, hasa pale unapokuwa mkubwa au unaoingiliana na mfumo wa homoni, unaweza kusababisha mzunguko wa hedhi kusababisha kuchelewa au hata kukosa hedhi kwa muda fulani.

4. Kuongeza hatari ya maambukizi: Uvimbe unaweza kuingiza mazingira ambayo yanarahisisha kuenea kwa bakteria au fangasi, jambo linaloweza kusababisha maambukizi ya via vya uzazi (PID) na kuathiri hedhi.

5. Dalili za mara kwa mara: Dalili nyingine ni uchovu, kushindwa kushika mimba kwa urahisi, na kuongezeka kwa maumivu wakati wa tendo la ndoa.

G. KUZIBA KWA MIRIJA YA UZAZI (Fallopian Tubes) NA ATHARI KWA HEDHI:

1. Kuathiri mzunguko wa hedhi: Kuziba kwa milija ya uzazi kunazuia mayai kutoka kufika kwenye kizazi, jambo linaloweza kusababisha hedhi isiyo ya kawaida au kuchelewa kwa hedhi.

2. Kuongezeka kwa maumivu: Mayai yanapokuwa yamefungwa ndani, kunaweza kutokea maumivu makali ya tumbo chini ya kitovu (pelvic pain) wakati wa ovulation au hedhi.

3. Kuzalisha tatizo la uzazi: Mayai yanayokosa kutoka kwenye milija husababisha tatizo la kuzaa (infertility), ambalo linaweza kuathiri homoni na mzunguko wa hedhi.

4. Kuongeza hatari ya maambukizi: Milija iliyoziba inaweza kuwa chanzo cha maambukizi, k**a PID (Pelvic Inflammatory Disease), ambayo pia huathiri hedhi na afya ya kizazi kwa ujumla.

H. MATUMIZI YA VIDONGE VYA MPANGO WA UZAZI NA HEDHI YA MWANAMKE

1. Mabadiliko ya mzunguko wa hedhi: Vidonge vya mpango wa uzazi vinaweza kusababisha hedhi kuwa hafifu (light bleeding) au kusimama kabisa (amenorrhea) kwa muda.

2. Kutofautiana kwa muda wa hedhi: Baadhi ya wanawake wanaweza kuona hedhi zinachelewa au kuanza mapema kuliko kawaida.

3. Kuongeza au kupunguza maumivu ya hedhi: Baadhi ya wanawake hupata kupungua kwa maumivu ya hedhi (dysmenorrhea), huku wengine wakiona maumivu yan**idi kwa miezi michache ya mwanzo ya matumizi.

4. Kuathiri homoni: Vidonge huingilia homoni za k**e (estrogen na progesterone), jambo linaloweza kuathiri mzunguko wa kawaida wa hedhi.

5. Dalili nyingine zinazoweza kuambatana: Kutokwa na damu zisizo za kawaida (spotting), kutokuwa na hedhi kwa muda mfupi, au hedhi kuwa nzito mara moja kwa mwezi.

MCHANGANYIKO WA MIMEA NA MBOGA KWA AFYA YA HEDHI NA UIMARA WA AFYA YA UZAZI KWA MWANAMKE:

K**a wewe ni mwanamke ambae ni muhanga wa changamoto k**a nilivyokwisha elezea awali, ni vyema ukazingatia Maelekezo hapo juu ya vitu vya kuepuka na kutekeza kabla ya kuanza kutumia dawa kwa matokeo dhabiti ya dawa.

MAHITAJI:
• Tangawizi (mbichi au unga) – kiasi kidogo
• Mdalasini ya unga – kiasi kidogo
• Manjano (mbichi au unga) – kiasi kidogo
• Unga wa karafu – kiasi kidogo
• Pilipilimanga – kiasi kidogo
• Jira (unga wa jira) – kiasi kidogo
• Unga wa iliki – kiasi kidogo

MAANDALIZI:
• Changanya viungo vyote (tangawizi, mdalasini, manjano, karafu, pilipilimanga, jira na iliki) na usage vizuri hadi viwe unga.
• Weka unga huo kwenye chombo/kopo lenye mdomo mpana,
• Tafuta Asali halisi ya nyuki wadogo ujazo wa chupa unao kupa nusu kilo,
• Maji ya safi na salama ya uvuguvugu,
• Kijiko kimoja cha chakula,
• Glasi au kikombe cha chai.

MATUMIZI:
• Wakati hedhi imeanza chota unga wako wa dawa, vijiko viwili (2) vya chakula,
• Weka kwenye asali (nusukilo) na koroga (kwa kijiko upande wa kushikia) mchanganyiko vizuri hadi unga wa dawa uchanganyike vizuri kabisa kwenye asali yako,
• Chota vijiko 2-3 vya mchanganyiko wa unga na asali, kisha weka kwenye glasi yenye iliyojazwa maji ya uvuguvugu,
• Koroga mchanganyiko wako huo vizuri kwenye maji kisha kunywa kutwa mara tatu kwa siku kwa siku saba (7),
Faida
• Huongeza mzunguko wa damu wakati wa hedhi, ikisaidia kuondoa mapande ya damu yaliyokaa ndani.
• Huongeza uimara wa mwili na kudumisha afya ya kiume na ya k**e.
• Huongeza ufanisi wa kudhibiti maumivu ya tumbo wakati wa hedhi.
• Huongeza uwezo wa mwanamke kushika mimba na kudumisha afya ya kizazi.

AGALIZO/USHAURI:
• K**a unaweza pata maziwa halisi ya ng’ombe au uji mwepesi sana, badala ya maji ya uvuguvugu itakuwa vizuri zaidi.
• Tumia dawa hii wakati wa hedhi tu kwa mwanamke,
• Hakikisha zingatia Maelekezo ya vitu gani vya kuepuka navyo na vitu gani vya kufanya ili kuifanya dawa hii iwe na matokeo na ufanisi wa kudumu,
• Zingatia hatua za maandalisi na kipimo sahihi k**a ulivyoelekezwa.


MADHARA:
• Dawa hii haina madhara yoyote.

MATOKEO:
• Wakati unatumia utaona hedhi yako inaanza kutoka ya mapande/mabonge mabonge hali iyo isikushtue kwani miraja yako ya uzazi
• K**a ulikuwa ushiki ujauzito sababu ya mirija yako kuziba utashika ujauzito haraka sana.
• Utapata hedhi yako kwa wakati, na changamoto zote zilizokuwa zinaambatana na hedhi yako zitapotea kabisa baada au kabla ya siku saba (7) za Kumaliza matumizi ya dawa yako.

JINSI YA KUANDAA NA KUTUMIA SPINACH KWA AFYA YA HEDHI:
Spinach ni miongoni mwa mboga muhimu zaidi kwa wanawake hasa wakati wa hedhi kwa sababu ina virutubishi vinavyosaidia kupunguza changamoto zinazotokea kipindi cha hedhi. Hapa kuna sababu kuu kwanini ni muhimu:

1. Chanzo kizuri cha madini ya chuma (Iron)
• Wakati wa hedhi, mwanamke hupoteza damu, hivyo mwili hupoteza pia madini ya chuma.
• Upungufu wa chuma husababisha uchovu, kizunguzungu na udhaifu.
• Spinach husaidia kurejesha kiwango cha chuma mwilini, na hivyo kupunguza dalili za upungufu wa damu (anemia).

2. Magnesiamu kwa kupunguza maumivu wakati misuli inatanuka na kusinyaa (Cramps)
Magnesiamu ni madini muhimu sana ambayo yanahitajika katika zaidi ya michakato 300 ya kibaolojia ndani ya mwili. Husaidia mfumo wa neva na misuli, Huimarisha kinga ya Mwili, Husaidia kuweka mapigo ya moyo katika hali ya kawaida na thabiti, Husaidia kuthibiti usawa wa sukari mwilini, Husaidia katika uzalishaji wa nishati Mwili hivi vyote ni muhimu sana katika afya ya mwil.
Hivyo,
i. Kupunguza Maumivu ya Tumbo (Cramps)
• Magnesiamu hulegeza misuli ya uterasi (kizazi), hivyo kupunguza mikazo na maumivu makali yanayotokea wakati wa hedhi.
• Hii hupunguza maumivu ya tumbo na mgandamizo wa misuli wakati wa hedhi.
ii. Kupunguza Uvimbe na Maumivu Mengine
• Ina uwezo wa kupunguza uchochezi (inflammation) mwilini, jambo linalosaidia kupunguza uvimbe na maumivu ya tumbo, kiuno au mgongo yanayoambatana na hedhi.
iii. Kusawazisha Homoni
• Magnesiamu huchangia katika kudhibiti homoni za uzazi k**a estrogeni na projesteroni, hivyo kusaidia mzunguko wa hedhi kuwa na mpangilio bora.
iv. Kusaidia Mfumo wa Neva na Hisia
• Magnesiamu huchochea utulivu wa mfumo wa neva, hivyo kupunguza wasiwasi, hasira na msongo wa mawazo (PMS).
• Pia huongeza ubora wa usingizi, jambo muhimu hasa wakati wa hedhi ambapo wanawake wengi hukumbwa na uchovu.

3. Vitamini K kwa kudhibiti mtiririko wa damu
• Vitamini K inayopatikana kwenye spinach ni muhimu kwa kuganda kwa damu.
• Husaidia kudhibiti hedhi nzito na kuhakikisha damu haitoki kwa wingi kupita kiasi.

4. Folate na Vitamini B
• Spinach ina folate (Vitamini B9) ambayo husaidia katika uzalishaji wa seli mpya za damu.
• Vitamini B pia hupunguza uchovu, msongo wa mawazo na mabadiliko ya hisia wakati wa hedhi (PMS).

5. Antioxidants na Vitamini C
• Spinach ina antioxidants na Vitamini C zinazolinda mwili dhidi ya uvimbe na kuimarisha kinga.
• Pia hupunguza hisia za kutojisikia vizuri ambazo mara nyingi hujitokeza kipindi cha hedhi.

6. Nyuzinyuzi (Fiber)
• Nyuzinyuzi katika spinach husaidia usagaji wa chakula na kupunguza kujaa gesi au kuvimbiwa, hali inayosumbua wanawake wengi wakati wa hedhi.

MAANDALIZI:
• Chagua spinach ya kienyeji (Spinach).
• Osha vizuri na kata vipande vidogo vidogo.
• Tia vipande hivyo kwenye kinu cha kiasili
• Ponda vizuri mpaka mboga ije k**a mboga ya kisamvu.
• Tia maji safi glasi ujazo robo tatu kisha vuruga/changanya kwa mkono wako ili kuchanganyika vizuri.
• Kamua kwa kutumia kitambaa safi k**a vile unavyokamua tui la n**i.
• Utapata juisi safi ya spinach.

MATUMIZI:
• Tumia wakati upo kwenye hedhi kunywa mara tatu kwa siku (nusu glasi asubuhi, nusu glasi mchana, na nusu glasi jioni).
• Kila siku tengeneza juisi mpya (fresh), usihifadhi ya jana.

FAIDA
• Husaidia kusafisha mirija ya uzazi,
• Husaidia kuondoa maumivu ya tumbo wakati wa hedhi,
• Huchangia kuongeza hisia na hamu ya kushiriki tendo la ndoa.
• Huweza kusaidia kuongeza uwezekano wa kupata ujauzito haraka iwapo unataka.
• Kwa ujumla, huchangia afya bora ya wanawake na kupunguza changamoto za hedhi kuvurugika, Kukosa hedhi, kupata maumivu makali wakati wa hedhi na mengine mengi.
Matokeo
• Utaanza kuona damu nyingi ya hedhi ikitoka iyo inaashiria mirija yako ya uzazi inasafishwa kabisa,

MADHARA:
• Dawa hii haina madhara yoyote.

ANGALIZI/USHAURI:
• Tumia dawa hii wakati wa hedhi tu kwa mwanamke kwa matokeo mazuri zaidi,
• Hakikisha zingatia Maelekezo ya vitu gani vya kuepuka navyo na vitu gani vya kufanya ili kuifanya dawa hii iwe na matokeo na ufanisi wa kudumu,
• Zingatia hatua za maandalisi na kipimo sahihi k**a ulivyoelekezwa.

🌿 MTI WA MBONO KABURI CHAPISHO ZIMA LENYE MAELEZO YA KINA NA TAARIFA ZOTE NITAWEKA KWENYE WhatsApp page hii:Jiunge hapa:...
17/10/2025

🌿 MTI WA MBONO KABURI

CHAPISHO ZIMA LENYE MAELEZO YA KINA NA TAARIFA ZOTE NITAWEKA KWENYE WhatsApp page hii:
Jiunge hapa: https://chat.whatsapp.com/BUJeu9yiTspBpFz177CT8f

Sehemu zinazotumika katika tiba:

Majani (leaves), Utomvu (latex), Magamba (magome), mizizi (Roots), na matunda yake (mbegu).

⚕️ Matumizi ya Kienyeji na Kiasili katika Tiba

Mmea huu umetumika kwa muda mrefu katika tiba za jadi kutokana na uwezo wake mkubwa wa asili katika kutibu na kudhibiti magonjwa mbalimbali, kwa baadhi ya changamoto hutumika wenyewe au kwa kuchanganya na mimea au vitu vingine kwa ufanisi zaidi. Baadhi ya matumizi yake muhimu ni k**a yafuatayo:

1. Kupunguza uvimbe na maumivu ya viungo.

2. Kuponya vidonda, kukata damu, na kusaidia uponyaji wa ngozi.

3. Kuzuia na kutibu maambukizi ya bakteria, fangasi, na baadhi ya virusi.

4. Kutibu matatizo ya tumbo na mmeng’enyo wa chakula, ikiwemo kuvuja damu ndani ya tumbo (internal bleeding).

5. Kushusha homa na kutibu malaria pamoja na homa ya manjano (jaundice).

6. Kuondoa maumivu ya misuli, baridi yabisi, na matatizo ya mishipa ya fahamu.

7. Kutibu maambukizi ya ngozi na magonjwa ya sikio.

8. Kutibu magonjwa ya zinaa, hasa kisonono (gonorrhea).

9. Kutibu maumivu ya jino, kutokwa damu kwenye fizi, na maambukizi ya mdamo.

10. Kupunguza uvimbe katika kizazi (k**a fibroids) na kurekebisha mzunguko wa hedhi — ikiwemo matatizo ya kutopata hedhi, kutokwa damu nyingi au damu mfululizo.

11. Kuzuia ujauzito kwa njia ya asili (traditional contraceptive).

12. Kusafisha tumbo kwa matumizi ya kiasi kidogo cha dawa ya kuharisha (purgative).

13. Kupunguza gesi tumboni na kuboresha mmeng’enyo wa chakula.

14. Kusaidia wanaume wenye changamoto ya nguvu za kiume, hususan kushindwa kusimamisha uume kwa muda wa kutosha wakati wa tendo la ndoa.

Leo tuangazie changamoto zifuatazo;

VIDONDA VYA TUMBO, KUHARISHA DAMU, MAAMBUKIZI KWENYE TUMBO au UTUMBO
Kuna chapisho niliwai elezea namna ya kutibu vidonda vya tumbo kwa kutumia Mmea wa mvuti, leo tuangazie mmea huu wa Mmbono kaburi.

Tafuta Mti wa mbono kaburi, kata tawi ambalo sio teke sana liwe limekomaa kiasi fulani, kisha ondoa hayo majani ubaki na fimbo ya ilo tawi, safisha vizuri iyo fimbo kwa maji safi ya chumvi, alafu bandua gamba la iyo fimbo vizuri.

Utatafuna kipande cha iloganda vizuri alafu meza ayo maji yake. Alafu tafuna karoti moja tu na kisha kunywa maji ya uvuguvugu glasi moja (1).

Fanya ivo asubuhi kabla ya kupata kifungua kinywa na jioni kabla ya chakula cha usiku kutwa mara mbili (2) kwa siku, endelea kutumia kila siku kwa mfululizo wa jumla ya siku tano (5) hadi (7).

Hakika shida ya vidonda vya tumbo, maumivu ya tumbo kwasabau ya maambukizi kwenye tumbo au utumbo, kuhara damu yatapona kabisa.

Tahadhari: Mjamzito k**a mimba yako ipo chini wa wiki 10 usitumie mmea huu.

🌿 Tumfafiya (Calotropis procera)Mmea wa Tumfafiya ni miongoni mwa mimea yenye historia ndefu na ya kipekee duniani, hasa...
12/10/2025

🌿 Tumfafiya (Calotropis procera)

Mmea wa Tumfafiya ni miongoni mwa mimea yenye historia ndefu na ya kipekee duniani, hasa katika Bara la Asia, hususan nchini India. Kwa watu wa imani ya Uhindu, mmea huu unahusishwa moja kwa moja na ibada zinazomhusu Mungu Shiva, hivyo hutumika sana katika matambiko, kutoa sadaka na kufanya ibada za maombi.

Mafusho ya magome ya mmea huu ufukuza Roho chafu (Mapepo, Majini, Mashwetani) kwa mtu na nyumba au ofisini, Maji ya Majani ya mmea huu ukitumia kufutia mwili (sio kuioga) huondoa nuksi na majanaba, Uvuta Mafanikio na kheri kwenye biashara, ofisi au utafutaji kipato. Uondoa magomvi na mafarakano ndani ya nyumba baina ya wapenzi.

Zaidi ya matumizi yake ya kidini na imani, Mmea wa Tumfafiya ni mmea muhimu sana katika mfumo wa tiba wa Ayurveda, ambapo huchukuliwa kuwa na nguvu kubwa za kiafya na kiroho. Kadhalika, katika maeneo mengi barani Afrika — ikiwemo Tanzania — mmea huu umetumika kwa karne nyingi katika tiba za kiasili kwa magonjwa ya mwili na masuala ya kiroho.

Makazi na Maeneo ya Ukuaji:
Tumfafiya hukua vizuri katika maeneo yenye hali ya joto na ukame, k**a vile nyika na miinuko yenye udongo wa mchanga. Ni mmea unaostahimili ukame na unaweza kustawi hata kwenye udongo usio na rutuba nyingi.

Tahadhari:
Ni muhimu kufahamu kuwa mmea huu una kiasi fulani cha sumu ya asili katika sehemu zake mbalimbali, hususan majani, utomvu na mizizi. Kwa hiyo, matumizi yake yanapaswa kufanywa kwa uangalifu mkubwa na kwa ushauri wa tabibu wa tiba asilia mwenye uzoefu, hususan kwa matumizi ya ndani na machoni. Kwani matumizi mabaya yanaweza kusababisha madhara kiafya k**a ilivyo kwa mitishamba yoyote inakiasi, na utaratibu wa kuandaa na kutumia.

🌱 Matumizi ya Kiasili na Kibiolojia

Katika tiba za jadi, mmea wa Tumfafiya hutumika kwa matumizi ya ndani na ya nje ya mwili, kutegemea aina ya tatizo linalotibiwa. Sehemu mbalimbali k**a majani, maua, mizizi, utomvu (maziwa meupe) na magome hutumika kwa kuchanganywa au peke yake.

Baadhi ya changamoto ambazo mmea huu hutumika kutibu au kupunguza ni k**a ifuatavyo:

1. Matende na minyoo
2. Kifafa na misuli kukak**aa
3. Baridi yabisi na gout
4. Vidonda na majipu
5. Kuvimba kwa korodani
6. Homa ya manjano
7. Kung’atwa na mbwa, nyoka, nge au wadudu wenye sumu
8. Alama nyeusi usoni
9. Kuhara na kuhara damu
10. Homa ya mishipa
11. Kaswende
12. Matatizo ya ini na wengu
13. Ukoma
14. Maumivu ya jino
15. Malaria na homa ya vipindi
16. Gout
17. Kipanda uso (migraine)
18. Kizunguzungu
19. Kupooza na maumivu ya neva
20. Kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi (menorrhagia)
21. Bawasiri
22. Mafua, kikohozi, pumu na bronchitis
23. Maumivu ya miguu
24. Saratani (aina fulani kwa hatua za awali)
25. Mashilingi/malengelenge
26. Mawe kwenye figo
27. Ugonjwa wa kisukari
28. Shinikizo la damu
29. Maambukizi ya ngozi k**a mba, ukurutu, upele na utangatanga
30. Maumivu ya sikio
31. Matatizo ya tumbo na mmeng’enyo wa chakula
32. Kuondosha uchawi, nuksi na bahati mbaya (matumizi ya kiroho)
33. Uvimbe na maumivu ya viungo
34. Kuota vinyama sehemu mbalimbali za mwili
35. Kuleta bahati, amani, pesa na mafanikio (matumizi ya kisaikolojia na kiroho)

Hitimisho:
Tumfafiya ni mmea wa ajabu unaounganisha tiba, imani na utamaduni. Ni ishara ya hekima ya kale inayothibitisha uhusiano wa binadamu na mazingira yake. Unaweza kutazama na kusikiliza video hapo chini kwa kujitibia magonjwa ya nje ya mwili k**a vile

- Maumivu ya Viungo
- Baridi yabisi na Gout
- Bawasiri iliyotoka nje
- Maambukizi ya Sikio,
- Kuvimba Miguu, kuuma na kuwaka moto,
- Maumivu ya Mgongo
- Kupooza,
- Kushusha na kuweka sawa shinikizo la damu,
- Kuweka mfumo wa neva vizuri (Kushusha Msongo wa mawazo na Kukosa usingizi)

🌿 **Tumfafiya (Calotropis procera)Utangulizi:Mmea wa Tumfafiya ni miongoni mwa mimea yenye historia ndefu na ya kipekee duniani, hasa katika Bara la Asia, h...

Address

Tanga

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tiba Asili ya Mimea na Chakula posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Tiba Asili ya Mimea na Chakula:

Shortcuts

Share

Category